Ukweli unauma!! Ni kweli vyombo vyetu vya habari havina wabunifu wa kujadili hoja, nilitegemea waandishi wetu wangekuwa wanatoa somo zaidi katika inshu nyingi kuelimisha jamii badala yake karibia waandishi wote wanaegemea kwenye kuripoti habari kutoka kwa wanasiasa zaidi. Vyombo vya habari vijifunze namna ya kujenga hoja zikakubalika kwenye jamii badala ya kukimbilia/kutegemea wanasiasa na watu wengine waropoke ndiyo wapate habari za kuandika.
Mkuu uko sahihi kabisa, waandishi wetu wanasubiri habari ya kuambiwa na mtu tu. Hawawezi kufanya uchambuzi, mimi kwa sasa huwa sinunui magazeti kwa kuwa kinachoandikwa ni ushabiki zaidi bila utafiti.