Rais Samia: Mgao wa maji unatokana na ubishi na ukaidi wa binadamu pia na kudra za mwenyezi Mungu

I did some writing juu ya shida ya maji kwa Tz na katika kuandika kwangu niliona kwamba shida ya Tz katika swala la maji haichochewi na swala la ubishi ila miundimbinu, rasilimali watu na sera ni viambata vikuu.
 
Ni ajabu na kweli!

Kiongozi wa Nchi fulani huko Duniani amewachenjia wananchi wake kwa kuwaita makaidi 😆

Hii ni baada ya Nchi hiyo kupitia kipindi fulani kigumu katika masuala kadhaa ambayo kwayo ni wazi hayajasababishwa na wananchi wale lakini ajabu wamegeuziwa kibao na kutupiwa gunia la lawama
 
, "Bado kuna wananchi wengi wameendelea kuvamia vyanzo vya maji kwa kuyachepusha kwa ajili ya matumizi mengine. Pia, kuna watu wanalima karibu na vyanzo vya maji. Haya yote yanapelekea Vyanzo vya Maji kupungua"
Hii ndio Tanzania bana,Wananchi wanalalamika,Mawaziri wanalalamika, Waziri Mkuu anadanganya,n.k

Na sasa Raisi na Amirijeshi Mkuu nae ameanza kulalamika.

Mimi nimejaaliwa kuishi Vinchi vingivingi kidogo, sijawahi kuona tabia hizi za kila mmoja akinung'unika.

Hili linaonyesha something is terribly wrong somewhere.
 
Hivi solution ya haya mama aliyoelezea leo ni nini? Kwa sasa vyanzo vingi vya maji, sehemu mbalimbali nchini vimevamiwa na wakulima na wafugaji (nenda Morogoro na Nyanda za Juu kusini, n.k), watu wanalima hadi mabonde ya mito, miti inakatwa hovyo kuchoma mkaa na kupata maeneo ya kilimo, n.k.Kama nchi nachelea kusema tumekalia maneno bila vitendo huku tukijua wazi hatari iliyopo mbele yetu.

China kwa mfano, kupitia Shelterbelt Program ina mpango wa kuondoa jangwa kwa ekari milioni 87 ifikapo 2050 na hadi sasa wameshapanda miti kwa zaidi ya ekari 13 milioni.

Ni imani yangu tunaweza kuibadilisha sehemu kubwa ya nchi yetu ikawa ya kijani ndani ya miaka 10 ikiwa watu watahamasishwa na kuwa na mipango madhubuti. Ili hili litokee kuna haja ya:

1. Kila halmashauri, kata na kijiji kupewa lengo l miti ya kupanda kila mwaka na ukaguzi wa dhati wa kilichofanyika uwepo.

2. Shule zote zipewe lengo la idadi ya miti kupanda na kuikuza kila mwaka.

3. Kambi zote za jeshi zipewe pia malengo.

4. Maeneo yote public ikiwa ni pamoja na mbuga zipewe JKT na mashule kupanda miti.

5. Kila mtanzania mwenye eneo la shamba apewe idadi ya miti kupanda (mfano miti kumi kuzunguka shamba kwa kila ekari moja).

Nawasilisha.
 
Mwambie na tembo hunywa lita 200 kwa siku
Kwa hiyo wazuiwe wasinywe au?
Pic%20Layer_2021111311215721.jpg
 
Hii ndio Tanzania bana,Wananchi wanalalamika,Mawaziri wanalalamika, Waziri Mkuu anadanganya,n.k

Na sasa Raisi na Amirijeshi Mkuu nae ameanza kulalamika.

Mimi nimejaaliwa kuishi Vinchi vingivingi kidogo sijawahi kuona tabia hizi za kila mmoja akinung'unika.

Hili linaonyesha something is terribly wrong somewhere.
Wapinzani wanalalamika na kulialia!
 
Back
Top Bottom