Rais Samia kuwa mgeni rasmi kongamano la BAWACHA siku ya wanawake duniani

iamLyenda

New Member
Jul 16, 2015
4
31
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lililoandaliwa na Baraza la Wanawake (Bawacha) wa chama hicho.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumapili, Machi 05, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, amesema Rais Samia amethibitisha kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo litakalofanyika Machi 08 Moshi mkoani Kilimanjaro.

“Kongamano hili la siku ya wanawake duniani ni la wanawake wote, lakini hapa Tanzania, Bawacha wamekuwa wakiliandaa kwa mafanikio makubwa kila mwaka na wamekuwa wakitoa hotuba zenye jumbe mbalimbali zinazowahusu wanawake wote bila kujali itikadi za vyama vyao.

“Napenda kuwatangazia kuwa Rais Samia ambaye nilikuwa na mazungumzo naye jana Jumamosi, amekubali kuwa mgeni Rasmi siku hiyo na mimi nitampokea mjini Moshi siku hiyo,” alisema Mbowe

Rais Samia kukubali kuhudhuria na kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano linaloandaliwa na chama kikuu cha upinzani ni matunda ya maridhiano ya kisiasa yanayoendelea kufanywa na chama chake (CCM) na Chadema.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKIWAPUNGIA WAJUMBE KWENYE MOJA YA MIKUTANO YA CHAMA CHAKE (CCM) AMBAPO YEYE NI MWENYEKITI TAIFA
Maridhiano hayo awali yalianza baada ya Rais Samia kuunda kikosi kazi cha kuishauri serikali kuhusu mwenendo wa kisiasa nchini.

Lakini maridhiano yalitiwa chachu baada ya kikao cha kwanza kati ya Rais Samia na Mbowe kukutana Ikulu, Machi 04, 2022 siku ambayo Mbowe alitoka gerezani baada ya Serikali kuifuta kesi ya ugaidi iliyokuwa inamkabili mwanasiasa huyo.

Kati ya mambo ambayo Chadema waliyapeleka kwa Rais na kutaka yarekebishwe haraka ni pamoja na kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa wa Chadema, jambo ambalo kwa asilimia kubwa limeshafanyika.

Jambo la pili ni kuweka usalama kwa wakimbizi wa kisiasa waliokimbia nchi. Tayari viongozi wa Chadema waliokimbia nchi wamesharejea. Viongozi hao ni Tundu Lissu, Ezekia Wenje na Godbles Lema.

Jambo la tatu lililodaiwa na Chadema ni kuondoa zuio la mikutano ya hadhara ambapo tayari Januari mwaka huu, Rais Samia ameondoa zuio hilo.

Jambo la nne ni upatikanaji wa Katiba mpya ambapo mpaka sasa mchakato haujaanza.

1302862A-747B-4411-956C-55FFF8E227BB.jpg
 
Nimependa kusikia kwamba Watanzania sasa wanaishi kama ndugu na wanashirikiana.

Watanzania miaka yote tumekaa pamoja kwenye familia, kwenye mahusiano, kanisani, kazini na maeneo mbalimbali yanayotuleta pamoja.

Lakini Watanzania hao hao tumekuwa maadui kwenye ulingo wa siasa. Maana yake tunaelewana na kusema NI ndugu kwenye kila kitu Ila inapokuja kwenye siasa tunafanya unafiki kwamba Sisi siyo ndugu.

Naamini makubaliano ya Mbowe na Mhe. Rais kuhusu Rais kuwa mgeni rasmi siku ya wanawake yamepokelewa Kwa mtizamo tofauti. Nini maoni yako?

Maoni yangu Mimi NI haya;

Mhe. Rais kuwa mgeni Rasmi kwenye mkutano wa chadema nikutuma salamu Kwa vyombo vya dola kwamba Tanzania sasa NI moja. Nikutuma salam Kwa viongozi Aina ya Muro, Makonda, Mnyeti, Gambo, Nape, Mwigulu, Ndugai, Mkumbo, Molel, Tulia, Bashiru, Kabudi, Lukuvi, nk kwamba siyo lazima uwe na roho ya kikatili Ndipo ukubalike au uongoze....Duniani tunapita ccm au CDM tutaviacha......Sisi NI ndugu.
 
