Tuweke ushabiki pembeni, ukweli ni kwamba Rais Samia ameshindwa kazi ya urais

Championship

JF-Expert Member
Aug 7, 2019
5,499
10,540
1. Mpaka sasa haieleweki dira yake hasa ni nini. Kila kitu ni kama kinajiendea tu. Hakuna concrete direction.

2. Nchi inakosa umeme kila mahali kwa zaidi ya miezi sita na wala hakuna kinachofanyika. Hapajawahi kutokea mgao mrefu hivi.

3. Kuna maeneo maji yanakatika hata wiki nne na hakuna anayejali. Yaani sasa hivi huduma za muhimu zimekuwa anasa.

4. Mfumuko mkubwa wa bei kwa bidhaa mbalimbali kutokana na uongezaji wa bei ya mafuta yanayoingia dar es salaam.

5. Nchi haijawezesha uzalishaji na uchakataji wa mazao na bidhaa ili angalau tuongeze mauzo ya nje.

6. Bei za magari zimeongezeka maradufu kutokana na kupandisha kodi. Mwaka 2020 nilimnunulia dogo kutoka yard IST kwa 10.8m leo hii inauzwa 17m.

7. Nauli za daladala zilikuwa shilingi 400 mwaka 2021 na sasa ni shilingi 600. Ongezeko la asilimia 50.

8. Hakuna uelekeo kwenye suala la kuongeza fursa za ajira kwa vijana wanaomaliza vyuo mbalimbali.

9. Ubadhilifu na ufisadi mkubwa katika halmashauri na mashirika ya umma. Ripoti za CAG zinapuuzwa.

10. Reli ya sgr haieleweki itaanza lini. Kuna dalili ikafika 2025 kabla haijaanza. Bwawa la Mwalimu Nyerere imekuwa siasa.
 
1. Mpaka sasa haieleweki dira yake hasa ni nini. Kila kitu ni kama kinajiendea tu. Hakuna concrete direction.

2. Nchi inakosa umeme kila mahali kwa zaidi ya miezi sita na wala hakuna kinachofanyika. Hapajawahi kutokea mgao mrefu hivi...
Hata na hivyo atawashinda kwa kishindo wanaume pamoja na vibaraka kwenye sanduku la kura2025 bila tashwishwi yeyote :D
 
1. Mpaka sasa haieleweki dira yake hasa ni nini. Kila kitu ni kama kinajiendea tu. Hakuna concrete direction.

2. Nchi inakosa umeme kila mahali kwa zaidi ya miezi sita na wala hakuna kinachofanyika. Hapajawahi kutokea mgao mrefu hivi...
Mawazo yako ni mazuri mtoa mada,mama ana Nia Njema Kwa kias kikubwa wasaidizi wake wanamwangusha baadhi Yao,ila mama ni msikivu anasikia na kuyafanyia kazi
 
Yaani na huyu Bibi anavyoupenda uraia kumtoa huko juu myauana ila statuacha sawa na zimbabwe
 
1. Mpaka sasa haieleweki dira yake hasa ni nini. Kila kitu ni kama kinajiendea tu. Hakuna concrete direction.

2. Nchi inakosa umeme kila mahali kwa zaidi ya miezi sita na wala hakuna kinachofanyika. Hapajawahi kutokea mgao mrefu hivi...
Kashindwaje kazi wakati ameruhusu maandamano?

Kashindwaje kazi wakati hafokei watu?

Kashindwaje kazi wakati hana kauli mbaya?

Kashindwaje kazi wakati hakuna tena watu wasiojulikana?

Kashindwaje kazi wakati alimtoa Mbowe jela?

Kashindwaje kazi wakati alimwalika Mbowe ikulu na kumpa juisi?

Samia ndo Rais mwenye mafanikio sana kuliko Rais yeyote mwingine yule kupata kutokea Tanzania, Afrika, na duniani kwa ujumla.

Hakuna kama Samia.
 
1. Mpaka sasa haieleweki dira yake hasa ni nini. Kila kitu ni kama kinajiendea tu. Hakuna concrete direction.

2. Nchi inakosa umeme kila mahali kwa zaidi ya miezi sita na wala hakuna kinachofanyika. Hapajawahi kutokea mgao mrefu hivi...
Nadhani umeanza kuelewa tunaposema,

HATOGOMBEA!!!
 
Back
Top Bottom