Ridhiwani Kikwete, thibitisha au kanusha

:shetani: ACHA KOROPOKA CHALII YANGU KWANI INGEKUWA NI WW, BABA YAKO NI RAIS UNGEJENGA CHUMBA KIMOJA TU. KAA UKIJUA KUA YEYE ANA NAFASI KUBWA SANA YA KUPATA MICHONGO TAZANIA NA NJE YA TANZANIA

NI HILO TU TAFAKARI

YEYE KWA DAKIKA KU DEPOSIT MAMILION SIONI JAMBO LA AJABU:flypig:
 
2015 tutagawana hizo mali za wananchi. Msihofu anatutengenezea mijengo ya bure
 
View attachment 57923Ridhiwani kikwete naomba uthibitishe au ukanushe umiliki wako wa jengo hili ndani ya Dodoma.Nitatoa nyaraka baada ya kusikia kauli.Naomba kuwasilisha.

Kwa maoni yangu mimi sioni kama ni tatizo kuwekeza au kuwa na mtaji huo kama atakuwa alifata taratibu za kitaalam na kisheria katika kuwekeza. ukiangalia mazingira yanamruhusu kufanya hivyo; mtu kazaliwa kwenye kkb, kula kulala bure, mshahara wake na familia unakuwa hauna kazi zaidi ya kuutumia katika kuwekeza, na nampongeza kuwekeza ndani maana kuna wezi ambao wanakimbiza pesa zetu nje.
Mimi binafsi nimezaiwa katika familia masikini sana, ajira yangu haizidi miaka 20, mshahara wangu unabajeti zote za kifamilia kuanzia kula, kulala, kusaidia ndugu n.k. lakini nimefanikiwa kujibana na kujenga kakibanda ka kuweka mbavu wakati wa usiku. So katika hili la la huyu ndugu na nafasi alionayo, iwapo hakuvunja sheria yoyote mi sina shida naye zaidi ya kumpongeza kwa kuwekeza ndani. Maana hata kama ningekuwa mimi binafsi nisingetofautiana nae katika kuwekeza; nafasi inaruhusu kufafanya hivyo.
 
Ndahani, nashawishika kuwa yawezekana wanatumia nafasi waliyonayo kupata mitaji kwa njia halali. Tofauti yake ni kuwa mimi na wewe tukienda bank kuomba mtaji, zengwe lake linaweza kuwa refu mpaka ufanikiwe, lakini Ridhwani dhamana yake ina faia mara dufu tu. Pia Ridhwani anajua mbinu nyingi ambazo nyingine anaweza kuwa anatengenezewa kabisa ambazo ni halali kwa wanaojipendekeza na akapata mitaji. Sitashangaa kusikia anadaiwa madeni mengi. Ila pia kingine mbacho hutokea kwa nchi nyingi za Afrika ni wawekezaji wetu wawe wazungu wawe wahindi, hupenda sana kutoa bahasha kwa familia za viongozi, na hizi wengi wa wanafamilia wameingia kwenye mtego, hope Ridhwani hajanasa.

Naona jamaa anaandamwa sana, ingawa sijui ni kwa mambo ya ukweli au yakupikwa. Time will tell
 
suala la msingi ni kwamba kwa vyovyote huyu dogo ni meneja wa biashara za familia na kama yasipompata yaliyompata Mtoto wa rais hapa jirani kusini kwa tanzania ni bahati
 
Baada ya 2015 tutakumbushana mambo mengi sana, maana watu wengi wataachwa bila nguo.
 
Badala na wewe kutafuta vyako unakaa hapa JF kuleta unafiki, kama yake wewe inakuuma nini bana? We kama unataka gorofa la hivyo unaweza kulipata pia. Nenda Saudi Arabia tu. Utarudi na mihela kibao.

