Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,668
- 10,092
Ndugu zangu Hali ya mafuta inazidi Kuendelea kuleta matumaini kwetu watanzania kwa kushuka Bei, Ikumbukwe kuwa miezi michache iliyopita Bei ya mafuta petrol,Dizel na mafuta ya Taa ilikuwa haishikiki Wala haikamatiki, Hali hii ilipelekea kupanda kwa bidhàa nyingi Sana hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa mafuta ndio injini ya uchumi wetu, Ndio moyo wa uchumi wetu, Ndio mboni ya shughuli nyingi za kiuchumi hasa za usafirishaji wa bidhàa kuelekea maeneo mbalimbali hapa nchini.
Jambo hili lili ilazimu serikali Ya mama yetu Mpendwa mama Samia kutoa kiasi Cha billioni moja kila mwezi Kama Ruzuku ili kupunguza makali ya Bei iliyokuwa imetokana na kupanda katika soko la Dunia,hali iliyotokana na Vita ya Ukrein, serikali ilifanikiwa katika Jambo hili ukilinganisha na majirani zetu ambao wananchi wao walipitia katika bonde la Moto na maumivu ya mfumuko wa Bei ya nishati hii adhimu na muhimu.
Sasa serikali yetu imetangaza Bei mpya zinazoonyesha kushuka kwa Bei za mafuta, Ni dhahiri Sasa mfumuko wa Bei unakwenda kupungua, Nauli zinakwenda kupungua, Bei za usafirishaji wa mizigo zinakwenda kushuka, watu Kama bodaboda ,waendesha bajaji,mafuta, magari na vyombo vyote vya Moto vinavyotumika kwa biashara ya usafirishaji wataanza kuiona faida sasa.
Rai yangu kwa serikali yangu ni kuwa Naiomba ipitie Tena ukokotoaji wa viwango vya Nauli ili kushuka kwa Bei ya mafuta kutuguse wananchi wa kipato Cha chini, tunataka kuona Nauli zinashuka, lazima wamiliki wa vyombo vya Moto wataarifiwe na kupewa miongozo ya kupunguza Bei za Nauli na watimize wajibu wao wa kushusha Bei Kama walivyopandisha, watanzania Tunaitegemea serikali yetu kutusaidia na kutusemea katika hili maana yenyewe ndio sauti na nguvu yetu watanzania na mtetezi wetu wanyonge
Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia Watanzania wanyonge kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.