Umeongea vizuri sana
 
Ni uthibitisho kuwa Viongozi wakuu wa Chadema wamelamba asali.

Rais anayeendelea kuwakumbatia wanawake 19 waliofoji nyaraka za chama, wakafukuzwa uanachama na bado anawakingia kifua ili wabaki bungeni waendeelee kula kodi za wananchi utamwalikaje kwenye kikao cha wanawake watiifu kwa chama?

Mbowe anaigeuza Chadema kuwa tawi la CCM.

Na ni ushahidi kuwa akina Mbowe wanampigia kampeni ya urais Samia in exchange ya viti vichache vya ubunge watakavyogawana akina Mbowe na genge lake.
 
Ni uthibitisho kuwa Viongozi wakuu wa Chadema wamelamba asali.

Rais anayeendelea kuwakumbatia wanawake 19 waliofoji nyaraka za chama, wakafukuzwa uanachama na bado anawakingia kifua ili wabaki bungeni waendeelee kula kodi za wananchi utamwalikaje kwenye kikao cha wanawake watiifu kwa chama?

Mbowe anaigeuza Chadema kuwa tawi la CCM.

Na ni ushahidi kuwa akina Mbowe wanampigia kampeni ya urais Samia in exchange ya viti vichache vya ubunge watakavyogawana alina Mbowe na genge lake.
Missile, do not speculate untill you spectate. Sikudhanii kama unaweza kuwa na such reasoning
 
Kuna kitu hakiko sawa sehemu😂😂😂. Wale manguli wa siasa sasa wanafanya kazi yao vizuri nyuma ya vijana wao.

Umpe manager msaidizi awe msimamizi wa wafanyakazi wako na utegemee asichukue popularity...
MNATEGEMEA ASITOE SELA ZA CCM HAPO😂😂😂
 
Kwani Samia ni rais wa ccm au rais wa nchi? Aise naona sukuma gang Mmechanganyikiwa kabisa, hamkuzoea siasa za urafiki na uzalendo. Mlizoea siasa za kibabe na kuua tu. Bashiru alipo anatamani ajizike mzima mzima
 
Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe amesema watakuwa na tukio la akina Siku ya Wanawake Duniani 8/3/2023 mjini Moshi

Mbowe amesema wamemualika Rais Samia kama mgeni rasmi katika tukio hilo naye amekubali

Hivyo mh Mbowe atakuwepo mjini Moshi kumpokea mh Rais
Samia amesema upinzani siyo uadui, bali ni mitzamo tofauti nmna ya kuongoza nchi! hii haina maana kuwa watakuwa chawa wake!
 
Naiona serikali ya mseto kwa siku za usooni.

Mbowe Waziri Mkuu

Tundu Lissu Waziri wa Sheria

Godblesss Lema Waziri wa Mambo ya Ndani

Hao ni kwa uchache.

Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni kabla ya 2025.

Serikali tatu znakuja.

Hata hivyo, Mama awe makini sana CCM hawapendi haya mambo.

Wanasiasa wa upinzani watalazimika kuunda serikali moja na CCM Kama njia ya rahisi ya kupunguza nguvu za dola za CCM na pia ni kwasababu watanzania wamekuwa waoga kupambana na dola kuindoa CCM madarakani

Mtanielewa yakitimia.

Nimemaliza.
 
Kwani Samia ni rais wa ccm au rais wa nchi? Aise naona sukuma gang Mmechanganyikiwa kabisa, hamkuzoea siasa za urafiki na uzalendo. Mlizoea siasa za kibabe na kuua tu. Bashiru alipo anatamani ajizike mzima mzima
Punguza hasira. CCM ifanye kazi yake, wengine wajipange kuchukua ofisi. Maswala ya Kenge anajichanganya na mamba, alafu mmasema raisi wa watanzania. Vipo vyama vinaunganisha watanzania wanawake. Sio mwana CCM kuwa mgeni rasmi kwenye kikao cha chadema. Ni trash hii.
 
Back
Top Bottom