DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 8,598
- 17,735
Nawasalimu Kwa jina la JMT...🇹🇿
Jana katika pita pita zangu nilikutana na Taarifa kutoka ikulu ikisema kuwa Rais amemteua Bw Hussein Massoro Kuwa balozi na kumuweka Balozi Ali Idi Siwa kuwa DG mpya TISS. (kongole kwake).
Japo jambo hilo lilizua mijadala mingi ikiwemo uwepo wa Tengua tengua Ya Wakurugenzi wa TISS kwa kipindi kifupi cha miaka mitano Ambapo mpaka sasa Wakurugenzi wapatao 3 tayari wamekwisha badilishwa, Na wengi wakahoji kuhusu Usalama wa Taarifa za kiulinzi za nchi na Kusema Huko TISS kuna siri gani Inayofanya kubadilishwa kwa Wakurugenzi mara kwa mara?.
Lakini Hilo sio swala kubwa Sana,kubwa ni kwamba Mama kwa kumteua Rt.DG kuwa Balozi, amepingana na sheria Ya usalama wa Taifa iliyopitishwa na Bunge mwaka July,2023 kifungu cha 6(6) Ambayo inatoa marufuku kwa Mkurugenzi wa TISS kuchaguliwa kushika nyadhifa yoyote ya kiutumishi katika sector yoyote ya Umma au nyadhifa yoyote ya kisiasa.
Au ilipotungwa sheria hiyo ilikuwa Tamu sehemu ya mamlaka ya TISS ila sehemu ya upande wa utawala haikuonekana?