Rangi za bendera ni ujumbe, uzalendo au urembo?

Nimekumbuka wimbo nilioimba miaka mingi iliyopita kuhusu bendera ya Tanzania

..Bendera ya Tanzania, ndiyo ya kujivunia Ilianza kupepea mwaka sitini na moja............................................
Bendera ya Taifa Kutumika katika mambo ya kutangaza nchi jambo zuri kwa kuwa ni alama mojawapo ya Taifa letu
 
Sifa, uzito na umuhimu wa bendera ya taifa ni kubwa. Sote tunayatambuwa haya. Nakumbuka baada tu ya uhuru wa Tanganyika aklitokeya mzungu mmoja akasherehekeya uhuru kwa namna yake. Alimvalisha mbwa wake bendera ya taifa. Kagundulika la alikiona cha mtema kuni. Mwishowe alifukuzwa nchi.

Tangu lilipoamka jazba jipya la taifa stars bendera yetu tuipendayo nayo imetumika kivyake. Kwanza mfadhili akaishoneya jezi shati la juu. Hivi karibuni bendera hiyo hiyo ikapepeya juu ya kila mlingoti wa daladala, teksi, basi, lori, baiskeli, pikipiki na kadhalika. Wengine wakaigeuza skarf ya shingoni na hata kilemba cha kichwani. Barabaraa sherehe hiyo.

Nilisikitika na kusononeka nilipomuona dereva wa teksi anaikoshea gari na mama mpita njia kaikaushiya jasho la usoni. Bendera yetu hii hii. LA HAULLAH!!!

Hakika bado tunakwenda. Si mbali tutakapo ona bendera yetu hii tuipendayo na kuiheshimu imeshonwa chupi au sidiriya kama wafanyavyo wamarekani na waingereza. Muhimu kwa sasa ni elimu husika kwa umma. "A stitch in time saves nine." Tuwajibike wakati ni huu.

Mh. spika naomba iungwe mkono hoja.

Sioni ubaya kwa watu kuitumia bendera ya taifa kama ufahari wa nchi yao kwa matumizi uloyataja hapo juu. Sema yapo matumizi mengine ambayo yanaidhalilisha,lakini bendera kupepea kwenye daladala,teksi nk sio dhambi ni matumizi tu.Bendera ya taifa pia inayosemwa hapa sio zile rangi unazoziona. Kisheria inayoitwa bendera ya taifa na kuheshimiwa ni ile yenye upana na urefu maalumu,kitambaa maalumu,mpangilio wa rangi na inayotundikwa pale mlingotini.Hizo nyingine zinazochorwa au kudariziwa kwenye nguo ni bndera ndio lakini hazina uzito huo unaopaswa kisheria.Bendera ya taifa pamoja na ngao ya taifa vinalindwa na sheria rasmi ya bunge na sheria hiyo inataja yapi ni makosa yanayohusiana na bendera na ngao ya taifa.
 
---Matumizi ya bendera ya Taifa kwa nia ya kudharilisha ndiko naweza kupinga na kukemea kwa nguvu zote.

---Kuwa na bendera chafu kwenye mlingoti mbele ya ofisi ya chama au ubalozi ni dhihaki kwa Taifa. Bendera ya Taifa inatakiwa kuwa safi wakati wote.

---Bendera ya Taifa kutumika kutengenezea chupi siyo dhihaki. Unless kama mtu mwenye kuivaa ni mchafu, hivyo nguo zake za ndani pia ni chafu achilia mbali nguo za nje.

---Bendera ya Taifa kutumika kutengenezea chupi siyo dhihaki. Kwani matumizi ya chupi mengine yanatumika kwenye kuwakilisha Taifa kwenye mashindano ya kuogelea kwa wanaume na wanawake wanakuwa na zile 'swimming costumes.'

---Matumizi ya bendera ya Taifa kwenye magari ya uchafu siyo dhihaki. Magari ya uchafu ni ishara kuwa Taifa linajali usafi na liko mstari wa mbele kutumia magari kusaidia usafi huo. Hivyo magari hayo hata kama ni ya watu binafsi bado yanaonesha mshikamano.

---Matumizi ya bendera ya Taifa kuoshea gari ni dhihaka kubwa. Anayefanya hivyo akamatwe na kupewa somo kubwa ikiwezekana apewe adhabu za kijamii, kama vile kuzoa uchafu n.k.
 
Tanzania tumepata uhuru Mwaka 1961.

Mwalimu Nyerere alianza na mkakati mzuri sana wa Ujamaa na Kujitegemea.

Alianzisha kampeni ya Kufuta maadai watatu (Ujinga, Maradhi na Umasikini)ambao walikuwa ni Hatari kuendelea kuwepo nao.
Kwa kweli Baba wa Taifa alijitahidi na akafanikiwa kwa kiwango fulani. Kama Rais wa Nchi alionyesha mfano katika kukemea Ufisadi na mtu aliyepokea au Kutoa Rushwa aliadhibiwa vikali.
Si ukweli wajameni??

Kipindi Kile Mwalimu Nyerere alijua kuwa Watanzania wengi hawajaelimika hivyo hakuwa na papara katika kuchimba madini. Aliacha Watanzania tujiandae kwanza.

Uongozi uliofuatia ulianza kuboronga kidogo na hata hatimae wala rushwa wakakomaa hadi kuwa mafisadi.

Viongozi wakaaza kuvunja maadili ya uongozi waliojiwekea Enzi za TANU na ASP.
Ubinafsi ukaanza kutawala.

Jamani Hebu tujiulize Kati ya Tanzania na BOtswana Au NAmibia ni Nchi ipi ina Rasilimali nyingi (maliasili)?
JIBU unalo

Je ni Nchi zipi zimeendelea Botswana Au Tanzania?

Kwa nini?

Tunaweza Kuhalalisha umaskini wetu 'can we justisfy our poverty'

Tanzania tunategemea misaada sana, tunawanyenyekea wazungu sana mpaka inabidi wanaingilia mambo yetu ya ndani ya Nchi. Ina maana wana tawala kinamna fulani hivi. (Remote control)

KAMa vile Ukoloni mamboleo??

So bado tunatawaliwa, uhuru tuliopata ni wa Bendera tu.

Sasa Ndugu wana jamii forums, tujadili huu ukoloni na tutafute njia mbadala za kuondokana nao.

Kila mtu ajitahidi kutoa mawazo yake. Hii itakuwa mwanzo na Chachu ya kuleta mabadiliko na Hatimae tutatoa katika Umma kupitia magazeti yetu uwe mjadala wa Kitaifa.
 
Tukirejea katika alama mbalimbali za uhuru wa nchi yetu, Bendera ya taifa haiwezi kusahaulika. Lakini mimi binafsi sifahamu kitu kimoja kuhusu bendera yetu ya taifa, kwamba bendera hii ilipaswa iwe juu ya mlingoti masaa 24 bila kushushwa, lakini bendera yetu inashushwa saa 12.00 jioni na kupandishwa saa 12.00 asubuhi. Je uhuru wetu ni wa mchana tu na sio usiku? Kikubwa ninachopenda kujua ni kwa nini bendera yetu inashushwa tunapoelekea usiku ua nyakati za usiku.
 
Kuhusu ajenda ya Bendera mie nina ajenda nyingine kabisa.
nafikiria namna ya kuiwasilisha hapa jamvini.
 
Kwa nini bendera ya taifa inashushwa nyakati za jioni kuelekea usiku ili isipepee usiku kucha wakati ni mojawapo ya alama za uhuru wa taifa letu?
 
Serikari inalala usingizi! mhh nahisi ni ushamba tu maana toka enzi hizo wakati material ya bendera ilikua issue. Mbona wenzetu zinapiga 24 7
 
Ni taratibu tulizojiwekea na inapendeza sana ,kwani tunajivunia utamaduni wetu ,sio lazima wala hakuna ulazima wa kuiga kila kitu ,ni kiasi tu tunaonyesha tupo tofauti na wengine anaetaka anaweza kuiga kutoka kwetu sio kila kitu iwe tunaiga ,bata wa kizungu kuku wa kizungu embe la kizungu hayo yametosha.
 
Bendela inapopeperushwa lazima kuwe na mwanga wa kutosha ili wapita njia waione. Kama giza limeshaingia na kama hakuna taa, hakuna maana ya kuiacha gizani. Hata marekani ambako wanaruhusiwa kuipeperusha usiku, sheria inawataka wote wanaotaka kupeperusha bendera zao usiku kuhakikisha kuwa sehemu ilipo pana taa za kutosha na si kuiacha gizani.
 
Aaah, si unajua waswahili walivyo, giza likiingia ndo maovu yanachukua nafasi. Hawakawii kuiiba bendera, bora iendelee kushushwa jioni !!!
 
Waheshimiwa wana JF,

Nimepata kuona malumbano mengi kati ya police na raia, na mara nyingi kwa sababu ambazo si za msingi sana. Hata hivyo kwa jinsi nilivyo makini nilikuwa siamini kabisa kama ingetokea siku nikakorofishana na police.

