Rais Samia kinara kupunguza vifo vya Mama na Mtoto Nchini

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, amefunguka mazito kuhusu maelekezo ya Rais kufanikisha Dk. Samia Suluhu Hassan katika mapambano shisi ya vifo vitokanavyo na uzazi kwa mama na moto.

Amesema hatua zilizochukuliwa na Rais Dk. Samia ndizo zilizofanikisha matokeo ya sasa ya ongezeko la uzazi salama na kuahidi kuwa maelekezo hayo wataendelea kuyatekelezwa kwa kishindo.

Ummy amésema sasa anatembea kifua mbele akiivunia uwajibikaji wa Bohari ya Dawa (MSD) katika mapambano dhidi ya vifo hivyo kutokana na usambazaji va vifaa vya huduma za dharula kwa uzazi pingamizi.

Akizungumza katika mahojiano maalumu, jana, Waziri Ummy alisema Rais Dk. Samia alionyesha kuguswa na vifo vya uzazi na kuchukua hatua kwa kutoa maelekezo ambayo yameleta matokeo chanya katika kufanikisha mapambano dhidi ya vifo hivyo.

Alitaja maagizo hayo ni kuimarisha miundombinu ya huduma ya uzazi wa dharura (CEMoC) kwa upasuaji kufanikisha kumtoa mtoto tumboni ambapo takwimu zinaonyesha kuwa kuna vituo vya afya 552 hadi sasa nchi nzima ambavyo vinatoa huduma hizo.

"Unakumbuka tulianza wote ambapo vituo vilikuwa 106 pekee mwaka 2016, ambapo vituo hivyo vya CEMoC vimewekewa vifaa tiba ikiwemo mashine za dawa za usingizi, 'ultra sound', vitanda vya upasuaji, taa maalumu zinazotumika chumba cha upasuaji, vitanda wa kujifungulia, sindano za OXYTOCIN mahususi kumsaidia mama anayejifungua kuchochea uchungu na kutokwa na damu na vingine," alisema

Waziri Ummy aliongeza kuwa maelekezo ya Dk. Samia ni kuhakikisha vifaa hivyo vinakuwepo hadi ngazi ya vituo va afya na hospitali za wilaya.

Alisema katika kuimarisha huduma hizo amehakikisha utekelezaji wa maagizo ya Rais yanafanyiwa kazi ipasavyo ikiwemo kupatikana kwa uhakika dawa za kifafa cha mimba katika ngazi zote.
Alitaja agizo lingine lililofanyiwa kazi ni kuajiri watumishi wa afya hususani wauguzi na wakunga.

Pia, alisema Rais Dk. Samia amemtaka Waziri Ummy na wizara yake kuhakikisha wanavutia wadau wa maendeleo kuongeza bajeti ya kuvutia maboresho sekta ya afya ukiwemo mfuko wa afya ya pamoja ambapo wizara imepata ongezeko la fedha na asilimia 90 zinaelekezwa katika ngazi ya zahanati.

Alisema katika mapambano hayo Rais Dk. Samia amefanikiwa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa mama na moto ambapo kwa watoto takwimu zinaonyesha vifo vimepungua kutoka 67 hadi 43 na mwishoni mwa mwezi huu wanataraiia kutoa takwimu mpya ya vifo va wajawazito.

"Kwetu Tanzania haya ni mafanikio makubwa, Rais wetu katika hili anaonekana bayana anavyoguswa na anawochukua hatua kwa vitendo na anafuatilia kila hatua." alisema.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy Rais Samia alianza kuguswa na afya ya uzazi kwa muda mrefu ambapo mwaka 2017 akiwa Makamu wa Rais alifanya kazi kubwa kuimarisha huduma ya mama na moto kwa kuwaelekeza wakuu wa mikoa na wilaya kutekeleza kampeni ya jiongeze ambayo inalenga kuimarisha uwajibikaji, miundombinu ya kujifungulia na matokeo ya uzazi salama.

Waziri Ummy alisema baada ya mafanikio hayo mwelekeo uliopo ni kupunguza vifo ya watoto wachanga kutoka umri wa siku moja hadi 28 kwa kuwa katika eneo hilo bado matokeo si mazuri na tayari Rais Dk. Samia ametoa zaidi ya sh. bilioni sita za mapambano hayo.

Alisema kwa sasa anatembea kifua mbele akijivunia maboresho yanayoendelea kufanyika ndani ya MSD hususani katika mapambano ya vifo vitokanavyo na uzazi ambapo hadi Julai 6, mwaka huu bidhaa za afya 296 kati ya 345 sawa na asilimia 85 za hudumaza CEMoC zimesambazwa katika
vituo va kutolea huduma.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa MSD Mavere Tukai, alisema kuwa watahakikisha maagizo ya Rais Dk. Samia katika mapambano ya kupunguza vifo va mama 'na mtoto wakati wa kujifungua yanaendelea kufanyiwa kazi kwa kuboresha huduma za afva vituoni.

Alisema wataendelea kushirikiana na wadau wa afya hususani Wizara ya Afya, Wizara ya Fedha, Wizara ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mkitaa (TAMISEMI), vuo vikuu na wataalamu wa afya katika mapambano hayo.

"Kwetu MSD haya ni maagizo ya Mkuu wa nchi, tulishaanza kuyafanyia kazi kwa kuhakikisha vifaa vya afya wa kisasa vinapatikana katika vituo vetu na katika mkakati wa kupunguza vifo va watoto wachanga, pia tumeanza kufanyia kazi ambapo vitanda vya ICU (chumba cha uangalizi maalumu) vifaa tiba vinasambazwa, tumeenda mbali zaidi kwa kuzingatia bora wa vifaa hivyo, unafu wa bei, upatikakanaji wa uhakika wa vifaa kutoka kwa washitiri, alisema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom