Rais Magufuli apingwa, ni kuhusu kutumbua majipu

Taratibu, tutaona rangi halisi za wanafiki waliokuwa wanaimba mabadiliko.
Hivi mtu anayesimamia kitengo 'kilichopeteza' makontena 11,000 unamfanyaje? Unamuacha ofisi wakati uchunguzi unaendelea?
Watu waadhibiwe chini ya Sheria, kanuni na taratibu. Kuadhibu mtu kinyume cha Sheria kunaweza kusababisha uonevu wa kusingiziwa.
 
Watu waadhibiwe chini ya Sheria, kanuni na taratibu. Kuadhibu mtu kinyume cha Sheria kunaweza kusababisha uonevu wa kusingiziwa.

Mimi sijaona mtumishi ameachishwa kazi isipokuwa wanasimamishwa kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili na ndio sheria inataka hivyo. ikibainika hajahusika anarudi kazini sasa ulitaka aachwe aharibu ushahidi wote?
 
Je, Mamlaka za kinidhamu zimezingatiwa?

Tatizo sio kumsimamisha mtu kazi, tatizo ni ,Je, Mamlaka sahihi imetumika katika kumuwajibisha mkosaji?
 
Lissu ni jipu...hawezi kuunga mkono kampeni ya kutumbua majipu.Halafi si alisusia bunge huyu,karudi lini?
Lissu aliiaminisha dunia kuwa Lowassa ni mwizi yaani fisadi,lakini kashiriki kumsafisha,sasa unategemea anategemea ataunga mkono kumtumbua fisadi wakati anao mwenyewe na ndo wanaendesha maisha yake?
 
Lisu yuko sawa anachosema hakina tofauti na kile kichofanyangwa na wananchi kuwachoma moto watu kwa wizi yaani sheria ichukue mkondo wake badala ya kujichukulia sheria mkononi. isipokuwa ni watu wenye busara tu,kama kina gogo la shamba wanaoweza kuliona hilo si rahisi kwa watu wenye akili ya kiccm ccm
 
KAMBI Rasmi ya Upinzani imepinga tabia ya ‘kutumbua majipu’ inayofanywa na serikali ya Dk John Magufuli hivyo imewataka watumishi na watendaji wa umma waliosimamishwa au kufukuzwa kazi na mawaziri, kufungua mashauri Mahakama Kuu ya Tanzania ili kupinga kufukuzwa kwao na baadhi ya mawaziri.

Hayo yamesemwa leo katika hotuba ya maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.

Kwa mujibu wa hotuba hiyo, Lissu amesema kuwa baadhi ya mawaziri waliosimamisha na au kufukuza kazi watumishi wa umma kwa jina maarufu kutumbua majipu, walifanya maamuzi hayo kinyume cha sheria.

Ameongeza kuwa Mawaziri hao hawakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo kwa sababu hawajakasimishwa mamlaka ya utekekelezaji wa majukumu yao kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 5(1) cha utekelezaji wa majukumu ya kiuwaziri.

Kutokana na hali hiyo kambi ya upinzani imewataka watumishi wote ambao wametumbuliwa wana haki na uwezo wa kwenda mahakamani na kuomba mahakama kutengua utumbuaji wa majipu uliofanywa na mawaziri wasiokuwa na mamlaka hayo kinyume cha sheria.

“Kambi rasmi ya upinzani inaamini kuwa kwenda kwa watumishi hao mahakamani hakutawasaidia pekee kupata haki zao, bali pia kutakomesha vitendo vya kuendesha nchi kienyeji na bila kufuata sheria vinavyoelekea kushamiri chini ya utawala wa Rais John Pombe Magufuli,” amesema Lissu.

Mambo ya kipumbavu kabisa! Ni dalili ya kukosa sera zenye tija, awatetee waliotumbuliwa manispaa ya Ilala na Kinondoni pia
 
Tundu Lissu na timu yake wamechemka vibaya sana kwa kupinga utumbuaji majipu. Kweli Chadema sasa kwishney kabisa!
 
