Serikali ya Rais Samia ni sikivu na inaendelea kusikia maoni ya Watanzania juu ya bei za mafuta na hali ya mafuta nchini

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,264
9,715
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeendelea kuzisikia Sauti za watanzania kupitia mitandao ya kijamii, kuona hali halisi katika vituo vya mafuta vilivyo karibu na mtaani kwangu. Nimeendelea kufanya utafiti wa karibu na uchunguzi wa hali ya upatikanaji wa mafuta katika vituo mbalimbali na nimeona kinachoendelea.Nimeona hali ya Bei na maoni ya watu, Nimesikia kauli za wamiliki wa vyombo vya moto na imani yao na maombi yao kwa serikali yao juu ya nini kingefanyika kuwasaidia kushuka kwa Bei hii.

Nachopenda kusema na ambacho nimewajibu baadhi yao mitaani ni kuwa serikali ya Rais Samia ni Sikivu sana na inasikia na kuona kila kitu kinachoendelea mitaani,inatambua usumbufu ambao watanzania wamekuwa wakiupata wa upatikanaji wa mafuta kila mwishoni kwa Mwezi, serikali yao inatambua changamoto wanayoipata wananchi hasa wa pembezoni na maumivu makali ya bei pale nishati hii inapokuwa Adimu.

Nimewaambia kuwa Serikali inafahamu ya kuwa mafuta ndio moyo wa uchumi wetu,ndio mboni yenyewe. Kwamba Mafuta yakipatikana kwa kusua sua au kwa Bei ya ulanguzi au Bei kubwa ina athari kubwa sana katika uchumi wetu,kwa kuwa hali hiyo ni lazima ipelekee mfumuko wa Bei kwa Bidhaa nyingi, kupanda kwa nauli kwa vyombo vyote vya usafirishaji na gharama nyingine nyingi lazima ziongezeka. Hali hii ni lazima ilete maumivu kwa mwananchi wa kipato cha chini,ni lazima imtoe jasho ,ni lazima impe suruba ,ni lazima iwe chungu kwa mtanzania mwenye kuhangaika kutwa nzima kupata mia mia.

Nimewaambia ya kuwa kwa kutambua haya na mengine mengi ndio maana mwaka jana serikali yetu iliamua kuchukua uamuzi na hatua za makusudi kabisa na wa kijasiri wa kuamua kutoa Ruzuku ya Billion mia moja kila mwezi katika mafuta ili kupunguza makali ya Bei.Nikawaambia ya kuwa hata Bungeni kupitia waziri wa fedha mh Dr Mwigulu nchemba iliahidi kuwa ikitokea mafuta yamepanda sana Bei Basi mama yetu Rais Samia atatoa fedha kwa ajili ya Ruzuku katika mafuta.

Hivyo watanzania wenzangu naombeni tuendelee kuwa watulivu na tuamini ya kuwa serikali yetu ni Sikivu na inaona kila kitu kinachoendelea. Sisi ndio wenye nchi sisi ndio waajiri wa serikali ndio maana serikali ya Rais samia imekuwa Sikivu na nyenyekevu sana kwetu watanzania.Tuendelee kuwa na imani na Rais wetu na Tuendelee kumwamini. Hawezi akatutelekeza au akatuacha tuteseke,tuhangaike,tuumie,Tulie machozi pasipo kutusaidia,kutushika mkono,kututua mzigo, kutupatia faraja, matumaini na kutufuta machozi .

Rais samia ni mwenye Huruma na upendo kwetu watanzania,anatambua vipato vyetu,anatambua uchumi na kipato cha kaya moja moja. Anajuwa hatuwezi kuhimili bei kubwa ya mafuta,anajuwa hatuwezi tukahimili bei kubwa za bidhaa,anajuwa ni lazima tutaishi kwa unyonge, taabu na shida kubwa sana asipotusaidia na kutushika mkono. Anajuwa maisha yetu ni ya aina gani na yanahitaji nini kumuinua kila mmoja wetu.

