Rais Sata wa Zambia ateua Baraza la Mawaziri.

JK nawe jitose basi? Kwa mfano ukaamua kama huyu Mbunge kwani itakuwaje? Jaribu bana
 
Je mtu mweusi anaweza kuwa makamu wa rais au rais usa au wazir mkuu uk,kwa vile tu amezaliwa huko?don't tell me about obama(half cast)mi naungana na bob mugabe kwamba africa ni bara la mtu mweusi hao jamaa wana kwao.kwetu ni kwao kwa nini?(kandoro saadan)
Kama Africa ni bara la weusi mbona babu yako Mugabe anamuunga mkono Gaddafi, kwani hajui kuwa Gaddafi sio mweusi? Mbona anamuunga mkono Bashir badala ya waasi wa Darfur ambao ni weusi kuliko hata yeye na wewe, au hajui kuwa bashiri ni mwarabu?
 
Miaka hamsini baada ya kuwafukuza kwa mbwembwe leo hii tunawarudisha kwa mbwembwe tena!! Ama kweli hii ndio Africa. Tumepitia Ukoloni Mkongwe, Ubeberu, Uhuru wa Bendera, Ukoloni Mamboleo na sasa tunarudi kwenye ukoloni mkongwe wa kutawaliwa na wazungu. Ina maana Waafrica tumeshindwa kabisa kujitawala kabisa kabisa!!

Nani amekwambia uhuru maana yake ni kuwafukuza watu weupe? Nani kasema ukoloni ni kuongozwa na mtu mweupe. Maana ya ukoloni ni kuongozwa bila kukubali kuongozwa i.e kuongozwa bila kufuata katiba iliyoandikwa na wananchi. kwahiyo Tanzania hatujawahi kupata uhuru maana hakuna katiba tuliyoiandika sie zaidi ya ile waliyoandika wakoloni weupe bila idhini yetu halafu wakoloni weusi wakawafukuza wakoloni weupe na kuendelea kututawala kikoloni mpaka leo. Tukiandika katiba yetu ndo tutakuwa tumepata uhuru.
 
Kati ya mimi na wewe kwa huo mtizamo nani anaonekana kilaza?
Unamaanisha kuwa Zambia nzima hamna mtu anayeweza kudeliver zaidi ya huyu mzungu?
Nyie ndio watu msiojiamini, mnawahusudu wazungu, mnaona wao ni kila ktu

Wee ndo kilaza. kwani mzambia maana yake nini. Mtu yeyote raia wa zambia ana haki ya kuongoza, na kama unaangalia mtu mwenye asili ya zambia huwezi kumpata kama ambavyo huwezi kupata mtu mwenye asili ya Tanzania kila kabila asili yake ni nje ya Tanzania.
 
hapo kwenye red ni 'shubiri' kuliongelea hapa TZ lakini ina kaulweli fulani. Mambo ya "Ideology" yana mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii yoyote unless kuamua kuishi kama (mfano) China ni bora

Acha kuendekeza udini wako wewe...ingekuwa ideology ya kikristo matters kibaki (kenya) angesubiri wafe watu 1000 nfio akasuluhishwe na JK.oops
 
As long as ni mzambia hata akiwa na colour gani haijalishi huo ndio msimamo utakaobaki duniani sasa...issue za colour zinazidi kwisha na muungiliano unazidi kuwa mkubwa katika kila taifa..
 
Badala ya kuzungumzia vipi rais mstaafu alivyo ondoka madarakani kwa amani na kumtakia rais mpya na serikali yake mafanikio na kuahidi watashirikiana kwa manufaa ya nchi. Sisi tunajadili kwa nini mzambia ambae si mweusi kachaguliwa katika serikali mpya, jampo mtu huyu naonekana ana kisomo na uzoefu mkubwa amayo Zambia itafaidika. Tuache ubaguzi usio na maana.
 
mhe MAKONGORO MAHANGA unasikia hiyoooooooooo

Siyo MAKONGORO tu mkuu!

Wako wengi sana waliochakachua na bado wameng'ang'ania!

Pale Shinyanga kuna jamaa anaitwa MASELE ameng'ang'ania kama Ruba. Sasa hivi anaishi kwa shida sana pale mjini hata kwenda kukojoa lazima asindikizwe na Polisi.

Mwaka huu Zambia imeamua kutoa somo kwa waafrika, yaani kila maamuzi wanayochukua yana fundisho kwetu. Naona huyu Cobra ndo anastahili kuitwa chaguo la MUNGU kwenye hiyo nafasi siyo huyu Mtalii wa kwetu na mwenzake mzee wa Kulialia!

MUNGU awasaidie Wa-Zambia maana wamedhamiria!
 
Zambia's newly elected President Michael Sata has dismissed the head of the country's anti-corruption watchdog.

A presidential statement said Godfrey Kayukwa would be replaced by Rosewin Wandi, without giving further details.

Mr Kayukwa is considered to be a close aide to former President Rupiah Banda, who lost last month's tightly-contested elections to Mr Sata.

