Remote control na simu za mkononi kwenye kitufe cha namba 5

mhondo

JF-Expert Member
Apr 23, 2011
968
342
Nimeangalia remote control nyingi na simu za mkononi na kubaini kuwa kwenye kitufe cha namba 5 kuna kinundu kidogo. Nataka nielewe kazi yake ni nini au kina maana gani?.
 
Mpwa hizo ni alama kwa ajili ya vipofu! ANgalia keyboard yoyote hata ya simu kama blackbery utakuta kuna kitufe 5 na photocopy machine pia zina hicho kitufe
 
Mpwa hizo ni alama kwa ajili ya vipofu! ANgalia keyboard yoyote hata ya simu kama blackbery utakuta kuna kitufe 5 na photocopy machine pia zina hicho kitufe

inamaana vipofu wanatumia namba 5 tu. Naomba unieleweshe zaidi.
 
Sio 'vipofu' bali ni 'wasioona' au walemavu wa macho. Bado hatujaeleweshwa vizuri kuhusu hizo alama. Tujuzeni jamani mnaofahamu.
 
inamaana vipofu wanatumia namba 5 tu. Naomba unieleweshe zaidi.

Kaka hiyo ni lead tu; Kwa mtu mwenye matatizo ya kutoona vizuri; akigusa kwenye key na kukuta kinundu anaelewa kuwa hiyo ni namba tano, kutoka hapo anajua upande wa kushoto kuna key zipi, halikadhalika kullia, juu na chini. Jaribu pia kuangalia kwenye keyboard ya computer yako, kwenye Herufi F na J kuna alama.
 
Kwa ajili ya vipofu kama walivyosema wengine, simu za touch zina system zengine kwa ajili ya vipofu, kuna story ya Stevie Wonder anaisifia iPhone kwa vile ni rahisi kutumia kwa vipofu.
 
Back
Top Bottom