Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,506
- 113,628
Wanabodi,
Kwa Maslahi ya Taifa kwenye Nipashe ya leo 5/02/2023
Makala ya leo, ni kuhusu haki za binaadamu, na kwa wale wenye kumbukumbu mzuri ya safu hii, makala za mwanzo kabisa zilikuwa ni makala mfullulizo za “Kilio Cha Haki” ambazo nilizungumzia sana haki jinai.
Mtu unapozungumzia haki jinai namna hii, kisha ukasikia Rais ameunda timu kuangalia haki jinai, iwe makala zako zilichangia au hazikuchangia, haijalishi, lakini kitendo cha kukizungumza kitu kisha kikafanyiwa kazi ni faraja tosha kwako mwandishi.
Mungu Mbariki Rais wetu Samia
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali
Update
Hatimaye usaidizi huu, unakwenda kufanyika, kupitia kipindi cha TV kwenye kituo cha Channel Ten, kila siku za Jumapili Saa 3:00 usiku na marudio kila Jumatano saa 9:30 Alasiri.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=IXfA8sZkNPxpaeZn
Usikose kuangalia!.
P
Kwa Maslahi ya Taifa kwenye Nipashe ya leo 5/02/2023
Makala ya leo, ni kuhusu haki za binaadamu, na kwa wale wenye kumbukumbu mzuri ya safu hii, makala za mwanzo kabisa zilikuwa ni makala mfullulizo za “Kilio Cha Haki” ambazo nilizungumzia sana haki jinai.
- Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?. Hoja hii imejibiwa kwa vitendo na matokeo yameonekana msikilize Rais Samia akizungumzia matokeo hayo
- Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
- Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana! Hongera sana, kazi umeianza vizuri. Sasa haki sio tu inatendeka, inaonekana! Kazi Iendelee…
- Ushauri kwa DPP: Kutekeleza nia njema ya Rais Samia, kuona Haki ikitendeka; je, tumchagize DPP kutumia Nolle kufuta kesi zote zinazosuasua?
- Pongezi kwa DPP Mpya. Kama itampendeza, aanze kwa kutumia Nolle, kusafisha Uchafu wote wa mtangulizi wake...
Mtu unapozungumzia haki jinai namna hii, kisha ukasikia Rais ameunda timu kuangalia haki jinai, iwe makala zako zilichangia au hazikuchangia, haijalishi, lakini kitendo cha kukizungumza kitu kisha kikafanyiwa kazi ni faraja tosha kwako mwandishi.
- Rais Samia ana nia njema na ya dhati kwa kauli thabiti na matendo, Watanzania wapate haki, ila imetokea Watanzania hawajui haki zao!. Je tumsaidie Rais Samia na kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au tuwaachie wenyewe?.
- Katiba japo ni kakitabu kadogo ka kurasa 143 tuu, lakini kukaelewa ni shughuli nzito!, ili Watanzania waielelewe katiba, kunatakiwa kufanyika kazi kweli kweli ya uelimishaji umma kuhusu Katiba, sheria na haki.
- Tanzania japo tuna wanasheria wengi ambao ni manguli wabobezi na wabobevu wa sheria, lakini wengi hawaijui katiba!.
- Serikali tunawasheria wengi manguli wabobezi na wabobevu wakiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa serikali ambao walipaswa kuijua katiba vilivyo lakini wengi wao, hawaijui katiba, ndio maana serikali inaweza kutunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba.
- Bunge letu nalo ambalo limeshehenezwa na wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, lakini wametunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, hivyo Bunge letu na wabunge wetu nao hawaijui katiba kikamilifu.
- Mahakama ndio mhimili pekee ambao angalau angalau unaijua Katiba na kuliambia Bunge na Serikali kuwa sheria fulani ni batili kwasababu iko kinyume cha katiba, ila very unfortunately Mahakama haina meno, badala ya kubatilisha sheria batili, ndio kwanza inayarudishia yale yale majinga yaliyotunga sheria batili ndio yaibadilishe!. Hivyo mahakama kwenye kuitekeleza katiba nayo inashikwa na kigugumizi!.
