Rais Magufuli apingwa, ni kuhusu kutumbua majipu

maana kizungu zungu tu sijui upinzani wanaitaji mabadiliko gani sasa maana hizo ni akili za ndugu wa mume au mtoto wa kambo kila kitu unaonewa tu #michezo huu auitaji hasira kabisa
 
Nashangazwa hasa na wote wanaombeza Lissu. Hivi hamuoni kinachofanywa na rais kwa kuivunja hiyo sheria? Ni wapi uliwahi kuajiriwa bila kupewa job description? Na akiachwa bila kukumbushwa yakitokea mabaya zaidi mtakuja hapa kusifu? Hao mafisadi yalipokuwa yanafisidi ccm haikuwepo wala ninyi mnaoshangilia sasa mlikuwa bado kuzaliwa? Afuate sheria zilizopo hata kama zinambana ili baadae aandae utaratibu wa kuzirekebisha. Lissu wape darasa hao buku 7 wa lumumba na wawinda ukuu wa wilaya. Si mmeona hata naibu waziri wa maji alikuwa anambwera mimbarini? Jipangeni.
 
Mpaka sasa upinzani umepwaya sana maana hivi karibuni walisema JPM anafanya waliyokuwa wanataka Leo wamegeuka tena duuuuu! Kwaheri lisu
Walitaka kuyafanya bila kukiuka sheria za nchi, kama kweli Ni mtumbuaji angemtumbua kwanza mwenyekiti wake wa ccm na katibu mkuu wake kwa ufisadi ujangili uliokubuhu
 
Taratibu, tutaona rangi halisi za wanafiki waliokuwa wanaimba mabadiliko.
Hivi mtu anayesimamia kitengo 'kilichopeteza' makontena 11,000 unamfanyaje? Unamuacha ofisi wakati uchunguzi unaendelea?
Hapa tusiongee kishabiki. Tatizo hapa siyo mtu kusimamishwa bali amesimamishwa kwa kufuata sheria na taratibu za ajira yake? Kiutaratibu aliyekuajiri ndiye mwenye mamlaka ya kukusimamisha au kukufukuza kazi. Kuna watu ni wateule wa Rais, hao anaweza kuwasimamisha kwa kufuata taratibu za ajira zao. Kuna watu ni waajiriwa wa mamlaka tofauti na Rais hawawezi kusimamishwa na Rais au Waziri lakini Rais au Waziri ana mamlaka ya kuziagiza mamlaka zinazohusika kuwasimamisha, na mamlaka hizo zitatekeleza agizo la Rais au Waziri kwa kadiri ya sheria na kanuni.

Mfano mzuri ni jeshi la Polisi, Rais alisema askari aliyemwadhibu dereva wa mke wa Waziri apandishwe cheo lakini IGP anasema watatekeleza agizo hilo kwanza kwa kumpeleka askari mafunzoni, siyo kumbandika tu tepe kienyeji eti kwa sababu Rais kaagiza.

Kuna wahalifu kama wauaji, wengine hukamatwa kukiwa na ushahidi wote lakini hatujasikia kwa sababu ushahidi upo basi muuaji huyo anyongwe hapo hapo.
 
Nimecheka mpaka basi. Hivi hawa watu mbona wanapenda sana kuhama na biti? Wao si ndio waliokuwa wakisema watu hawachukuliwi hatua na utawala uliopita? Wao si ndio waliojibainisha kama chama cha wapigania haki na kupambana na ibadhirifu? Leo wanasema mambo gani tena? Unataka kuniambia mtu alieiba makontena maelfu umwache aendelee na kazi huku unajua kuna kosa limefanyika chini ya usimamizi wake? Mtu ana watumishi hewa wengi, bado usihoji au kupitisha uchunguzi? Inaingia akilini kweli?
 
