Rais Magufuli: Wastaafu wengine hawachoki kusema, wanawashwa washwa

Kwani kuwashwa washwa ni neno baya!? Nini hasa lengo lako kuandika hayo yote kunzungumzia Raisi wetu mpendwa!?
Unahitaji kujiongeza na ujicheke... na sio kuja kutafuta kiki humu
eti "rais wetu mpendwa" yupi huyo faru john ama
 
Kuna uzi mwingine ushaanzishwa toka mchana, nadhani mods muusogeze na huu kule.

Ahsante mkuu BAK.

Mi nawashwa na kunguni tu hapa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wacha waendelee kuwashwa mpaka kwenye makalio! Si walimpitisha wenyewe kwa majina ya mfukoni
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hii ya kuwashwawashwa ni kali. Ni juzi tu baadhi ya wastaafu walikuwa magogoni wakaambiwa msisite kutushauri. Je, huo nao siyo kuwafanya wawashwe?
Rais amesema wengi wana kwenda Ikulu na kumpa ushauri sio hao wengine ambao wanatoa ushauri kwenye majukwaa au vyombo vya habari!
 
Kwani kuwashwa washwa ni neno baya!? Nini hasa lengo lako kuandika hayo yote kunzungumzia Raisi wetu mpendwa!?
Unahitaji kujiongeza na ujicheke... na sio kuja kutafuta kiki humu
EATV redio jana wametangaza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja tu kumekuwepo na ongezeko kubwa la wagonjwa wa akili hapa nchini, kutoka watu laki sita hadi laki saba!
 
Rais amesema wengi wana kwenda Ikulu na kumpa ushauri sio hao wengine ambao wanatoa ushauri kwenye majukwaa au vyombo vya habari!
Kwahiyo awamu hii kutoa maoni kwenye vyombo vya habari ni kuwashwawashwa, unataka watu wote waende Ikulu kutoa ushauri? Haishangazi EATV redio jana wameripoti kuwa idadi ya watu wenye ugonjwa wa akili hapa nchini imeongezeka kwa kasi kubwa katika kipindi cha mwaka mmoja kutoka laki sita hadi laki saba!
 
Ni Sumaye na Lowassa, wameshiriki kuiharibu nchi kama wasaidizi wakuu wa Marais, leo eti na wenyewe wanajidai clean

Sent using Jamii Forums mobile app
Alipojiuzuru Lowasa nani alichukua mikoba PINDA alifanya nini kipindi chake kumshauri JK? Mkapa alipomteua Sumaye alifuata ushauri wake kama aliufuata mbona maneno yaliyokuwa yanamtoka kinywani S. hajawahi sikika akitoa neno lolote la matusi na kashfa? Tumia akili siyo mihemko.
 
Wastaafu wa mihimili mingine wanawashwa-washwa,lakini mahakama safi. Huwezi kumsikia jaji mstaafu akimsema aliyeko kwenye kiti.
Kuwashwa ni ugonjwa, kukuna/kukunwa ni hatua ya awali ya tiba. Bibi yangu alikuwa anatuagiza wajukuu kukuna mgongo wake uliomwasha kwa kitu cha moto/joto,kama jiwe.
 
YAANI kuna raha falni hivi kumpenda mzee JPM maana kila hotuba zake kuna kakionjo flani.
'Kakionjo flani' ni matusi au kashfa mkuu!

'Sikwenda ikulu kutafuta wachumba' ina maana kuna waliowahi kuwa pale kwa ajili ya wachumba.

'Wastaafu wengine hawachoki kuongea, wanawashwa washwa' ina maana kila mstaafu anaeongea hii kauli inamhusu, sio waziri mkuu wala rais!

Amepotoka bila shaka! Hapa ameharibu!
 
Huyu mzee sasa anakokwenda ni kubaya.....

Sasa yeye anataka kusikia tu wale watu wanamsifia tuuu.......

Akitokea mtu anayemwambia ukweli kuhusu mfumo wake wa utendaji ndani ya mfumo wa vyama vingi, anamuita anawashwawasha!

Hakika huyu Baba Jesca amatamani nchi iwe katika mfumo wa Chama kimoja, ila tu kaukuta tu mfumo hana uwezo wa kuubadilisha!
 
Back
Top Bottom