Rais Magufuli ateua Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya za Tanzania Bara

Kwa wasiojua uwezo wa Rais wetu shauri yao
Mh JPM katika teuzi ametumia ajili zaidi ya tunavyodhani
Wengi wanaangalia UKada ila mkuu kaenda mbali zaidi,baada ya mashinikizo ya CCM kuwapa vijana ajira Rais ameamua kuwapa kazi makada wasio na uwezo nazo ili washindwe mapema Sana na ajivue kwenye lawama.
Wateule wengi watashindwa kazi mapema na watatumbuliwa hapo Rais hata kuwa kabisa na lawama kutoka CCM maana watakuwa wameshindwa wenyewe,kwa mfano
Ma DED watakapoenda kupeleka vyeti kuna watakaokimbia mchezo au kughushi vyeti(huu ni mtego mzuri)hapo watabainishwa kadhaa .jambo jingine ni katika kusimamia majukumu kuna watakao on a kazi ni ngumu na watajiengua na hii sasa itampa Rais kufanya teuzi ambazo Hana shinikizo nazo tena za ki siasa wala lawama
Wale ambao walikuwa hawajaelewa kinachoenda kutokea basi ni swala la muda tu wengi wataondoka bila Malipo na wengine watajiondoa kwa kushindwa na hawatakuwa na pa kudai wala kulaumu
Kama hukuuelewa mpango huu wa kisayansi basi tukutane baada ya mwaka mmoja kuanzia leo
 
Thermos ikipasuka yai lake huwa haina kazi
Nafasi za ukuu wa wilaya ni kama thermos iliyopasuka yai lake ni nafasi ya isiyokuwa na kazi(vaccum).Hali hii hupelekea wakuu wa wilaya kudandia treni kwa mbele na kufanya vituko vya ajabu,rejea mkuu wa wilaya ya Iringa,na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Moshi vijijini.
Kimsingi ofisi ya mkuu wa wilaya haiwezi kutatua tatizo lolote hata ikitokea bahati mbaya mwananchi akafikisha kero yake,Dc atalazimika kuipeleka Halimashauri maana ndio mamlaka halali,kisheria na kiutaratibu.DC ana vikao viwili vya kisheria yaani kikao cha ulinzi na usalama cha wilaya,na DCC yaani kamati ya ushauri ya wilaya.Vikao vyote viwili sio vya maamuzi bali mashauriano.
Halimashauri ndio mamlaka halali yenye vikao vya maamuzi,na maamuzi yake yanaweza kuhojiwa mahakamani,halimashauri inaweza kushtakiwa/kushtaki etc,halimashauri ina bajeti na ina uwezo wa kukusanya mapato yake,ikiwa ni pamoja na kujitungia sheria ndogo ndogo.

DC mpya wa Arusha mjini ameanza vibaya,hajui wajibu wake,na kimsingi anafanya kazi ya UKADA(inajulikana kuwa ni mjumbe wa kamati ya siasa ya ccm wilaya).Tangu amekuja Arusha amefanya matukio mawili ambayo yana ukakasi wa hali ya juu
#MOSI# alienda soko la Kilombero na kujifanya ameenda kutafuta kero za soko na baada ziara yake hiyo aliandika kwenye FB wall yake kuwa eti amekuta kero ya maji,na tatizo mikataba
#Usahihi
Kilombero hakuna tatizo la mikataba,jiji la Arusha chini ya CHADEMA imekuwa halimashauri pekee nchini ambako wamama na vijana kwenye masoko yetu wamepewa mikataba ya upangaji,na kodi wanalipa au benk au kwa njia ya electronic,yaani hata mtu mwenye kizimba/meza na mtaji wa 20,000 au hata asiyekuwa na mtaji ana mkataba ambao anaweza kuutumia kwenye taasisi za fedha ili kuongeza mtaji.
Kuhusu maji Halimashauri imelipia maji na hata kwenye vitengo nyeti kama nyama na samaki halimashauri imeweka sink za kisasa ili kudumisha afya za walaji
#PILI# Jana ameend kata ya Muriet na ameandika tena FB wall yake kuwa eti ameagiza Tanesco wamalize tatizo la umeme hadi kufikia Septemba
#Usahihi
Swala la umeme katika maeneo haya limeshafanyiwa kazi na Diwani wa kata ya Muriet pamoja na Meya wa Jiji tangu Januari na kazi hiyo ya kuweka umeme imeshaanza na tayari Tanesco wapo site wakianza na kata ya Sokoni 1.Leo dc kusema eti yeye ndio ameagiza ni wazi kuwa ni upotoshaji wa hali ya juu kwa malengo mabaya
#Hitimisho
Arusha ni ukanda huru ni mji wa watu wanaojitambua,na CHADEMA ndio Chama tawala hapa.
We have God we have the power
 
Mleta uzi ulichelewa wapi mpaka nafasi za uteuzi wa ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa, DAS ukakupita?sasa umeleta uzi ikiwa too late
 
Huu Ujinga Ulio uleta Hapa Kakwambia Mwenyewe Au Unamlisha Tu Maneno??
 
Kwa wasiojua uwezo wa Rais wetu shauri yao
Mh JPM katika teuzi ametumia ajili zaidi ya tunavyodhani
Wengi wanaangalia UKada ila mkuu kaenda mbali zaidi,baada ya mashinikizo ya CCM kuwapa vijana ajira Rais ameamua kuwapa kazi makada wasio na uwezo nazo ili washindwe mapema Sana na ajivue kwenye lawama.
Wateule wengi watashindwa kazi mapema na watatumbuliwa hapo Rais hata kuwa kabisa na lawama kutoka CCM maana watakuwa wameshindwa wenyewe,kwa mfano
Ma DED watakapoenda kupeleka vyeti kuna watakaokimbia mchezo au kughushi vyeti(huu ni mtego mzuri)hapo watabainishwa kadhaa .jambo jingine ni katika kusimamia majukumu kuna watakao on a kazi ni ngumu na watajiengua na hii sasa itampa Rais kufanya teuzi ambazo Hana shinikizo nazo tena za ki siasa wala lawama
Wale ambao walikuwa hawajaelewa kinachoenda kutokea basi ni swala la muda tu wengi wataondoka bila Malipo na wengine watajiondoa kwa kushindwa na hawatakuwa na pa kudai wala kulaumu
Kama hukuuelewa mpango huu wa kisayansi basi tukutane baada ya mwaka mmoja kuanzia leo
Lakini ukurugenzi ,RAS na DAS lakin hasa ukurugenzi ,si sehemu salama kufanyia majaribio hayo hasa kutokana na unyeti wa vyeo hivyo.
 
Tutasikia mengi sana. Kwani naona wengi walioteuliwa wapo kimkakati
 
Kwa hali tulionayo, tunafaa kuufanya uongozi kuwa moja ya majaribio kwa watu wasiostahili?
 
Hivi vetting inafanyika kabla ya kuteuliwa au baada ya kuteuliwa Hahahahahaahaa? Mleta mada Usiache watu Watumie maneno ya Kweli ambayo yataonekana unananihii taasisi ya uheshimiwa
 
Back
Top Bottom