Rais Samia: Kwa sura nazoziona hapa (CHADEMA) hamna dhamira ya kushika dola 2025, mnajua mama yupo


Rais Samia akiwa katika Maadhimisho amezungumza mambo mbalimbali. Akiwa anajibu hoja ya Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa BAWACHA kuhusu nia yao ya kushika dola 2025 Rais Samia amesema:

"Ndugu zangu siasa ni mchezo wa kulumbana kwa hoja Wote tukiwa na lengo la kushika dola kama alivyosema Mwenyekiti wa BAWACHA na Freeman Mbowe. Kwa sura nazoziona hapo hamna nia ya kushika dola 2025 mnajua Mama yupo dhamira hiyo haipo."

"Lakini niseme yes wote tuna lengo hilo lakini tukafanye kistaarabu kama Wanaadamu kama watu. Tuheshimiane, tuheshimike duniani."

Aidha Rais Samia ameongeza;

"Nataka niwaambie kitu kwa kipindi hiki kifupi nchi yetu inaheshimika sana duniani. Kwahiyo tusiirudishe chini, tusiirudishe nyuma. Twendeni na mwendo huu tuweke heshima ya nchi yetu pale inapostahiki.


Tanzania ni taifa kubwa tusilitolee sifa yake."
Mama alikuwa anajipakulia minyama bana Ulitaka aseme kuna mpinzani anamuhofia?
Hata kwenye chama chake mwendo ni huo huo.
 
Mimi ni mwananchi mmoja wapo ninayetaka Dr. SSH 🇹🇿 2025 awe Rais mgombea pekee nchini, Hii Amani tuliyonayo tuendelee kuifurahia na miaka mingne mitano maana hatujui atakayekuja badae atakuwaje.
Lini Tanzania ilikosa amani? Tanzania miaka yote huwa inajivunia amani tu sio maendeleo utafikiri nchi zote zipo vitani kasoro yeye.
 
Back
Top Bottom