Rais Magufuli: Ole wake atakayeandamana, kama kuna baba zao wanawatuma, watakwenda kuwasimulia vizuri

Ninakumbuka siku kadhaa kabla walibya hawajaamua kumng'oa Muammar Gaddafi,kulikuwa na tetesi tu za watu kuandamana,Gaddafi alichimba mkwara mzito sana,ikiwemo kuwaita mende wataondamana,
"Ninatoa tahadhari kwa mende wanaokusudia kuandamana......"
Maweeee mende wakajaa barabarani,vifaru vya kijeshi vikaingizwa mtaani kupambana na mende,mende wakapata usaidizi kutoka Magharibi,mbabe aliyekuwa ikulu akatafuta mlango wa kuchomokea aachie ikulu,akakimbia kunusuru maisha yake,mende wakamzidi nguvu,mwishowe wakamkamata,wakamsokomezea miti njia yake ya haja kubwa,akauwawa kifo cha aibu.Vifaru,silaha za kivita,ndege za kijeshi na risasi lukuki hazikuweza kumnusuru na hasira ya umma!
Sishabikii wala kufurahia mauaji ya mzee Gaddafi,lakini najifunza jambo kubwa kwamba,sio kila jambo linaweza kumalizwa kwa vitisho vya kupiga watu risasi,au minguvu ya majeshi,kuna baadhi ya mambo yanaweza kumalizwa kwa kuzingatia mahitaji ya watu wako na kufanya mazungumzo chanya!
Uhuru Kenyatta kufanya mazungumzo na Raila Odinga na kuafikiana ni silaha kubwa zaidi ya kuinusuru nchi ya Kenya na machafuko ya kisiasa kuliko angewaambia "ole wenu munijaribu,mtaenda kuhadithia waliowatuma"
Baba usijawe na kiburi kwa kutazama ukubwa wa mizinga ya kijeshi,wingi wa risasi na mabomu,uwepo wa ndege za kivita katika makambi yetu ya majeshi,kwani hayo yote ni kwa ulinzi wa mipaka ya nchi yetu,si kwa ajili ya kuwashughulikia RAIA wa nchi yako!
Lakini kubwa zaidi ni kwamba hata waliojaribu kutumia nguvu kama unavyotishia kutumia nguvu,hawakufanikiwa!
Tujitafakari

this can happen anywhere in the world but not in Tanzania!!!!
Watanzania tunajifahamu wenyewe au tumeshika sana maandiko ya kwenye biblia!!
 
Hili ndilo jibu sahii.

Magufuli hajiamini. Wanaomzunguka hawaamini. Police hawaamini na usalama wa Taifa hauamini. Yeye anaamini wale tu aliopewa kumlinda toka Rwanda.

Hebu fikiria hii scenario sasa. Watu wameandamana kwa Amani, maelfu na maelfu. Vyombo vya habari vya ndan na nje vinaonesha live. Waandamanaji wamekaza kuwa magufuli atoke.

Magufuli kagma kutoka na kaenda kujificha huku akiagiza jesh la polce lisitishe maandamano. Mara jesh nalo likagoma au likashindwa kuzuia maandamano sababu yawingi wa watu au nao wakaogpa kuwashambulia waandamanaji maana ni hatari kwao na familia zao. Mawazir mara nao wakaanza kujiuzuru mmoja baada ya mwingne.

Mara CCM nao wakina pole pole wanamgeuka maana hata yy anajua CCM wenzake ni wengi tu wanamnafkia. Maandmano yakikaza nao wanaanza mgeuka maana unafiki ni asili yao.

Hapo mtamsikia magufuli kakimbilia Rwanda na hatorudi milele.

Hiki ndicho kinamuogopesha.
 
Hajaogopa kawaambia mfanye maandamano lakini mtarudi nyumbani na hadithi. Nachoona waandamaji wameaanza kuogopa.
 
mtu mwenyewe jina lake la kati lina wasifu wa kilevi ..halafu mnataka awe na akili timamu !!?

AU NA NYIE MMESHALEWESHWA NA HICHO KILEVI ...!!?
 
Tumrudie Mwenyezimungu na tufanye Ibada kwa dhati ya kutoka moyoni,na tuombe dua nzuri nzuri kama vile: MWENYEZIMUNGU tunakuomba UTUONESHE haki na tuifuate
MWENYEZIMUNGU tunakuomba UTUONESHE batwil na tuiache.
 
IMG_1520665335.342351.jpg
 
Tatizo si kuogopa bali kuonya kuepusha maafa yasiyo na lazima. Pengine watu hawajui maana ya kuandamana kumtoa Rais madarakani. Hili ni kosa la uhaini ....hakuna mwenye akili timamu anaweza hata kujihusisha! Pengine wapo wachache watafanywa mfano kabla hata ya hayo maandamano ili mjue nini mnakitaka. Malengo ya maandamano mnayoyataja ni uhaini mtupu na hakuna atakayewaunga mkono hata international communities ...bora mngeweka malengo ya kudai vitu kama katiba mpya lakini si kumtoa Rais ....mtajikuta matatizoni na kutesa familia zenu ....
 
this can happen anywhere in the world but not in Tanzania!!!!
Watanzania tunajifahamu wenyewe au tumeshika sana maandiko ya kwenye biblia!!
Uko sahihi Mkuu,lakini binadamu ni binadamu tu!
Kuna point hufikia thamani ya maisha yake ikitoweka ni mbaya sana!
Hatujawahi kufika huko kwa sababu hatujawahi pia kuwa compressed kwa kiasi cha kushindwa kupumua!
Kuna watu wana hasira sana sana sana,mfano waliovunjiwa nyumba zao wakakosa pa kuishi,halafu wanasikia sehemu fukani hawatakiwi kuvunjiwa hata kama walijenga kimakosa,unadhani waliovunjiwa wanajisikiaje mioyoni!!???)
Naamini hata maeneo mengine duniani,walidhani hayawezi kutokea,kwa uwezo wa nguvu zao kijeshi,kwani ingekuwa wanajua RAIA wao wana ujasiri basi wasingejaa kiburi cha kuwashughulikia raia wao kwa silaha za kivita!
 
Inakuwaje raisi wa nchi kubwa hii anatetemeshwa na maandamano kwenye mitandao hajiamini huyu lazima atakimbia siku wakiandamana
 
Anayaogopa kwasababu yana athari kubwa: hata kama hapa Tanzania hatutaandamana...diaspora wa kila nchi wataandamana kwenye balozi zao, hili litapelekea nchi hizo/UN kupitia marekanai na NATO kutuma wachunguzi kwa nguvu kama ilivyotokea Saudi Arabia...yaani hamna ile eti "hatutawaruhu wachunguzi huru wa kimataifa:....wanaingia by force na show utaielewa tuuu.
 
Back
Top Bottom