Tarehe 05/03/2011 nilikuwa Mbeya, na ni mgeni. Jioni saa 12 hivi nilitoka nilipofikia na kushika njia inayotoka uhindini na kuelekea hospitali ya rufaa. Wakati natembea niliweka earphone za simu maskioni nikawa nasikiliza redio na wakati mwingine naongea na simu. Njiani magari yalikuwa ni mengi hivyo ilibidi niwe makini na barabara. Nilipokuwa nakunja kona ya kuelekea rufaa baada ya kupita fire, na police mtu moja alinisimamisha kwa ishara huku akinionesha kitu nyuma yangu.

Kugeuka nikawaona police wawili wapo ng'ambo ya barabara mbele ya kituo cha Police wameshikilia bendera mbele ya milingoti miwili. Na moja wa kike ambaye alikuwa ameshikilia bendera ya Taifa nikamuona kwenye uso kama anayetoa maneno ya kunifokea. Kuona hivyo nikatoa zile earphone masikioni haraka na nikaenda karibu na walipokuwa wamesimama. Na mambo yakawa kama ifuatavyo:

Police: Wewe ni jeuri sana siyo?

Mimi: Hapana, kwani kuna nini?

Police: Unajifanya hujui sivyo?

Mimi: Samahani sifahamu kilichotokea naomba nifahamiswe.

Police: Ahaa, unataka ufahamishwe? Yaani unataka tukufahamishe basi tutakufahamisha.

Mimi: Samahani mkuu kama ulivyoniona nilikuwa nimevaa hizi earphone tena magari ni mengi sifahamu ni wapi nilipokosea.

Police: Wewe umeshasema unataka ufahamishwe basi leo tutakufahamisha police ni nani, tutakupiga kwanza halafu tukuweke ndani, maana umetaka mwenyewe kufahamishwa.

Niliposikia hivyo hofu ikaanza kunipata na hasa kwakuwa mimi hapa Mbeya ni mgeni.

Yule askari akaendelea kunifokea mpaka povu linamtoka mdomoni na kuendelea kuniambia kuwa siku hiyo ningekiona. Katika kunifokea huko niligundua kuwa inaelekea wakati napita wao askari walikuwa wanashusha bendera na nadhani walipiga filimbi ambayo mimi sikuisikia kutokana na zile earphone masikioni pamoja na ule umakini niliokuwa nao wa kuangalia magari yanayopita yasije yakanigonga. Kwa hiyo kile kitendo cha mimi kuendelea na safari yangu ya miguu barabarani na wao wanashusha bendera ndicho kilichowakera.

Baada ya vitisho hivyo nikaona niendelee kuomba msamaha. (Mara nyingi nimeona police huwaweka watu ndani na wakati mwingine na kichapo juu na kisha kuwachia siku ya pili yake). Basi nikaendelea kuomba msamaha kama zuzu.

Mara yule police wa pili akasema niondoke pale niende zangu. Nikaondoka hata nikasahau kupitia Hosp. ya rufaa.

Swali kwa wana JF ambao wanafahamu sheria:
(1) Je utaratibu na lugha aliyoitumia huyo askari kunifahamisha kosa langu ni sahihi?
(2) Je mtu anayepita barabarani na bendera ya taifa inashushwa ng'ambo ya barabara avunja sheria?
(3) kama avunja sheria je wale wanaopita na gari na pikipiki kwanini sheria hii haiwahusu?
(4) Je askari ambaye kashika bendera ya taifa anaruhusiwa kumfokea mtu aliye barabarani?

Wa JF naomba mnifahamishe ili siku ingine niwe makini, lakini pia watanzania wengine wajifunze lisije likawapata, maana kama nisingeomba msamaha kama mjinga siku ile lazima ningeonja ndani.
 
POLE SANA,

Mimi siyo mwanasheria naamini wanasheria watakujibu kisheria zaidi,,,ila japo siyo mwanasheria lakin bado naona hao askari hawapaswi kukufokea bali kukuelezea kosa lako KAMA LIPO KWELI, manake iweje magari na pikipiki zisisimame wakati huo kama zifanyavyo kwenye misafara ya wakubwa pindi wapitapo?? ila wewe tu ung'ang'aniwe tena pamoja na lugha isiyo ya uelimishaji bali utishaji. Hata sijui lini polisi wataacha lugha zao za vitisho kwa raia......

MTU AKIVUNJA SHERI KABLA YA KUMUADHIBU NI VIZURI KUMWELIMISHA KWANZA......

