Rangi za bendera ni ujumbe, uzalendo au urembo?

Wanaotakiwa kuwafundisha wadogo zetu heshima ya Bendera wanabadili mitaala daily. Wako busy wanachumia matumbo yao.

Kama unabisha nenda kwa kiongozi yeyote now mwambie akuimbie nyimbo ya "Tanzania Tanzania Nakupenda kwa moyo wote, nchi yangu Tanzania......" japo beti mbili kama uwasikii wakinyingata ngata. Lakini waulize mikataba yenye 10% inakuja lini? Watakutajia mpaka wajukuu wa hao investors...
 
wewe haujui familia yako itakula nini.. Ukasimame kwasababu filimbi imepigwa. Heshima ya taifa kwanza ni mahitaji muhimu ya mwanadamu!

mbona kipindi hicho tulishindia muhogo na chai lakini tuliweza kusimama.halafu inakuaje unapoteza masaa kwenye foleni ya magari na haugopi kushinda na njaa?
 
bendera ni alama muhimu ya uhuru wetu na sio kipande cha kitambaa!

Alama muhimu ya uhuru upi?uhuru uliochakachuliwa na mafisadi huo nao ni uhuru wa kujivunia?uhuru uliozaa matunda yanayoliwa na wachache!Tunachosema ni kwamba bendera yetu imepoteza maana yake halisi imebaki kuwa kama kipande cha kitambaa tu.
 
Alama muhimu ya uhuru upi?uhuru uliochakachuliwa na mafisadi huo nao ni uhuru wa kujivunia?uhuru uliozaa matunda yanayoliwa na wachache!Tunachosema ni kwamba bendera yetu imepoteza maana yake halisi imebaki kuwa kama kipande cha kitambaa tu.

inawezekana hali ya maisha imekuwa ngumu sana lakini hii haimaanishi tuifanyie dharau bendera yetu!
 
Wana JF naomba kuelezwa nimekuwa najiuliza maswali mengi bila kufikia muafaka ukifika au kuangalia ukumbi wa bunge chini kuna aina fulani ya kapeti lenye rangi za bendera ya taifa Tanzania na utaona wabunge wanakanyaga juu ya kapeti hilo naona maoni yenu wana JF
 
Sijui ni kwa nini walifikieia kuiweka bendera hapo chini na kuanza kuikanyaga. Ni uzalendo kweli au walipitiwa kwa kudhani kuwa ni kujenga uzalendo?
Mwanakadimu
 
Hiyo ni kudharau bendera na taifa kwa ujumla.
Unatoka msalani then unakanyaga bendera ya taifa.
 
Kwanza nitoe pole kwa msiba wa dada yetu. Mungu amtunze pahala stahiki.

Nataka kujua hivi Tanzania tuna heshimu bendera yetu? Ni heshima gani tunayoipa bendera yetu kama alama ya utaifa wetu?

Wote ni mashahidi tumeona bendera yetu ikitumika hata kwenye matangazo ya bia (mf Kilimanjaro). Where is the limit? Mtu

anaweza kushona tu sare ya bendera na kuvaa mitaani? (maana tumeona kwaya na hata wakina Kamata wameshona). Kama

nguo za jeshi ni kosa kwa asiye mwanajeshi kuvaa vipi bendera yetu?


See in USA
[h=3]United States Code Title 4 Chapter 1 — The Flag[/h]S. (i) The flag should never be used for advertising purposes in any manner whatsoever. It should not be embroidered on such

articles as cushions or handkerchiefs and the like, printed or otherwise impressed on paper napkins or boxes or anything that is

designed for temporary use and discard. Advertising signs should not be fastened to a staff or halyard from which the flag is

flown


(j) No part of the flag should ever be used as a costume or athletic uniform. . .

Idia
The Emblems and Names (Prevention of Improper uses) ACt of 1950


This Act also forbid used of Indian national flad for commercial purposed or as a costume!
 
Kila Taifa huru lina katiba na kaanun zake.

Si lazima zifanan na mataifa makubwa. Sheria zenu zinatokana na mila, desturi na sirka zenu na sio za wenzenu.

Funguka kiakili.
 