KAMBI Rasmi ya Upinzani imepinga tabia ya ‘kutumbua majipu’ inayofanywa na serikali ya Dk John Magufuli hivyo imewataka watumishi na watendaji wa umma waliosimamishwa au kufukuzwa kazi na mawaziri, kufungua mashauri Mahakama Kuu ya Tanzania ili kupinga kufukuzwa kwao na baadhi ya mawaziri.

Hayo yamesemwa leo katika hotuba ya maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.

Kwa mujibu wa hotuba hiyo, Lissu amesema kuwa baadhi ya mawaziri waliosimamisha na au kufukuza kazi watumishi wa umma kwa jina maarufu kutumbua majipu, walifanya maamuzi hayo kinyume cha sheria.

Ameongeza kuwa Mawaziri hao hawakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo kwa sababu hawajakasimishwa mamlaka ya utekekelezaji wa majukumu yao kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 5(1) cha utekelezaji wa majukumu ya kiuwaziri.

Kutokana na hali hiyo kambi ya upinzani imewataka watumishi wote ambao wametumbuliwa wana haki na uwezo wa kwenda mahakamani na kuomba mahakama kutengua utumbuaji wa majipu uliofanywa na mawaziri wasiokuwa na mamlaka hayo kinyume cha sheria.

“Kambi rasmi ya upinzani inaamini kuwa kwenda kwa watumishi hao mahakamani hakutawasaidia pekee kupata haki zao, bali pia kutakomesha vitendo vya kuendesha nchi kienyeji na bila kufuata sheria vinavyoelekea kushamiri chini ya utawala wa Rais John Pombe Magufuli,” amesema Lissu.

Nilidhani akina Lissu na wengine wa kambi yake walikuwa wanatetea maslahi mapana ya jamii kumbe kumba sasa wanajinasabisha kutetea wezi na wabadhirifu wa mali ya umma!...shameful!
 
Je, Mamlaka za kinidhamu zimezingatiwa?

Tatizo sio kumsimamisha mtu kazi, tatizo ni ,Je, Mamlaka sahihi imetumika katika kumuwajibisha mkosaji?

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mh.
Boniface Jacob mapema leo Mei 5.2016
ametangaza kuwasimamisha kazi kwa
watumishi wawili wa Manispaa ya
Kinondoni, akiweo Mwanasheria Mkuu
BW. Burton Mahenge na Mthamini wa
Manispaa Bw. Einhard Chidaga baada ya
Madiwani kuamua kwa kauli moja
kuwachukulia hatua hiyo. Vipi hii imekaaje kisheria meya au baraza la madiwani wana mamlaka ya kutimua mtumishi?
 
Watu wengi kutokana na upeo mdogo hawajui kuwa Lisu anaisaidia serikali. Kuna watu ni wahalifu, wamekiuka maadili ya kazi zao lakini wamefukuzwa na watu ambao kisheria hawana mamlaka ya kuwafukuza kwa sababu Rais, kisheria hajawapa madaraka hayo .

Hawa wanaoshangilia umbumbumbu, hawa watumishi wakienda mahakamani, wakarudishwa kazini na kulipwa mishahara yao wakati hawakuwa kazini, aibu na hasara itakuwa kwa nani? Itakuwa kwa Lisu au Magufuli na Mawaziri wake? Tutaishia kusema ooh majaji wamekula rushwa kumbe rushwa yenyewe ni umbumbumbu wa sheria.

Hii tabia ya kusifia kila kitu ndio hiyo iliyosababisha uchaguzi wa ZnZ kurudiwa kinyemela bila kufuata sheria zinasemaje. Kwa sasa watu wamenogewa kiasi kwamba wanaona ni sawa tu sheria kutokufuatwa. Ila mtu huyo huyo atakapoona anaweza kufanya chochote bila kufuata sheria na hakuna anayehoji wala kukaripia atafanya jambo baya na asiwepo wa kuhoji. Sintoshangaa huko mbeleni akagomea kutoka madarakani muda wake ukiisha kisa anasifiwa.
 