- Lakini huku mitaani kuna wanasheshia wa kawaida tuu na taasisi za kisheria, wanaweza kabisa kusaidia kuelimisha umma elimu ya katiba sheria na haki, ili kumuwezesha Rais Samia kutimiza azma yake ya kutaka Watanzania kutendewa haki ni lazima kwanza hawa Watanzania wazijue haki zao.
- Hivyo hizi kauli dhabiti za Rais Rais Samia katika utoaji haki, nimeanza kuzifuatilia kwa muda mrefu, na wiki hii amezitoa tena katika matukio makubwa mawili, tukio la kwanza ni siku ya uzinduzi wa Tume ya Haki Jinai jijini Dodoma siku ya Jumatatu iliyopita ya tarehe 30 January na kesho yake tarehe mosi February kwenye Siku ya Sheria jijini Dodoma.
- Kwenye utetezi wa haki nchini Tanzania, tukubali tukatae, Rais Samia ana nia njema na ya dhati ya kuhakikisha Watanzania wanatendewa haki kwenye vyombo vya utoaji haki, na moja ya udhaifu mkubwa katika utoaji haki Tanzania, ni Watanzania, hawazijui haki zao!.
- Haki hailetwi kwenye kisahani cha chai, haki ni stahili na stahiki inayopaswa kutolewa bila wewe kuiomba, na ikitokea haki haikutolewa au haikutendeka, haki haiombwi, bali inapaswa kudaiwa, sasa ukiwa mtu hujui haki yako, huwezi kudai kitu usichokijua!
- Hiki kitu cha Watanzania kutokujua haki zao, nimesikia tena wiki hii, Rais Samia, akirudia kulisema jambo hili, kwenye kilele cha siku ya sheria iliyoadhimishwa kitaifa uwanja wa Chinangali, jijini Dodoma.
- Rais Samia, alisema mambo mengi makubwa mazuri katika utoaji haki nchini Tanzania, kubwa nililo ondoka nalo mimi leo katika makala hii ni hili la Watanzania hawajui haki zao!.
- Kwenye hili, Rais Samia amesema, na naomba nimnukuu “Wanasema, kuna msemo maarufu kwamba haki hupewi mkononi, lazima uitafute, lakini katika kutafuta haki kuna ujuzi, wananchi wetu wengi hawana ujuzi wa kutafuta haki zao kwa hiyo tuwasaidie kutafuta au kupata haki zao” mwisho wa kunukuu.
- Hii sii mara ya kwanza kwa Rais Samia kuzungumzia changamoto ya haki kwa Watanzania wengi wasiojua haki zao, mwaka jana siku maadhimisho ya miaka 10 ya taasisi ya mtandao wa watetezi wa haki za binaadam, THRDC inayoongozwa na mwanasheria, Onesmo Ole Ngurumwa.
- Rais Samia alisema, “Mtetezi mkubwa wa haki za binaadamu ndani ya Tanzania ni katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo serikali ndiyo inaitekeleza, ndio sheria mama ambayo haki zote za binadamu wanaoishi Tanzania”.
- Rais Samia anaendelea, “swala langu kwenu ni “jee hawa wanadamu tunao watetea, wanaijua hiyo katiba?, na nataka niache kazi kwenu katika eneo la elimu kwa umma, muifanye kazi hii ya kuwaelekeza watu waijue katiba yao, kwasababu wanapodai haki, lazima wajue na wajibu wao, haki ziko kwenye katiba na wajibu uko kwenye katiba wakielekezwa vizuri wataujua na wajibu wao nini kikatiba”, mwisho wa kunukuu. Msikilize Rais Samia mwenyewe
- Hivyo hiki ambacho makala hizi zinafanya, kuwaelimisha Watanzania kuhusu haki zao na katiba yao, ni kuwasaidia Watanzania, kulisaidia taifa, na kumsaidia Samia kutimiza nia Njema yake.
