benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kigoma imewaachia huru kwa masharti ya dhamana washtakiwa wa tano kati ya 11 waliokuwa wameshtakiwa kwa makosa 11 likiwemo la utakatishaji fedha Sh463.5 milioni, huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Igunga, Athumani Msabila na wenzake watano wakiendelea kusota mahabusu.
Katika kesi namba 3 ya mwaka 2023 iliyofikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Novemba 7, 2023 na washtakiwa kusomewa mashtaka hayo yakiwemo kula njama kwa nia ya kutenda kosa, kugushi nyaraka, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh463.5 ambapo hawakutakiwa kujibu chochote.
Akisoma uamuzi huo leo Jumatatu Novemba 20, 2023; Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, Hassan Momba amesema Mahakama imejiridhisha kuwa, mashtaka walionayo hayana pingamizi kisheria kupata dhamana.
Walioachiwa huru kwa dhamana ni mshtakiwa namba saba, Joel Shirima, Jema Mbilinyi mshtakiwa namba nane, Kombe Kabichi mshtakiwa namba tisa, Frank Nguvumali mshtakiwa namba 10 wote kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na Bayaga Ntamasambilo mstakiwa namba 11 kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.