Wewe waache ili waje wapoteze kura nyingi zaidi 2020...wapinzani wako mtegoni, kwa hakika ule usemi 'wataisoma namba' unatimia. wapinzani wataupoteza umma....

Hicho kitisho eti wapinzani watapoteza kura hiyo 2020 ni kama cha kitoto hivi. Katika mazingira haya ya ushindani ambapo mwenyekiti wa ccm ndiye anayechangua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi unategemea mpinzani atangazwe? Kumbuka jeshi na jeshi la polisi zote zinajiona ni taasisi za ccm kiasi kwamba wanahakikisha lazima ccm ishinde. Hivyo eti kwamba wapinzani watapoteza kura hiyo 2020 sio kwa kigezo cha ccm kukubalika bali ni kwa aina ya ushindani na mazingira ya dola kuwa upande wa ccm. Kwa hiyo kwa mtazamo wako ili wapinzani wakubalike ni lazima wakubaliane na kumsupport rais hata kama hafuati sheria za nchi!!?
 
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mh.
Boniface Jacob mapema leo Mei 5.2016
ametangaza kuwasimamisha kazi kwa
watumishi wawili wa Manispaa ya
Kinondoni, akiweo Mwanasheria Mkuu
BW. Burton Mahenge na Mthamini wa
Manispaa Bw. Einhard Chidaga baada ya
Madiwani kuamua kwa kauli moja
kuwachukulia hatua hiyo. Vipi hii imekaaje kisheria meya au baraza la madiwani wana mamlaka ya kutimua mtumishi?
Mbona rahisi uamuzi wa halmashauri utafuatia mamalaka za uteuzi kulipima na kuzitolea maamuzi kwa taratibu na sheria za utmishi wao
 
Kuna baadhi ya mambo ungeniambia yanawezekana kutokea ningepinga. Kama wanasheria wanaamini hili watoe mwaliko kuwasaidia waliowajibishwa kupata haki zao. Wafanye kazi hiyo pro bono tuamini kweli wanataka kuwatetea.

Siku hizi toka umejiingiza kwenye ushabiki wa kiitikadi umepoteza heshima yako uliyojijengea kwa muda mrefu hapa jukwaani. Nadhani kila kitu kiko wazi kabisa, kutumbua majipu ni sawa kabisa, ila utumbuaji huo ufuate sheria. Kitendo cha kuruhusu kutumbua majipu bila kufuata sheria kunaweza kuleta shida huko mbele ya safari.
 
hapo hajatetea ufisadi sheria imezingatiwa? kesi nyingi serikali inashindwa kufuatana na ukurupukaji huu mwisho wa siku wanaanza kusingiziwa mahakimu mana kesi zinakuwa zishaharibika toka huko chini.
 
Taratibu, tutaona rangi halisi za wanafiki waliokuwa wanaimba mabadiliko.
Hivi mtu anayesimamia kitengo 'kilichopeteza' makontena 11,000 unamfanyaje? Unamuacha ofisi wakati uchunguzi unaendelea?

Ungetafakari usingepata tabu ya kutokumfahamu Lissu., Lissu hapa anachokisema ni kwamba hii nchi tulikubali tuwende kwa mujibu wa katiba na sheria hivyo amejaribu kueleza mipaka ya hawa mawaziri na wakuu wa mikoa ama Wilaya kisheria hawapaswi kutumbua labda nilivyomfahamu mimi ni kuna chombo ama taasisi maalum kisheria ndio inapaswa kufanya hiyo kazi ya kutumbua. Ndivyo ambavyo nimemuelewa na si kwamba CHADEMA inaunga mkono ufisadi la yeye Ameelezea kisheria zaidi.
 
Back
Top Bottom