During the campaign, Mr Sata pledged to stem out corruption among government officials. And during the swearing-in
ceremony last week he said: "Corruption has been a scourge in this country and there is a wide link between corruption and poverty."

The previous government was criticised for not being tough on tackling graft.

Source: BBC
 
huyu ndo prezida..hivi hatuweI tukamchukuwa kwa secondment aje tz hata 6 months hivi
 
MZEE SATA USIJE UKAMDHALILISHA HUYO 'DR HOSEA' WAKO AKASHINDWA KAZI:
TAFADHALI JITOFAUTISHE NA WINGI WA MARAIS WA BARA HILI KWA KUMUIGA KAMANDA PAULO KAGAME

Jamani; this guy seem to have made himself a MOST DEFINING programme siku nyingi hata kabla hajachaguliwa kuwa rais na kwa kule kutafuta urais kulikua tu ni jambo la pili katika harakati zake.

Kuna kila dalili kwamba Mzee Paulo Kagame, mzee wa kushindia kikombe cha chai ya rangi tu huku akichapa kazi yenye TIJA kwa taifa la, anaelekea kumpata mwenzake mwenye KUUMWA NA UMASIKINI wa taifa lake kwa jina la Mikaeli Sata.

Sasa naanza kuelewa kwa nini Satta amewakonga sana nyo Wa-Matumbi wenzangu nami nikiwemo. Ni kutokana na ukweli kwamba kwetu Bongo watu hutafuta URAIS kwanza tena kwa udi na uvumba, halafu baadaye ndipo anapoanza kufanya WINDOW SHOPPING kwa watu kama Tambwe Hiza, Yussuf Makamba na kuwakimbia akina Prof Mkandala, Baregu, Lipumba ...

... hala mwisho wa siku tunajikuta mbele hakuendeki nyuma hakurudiki kama hivi sasa ambapo kama taifa TUPO TUPO KWANZA kwa kipindi kisichojulika.

Mzee Sata, kwa kuwa huyo 'Dr Hosea' wa Zambia umemteua mwenyewe kwa malengo maalum ya kutokomeza UFISADI katika taifa lenu, sasa usije ukamdhalilisha kwa kumbana asifanye kazi yake ipasavyo.

Sote tunakagua kila unapotoa unyayo wako kwa sababu siku zote tunamini safari ya mbali kuwa salama au la hutambulishwa namwelekeo wa guu la kwanza. Kwako wewe mpaka hapo umefaulu sana mtihani.

Big Up Uncle Sata, mpaka hivi sasa kidogo nimeanza kuwa muumini wa aina ya Mtiririko wa Fikra zilizokufnya ujihisi unao mchango wa kutumikia wananchi wako. Naona kama vile Balozi wako atakua na kazi laini sana hapa maana hana haja tena kutueleza ya kwamba wewe ni mwanamageuzi kiasi gani.

Kusema kweli, barani Afrika tunao Marais (52) wengi sana lakini wale waliokwisha kutambua 'KITU GANI WAKAKIFANYIE' mataifa yao ili maisha yawe mazuri zaidi ni wachache mnoooo; hao ni pamoja na Kamanda Paul Kagame wa Rwanda, Rais wa Botswana kama walivyoasisiwa na Mzee Masire, na hivi sasa japo kwambaaaali sana, jinsi anavyowafanyia Wa-Kongo yule kijana wetu wa Mbezi hapa Bongo.

Mbali na hao, marais wengine wooote ndio vyanzo nya umasikini Barani kwetu kwa kwa kuendekeza mtazamo wa 'KITU GANI LAKE LIKAMFANYIE YEYE' kwa kuwa keshavishwa joho la Bwana Mkubwa.

Bure kabisa, hamna kitu kwa hao wengine - kila siku kupora kila kitu hadi mbegu ya kustahili kupandia msimu unaofuatia.
 
Mkuu umeweza kunifanya nifikirie na kutafakari juu ya Taifa langu Tanzania ... Tutoke vip?
 
Rais Michael Sata wa Zambia, amewafukuza kazi mara moja wakuu wote wa wilaya 72.

Akitoa tangazo la kuwafukuza kazi amesema sii vema kuwa na wakuu hao wanaoteuliwa kisiasa na badala yake ameamuru ofisi zao kushikiliwa na civil servant.

Ameongeza kuwa kutakuwa na mfumo utakaokuwa ukiwaingiza hao wafanyakazi wa serikali katika ofisi hizo na kwamba chama chochote cha siasa kitafanya kazi nao maana watakuwa sii wanasisa wala kuteuliwa kisiasa.

Source: ZNBC news
 
Good news!tanzania ma RC na DC WOTE MAKADA WA CCM!wanaongeza gharama tuu za uendeshaji serikalini .hapo ndipo tunaona umuhimu wa majimbo.jamani zambia itakua ulaya muda si mrefu sata kajipanga
 
Back
Top Bottom