Rais wetu kama kiongozi,mama na mlezi wa Taifa letu ana uchungu mkubwa sana na watanzania.ana uchungu na Taifa letu,ana kiu ya kutaka kuona wananchi wanakuwa wenye furaha , Tabasamu na matumaini makubwa wakati wote.Asingependa kuona tu wanyonge na wapweke ndani ya Taifa letu. Ndio maana wakati wote anataka serikali yake iwe mikononi mwa wananchi na wakati wote iwasikilize watu wanataka na wanaumizwa na nini.

kwa sasa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania amesikia kilio cha watanzania na atakifanyia kazi na kuchukua hatua zitakazo hakikisha mafuta yanapatikana na kufika maeneo yote nchini pamoja na kuweka mikakati ya kuhakikisha uchumi wetu Hauathiriki na mabadiliko ya ghafla kwa bidhaa tunazotegemea kutoka nje ya nchi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeendelea kuzisikia Sauti za watanzania kupitia mitandao ya kijamii, kuona hali halisi katika vituo vya mafuta vilivyo karibu na mtaani kwangu. Nimeendelea kufanya utafiti wa karibu na uchunguzi wa hali ya upatikanaji wa mafuta katika vituo mbalimbali na nimeona kinachoendelea.Nimeona hali ya Bei na maoni ya watu, Nimesikia kauli za wamiliki wa vyombo vya moto na imani yao na maombi yao kwa serikali yao juu ya nini kingefanyika kuwasaidia kushuka kwa Bei hii.

Nachopenda kusema na ambacho nimewajibu baadhi yao mitaani ni kuwa serikali ya Rais Samia ni Sikivu sana na inasikia na kuona kila kitu kinachoendelea mitaani,inatambua usumbufu ambao watanzania wamekuwa wakiupata wa upatikanaji wa mafuta kila mwishoni kwa Mwezi, serikali yao inatambua changamoto wanayoipata wananchi hasa wa pembezoni na maumivu makali ya bei pale nishati hii inapokuwa Adimu.

Nimewaambia kuwa Serikali inafahamu ya kuwa mafuta ndio moyo wa uchumi wetu,ndio mboni yenyewe. Kwamba Mafuta yakipatikana kwa kusua sua au kwa Bei ya ulanguzi au Bei kubwa ina athari kubwa sana katika uchumi wetu,kwa kuwa hali hiyo ni lazima ipelekee mfumuko wa Bei kwa Bidhaa nyingi, kupanda kwa nauli kwa vyombo vyote vya usafirishaji na gharama nyingine nyingi lazima ziongezeka. Hali hii ni lazima ilete maumivu kwa mwananchi wa kipato cha chini,ni lazima imtoe jasho ,ni lazima impe suruba ,ni lazima iwe chungu kwa mtanzania mwenye kuhangaika kutwa nzima kupata mia mia.

Nimewaambia ya kuwa kwa kutambua haya na mengine mengi ndio maana mwaka jana serikali yetu iliamua kuchukua uamuzi na hatua za makusudi kabisa na wa kijasiri wa kuamua kutoa Ruzuku ya Billion mia moja kila mwezi katika mafuta ili kupunguza makali ya Bei.Nikawaambia ya kuwa hata Bungeni kupitia waziri wa fedha mh Dr Mwigulu nchemba iliahidi kuwa ikitokea mafuta yamepanda sana Bei Basi mama yetu Rais Samia atatoa fedha kwa ajili ya Ruzuku katika mafuta.

Hivyo watanzania wenzangu naombeni tuendelee kuwa watulivu na tuamini ya kuwa serikali yetu ni Sikivu na inaona kila kitu kinachoendelea. Sisi ndio wenye nchi sisi ndio waajiri wa serikali ndio maana serikali ya Rais samia imekuwa Sikivu na nyenyekevu sana kwetu watanzania.Tuendelee kuwa na imani na Rais wetu na Tuendelee kumwamini. Hawezi akatutelekeza au akatuacha tuteseke,tuhangaike,tuumie,Tulie machozi pasipo kutusaidia,kutushika mkono,kututua mzigo, kutupatia faraja, matumaini na kutufuta machozi .

Rais samia ni mwenye Huruma na upendo kwetu watanzania,anatambua vipato vyetu,anatambua uchumi na kipato cha kaya moja moja. Anajuwa hatuwezi kuhimili bei kubwa ya mafuta,anajuwa hatuwezi tukahimili bei kubwa za bidhaa, anajuwa ni lazima tutaishi kwa unyonge, taabu na shida kubwa sana asipotusaidia na kutushika mkono. Anajuwa maisha yetu ni ya aina gani na yanahitaji nini kumuinua kila mmoja wetu.