Wewe ulienda Saudi Arabia? Au ndo mchezo wako mtoto hatumwi haambiliki..
 



wabongo bana... kama anamiliki kihalali na kufuata taratibu zote .. kutakuwa na tatizo gani.. mbona wapo watanzania wakawaida wanamiliki vitu kama hivo..? au yoyote anyekuzidi ni ndio definition mpya ya fisadi ..?

ni kweli, kuna watu wa kawaida wana majengo ya namna hiyo sasa huyu kwa kua ni mtoto wa rais basi ni issue, at least ana invest hapa nyumbani na kubadilisha sura ya nchi. watanzania badala ya kulalamika na nyie mchape kazi mjiendeleze mbona bank zipo na mikopo inatoa na nyie mtaweza kufanya anachofanya
 
Baada ya 2015 tutakumbushana mambo mengi sana, maana watu wengi wataachwa bila nguo.
Kinachotokea baada ua uongozi husika kundoka madarakani, huwa hata kama mali zilizopatikana zilipatikana halali, bado mkakati wa kulipiza kisasi (mfano kama kulikuwa na tukio la mauaji au nguvu kupita kiasi kwa upinzani halafu upinzani ukamshinda laiyefanya hivyo), basi kesi hutengenezwa kumwadabisha yeye na familia yake. Na kwa tiabia hii ya vitisho vya kulipiza kisasi kabla ya chaguzi mkuu, huwafanya wengi wanaotawala kufoji mikakati ya kuenelea kulinda maslahi yao kwa nguvu au kwa ujanjaujanja. So nawasihi Vyama vya siasa vilivyopo madarakani viepuke kutumia lughahii ili kupunguza uwezekano wa vurugu.
 
attachment.php

Ridhiwani kikwete naomba uthibitishe au ukanushe umiliki wako wa jengo hili ndani ya Dodoma.Nitatoa nyaraka baada ya kusikia kauli.Naomba kuwasilisha.
CCM na uzao wake ni janga la kitaifa, wizi kila kona weka na LAKE OIL CO's weka pia masemitrailer kibao toka bandarini, mbona Watanzania ni wakunyanyasa tuu!!!!Wanachukua kama zao vile, hukuna kizuizi??
 
sina tatizo na uwekezaji hasa wa hapa nchini ilimradi ufuate sheria . ila ningekuwa na mamlaka kama ... ninge anza kutafuta fedha zetu zilizo fichwa nje ya nchi ili zije kusaidia kfufua na kuendeleza viwanda na ajira ya kutosha hapa nchini
ndio maana nasema ningekuwa radhi kuwasamehe wote walio iba na kuwekeza hapa nchini na kuwapa ajira watanzania wenzao na pia serikali kupata kodi yake vizuri kwa maendeleo ya taifa na wananchi wake kwani hela hizo ni zao watz. ila walio iba fedha zetu na kupeleka nje ningekula nao sahani moja na fedha ingerudi kusaidia watanzania wangu

please hayo ni mawazo yangu tuu
 
Kwa mtazamo wangu, ingekuwa bora kwa mtoa mada kuweka hadharani kwanza kila ushahidi alionao kama vile:

- Nyaraka zinazoonesha mmiliki.
- Njia jengo lilivyopatikana (kama kuna harufu ya rushwa na upendeleo).
- Kama kuna wenye madai kuhusu umiliki huo au kudhulumiwa n.k.,
kuliko kuweka picha ya jengo tu na kumtaja mtu athibitishe kama ni la kwake au la.
Vyenginevyo tunaigeuza JF kama jukwaa la mipasho.
 
nilishasema hapo nyuma kitambo kuwa wanaJF wengi wamejawa na ushabiki na chuki na watuwa tabaka fulani fulani hivi ambao wao huwaona hawastahili kumiliki properties... kama kuyu kijana. Haya mambo ya chuki kwa watu tunaojiita great thinkers hayatusaidii kutuvusha hatua kuelekea maendeleo chanya.kuna mambo mengi tunapashwa kuyaangalia na kutoa way forwad kwayo kama mambo ya ufisadi ambao wengi mafisadi tumetajiwa na tunawafahamu kwa majina.... Chenge, Lowasa,n.k list ni ndefu. hawa ndio wame-drain pesa toka serikalini mpaka leo serikali haina pesa ya kuwalipa madaktari wanaogoma leo. maoni yangu kama mwanaJF ni kuwa tuelekeze mijadala yetu huko ili tuliokoe taifa hili kutoka mikononi mwa wanyonyaji hawa........mnaionaje hiyo?
 
Back
Top Bottom