Atawasaidia nini WaZambia kwa UMRI ule? Mpeni Mzee Malecela Urais mwaka 2015.
Mbunge wa mmd jimbo la Chongwe katika Lusaka province huko Zambia amejiuzulu. Akitoa sababu za kujiuzulu, alisema wananchi wa Chongwe hawamtaki. Alipoulizwa alishindaje ikiwa wapiga kura wake hawamtaki, alijibu kwamba hata yeye mwenyewe hajui.
Ukweli wa mambo ni kwamba Rais aliyeng'olewa madarakani Banda alikuwa amemhakikishia mgombea wa chama cha Sata ambae ni mwanamke Silvia Masebo kuwa hatapewa jimbo kwa namna yoyote ile. Hii ni kwa sababu mwanamke huyu alikuwa amekihama chama cha MMD na kujiunga na upinzani, huku akiwa ni waziri katika serikali ya Banda. Zambia ni nchi ya kikristo na raia wake ni watu wanaopenda haki, hivyo imepelekea yule aliyetangazwa mshindi bila kushinda katika sanduku la kura kuukataa huo ubunge, na badala yake amedai anataka kuishi na familia yake kwa furaha na amani.
.
Uko sahihi Mkuu!. Mara zote huwa ninajiuliza kwa nini TZ (mfano tu miongoni mwa nchi za Afrika) na umasikini wake inakuwa na mawazir 60 wakati nchi zilizoendelea daima hawazidi 20. Sababu ni hizo: ukanda, ukabila, undugu, urafiki, ulipaji fadhila n.k.Wakitaka kuchagua mawaziri ramani ya tanzania lazima iwepo the reason is kila mkoa utoe angalau waziri au naibu, kigezo kimekua maeneo ya kiutawala mikoa na wilaya kuliko uwezo wa mtu. Ndio maana miaka 50 baada ya uhuru nchi afadhali ya jana
TANZANIA INAELEKEA WAPI!!!!!!
Hapo mmekutana wote wadini. Wewe pamoja na yule unayemkosoa mko kapu moja.
Ni mfano wa kuigwa.
Mr. Guy Scott ameula..
Color is not an issue so long is living on leadership ethics!
Miaka hamsini baada ya kuwafukuza kwa mbwembwe leo hii tunawarudisha kwa mbwembwe tena!! Ama kweli hii ndio Africa. Tumepitia Ukoloni Mkongwe, Ubeberu, Uhuru wa Bendera, Ukoloni Mamboleo na sasa tunarudi kwenye ukoloni mkongwe wa kutawaliwa na wazungu. Ina maana Waafrica tumeshindwa kabisa kujitawala kabisa kabisa!!