POLE KWA YOTE, nami nawasubiri wanasheria watufafanulie hili kisheria zaidi....
 
Hii nimekuwa nikijiuliza hivi kwann huwa inashushwa Bendera ifikapo jioni ya saa kumi na mbili?na kupandishwa asubuhi?
au ndio kusema serikali inaenda kulala?....

Waswahili wanasema kuuliza si ujinga..nami nimeuliza tu?
 
Hii nimekuwa nikijiuliza hivi kwann huwa inashushwa Bendera ifikapo jioni ya saa kumi na mbili?na kupandishwa asubuhi?
au ndio kusema serikali inaenda kulala?....

Waswahili wanasema kuuliza si ujinga..nami nimeuliza tu?

ni ishara ya kuwa sheria na kanuni zinaisha kutumika officily.. mapka kesho saa kumi na mbli asubuhi... we huoni matukio mengi yanatokea usiku na hakuna la maana linafanyika... .. kwasababu hao wasimamia sheria wanakuwa wako off
 
Bendera ni alama ya Taifa huru, hivyo, kama nyara ya serikali huwezi kuiacha nje wakati watu wanarudi ndani!
MBONA huulizi kuhusu lile SIWA kwanini linaondolewa kama bunge halipo kwenye session?
 
Kwa wale wenye macho makali na upembuzi wa picha za TV na za mnato mtakuwa mmetupia macho maeneo maarufu mawili hapa nchini. La kwanza ni kwenye njia za ndani ya ukumbi wa Bunge toka milangoni kuja mpaka kwenye eneo la Spika. Hapa kuna zulia ambalo limetengenezwa makusudi kufuata rangi za bendera ya Tanzania kwenye fito zake.

Sehemu ya pili ni uwanja wa ndege wa JNIA (Dsm) wakati ambapo anakuja kiongozi wa nje kwenye ziara ya kitaifa. Hapo huwa linatandazwa zulia jekundu lenye fito za rangi za bendera ya taifa pembeni pia.

Ninavyoamini na kufahamu ni kwamba bendera ndiyo kitambulisho kikuu cha nchi yoyote duniani na kwa utaratibu wa kistaarabu haipaswi kugusa ardhi "deliberately, accidentally or permanently". Ndiyo maana hata wakati inashushwa huwa askari anayeishusha anahakikisha haivuki hata usawa wa magoti yake kuelekea ardhini.

Je, ni busara gani kama si dharau kuruhusu watu bila kujali wadhifa gani wanao kuikanyaga bendera ambayo ndiyo sura ya taifa aidha wanapoteremka kwenye ndege au wanapoingia na kutoka Bungeni?
 
Naona umejibiwa - Hata hivyo niongeze tu.

Watanzania tuliheshimu sana bendera na tukasahau utaifa. Enzi hizo ilikuwa ndra kukuta bendera ndogo au kubwa kwenye ofisi yoyote isipokuwa ya serikali. Watu wanapojivunia utaifa, huvaa alama za bendera ya taifa lao kama skafu, kitambaa kichwani na kushonea kwenye mashati nk. na hii haimaanishi dharau kwa namna yoyote ile.

Tunahitaji tujivunie utaifa wetu na kuutangaza.
 
Kuhusu Bungeni ngoja tumsubiri Mh. Tundu Lissu na Makinda watupatie ufafanuzi kuhusu jambo hili, nadhani wako humu JF watatujibu muda siyo mrefu. Kuhusu zulia kwenye uwanja wa ndege, ndiyo maana kuna rangi nyekundu hivyo mgeni hukanyaga wekundu.
 
Naona umejibiwa - Hata hivyo niongeze tu.

Watanzania tuliheshimu sana bendera na tukasahau utaifa. Enzi hizo ilikuwa ndra kukuta bendera ndogo au kubwa kwenye ofisi yoyote isipokuwa ya serikali. Watu wanapojivunia utaifa, huvaa alama za bendera ya taifa lao kama skafu, kitambaa kichwani na kushonea kwenye mashati nk. na hii haimaanishi dharau kwa namna yoyote ile.

Tunahitaji tujivunie utaifa wetu na kuutangaza.

Nakubaliana na wewe asilimia mia kutumia bendera kujivunia utaifa, lakini je, kuiweka ardhini na kuikanyaga ni heshima? Kuna mtu kasema zile ni rangi tu na si bendera yenyewe lakini nadhani hajaelewa context ya swali ambayo ni bendera kuwa chini kiasi cha kukanyagwa.
 
Back
Top Bottom