BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
- Thread starter
- #41
Posted Date::12/19/2007
Chadema wadai ripoti ya ukaguzi BoT
*Wahoji serikali inasubiri nini?
Muhibu Said na Mwanaid Omary
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitaka serikali kuiweka hadharani ripoti ya ukaguzi wa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo tayari mkaguzi ameiwasilisha serikalini.
Tamko hilo lilitolewa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho, katika Hoteli ya Land Mark, jijini Dar es Salaam jana.
Alisema wamefikia uamuzi huo kwa kuwa muda uliotolewa kwa Kampuni ya Ernest and Young kuchunguza tuhuma hizo, kumalizika, huku ripoti ya uchunguzi huo ikiwa imekumbatiwa serikalini.
"Hivyo, tunamtaka Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Waziri wa Fedha, Zakhia Meghji watupe ripoti hiyo," alisema Mbowe.
Alisema ameshangazwa kusikia ripoti hiyo kwamba imepelekwa kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa ajili ya kupitiwa, kitendo alichodai kuwa, kinatia shaka huenda kuna njama za makusudi zinazofanywa na serikali ili kutaka kuificha.
"CAG anaipitia nini? Au wanataka kuificha? Fedha zetu tumeibiwa, tumewatangazia, sasa tunataka ripoti iwekwe hadharani," alisema Mbowe.
Alisema pamoja na kuwataja hadharani watuhumiwa wa ufisadi, hadi sasa serikali imeshindwa kuchukua hatua dhidi yao na pia dhidi ya wale walioibua tuhuma hizo kuthibitisha kama waliyoyadai ni ya uongo.
Alihoji safari za mara kwa mara za Rais Kikwete nchini Marekani akiitaka serikali kueleza kilichoko nchini humo, zinawanufaisha nini wananchi na sababu za safari hizo kutogharamiwa na serikali.
Pia aliitaka serikali kueleza sababu za mkutano wa Sullivan unaotarajiwa kuwashirikisha wafanyabiashara Wamarekani weusi zaidi ya 1,000, kufanyika nchini.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika mkoani Arusha Juni 2-6, mwakani.
Pia aliitaka serikali kueleza tuzo alizopewa Rais Kikwete katika ziara yake ya hivi karibuni nchini Marekani, kwamba zinasaidia vipi maisha ya Mtanzania wa kawaida.
Katika ziara yake aliyoifanya Marekani Desemba 12-14, mwaka huu, Rais Kikwete alitunukiwa tuzo kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo na kwa kuhutubia kweye mkutano wa nchi hiyo.
Pia Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk Asha-Rose Migiro alitunukiwa tuzo kwa mchango wake wa kuleta amani katika nchi za Maziwa Makuu.
"Mwekezaji akikusifu, ujue kuwa wewe ni ndondocha. Wawekezaji wananeemeka kupitia kwa Kikwete, sisi tunateseka," alisema Mbowe.
Kutokana na hali hiyo, Mbowe alisema wasiwasi juu ya mkutano wa Sullivan mjini Arusha, unakuja kutokana na mwanzilishi wake (Sullivan) kuwamo miongoni mwa washauri wakubwa wa Kampuni ya madini ya Barrick inayomiliki migodi kadhaa hapa nchini.
Alidai wasiwasi huo unatiwa nguvu kutokana na safari za Rais Kikwete Marekani, kugharamiwa na wawekezaji waliompa tuzo hizo.
"Huyu Sullivan ndiye aliyesababisha mgogoro wa mafuta Nigeria. Kama Tanzania kutagundulika kuna mafuta chini ya utawala wa CCM, basi tumekwenda na maji, Rais anaingizwa kwenye kiini macho," alisema Mbowe.
Naye Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amemjibu Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, kuhusu tuhuma za ubaguzi na upendeleo alizozielekeza kwa chama hicho na kusema kwamba, hajui analolisema.
Dk Slaa alitoa kauli hiyo alipozungumza na Mwananchi katika mahojiano maalum, jijini Dar es Salaam jana.
Alisema Wangwe ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, hawezi kuthibitisha tuhuma hizo na kwamba, ana wasiwasi huenda matamshi aliyoyatoa yana lengo la kupandikiza jambo katika chama na kuupotosha umma.
"Anayetoa tuhuma hizo hajasoma na hajui analosema. Matamshi yake yanapandikizwa kimalengo. Kama ana ushahidi wa hayo anayoyasema autoe na siyo maneno matupu," alisema Dk Slaa.
Dk alisema madai ya Wangwe kwamba fedha za ruzuku zinaishia makao makuu ya chama, hayana ukweli, badala yake fedha hizo zimekuwa zikipelekwa pia mikoani.
Alisema katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, chama kilisambaza Sh 60 milioni katika mikoa yote nchini, isipokuwa Lindi na Mtwara, kwa ajili ya kugharamia ziara zilizofanywa na viongozi katika mikoa hiyo.
Pia alisema zaidi ya Sh 200 milioni zilisambazwa katika mikoa yote nchini kugharamia manunuzi ya vifaa mbalimbali vya chama, kama vile bendera na kadi, kitu ambacho hakuna chama chochote kilichoweza kufanya hivyo.
Kuhusu madai ya ubaguzi na upendeleo wenye misingi ya kidini na kikanda, Dk Slaa alisema hayana ukweli wowote na kwamba, kinachozingatiwa na chama katika uteuzi wa viongozi, hasa wabunge wa viti maalumu, ni uwezo na sifa na si sura wala vigezo vilivyotajwa na Wangwe.
"Chadema ni chama pekee cha kitaifa, hakifanyi ubaguzi, hakuna masuala ya kifamilia kama anao ushahidi wa watu hao na autoe. Nina uhakika hata mkimfuata (Wangwe) sasa hivi atoe huo ushahidi, hana," alisema Dk Slaa.
Wangwe alitoa tuhuma hizo kupitia vipeperushi vilivyosambazwa nchi nzima na wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mkono vikiwatuhumu baadhi ya viongozi wa Chadema kuendesha chama kwa upendeleo, hasa katika mgao wa ruzuku na ubaguzi wa misingi ya kidini na kikanda.
Akizungumza na mwandishi wa Mwananchi muda mfupi kabla ya kuingia kwenye kikao cha Kamati Kuu juzi, Wangwe alisema kutokana na kasoro hizo, atahakikisha analeta mabadiliko ya kweli ndani ya chama ili kukiepusha kuendeshwa kama Shirika lisilo la kiserikali (NGO).
Alisema jambo kubwa linalokitia dosari chama ni ofisi za wilaya na kata kutokuwa na mawasiliano na makao makuu, hasa katika mgao wa ruzuku na uteuzi wa wabunge wa viti maalum.
Wangwe alidai mgao wa ruzuku pamoja na uteuzi wa wabunge wa viti maalum, vimekuwa vikitolewa na uongozi wa Chadema kwa kuangalia upande mmoja wa wanachama wanaotoka katika Kanda ya Kaskazini nchini.
"Chama kimekuwa mali ya koo na familia fulani. Tunataka kiwe cha wanachama," alisema Wangwe ambaye anawania nafasi hiyo na Mbunge wa Mpanda Kati (Chadema), Said Arfi.
Wakati Wangwe akisema hayo, wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mbunge huyo (Wangwe) katika kinyang'anyiro hicho, jana walisambaza vipeperushi vinavyotuhumu kuwapo na upendeleo katika mgao wa ruzuku za chama na ubaguzi wa kidini na kikanda katika chama hicho.
Vipeperushi hivyo vilivyotawanywa Makao Makuu ya Chadema, mikoani na katika eneo ambalo Kamati Kuu ilikutana jana, vinadai kwamba chama hicho kimekuwa kikipata ruzuku ya Sh 60 milioni kila mwezi, lakini fedha hizo zimekuwa zikiishia makao makuu matumizi yake hayawekwi bayana.
"Tunasema inawezekana kila mkoa ukapata Sh 1.5 milioni kila mwezi na Makao Makuu itabaki na zaidi ya Sh10 milioni ambazo zinawatosha kwa shughuli za chama," ilieleza sehemu ya kipeperushi hicho.
Kipeperushi hicho ambacho Mwananchi inayo nakala yake, pia kimedai kuwapo kwa "ubinafsi" katika chama ambao umesababisha karibu wabunge wote wa viti maalum kuteuliwa kutoka katika mkoa mmoja ulioko eneo la Kaskazini mwa nchi.
"Wabunge viti maalum karibu wote wanatoka upande mmoja na kutoa ruzuku ya chama kwa upande mmoja (Kaskazini) haya yote yanatukera," kilieleza kipeperushi hicho na kuwataka wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho kumchagua Wangwe ili kukinusuru chama na mambo hayo.
Wabunge hao ambao wote wanatoka katika Mkoa wa Kilimanjaro, ni Halima Mdee na Grace Kihwelu, Maulida Komu na Lucy Owenya.
Katika kipindi cha mwezi mmoja, Wangwe amekuwa akiibua hoja ambazo zimezua mjadala mkubwa ndani ya chama hicho. Hoja ya hivi karibuni ni ile aliyodai kuwa Zitto hakupaswa kuingia katika Kamati ya kupitia upya mikataba ya madini.