Rais Samia: Mgao wa maji unatokana na ubishi na ukaidi wa binadamu pia na kudra za mwenyezi Mungu

Soma tena ulichoandika na ulinganishe nilichokuuliza.....
Ngoja nibadilishe swali ili unielewe
Dar wanategemea mto ruvu, mto ruvu maji yamepungua.nakubaliana na mgao
Mikoa ya Kanda ya ziwa wanategemea maji ya mradi wa ziwa Victoria, mradi ulishaisha na maji yalishaanza kutoka. Ila Sasa hivi hayatoki. Ndio nikakuuliza huko napo sababu ni nini?
Hapo nakuelewa. Hoja yako ya mwanzo ilikuwa jumuishi (general).
 
Dar es Salaam kuna mgao mkubwa wa maji kwa sababu mto Ruvu umevamiwa na binadamu na kuchepusha maji.

Pili maelfu ya mifugo yanayoingizwa kwenye mito kunywa maji yamepunguza kiasi cha maji kwani ng'ombe mmoja kwa mfano hunywa lita 40 za maji kwa siku.

Tatu ni ukataji miti hovyo hali inayoharibu ikolojia ya nchi.

Nne ni tatizo la tabia nchi.

Hivyo mgao wa maji hauepukiki

Na kwahiyo naagiza Wakuu wote wa mikoa kuweka ulinzi katika mito yote ili kulinda maji ya watu wetu.

========

Rais Samia Suluhu Hassan amesema anatambua Miji mingi mikubwa inakabiliwa na uhaba wa maji unaopelekea mgao wa maji na upungufu wa umeme

Amesema hiyo imetokana na mambo mawili makubwa ambayo ni Ubishi na ukaidi wa wanadamu na Kudra za Mungu

Amefafanua, "Bado kuna wananchi wengi wameendelea kuvamia vyanzo vya maji kwa kuyachepusha kwa ajili ya matumizi mengine. Pia, kuna watu wanalima karibu na vyanzo vya maji. Haya yote yanapelekea Vyanzo vya Maji kupungua"
#JamiiForums

"Nimefatana na viongozi wote hawa wa dini kwanza, kufuatana na viongozi wa dini wote hawa ni baraka kama kuna mapepo huko njiani yanapeperuka...pili nimeipa heshima Mwanza, tutaanza hapa dua za kuomba mvua zenye neema kwa Taifa letu"-Rais Samia.

Unanunua madege huwekezi kwenye kuvuma maji. Una bambika kesi Mungu yupi akusikie wewe?
 
Ni mipango mibovu pia ya watendaji, mvua huwa inanyesha ya kutosha tu, mbona sijawahi ona maeneo ya kutunza maji........nchi hii wanasiasa wanaongea rahisi sana mambo magumu
 
Mvua zinanyesha Mwanza muda huu😍
2919449_079E2A09-4AEF-4AB7-B330-422CE107A946.jpeg
 
Back
Top Bottom