Rufaa ya DPP kupinga kuachiwa huru kwa Sabaya na wenzake kusikilizwa leo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,707
218,255
Rufaa ya DPP dhidi ya Ole Sabaya , ya kupinga kuachiwa huru inaanza kusikilizwa leo .

Mitaani huwa tunasema hivi , " HAIJAISHA MPAKA IISHE "

---
Mahakama ya Rufani leo Novemba mosi, 2023 imepanga kusikiliza rufaa ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, (DPP) dhidi ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili.

Katika rufaa hiyo Jamhuri inapinga hukumu ya Mei 8, 2022 iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, iliyomuachia huru Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura baada ya mahakama hiyo kubaini kulikuwa na upungufu katika mwenendo wa kesi hiyo, ikiwepo hali ya kutofautiana kwa ushahidi.

Rufaa hiyo namba 231/2022 itasikilizwa na jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Jacobs Mwambegele, Ignas Kitusi na Leila Mgonya.

Leo Sabaya ameingia mahakamani hapo akiwa na mke wake ambapo baada ya kuwasili mahakamani hapo majira ya saa tatu kasoro, alipokelewa na baadhi ya ndugu na jamaa waliokuwa wamekusanyika nje ya mahakama hiyo kwa ajili ya kufuatilia kesi hiyo.

Baada ya kuingia mahakamani hapo ambapo kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa saa tatu asubuhi ila mmoja wa majaji hao ameeleza kuwa wanaanza na kesi za madai kisha kesi hiyo itasikilizwa ya mwisho kwa kuwa itasikilizwa muda mrefu.

Awali Sabaya na wenzake walikata rufaa kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Oktoba 15, 2021 katika kesi hiyo ya jinai namba 105/2021.

Hukumu anayoipinga DPP ilitolewa Mei 6, 2022 na Jaji Sedekia Kisanya wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma ambaye alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuona kulikuwa na mkanganyiko kwenye mwenendo wa usikilizwaji wa shauri kwenye mahakama ya haki mkazi Arusha.
 
Ajabu sana, wale waliomuachia huru ndio wanaotaka kumkamata tena, kwani ilikuwaje wakamuachia mwanzo? ground za kukata rufaa zilikuwa wazi kila mtu anaziona, lakini wakaamua kunyamaza mpaka walipoona reaction toka kwa jamii ambayo haikuridhishwa na ule uamuzi wa kumuachia huru Sabaya..

Leo wanamrudisha mahakamani kwa style ya funika kombe mwanaharamu apite, wanasubiri mambo yakitulia waache kumsumbua, hapa najiandaa na siku nitakayoona Sabaya akilamba teuzi, lakini siamini kama anaweza kurudishwa gerezani tena.
 
Ngoja tuone
 
Swaga tu hizo...
Ataachiwa huru!
NB: ashauza ardhi, atamwaga hela anunue uhuru wake!
 
Wasted of times and other resources kama makonda aliyefanya unyama uliopitiliza mpaka Wamarekani wanamwona kwa jicho la mwewe wakamfungia amerudishwa ccm hawana aibu ni kama ukoo wa panya wote wezi tuu
 
Mahakama ya Rufani leo Novemba mosi, 2023 imepanga kusikiliza rufaa ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, (DPP) dhidi ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili.

Katika rufaa hiyo Jamhuri inapinga hukumu ya Mei 8, 2022 iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, iliyomuachia huru Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura baada ya mahakama hiyo kubaini kulikuwa na upungufu katika mwenendo wa kesi hiyo, ikiwepo hali ya kutofautiana kwa ushahidi.

Rufaa hiyo namba 231/2022 itasikilizwa na jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Jacobs Mwambegele, Ignas Kitusi na Leila Mgonya.

Leo Sabaya ameingia mahakamani hapo akiwa na mke wake ambapo baada ya kuwasili mahakamani hapo majira ya saa tatu kasoro, alipokelewa na baadhi ya ndugu na jamaa waliokuwa wamekusanyika nje ya mahakama hiyo kwa ajili ya kufuatilia kesi hiyo.

Baada ya kuingia mahakamani hapo ambapo kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa saa tatu asubuhi ila mmoja wa majaji hao ameeleza kuwa wanaanza na kesi za madai kisha kesi hiyo itasikilizwa ya mwisho kwa kuwa itasikilizwa muda mrefu.

Awali Sabaya na wenzake walikata rufaa kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Oktoba 15, 2021 katika kesi hiyo ya jinai namba 105/2021.

Hukumu anayoipinga DPP ilitolewa Mei 6, 2022 na Jaji Sedekia Kisanya wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma ambaye alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuona kulikuwa na mkanganyiko kwenye mwenendo wa usikilizwaji wa shauri kwenye mahakama ya haki mkazi Arusha.
 
Rufaa ya DPP dhidi ya Ole Sabaya , ya kupinga kuachiwa huru inaanza kusikilizwa leo .

Mitaani huwa tunasema hivi , " HAIJAISHA MPAKA IISHE "

---
Mahakama ya Rufani leo Novemba mosi, 2023 imepanga kusikiliza rufaa ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, (DPP) dhidi ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili.

Katika rufaa hiyo Jamhuri inapinga hukumu ya Mei 8, 2022 iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, iliyomuachia huru Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura baada ya mahakama hiyo kubaini kulikuwa na upungufu katika mwenendo wa kesi hiyo, ikiwepo hali ya kutofautiana kwa ushahidi.

Rufaa hiyo namba 231/2022 itasikilizwa na jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Jacobs Mwambegele, Ignas Kitusi na Leila Mgonya.

Leo Sabaya ameingia mahakamani hapo akiwa na mke wake ambapo baada ya kuwasili mahakamani hapo majira ya saa tatu kasoro, alipokelewa na baadhi ya ndugu na jamaa waliokuwa wamekusanyika nje ya mahakama hiyo kwa ajili ya kufuatilia kesi hiyo.

Baada ya kuingia mahakamani hapo ambapo kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa saa tatu asubuhi ila mmoja wa majaji hao ameeleza kuwa wanaanza na kesi za madai kisha kesi hiyo itasikilizwa ya mwisho kwa kuwa itasikilizwa muda mrefu.

Awali Sabaya na wenzake walikata rufaa kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Oktoba 15, 2021 katika kesi hiyo ya jinai namba 105/2021.

Hukumu anayoipinga DPP ilitolewa Mei 6, 2022 na Jaji Sedekia Kisanya wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma ambaye alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuona kulikuwa na mkanganyiko kwenye mwenendo wa usikilizwaji wa shauri kwenye mahakama ya haki mkazi Arusha.
Ibrahim Juma atakuwa kesha penyeza mkono wake, hakuna kitu hapo
 
Back
Top Bottom