Makuku Rey
JF-Expert Member
- Dec 31, 2013
- 3,387
- 3,575
Ninakumbuka siku kadhaa kabla walibya hawajaamua kumng'oa Muammar Gaddafi,kulikuwa na tetesi tu za watu kuandamana,Gaddafi alichimba mkwara mzito sana,ikiwemo kuwaita mende wataondamana,
"Ninatoa tahadhari kwa mende wanaokusudia kuandamana......"
Maweeee mende wakajaa barabarani,vifaru vya kijeshi vikaingizwa mtaani kupambana na mende,mende wakapata usaidizi kutoka Magharibi,mbabe aliyekuwa ikulu akatafuta mlango wa kuchomokea aachie ikulu,akakimbia kunusuru maisha yake,mende wakamzidi nguvu,mwishowe wakamkamata,wakamsokomezea miti njia yake ya haja kubwa,akauwawa kifo cha aibu.Vifaru,silaha za kivita,ndege za kijeshi na risasi lukuki hazikuweza kumnusuru na hasira ya umma!
Sishabikii wala kufurahia mauaji ya mzee Gaddafi,lakini najifunza jambo kubwa kwamba,sio kila jambo linaweza kumalizwa kwa vitisho vya kupiga watu risasi,au minguvu ya majeshi,kuna baadhi ya mambo yanaweza kumalizwa kwa kuzingatia mahitaji ya watu wako na kufanya mazungumzo chanya!
Uhuru Kenyatta kufanya mazungumzo na Raila Odinga na kuafikiana ni silaha kubwa zaidi ya kuinusuru nchi ya Kenya na machafuko ya kisiasa kuliko angewaambia "ole wenu munijaribu,mtaenda kuhadithia waliowatuma"
Baba usijawe na kiburi kwa kutazama ukubwa wa mizinga ya kijeshi,wingi wa risasi na mabomu,uwepo wa ndege za kivita katika makambi yetu ya majeshi,kwani hayo yote ni kwa ulinzi wa mipaka ya nchi yetu,si kwa ajili ya kuwashughulikia RAIA wa nchi yako!
Lakini kubwa zaidi ni kwamba hata waliojaribu kutumia nguvu kama unavyotishia kutumia nguvu,hawakufanikiwa!
Tujitafakari
this can happen anywhere in the world but not in Tanzania!!!!
Watanzania tunajifahamu wenyewe au tumeshika sana maandiko ya kwenye biblia!!