Rais wetu kama kiongozi, mama na mlezi wa Taifa letu ana uchungu mkubwa sana na watanzania.ana uchungu na Taifa letu, ana kiu ya kutaka kuona wananchi wanakuwa wenye furaha , Tabasamu na matumaini makubwa wakati wote. Asingependa kuona tu wanyonge na wapweke ndani ya Taifa letu. Ndio maana wakati wote anataka serikali yake iwe mikononi mwa wananchi na wakati wote iwasikilize watu wanataka na wanaumizwa na nini.

kwa sasa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania amesikia kilio cha watanzania na atakifanyia kazi na kuchukua hatua zitakazo hakikisha mafuta yanapatikana na kufika maeneo yote nchini pamoja na kuweka mikakati ya kuhakikisha uchumi wetu Hauathiriki na mabadiliko ya ghafla kwa bidhaa tunazotegemea kutoka nje ya nchi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Mshenzi huna hata kigari wala mitambo inayotumia nishati lakini unabwabwaja tu ati msikivu wakati watu wanaendelea kuumia. Huu upumbavu utaacha lini?!
Acha matusi na dharau ndugu yangu maana hapa siyo kituo cha maonyesho ya magari .
 
Upuuzi mtupu...!!! Yale makodi na madali yaliyomo kwenye kila lita ya mafuta unadhani serikali haihusiki??? Kuna migao lukuki kwenye mafuta mingine ya kisengerema tu..!! Yaani mtu atengeneze tatizo na akina nyie mshangilie, halafu siku akilibadili una mwita msikivu..!! Upumbavu mtupu
Kuweka Tozo katika mafuta siyo jambo gani nchini wala nchi yoyote ile. Ni jambo la kawaida na hufanyika kwa nchi nyingi tu kuweka Tozo au ushuru katika bidhaa fulani.

Mwaka jana mafuta yalipo panda kutokana na vita vya ukrein tuliona ikichukua uamuzi wa kuweka Ruzuku ya Billion mia moja kila mwezi.

Hivyo hata mwaka huu inaweza ikafanya hivyo kwa kuangalia hali na mwenendo wa bei katika soko la Dunia kwa siku zijazo na miezi ijayo baada ya huu kuisha.
 
Kuweka Tozo katika mafuta siyo jambo gani nchini wala nchi yoyote ile. Ni jambo la kawaida na hufanyika kwa nchi nyingi tu kuweka Tozo au ushuru katika bidhaa fulani. Mwaka jana mafuta yalipo panda kutokana na vita vya ukrein tuliona ikichukua uamuzi wa kuweka Ruzuku ya Billion mia moja kila mwezi.Hivyo hata mwaka huu inaweza ikafanya hivyo kwa kuangalia hali na mwenendo wa bei katika soko la Dunia kwa siku zijazo na miezi ijayo baada ya huu kuisha.
Acha ujinga. Aliyekuambia kila kawaida inabidi iigwe kisa kuna nchi zina kawaida hiyo ni nani? Haya, kuna nchi ushoga ni kawaida, unataka kutuambia nini?
 
Mengine upige tu kimya hata hao wanaokuona unanjaa ya teuzi watakuona hayawani,mp*mbavu msaka teuzi.
Kuna muda jiweke kwenye ukweli.
Sikiliza mkuu siyo kila mtu yupo hapa jukwaani kwa ajili ya kusaka uteuzi kama ilivyo wewe kuporomosha matusi kama hayawani na kichaa.
 
Mengine upige tu kimya hata hao wanaokuona unanjaa ya teuzi watakuona hayawani,mp*mbavu msaka teuzi.
Kuna muda jiweke kwenye ukweli.
Sikiliza mkuu siyo kila mtu yupo hapa jukwaani kwa ajili ya kusaka uteuzi kama ilivyo wewe kuporomosha matusi kama hayawani na kichaa
 
Serikali ni moja na inafanya kazi kwa pamoja na umoja na kila kitu kinaamuliwa na kupitia katika vikao vya Baraza la mawaziri.
Hujawahi sikia kauli za kupishana kwenye hii hii serikali moja? Mfano, habari ya ndoa na cheti cha kuzaliwa, Mwakyembe alisema kama leo, na kesho yake Magu akabatilisha..!! ndo ujuwe serikali hii haifanyi kazi kwa pamoja
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom