Rais wa Malawi Awananga Waandishi wa Habari wa Tanzania

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
President Joyce Banda Sunday commended journalists in the country for their professional reporting on the wrangle between Malawi and Tanzania over Lake Malawi.


The President made the commendation in Lilongwe the during press conference soon after her arrival from Mozambique saying if journalists in the country reported in the same way their counterparts in Tanzania were doing, the two countries could have been involved in a war.


“Thank you so much for articulating this story with sober minds,” President Banda said amidst applause from party supporters.

Source: Nyasa Times


My Take: Waandishi wa habari wa Tanzania wanaandika yale yanayosemwa na wanasiasa kuhusu suala la mpaka.
 
Ukweli unauma!! Ni kweli vyombo vyetu vya habari havina wabunifu wa kujadili hoja, nilitegemea waandishi wetu wangekuwa wanatoa somo zaidi katika inshu nyingi kuelimisha jamii badala yake karibia waandishi wote wanaegemea kwenye kuripoti habari kutoka kwa wanasiasa zaidi. Vyombo vya habari vijifunze namna ya kujenga hoja zikakubalika kwenye jamii badala ya kukimbilia/kutegemea wanasiasa na watu wengine waropoke ndiyo wapate habari za kuandika.
 
Joyce anatapa tapa alikuwa anapima kina cha maji amegundua kina marefu...sisi watanzania tutatofautiana kwenye yote lakini kuimega na kuhamisha ardhi yetu wote tunaungana kama anabisha alete chokochoko tena na kauli za tata za serikali yake.
 
ushalow na kutokuzingatia weledi wa kazi yao ni sifa ya waandishi makajanja wa tanzania ambao hata wanakosomea hapajulikani ndio mana hata Mkapa enzi zake akawa anawakwepa,upuuzi wao unajulikana kila mahali,ndo mana wamebaki kujiandalia tuzo wenyewe coz viwango vyao ni duni kushindanishwa na wa nchi zingine,shame on them
 
uyu bibie wa malawi si alikana kabisa CCTV channel,kwamba hajasema ziwa lote la kwao na watakaa chini na jk wayaongee
 
Huyu ni rais wa pili kutamka ubovu waandishi wa Tanzania. Wa Kwanza alikuwa ni Rais Benjamin ambaye November 24, 2001 alitamka kwamba waandishi wa Tanzania wanatakiwa kuacha uvivu wa kutafiti.

Iliwauma hadi leo wanaikumbuka baadhi ya waandishi.
 
anataka kuwasema akina nani sasa ...kama yule wa kipindi cha DAKIKA 45???
 
Ukweli unauma!! Ni kweli vyombo vyetu vya habari havina wabunifu wa kujadili hoja, nilitegemea waandishi wetu wangekuwa wanatoa somo zaidi katika inshu nyingi kuelimisha jamii badala yake karibia waandishi wote wanaegemea kwenye kuripoti habari kutoka kwa wanasiasa zaidi. Vyombo vya habari vijifunze namna ya kujenga hoja zikakubalika kwenye jamii badala ya kukimbilia/kutegemea wanasiasa na watu wengine waropoke ndiyo wapate habari za kuandika.

Wanasiasa wenyewe wanao wasikiliza ni akina Lusinde na Wassira, unategemea watapata habari za namna gani?
 
Alichokoza akajua tutakimbilia mahakama ya kimataifa akashangaa watu wanajipanga kwa vita!!hawataki story akaona heee hawa vipi mbona hawaendi mahakamani??

Bila shaka tabia ya kukimbilia mahakamani kwenye kila mgogoro wa serikali na wananchi Banda akadhani na hili jamaa ataenda mahakamani. Pamoja na kuwa vita ni mbaya, kwenye hili ni muhimu watanzania tukawa wamoja. Siamini kama opposition parties wanaangalia tu madaraka bali wanauchungu na nchi yao pia. Utani anaouleta mkuu wa kaya kwa kutugawa kwa mtazamo wa itikadi za kisiasa kwenye mgogoro huu ni vema tukaukataa kwa sasa.
 
Huyo mhalalisha ushoga mbona vyombo vya kwao pia vilikuwa vikiegemea upande mmoja tu kwamba ziwa lote 100% ni lao je huo si uchochezi?
nimefuatilia sana matamko yake ya kila siku, nimegundua huyu mwanamke hana msimamo (kiherehere)... anyway ni matatizo ya wanawake
 
MMMHHH! JE NI KWELI? Hakuna cha kujikosha kwa waandishi wa nchini mwake. Ukweli waandishi wote wa pande zote waliandika kutegemea na upande walipo. Kilichotokea kwa upande wetu ni kwa matamko yaliyotolewa na viongozi wa serikali MEMBE, SITA NA LOWASA kuandikwa na kuelezwa bayana. Turudi nyuma sisi waTZ mara nyingi tunajizadharau na kutukuzawengine. Naamini hawa viongozi wasingetoa matamko na waandishi wasingeyaandika INGEKULA KWETU ZIWA LOTE LINGEENDA.
Yaani hii inanikumbusha mechi za timu za Tanzania na za Waarabu hasa Misri & Ethiopia. Wakija kucheza kwetu polisi inawalinda na wananchi wanatishwa na kuogopeshwa japo wanacheza kibabe wasifanywe chochote, Timu zetu zikienda kwao ni ubabeubabe tu kuanzia mapokezi na hata kwenye mchezo wenyewe na hakuna vikosi vyao vyovyote vya ulinzi vinavyojali na kufungwa Tunafungwa. Tukisharudi nchini tunaanza kulalamika na kulialia tumeonewa, tutambue DUNIA HAINA HURUMA wakati mwingine usipo kuwa mbabe watu watakuchokonoa Machoni.
 
Huyo mhalalisha ushoga mbona vyombo vya kwao pia vilikuwa vikiegemea upande mmoja tu kwamba ziwa lote 100% ni lao je huo si uchochezi?

wamalawi wasipoangalia huyu mama atawapoteza ni kama mtu anayetafuta umaarufu/sifa kwa njia yoyote. Wote humu tuliona habari za mgogoro kupitia media za malawi na jinsi walivyoweka ushabiki wa kuingia vitani. Leo hii anataka kugeuza yale magazeti ya malawi yaliandikwa na watanzania. Angalie umakini wake sasa..
 
huyu si aliambiwa na mkuu wa nchi kuwa waliotangaza vita ni wapinzani sasa haya ya waandishi wa habari yametoka wapi tena?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom