Ni Asubuhi tulivu siku ya Jumatano tarehe 8 March ikiwa ni kilele Cha Siku ya Wanawake Duniani.
Macho na masikio ya Watanzania leo yanaelekezwa katika mji maarufu wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
Chama kikuu Cha Chadema chenye wafuasi takribani Milioni 10 nchini kupitia Baraza lake la Wanawake Bawacha linafanya Kongamano kubwa la kuadhimisha siku hii ya Wanawake Kitaifa katika Ukumbi wa KURINGE.
Kinachovutia kwenye Kongamano hili la Bawacha mwaka huu ni mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye atakuwa mgeni Rasmi kwenye Kongamano hilo.
Kukubali kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni Rasmi kwenye Kongamano la Chadema kumevuta hisia za mamilioni ya Watanzania na hata Jamii ya Kimataifa.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ndiye atakayekuwa mwenyeji wa Rais Samia na anatarajia kumpokea kuanzia saa 3 asubuhi.
Rais Samia kuhutubia Jukwaa moja na Chama kikuu Cha Upinzani Chadema kinaonyesha kilele Cha mafanikio ya Maridhiano ya kisiasa yaliyoasisiwa na Rais pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.
Rais Samia Suluhu Hassan amesikika mara kadhaa akitangaza hadharani kwamba wapinzani nchini siyo maadui wake tofauti na mtangulizi wake John Magufuli aliyejiapiza kuangamiza upinzani nchini na hatimaye kuuvuruga uchaguzi mkuu wa mwaka 2020
Mji wa Moshi ambao ni Kati ya ngome kuu za Chadema nchini umepambwa na bendera nyingi za chama hicho kikuu Cha Upinzani huku mazungumzo katika mikusanyiko mbalimbali ikiwa ni tukio hili la kihistoria.
Molemo Media tunatarajia kuwaletea mubashara matukio yote muhimu yatakayoendelea hapa ukumbini mjini Moshi kabla na wakati wa Kongamano hilo
Karibuni Sana
Mbowe Awasili Ukumbini
Mwenyekiti Freeman Mbowe anaingia hapa Ukumbini saa 5 kamili na kulakiwa kwa Shangwe kubwa hapa Ukumbini
Mwenyekiti Mbowe amewasili tayari kumlaki Mgeni Rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Rais Samia Suluhu Awasili saa 5.10
Rais anawasili hapa kwenye viwanja vya Kuringe na kulakiwa kwa Shangwe kubwa na Wanawake wa Bawacha.Mwenyekiti Freeman Mbowe anamlaki na kumkaribisha kwa ajili ya tukio hili la kihistoria
Yanayoendelea Ukumbini
Zimeimbwa nyimbo tatu baada ya Rais kuingia Ukumbini umeanza wimbo wa Taifa, wimbo wa Afrika Mashariki na Wimbo wa Peoples Power
Viongozi wa dini wameongoza Dua ambao ni Askofu Mkuu wa KKKT na Sheikh wa mkoa wa Kilimanjaro
Zimefuata salaam za Bawacha mkoa zilizotolewa na Katibu wa Mkoa na pia Salam za mkoa kupitia mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu
Mbowe Ahutubia
Mwenyekiti Freeman Mbowe ameanza hotuba yake kwa kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukubali mwaliko wa kuwa mgeni Rasmi kwenye Kongamano la Bawacha.
Mwenyekiti Mbowe ameeleza mbele ya Rais Samia kuhusu madhila mbalimbali ambayo wafuasi wa Upinzani waliyopitia katika awamu ya 5
Mbowe amemhakikishia Rais Samia kwamba Chadema itaendeleza Maridhiano kutokana na nia njema ya Rais.
Mwenyekiti Mbowe amemueleza Rais umuhimu wa Katiba Mpya na ulazima wa kuharakisha mchakato huo.
Mwenyekiti Mbowe amemalizia hotuba yake kwa kueleza kwa uchungu jinsi Serikali iliyopita kwa kushirikiana na waliokuwa Viongozi wa Bawacha kuhujumu chama hicho kwa kupeleka bungeni Wanawake 19 ambao hawakuwahi kuteuliwa na Chama hicho.Mbowe amesema katika hali ya kusikitisha Viongozi wa bunge nao walihusika na uharamia huo.Kiongozi huyo amemtaka Rais kutumia mamlaka yake kuwaondoa watu hao wanaojiita wabunge wa viti Maalum wasio na Chama kinyume kabisa na Katiba ya nchi.
Rais Samia Suluhu Hassan ahutubia Taifa
Rais Samia alipokaribishwa kuhutubia amewapongeza Sana akina mama wa Bawacha kwa kuandaa Kongamano kubwa na zuri linalovutia.
Pa Raia Samia amewashukuru Bawacha na Chadema kwa Ujumla kwa kumkaribisha kuwa mgeni Rasmi na kusema ni kitu ambacho hakutarajia
Rais Samia amesema ataendeleza maridhiano ya kisiasa kutokana na ukweli kwamba ndiyo njia pekee ya kuleta utengamano na kuleta Amani na utulivu nchini.
Rais Samia amesema mwanzoni hakueleweka ndani ya chama chake kutokana na kusimamia Maridhiano na hata Mpaka Sasa wapo wahafidhina wenye nia ya kukwamisha maridhiano
Kuhusu mchakato wa Katiba Mpya Rais Samia ameahidi siku siyo nyingi atatangaza kuundwa kwa Tume ya Rais itakayosimamia mchakato wa Katiba Mpya kwa mujibu wa Sheria.
Kuhusu wabunge wa viti Maalum waliopo bungeni kinyume na Katiba Rais Samia ameomba suala hilo liachwe mikononi mwa mahakama mpaka liishe kwa sababu itakuwa vigumu kwake kuingilia mhimili wa mahakama.
Mwisho Rais amemalizia kwa kuwashukuru tena Bawacha kwa heshima waliyompatia.