Ramadhani Madabida na wenzake waachiliwa huru, walituhumiwa kusambaza ARV feki

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,832
Leo Alhamisi Februari 24,2022 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano baada ya Serikali kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao likiwemo la kusambaza dawa bandia za kufubaza Virusi vya Ukimwi.

Soma=> Madabida na wenzake watano wafutiwa mashtaka ya kusambaza ARV feki, wakamatwa tena

Pia, soma=> Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

============

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano baada ya Serikali kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao likiwemo la kusambaza dawa bandia za kufubaza Virusi vya Ukimwi.

Madabida ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Ltd cha Dar es Salaam (TPI) na wenzake walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matano likiwemo ya kusambaza makopo 7,776 ya dawa bandia za kufubaza Virusi vya Ukimwi (ARV) aina ya Antiretroviral, wakijaribu kuonyesha kuwa dawa hizo zilikuwa halali na zimetengenezwa nchini.

Uamuzi huo wa kuwaachia huru umetolewa leo Alhamisi Februari 24, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya uamuzi kama washtakiwa wanakesi ya kujibu au laa.

Soma zaidi:Madabida wenzake waenda mahabusu

Mbali na Madabida, washtakiwa wengine ni Mkurugenzi wa Operesheni wa TPI, Seif Shamte, Meneja Masoko, Simon Msofe, Mhasibu Msaidizi, Fatma Shango pamoja na wafanyakazi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Sadick Materu na Evans Mwemezi.

Hakimu Shaidi amesema upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi 13 na vielelezo zaidi ya 10, lakini umeshindwa kudhibitisha mashtaka dhidi ya washtaka wote, hivyo amewaachia huru washtakiwa wote.
 
Hongera Madabida…hongera sana Zarina

Ilipaswa isomeke imemuachia huru Mfanyabiashara maarufu…

Ni sawa na ku report aliekuwa Mmiliki wa Ukumbi wa Muziki wa Katikati ya jiji wa Bilicanus afikiswa Mahakamani kwa tuhuma za ugaidi
 
Wahanga wa Mwendazake wote wanaachiwa. Hii inaonyesha kuwa kuna tatizo. Mwendazake pamoja na kujidai mpanga ufisadi na mafisadi miaka yote 6 hakufanikiwa kufunga mtu yeyote kwa ufisadi ingawa alifanikiwa sana kuwa funga wapinzani..... Hapo ndipo utaona ni jinsi gani alikuwa anatuchezea akili.
 
Hakuwa na lolote kipya yule zaidi ya kelele tu. Kujinasibu kote kupambana na ufisadi hajabadilisha hata sheria yenyewe ya kupambana na RUSHWA. Afu kuna wapuuzi wanamwita shujaa wa AFRICA ????
 
Leo Alhamisi Februari 24,2022 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano baada ya Serikali kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao likiwemo la kusambaza dawa bandia za kufubaza Virusi vya Ukimwi.

Soma=> Madabida na wenzake watano wafutiwa mashtaka ya kusambaza ARV feki, wakamatwa tena

Pia, soma=> Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

============

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano baada ya Serikali kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao likiwemo la kusambaza dawa bandia za kufubaza Virusi vya Ukimwi.

Madabida ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Ltd cha Dar es Salaam (TPI) na wenzake walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matano likiwemo ya kusambaza makopo 7,776 ya dawa bandia za kufubaza Virusi vya Ukimwi (ARV) aina ya Antiretroviral, wakijaribu kuonyesha kuwa dawa hizo zilikuwa halali na zimetengenezwa nchini.

Uamuzi huo wa kuwaachia huru umetolewa leo Alhamisi Februari 24, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya uamuzi kama washtakiwa wanakesi ya kujibu au laa.

Soma zaidi:Madabida wenzake waenda mahabusu

Mbali na Madabida, washtakiwa wengine ni Mkurugenzi wa Operesheni wa TPI, Seif Shamte, Meneja Masoko, Simon Msofe, Mhasibu Msaidizi, Fatma Shango pamoja na wafanyakazi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Sadick Materu na Evans Mwemezi.

Hakimu Shaidi amesema upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi 13 na vielelezo zaidi ya 10, lakini umeshindwa kudhibitisha mashtaka dhidi ya washtaka wote, hivyo amewaachia huru washtakiwa wote.

Kwa jinsi mambo yanavyojitokeza SHAMTE aliyehusishwa na mkonge kufilisika kule Tanga na akafia mahabusu, angekuwa yu hai naye angeachiwa huru!!
 
Wahanga wa Mwendazake wote wanaachiwa. Hii inaonyesha kuwa kuna tatizo. Mwendazake pamoja na kujidai mpanga ufisadi na mafisadi miaka yote 6 hakufanikiwa kufunga mtu yeyote kwa ufisadi ingawa alifanikiwa sana kuwa funga wapinzani..... Hapo ndipo utaona ni jinsi gani alikuwa anatuchezea akili.
Pale tulipigwa mkuu. Kelele nyingi zilikua na lengo la kuficha udhaifa. Aliposhindwa kuuficha akatumia mitutu.
 
Leo Alhamisi Februari 24,2022 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano baada ya Serikali kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao likiwemo la kusambaza dawa bandia za kufubaza Virusi vya Ukimwi.

Soma=> Madabida na wenzake watano wafutiwa mashtaka ya kusambaza ARV feki, wakamatwa tena

Pia, soma=> Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

============

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano baada ya Serikali kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao likiwemo la kusambaza dawa bandia za kufubaza Virusi vya Ukimwi.

Madabida ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Ltd cha Dar es Salaam (TPI) na wenzake walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matano likiwemo ya kusambaza makopo 7,776 ya dawa bandia za kufubaza Virusi vya Ukimwi (ARV) aina ya Antiretroviral, wakijaribu kuonyesha kuwa dawa hizo zilikuwa halali na zimetengenezwa nchini.

Uamuzi huo wa kuwaachia huru umetolewa leo Alhamisi Februari 24, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya uamuzi kama washtakiwa wanakesi ya kujibu au laa.

Soma zaidi:Madabida wenzake waenda mahabusu

Mbali na Madabida, washtakiwa wengine ni Mkurugenzi wa Operesheni wa TPI, Seif Shamte, Meneja Masoko, Simon Msofe, Mhasibu Msaidizi, Fatma Shango pamoja na wafanyakazi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Sadick Materu na Evans Mwemezi.

Hakimu Shaidi amesema upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi 13 na vielelezo zaidi ya 10, lakini umeshindwa kudhibitisha mashtaka dhidi ya washtaka wote, hivyo amewaachia huru washtakiwa wote.
Muuaji wa kusambaza dawa feki anaachwa huru huku mwenyekiti mbowe asiye na hatia anasoteshwa gerezani, ssh ana msukumo wa Udini katika maamuzi yake? Tutafakari
 
Wahanga wa Mwendazake wote wanaachiwa. Hii inaonyesha kuwa kuna tatizo. Mwendazake pamoja na kujidai mpanga ufisadi na mafisadi miaka yote 6 hakufanikiwa kufunga mtu yeyote kwa ufisadi ingawa alifanikiwa sana kuwa funga wapinzani..... Hapo ndipo utaona ni jinsi gani alikuwa anatuchezea akili.
Aliishia kumuadhibu aliyekua kamishna wa TRA na mzee wa VIP Engineering na singasinga wake kwa kosa la kuwa matajiri.
Lkn pia kuwavunjia nyumba watu ambao hawakua hata na Nia ya kugombea uwenyekiti wa mitaa kule Kimara.
Yeye aliona hayo ni mafanikio
 
Wahanga wa Mwendazake wote wanaachiwa. Hii inaonyesha kuwa kuna tatizo. Mwendazake pamoja na kujidai mpanga ufisadi na mafisadi miaka yote 6 hakufanikiwa kufunga mtu yeyote kwa ufisadi ingawa alifanikiwa sana kuwa funga wapinzani..... Hapo ndipo utaona ni jinsi gani alikuwa anatuchezea akili.
Hii kesi ni ya JK era.

Ilikua 2014.

Magu hahusiki kwa hili.
 
Hongera ya nini?
Hongera Madabida…hongera sana Zarina

Ilipaswa isomeke imemuachia huru Mfanyabiashara maarufu…

Nu sawa na ku report aliekuwa Mmiliki wa Ukumbi wa Muziki wa Katikati ya jiji wa Bilicanus afikiswa Mahakamani kwa tuhuma za ugaidi
 
Madabida ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Ltd cha Dar es Salaam (TPI) na wenzake walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matano likiwemo ya kusambaza makopo 7,776 ya dawa bandia za kufubaza Virusi vya Ukimwi (ARV) aina ya Antiretroviral, wakijaribu kuonyesha kuwa dawa hizo zilikuwa halali na zimetengenezwa nchini.
Kwahiyo wana haki kuishtaki serikali kwa kuwasingizia
 
Back
Top Bottom