Rais Magufuli: Wastaafu wengine hawachoki kusema, wanawashwa washwa

Watawala wa Afrika wana hulka ya kutunga Sheria ambazo zinakuja kuwaumiza wenyewe.
Wewe unakumbuka Bwana January Makamba alivyokuwa wa kwanza kushededea CYBER CRIMES ACT ???
Leo hii ile sheria ndiyo inamkanyaga kama mavumbi na kumuua kisiasa.


Africa iko maneno. Watu wanapokuwa katikati ya nguvu za kiutawala wanasahau yote. Sababu kubwa ni kuwa wako pale sio kuongoza ila kula na kushiba halafu kusaza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kushauri pia ni kuwashwa? Nauliza tu. Nahofia watu watakuwa wanakaa kimya hata mahali ambapo wangeweza kushauri, kwa kuhofia kuonekana wanawashwa.
 
Kwani kuwashwa washwa ni neno baya!? Nini hasa lengo lako kuandika hayo yote kunzungumzia Raisi wetu mpendwa!?
Unahitaji kujiongeza na ujicheke... na sio kuja kutafuta kiki humu
Natamani siku moja babako akwambie, "wewe binti unawashwawashwa" mbele za watu halafu utuambie utajisikiaje!
Kakosea tena sana kwasababu hao wastaafu wamemzidi umri na huenda akikutana nao huwaamkia shikamooni wastaafu!
Angenyamaza tu hata kama wayasemayo yanamkera. Anahitaji counseling tena mara mbili kw siku!
 
Uzi huu hauna lengo la kukashifu wala kuchochea,bali kutaka kujua tu orodha kamili ya kile alichokisema Mheshimiwa sana na mzalendo pekee kwa sasa katika Taifa hili.



Nanukuu sehemu ya hotuba yake ambayo ndio ilibeba dhima nzima ya hotuba yake leo Ikulu...."

"Hawa majaji ni waadilifu sana. Huwezi kumsikia jaji Chande anazungumza chochote au majaji wengine. Tofauti na wastaafu wa sehemu nyingine, wanawashwa washwa sana. Nawapongeza sana waheshimiwa majaji"

Najaribu kuwaza,kuwashwa huko anakokutaja mheshimiwa mtukufu sana ni kule kukosoa utawala wake ama muwasho wa wapi na kwa wakati gani?!

Benjamin Mkapa ambae haishi kuita Watanzania wajinga na wapumbavu ni sehemu ya wastaafu haowanaowashwa washwa?! Ama hahusiki kwa kuwa amekuwa akisifia utawala huu na kwa kuwa kama ni mhunzi basi alishiriki kuchonga kinyago cha sebuleni?!!

Dhana ya wanaowashwa washwa ni kwa wanaosifu utawala huu na raisi wake pia ama ni kwa wakosoaji tu?! Mfano raisi Mwinyi alisema anatamani Magufuli atawale milele,nae alikuwa anawashwa washwa?! Je ni kosa la jinai ama uhaini kuwashwa katika awamu hii?!!!

Watu wakisema raisi hashauriki na wala haambiliki na ukitoa maoni yako tarajiwa kushutumiwa ama kufunguliwa kesi kama za Lissu na ikibidi mitutu juu,ni kosa?!!!

Hotuba hizi za rasha rasha na jumla jumla,huandaliwa na muandishi wa hotuba wa raisi ama ni mahaba yake msemaji kadri imfaavyo?!! Kama ni maneno ya muandishi wa hotuba wa raisi,kwa nini nae asikamatwe na kufunguliwa kesi za uchochezi za kumchochea muongeaji mbele ya umma?! Kama hotuba hizi ni za msemaji mwenyewe,mwandishi wa hotuba wa raisi sio mtumishi hewa?!!

Huyu mshamba nchi imemshinda.

Uchaguzi mwingine msituletee mtu mshamba mshamba awe rais.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sijaona tatizo katika hiyo statement, ni kiswahili sahihi kabisa, elimu ni kitu muhimu sana sana ....Angeongea kwa lugha ya kiingereza angeonekana yupo sawa. Tatizo JFM kumejaa utitiri wa wahuni, lengo la awali la hii forum lilikuwa zuri tu, ndio maana hoja zenye akili wachangiaji ni wachache sana, Ndio maana kielimu Tanzania tunazidi kudidimia kwa kuendekeza tafsiri za kipumbavu. Kuna siku nilienda dukani kuulizia mayai tafsiri niliyopata nilibaki kusikitika sana, Ukweli Afrika hasahasa Tanzania tutaendelea kuwa watumwa kifikra... Hopeless kabisa
 
Kikwete:

fullsizerender_8-jpg.586465


Mwinyi:
Mwinyi: Nchi sasa inakwenda kama Gari bovu

img-20161014-wa0025-jpg.586466



Warioba
Jaji Warioba: Nchi imepoteza mwelekeo, inaendeshwa na matukio

Butiku:

Butiku: Rais tembo hatufai


Na JONAS MUSHI

DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, amesema kutokana na miiko iliyowekwa na mwasisi wa Taifa, Hayati Mwalimu Julias Nyerere, mtu yeyote anayekuwa rais wa nchi lazima atambue watu wote ni sawa na “usiwe wewe ni rais tembo.”

Hayo aliyasema jana wakati akiwasilisha mada ya miiko ya uongozi katika kongamano la kumbukizi ya Mwalimu Nyerere lililofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Alisema kwa mujibu wa Katiba ya TANU ya mwaka 1954 imani ya chama ilikuwa binadamu wote ni sawa, kila mtu anastahili heshima na kwamba kila raia ni sehemu ya Taifa.

Alisema nchi ambayo mwalimu aliijenga ilikuwa na misingi ya “binadamu wote ni ndugu zangu” na kwamba msimamo kama huo aliuweka hata alipotoka nje ya mipaka ya Tanzania.

“Tunachosema ni kwamba miiko ilikuwa inasema ukitaka kuwa rais utambue na uwe na imani kuwa watu wote ni sawa usiwe wewe ni tembo,” alisema Butiku na kuongeza:

“Lazima utambue kuwa unatokana nao (watu) na lazima kiongozi huyo atambue kuwa anaongoza watu hivyo anapaswa kuwaongoza kwa heshima.”

Akizungumzia miiko ya uongozi, Butiku alikumbusha hoja ya kutenga siasa na biashara ambayo alisema imeonekana kupuuzwa na viongozi katika miaka ya hivi karibuni.

Alisema miiko ya uongozi ilikuwa ni pamoja na kiongozi lazima awe mkulima au mfanyakazi na asishiriki katika shughuli zozote za ubepari.

Katika hilo aliwataka viongozi kuchagua ama kuwa kuwatumikia watu au kutafuta utajiri.

“Katika siasa za hivi sasa wanasiasa wote wanajitahidi sana kukataa kanuni hii na wamekuwa wakibabaisha. Msibabaishe,” alisisitiza Butiku.

Hawa bado hawajawa Wastaafu lakini si ajabu nao wanawashwa washwa

kinana


pole pole
 
Madaraka kweli baadhi huwalevya!

Kabla ya kuingia Ikulu alilijua neno unyenyekevu:



Baada ya kuingia Ikulu hata kabla ya miaka miwili kutimia ni matusi, vitisho, chuki, visasi vya kutisha! Neno unyenyekevu limepotea kinywani mwake! Kweli madaraka hulevya.



 
Back
Top Bottom