Sifikiri kama kuna cha kufunguka kiakili hapo! Ninachouliza ni nini heshima ya bendera yetu kama Taifa la Tanzania. Marekani na India

nimefanya kama reference ili ifahamike kuwa kila nchi ina taratibu na tamaduni zake. Sasa za kwetu ni zipi? Kwa mfano kuruhusu

Tanzania Breweries watangaze bia yao kwa kutumia bendera ya taifa yaweza kuwa ni utamaduni wetu? Au wewe kutumia bendera ya

taifa kama cushion za sofa zako au shuka kwa kitanda chako yaweza kuwa ni utamaduni wa taifa letu? Au vipi kikundi cha uimbaji

kikashona sare kwa kutumia bendera ya taifa, huo ndio utamaduni wetu? Mwenye akili timamu atafahumu kati yangu na yako nani

anapaswa kufunguka kiakili!
 
images

Jamani nakumbuka hapo nyuma sio kitambo sana ni kama miaka ya 80 - 90 ilikua ikifika jioni saa 12 bendera ya taifa la Tanzania ikishushwa ilikua inapigwa filimbi halafu hata wewe ulikua ukisikia filimbi ile na ukaona bendera ya taifa ikishushwa basi ni lazima ilikua usimame hadi hapo itakapopigwa filimbi nyingine kuashiria kua bendera imeshushwa halafu nyie mnaendelea na shughuli zenu.

Cha kunishangaza hapo juzi nikia karibu na kituo cha polisi mjini kati hapa jiji la Arusha ilipigwa filimbi kuashiria bendere inashushwa na mimi nilishudia lakini hakuna mtu alikua na time na hilo tukio na watu kuliona kama ni kama tukio la kawaida na maaskari hawakua na shauku ya kuwalazimisha watu kuitii bendera ya taifa kama ilivyokua huko zamani. Jamani hii imekaaje naomba kuwasilisha.
 
Wakuu nimepigwa na butwaa nilipokuwa naingia kwenye viwanja vya maonyesho ya Sabasaba DITF nikielekea katika banda letu. Nilipofika banda la Bunge la Tanzania, nilikuta kijana mmoja akiteremsha bendera ya Taifa iliyopo hapo 'bungeni' muda ambao sijazoea kuona bendera ya taifa ikiteremshwa, ilikuwa saa 12.46 asubuhi (niliwahi sana leo kuingia mle kuweka mambo sawa). Ajabu zaidi ni kwamba jamaa alikuwa yuko pekupeku bila viatu, mguu mmoja suruali imekunjwa na wala hakupiga filimbi kuashiria anataka kuteremsha bendera. Kwa haraka haraka nilimuona ni kama vile mtu wa kufanya usafi, ingawa kwa hilo sina uhakika sana, na najuta sikuwa na camera yangu muda huo. Sasa sijui inakuwa vipi hapa, naona kila mahali heshima ya serikali inapungua. Naombeni mwongozo kuhusu taratibu za kupandisha na kuteremsha bendera ya taifa.
 
Sijaona jambo la ajabu hapo ikizingatiwa ilikuwa sio muda unaostahili
 
Hata kama ingelikua ni muda muafaka nani siku hizi anamuda wakupoteza na kusimama kuiheshimu bendera ya taifa?? Kama ni kweli bendera ya taifa inaheshimika mbona machinga siku hizi wanatuuzia vitambaa hivyo na tunatolea makamasi!
 
hatuwezi kuheshimu mitambara hiyo isiyo na maana ...mi nafanya tambara la deki kwangu
 
dah! mkuu hizo ishu zilikua kitambo sana bendera inapandishwa morning na kushushwa jion na sheria ilikua ukiwa umbali fulani toka mlingoti wa bendera ni lazima usimame mguu sawa, hata kama una mguu mmoja, siku hizi hiyo makitu hakuna tena.
 
Wakuu nimepigwa na butwaa nilipokuwa naingia kwenye viwanja vya maonyesho ya Sabasaba DITF nikielekea katika banda letu. Nilipofika banda la Bunge la Tanzania, nilikuta kijana mmoja akiteremsha bendera ya Taifa iliyopo hapo 'bungeni' muda ambao sijazoea kuona bendera ya taifa ikiteremshwa, ilikuwa saa 12.46 asubuhi (niliwahi sana leo kuingia mle kuweka mambo sawa). Ajabu zaidi ni kwamba jamaa alikuwa yuko pekupeku bila viatu, mguu mmoja suruali imekunjwa na wala hakupiga filimbi kuashiria anataka kuteremsha bendera. Kwa haraka haraka nilimuona ni kama vile mtu wa kufanya usafi, ingawa kwa hilo sina uhakika sana, na najuta sikuwa na camera yangu muda huo. Sasa sijui inakuwa vipi hapa, naona kila mahali heshima ya serikali inapungua. Naombeni mwongozo kuhusu taratibu za kupandisha na kuteremsha bendera ya taifa.
na umesahau ile kanuni ya kusimama au kuinama kama roboti wakati wa kupandisha bendera na kushusha,hii safi sana
 
Back
Top Bottom