Revealed: Viongozi Jukwaa la Wahariri walimwalika Nchimbi katika maandamano

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Wana JF

Nimethibitishiwa na msaidizi wa karibu wa Waziri wa mambo ya ndani kuwa mmoja wa viongozi wa juu wa Jukwaa la wahariri na aliyekuwa na jukumu la kuandaa maandamano hayo Bwana Nevil Meena ndie aliyemwalika waziri nchimbi kuhudhuria maandamano ya wanahabari

Bwana Meena anadaiwa kumruhusu waziri kuja kwenye maandamano kama mtu wa kawaida sababu watu wote walikuwa wanakaribishwa. Hii ndio sababu ilimfanya Meena kupatwa na aibu pale waandishi walipomkataa waziri kuhutubia huku yeye akiwaomba wamsikilize lakini nguvu za umma za waandishi zikamshinda.

Hivyo itakuwa ni makosa kulaumu ujio wa waziri pale na madai kuwa alivamia. Ukweli ni kwamba alipewa ruhusa ya kuwepo pale tena ruhusa toka kwa waandaaji wa maandamano wenyewe, yaani Jukwaa la wahariri.

Nawasilisha
 
Nyongeza: Taarifa aliyoitoa leo Nchimbi ndio aliyotaka kuwaeleza wanahabari pale kwenye maandamano lakini akakosa forum hiyo
 
Yani kama Meena kakubali kupokea bahasha ili amsafishe Mh.Nchimbi, basi taaluma ya habari haitakaa iheshimike na kuaminika kwa 100%
 
Hata mie nilitilia mashaka. Mtu mzima na PhD yake aende sehemu bila kualikwa, how come? Afu em jaribu kusoma(japo vichwa vya habari) makala za nevin meena kwenye mwananch jumapili, utajuwa tu kuwa ni gamba anayefunga na kuomba apewe ukuu wa wilaya.
 
Ni kweli kabisa. Unajuwa iko hivi, waliokuwa wana andamana ni waandishi wa habari na siyo wahariri. Wahariri walikwenda pale kwa ajili ya kuwapokea wana taaluma wenzao tu. Lakini je nani alitakiwa apewe hayo malalamiko ya unyanyasaji wa vyombo vya habari uliopelekea kuuwawa kwa Mwangosi? Ni serikali obvious, sasa lawama ilikuwa ni kwa jeshi la polisi ambalo liko chini ya Waziri wa mambo ya ndani. Hivyo wahariri walimualika Nchimbi kuja kupokea malalamiko ya jeshi lake. Full stop
 
Wana JF

Nimethibitishiwa na msaidizi wa karibu wa Waziri wa mambo ya ndani kuwa mmoja wa viongozi wa juu wa Jukwaa la wahariri na aliyekuwa na jukumu la kuandaa maandamano hayo Bwana Nevil Meena ndie aliyemwalika waziri nchimbi kuhudhuria maandamano ya wanahabari

Bwana Meena anadaiwa kumruhusu waziri kuja kwenye maandamano kama mtu wa kawaida sababu watu wote walikuwa wanakaribishwa. Hii ndio sababu ilimfanya Meena kupatwa na aibu pale waandishi walipomkataa waziri kuhutubia huku yeye akiwaomba wamsikilize lakini nguvu za umma za waandishi zikamshinda.

Hivyo itakuwa ni makosa kulaumu ujio wa waziri pale na madai kuwa alivamia. Ukweli ni kwamba alipewa ruhusa ya kuwepo pale tena ruhusa toka kwa waandaaji wa maandamano wenyewe, yaani Jukwaa la wahariri.

Nawasilisha

Njaa itaua waandishi wetu
 
In his right mind Nchimbi aliona ni busara kuhudhuria hiyo event? It is easy to kusema kaalikwa ni huyu au na yule, but the buck stops with him - Nchimbi.

Kama anashindwa kufanya judgement kwa jambo lililowazi kama la kutohudhuria maandamano ya watu wanaoombeleza kifo ambacho kimesababishwa na watendaji wake, anaweza nini?
 
Ni kweli kabisa. Unajuwa iko hivi, waliokuwa wana andamana ni waandishi wa habari na siyo wahariri. Wahariri walikwenda pale kwa ajili ya kuwapokea wana taaluma wenzao tu. Lakini je nani alitakiwa apewe hayo malalamiko ya unyanyasaji wa vyombo vya habari uliopelekea kuuwawa kwa Mwangosi? Ni serikali obvious, sasa lawama ilikuwa ni kwa jeshi la polisi ambalo liko chini ya Waziri wa mambo ya ndani. Hivyo wahariri walimualika Nchimbi kuja kupokea malalamiko ya jeshi lake. Full stop

It sounds good mkuu
 
Dah nilihisi k2 kama hicho especial kutokana na hotuba aliyoitoa MEENA muda mfupi baada ya waziri kufukuzwa

ni kweli wengi walikuwa na hisia hizo baada ya kumuona waziri pale, hata mie niliwaza hivyo kisha mawazo nikayapotezea, lakini baada ya kuambiwa jioni hii na msaidizi wa waziri huyo nikajua kuwa kumbe hisia zangu zilikuwa sahihi
 
Back
Top Bottom