Rais Samia: Mgao wa maji unatokana na ubishi na ukaidi wa binadamu pia na kudra za mwenyezi Mungu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
85,095
143,945
Dar es Salaam kuna mgao mkubwa wa maji kwa sababu mto Ruvu umevamiwa na binadamu na kuchepusha maji.

Pili maelfu ya mifugo yanayoingizwa kwenye mito kunywa maji yamepunguza kiasi cha maji kwani ng'ombe mmoja kwa mfano hunywa lita 40 za maji kwa siku.

Tatu ni ukataji miti hovyo hali inayoharibu ikolojia ya nchi.

Nne ni tatizo la tabia nchi.

Hivyo mgao wa maji hauepukiki

Na kwahiyo naagiza Wakuu wote wa mikoa kuweka ulinzi katika mito yote ili kulinda maji ya watu wetu.

========

Rais Samia Suluhu Hassan amesema anatambua Miji mingi mikubwa inakabiliwa na uhaba wa maji unaopelekea mgao wa maji na upungufu wa umeme

Amesema hiyo imetokana na mambo mawili makubwa ambayo ni Ubishi na ukaidi wa wanadamu na Kudra za Mungu

Amefafanua, "Bado kuna wananchi wengi wameendelea kuvamia vyanzo vya maji kwa kuyachepusha kwa ajili ya matumizi mengine. Pia, kuna watu wanalima karibu na vyanzo vya maji. Haya yote yanapelekea Vyanzo vya Maji kupungua"

"Nimefatana na viongozi wote hawa wa dini kwanza, kufuatana na viongozi wa dini wote hawa ni baraka kama kuna mapepo huko njiani yanapeperuka, pili nimeipa heshima Mwanza, tutaanza hapa dua za kuomba mvua zenye neema kwa Taifa letu"-Rais Samia.
 
Leo akiwa mkoani Mwanza mama Samia amesema binadamu na kudra za mwenyezi Mungu ndio sababu za uhaba wa maji na mgao wa umeme.

Vipi kwa wale waliokataa kuwa hakuna mgao wa umeme?

Leo mama mwenye kasema, au kaongopa? Au kajisahau? Kajichanganya?

Screenshot_20211118-124706_1.jpg
 
Hii nchi tu na hali mbaya sana kama kiongozi tulie naye ndio huyu basi kama taifa tuna janga kubwa sana
Janga gani na wewe? Yaani huoni haya mabadiliko ya tabia ya nchi? Joto kali sana na maeneo mengine kama Morogoro mvua haijanyesha kabisa, na hii ni November inaenda mwishoni. Yeye afanyeje kama maji yamepungua kutokana na sababu hizo? Kazi tu kukariri corus bila ya kufanya tafakari.
 
Back
Top Bottom