- Hivyo natoa wito kwa wanasheria kote nchini, haijalishi wewe ni nani kuanzia JM, majaji, mahakimu, mawakili na wasaidizi wa sheria, na bila kujali uko wapi ni mahakamani, serikalini, taasisi za umma, mashirika au wanasheria binafsi, tukiwemo sisi mawakili, sote tumuunge mkono Rais Samia katika kutimiza azma njema ya Rais Samia, kuhakikisha Watanzania wanatendewa haki.
- Tume hiyo ya haki jinai inayoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande, akisaidiawa na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Balozi Ombeni Sefue, ameipa tume hii miezi 4 kuangalia mifumo ya utendaji wa taasisi zote za utoaji haki na kuahidi kuyafanyia kazi matokea ya Tume hiyo,
- Yakiwemo lile “zumari” fulani ambalo Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma, alilizungumzia kuhusu zumari hilo lililopigwa kutokea Zanzibar, mlio wake ufike na huku bara,
- Rais Samia amesisitiza, kwa vile na yeye ametokea Zanzibar, “Lile zumari litalia, na mimi ni Mpemba, najua sana kupuliza zumari, kwa lile zumari litapulizwa, nitakapo pokea taarifa ya tume, na kusema ndio, mama puliza zumari, nitakwenda kufanya hivyo”,
- Hivyo sasa taasisi za haki serikali, pingeni kongole sana kwa Rais Samia, kusikia kilio chenu kilichowasilishwa kwa Rais Samia, na Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, sasa kaeni mkao wa kula!.
- Kauli za vingozi wa kisiasa zinazotolewa kwenye hotuba, ziko za aina mbili, kwanza kiongozi anaandikiwa hotuba, kisha anapewa kuipitia, katika kuipitia huko, huongeza yale yak wake ya moyoni ambayo hakuandikiwa, na pili inawezekana hayo aliyoandikiwa, akakubaliana nayo na kuyangiza mayoni kwake hivyo akihutubia yanakuwa ni ya kwake.
- Sisi wasikilizaji wa hotuba za viongozi, pia tuko wa aina mbalimbali, kuna baadhi yetu tumejaaliwa uwezo wa ziada, unaposikiliza hotuba ya kiongozi, unakuwa na jicho la rohoni na sikio la ndani, ambapo kiongozi akisoma hotuba aliyoandikiwa, lakini anayoyasoma hayatoki moyoni kwake, baadhi yetu tunajua!.
- Kiongozi anayesoma hotuba aliyoandikiwa, huku hayo anayoyasema, hayatoki moyoni, bali yanatoka mdomoni tuu, wenzetu wazungu wanaita kwa Kiingereza, “paying lip services”, kuna wanasiasa wengi wanatoa hotuba za kuandikiwa, au hata bila kuandikiwa, bali wanasema kile kitu watu wanachotaka kusikia, lakini hakitoki moyoni mwao!.
- Ndio maana kwenye mikutano mingi ya kampeni, wanasiasa, wanaahidi vitu vingi, vingine ni vya uongo, au hata vya kweli lakini havitekelezwi!.
- Mimi nikimuangalia Rais Samia, na kusikiliza kauli za Rais Samia katika hili la haki, kusema la ukweli kabisa, Rais Samia, ana nia ya dhati kutoka moyoni mwake kuhakikisha Watanzania wanatendewa haki.
- Kauli za Rais Samia kuhusu haki sio paying lip services, anamaanisha kabisa hicho anachoongea.
- Na kuna msemo “haki huinuia taifa”, hivi hiki anachokifanya Rais Samia kwenye utoaji wa haki Tanzania, Rais Samia ataliinua sana Taifa la Tanzania, hivyo atabarikiwa sana, na Tanzania itabarikiwa sana!.
Mungu Mbariki Rais wetu Samia
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali
Update
Hatimaye usaidizi huu, unakwenda kufanyika, kupitia kipindi cha TV kwenye kituo cha Channel Ten, kila siku za Jumapili Saa 3:00 usiku na marudio kila Jumatano saa 9:30 Alasiri.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=IXfA8sZkNPxpaeZn
Usikose kuangalia!.
P