Hata kama unatenda jambo jema namna gani, sheria na taratibu ni lazima vifuatwe. Tusishangilie utawala holela. Wahalifu waadhibiwe, watuhumiwa wasimamishwe ili kupisha uchunguzi lakini yote yafanyike kwa kufuata sheria za nchi na kanuni za ajira. Tusipofanya hivyo kuna watu wanaweza kuonewa pia. Sheria na kanuni huwekwa ili kulinda haki ya kila raia. Hata mfungwa naye ana haki zake.
 
Taratibu, tutaona rangi halisi za wanafiki waliokuwa wanaimba mabadiliko.
Hivi mtu anayesimamia kitengo 'kilichopeteza' makontena 11,000 unamfanyaje? Unamuacha ofisi wakati uchunguzi unaendelea?
HATUKUHUBIRI mabadiliko ya KUWANYANYASA watumishi wa umma.
 
Hata kama unatenda jambo jema namna gani, sheria na taratibu ni lazima vifuatwe. Tusishangilie utawala holela. Wahalifu waadhibiwe, watuhumiwa wasimamishwe ili kupisha uchunguzi lakini yote yafanyike kwa kufuata sheria za nchi na kanuni za ajira. Tusipofanya hivyo kuna watu wanaweza kuonewa pia. Sheria na kanuni huwekwa ili kulinda haki ya kila raia. Hata mfungwa naye ana haki zake.
Sawa. Sasa ni kipi ambacho mnataka? Unaweza kuzitaja sheria zilizovunjwa wakati wa kuwasimamisha? Unadhani hayo maamuzi ya kuwasimamisha hayafanyiwi uchunguzi wa kitaalamu kwa kuzingatia sheria stahiki kwa ushauri wa kitaalamu?
Unamchunguza mtu vipi wakati akiendelea na kazi? Je akiingilia ushahidi?
 
Atumbue kwa kufuata sheria otherwise kwa design hii yake atakuja kujikuta serikali ndiyo inapoteza.
 
Hamjamwelew lissu,sio level yenu mpaka muelewe!Ninyi mmeshazoea porojo,mnakuja na mihemko bila kujua lissu alichozungumza!
Kiufupi kwa kuwatafunia ili muelewe,lissu hajapinga utumbuaji wa Magufuli.Amepinga utumbuaji unaofanywa na mawaziri wake kwani kisheria maamuzi yoyote yanayofanywa na mawaziri wake ni batili.Hii inatokana na matakwa ya kikatiba yanayomtaka Rais kukasimisha madaraka kwa mawaziri wake,yaani instrument!Na sheria inataka gazeti la serikali lichapishe mgawanyo wa kazi wa mawaziri!Na huu mgawanyo unategemea rais na rais,sio wa kudumu!
Lissu ni waziri kivuli wa sheria na katiba,akifumbia macho huu ukiukwaji wa katiba si ni aibu kwa taaluma yake!
Amewashukia washauri wa serikali kwa kushindwa kumshjauri rais kuwapa instrument mawaziri ili basi utumbuaji wao uwe halali kisheria na kikatiba!
Ni kweli hawa watu wakienda mahakamani wakadai kuwajibishwa na watu ambao hawajapewa mamlaka na Rais kisheria wana strong case na wanaweza kushinda!
Msipende kukurupuka na kuendeshwa kwa hisia,nchi hii lazima tuheshimu sheria na kanuni ndio tuweze kusonga mbele!
Watu wengi kutokana na upeo mdogo hawajui kuwa Lisu anaisaidia serikali. Kuna watu ni wahalifu, wamekiuka maadili ya kazi zao lakini wamefukuzwa na watu ambao kisheria hawana mamlaka ya kuwafukuza kwa sababu Rais, kisheria hajawapa madaraka hayo .

Hawa wanaoshangilia umbumbumbu, hawa watumishi wakienda mahakamani, wakarudishwa kazini na kulipwa mishahara yao wakati hawakuwa kazini, aibu na hasara itakuwa kwa nani? Itakuwa kwa Lisu au Magufuli na Mawaziri wake? Tutaishia kusema ooh majaji wamekula rushwa kumbe rushwa yenyewe ni umbumbumbu wa sheria.
 
Atumbue kwa kufuata sheria otherwise kwa design hii yake atakuja kujikuta serikali ndiyo inapoteza.
Taratibu zipi zimewekwa kwa ajili ya kutumbua majipu?

Mwl alipokuwa anadai watumishi wa serkali wasiwe wafanyabiashaya alikuwa anakwepa haya majipu. Sasa mawaziri wengi wanamiliki makampuni ya biashara n.k tutegemee kumpata yupi wa kutetea wasio nacho?
 
Lissu hawezi kuwa msimamizi wa good governance na wala hana moral autherity kujadili anathing remotely kinachofanana na good governance. Lissu is on record akiwaambia Watanzania kuwa yeye ndiye aliyeandaa list of shame. Kwa maana hiyo yeye ndiye mwanzilishi wa kampeni ya kumtangaza Lowassa kuwa fisadi. Kwa miaka nane (8) ameongoza kampeni hiyo akiimba kuwa Lowassa ni fisadi lakini ghalfa akaanza kuzunguka na Lowassa nchi nzima akitaka wananchi wamchague awe rais.

Kama kweli Lissu anasimamia good governance kama unavyodai aeleze ni kwanini 'alimchafua' Lowassa kuwa ni fisadi? Anaamini Lowassa ni fisadi au ni msafi? Kama ni fisadi, kwanini alitaka wananchi wamchague mtu ambaye anaamini hana sifa? Na kama sio fisadi kwanini alimchafulia jina Mzee wa watu?, na lini amemuomba msamahama Lowassa kwa kosa hilo au lini amewaomba Watanzania radhi kwa kuwadanganya miaka 8?

Na kwa historia hiyo ya Lissu kubadili gia angani, nani ana uhakika hata kwenye hili la 'good governance' hatobadili gia angani? Mtu akisema Lissu ana ndimi mbili atakuwa anamuonea?

Hizo ndio dynamics za siasa mazee! A week in politics is like a decade; let alone 8 years unazosema na unakotaka tubakie! We have moved on bro! Lissu anabaki na haki yake ya kikatiba kuangalia na kujadili mustakabali wa taifa "as is today"; without prejudice kwamba jana katika swala jingine alikuwa na msimamo gani?! Maisha hayagandi; you can not hold Lissu hostage kuhusu "ya kale", ilhali hata EL mwenyewe unayemtetea alishahama huko na ndio maana alikubali kuzunguka na Lissu kwenye kampeni; sembuse wewe?! Waliyazungumza wakayaweka into proper perspective, Dr Mihogo yakamshinda akabwaga manyanga wenzie wanasonga mbele.
 
Nashangazwa hasa na wote wanaombeza Lissu. Hivi hamuoni kinachofanywa na rais kwa kuivunja hiyo sheria? Ni wapi uliwahi kuajiriwa bila kupewa job description? Na akiachwa bila kukumbushwa yakitokea mabaya zaidi mtakuja hapa kusifu? Hao mafisadi yalipokuwa yanafisidi ccm haikuwepo wala ninyi mnaoshangilia sasa mlikuwa bado kuzaliwa? Afuate sheria zilizopo hata kama zinambana ili baadae aandae utaratibu wa kuzirekebisha. Lissu wape darasa hao buku 7 wa lumumba na wawinda ukuu wa wilaya. Si mmeona hata naibu waziri wa maji alikuwa anambwera mimbarini? Jipangeni.
umesikia meya wa kinondoni alichofanya muulize lisu atoe maoni yake
 
Sawa. Sasa ni kipi ambacho mnataka? Unaweza kuzitaja sheria zilizovunjwa wakati wa kuwasimamisha? Unadhani hayo maamuzi ya kuwasimamisha hayafanyiwi uchunguzi wa kitaalamu kwa kuzingatia sheria stahiki kwa ushauri wa kitaalamu?
Unamchunguza mtu vipi wakati akiendelea na kazi? Je akiingilia ushahidi?
Bado unarudia kitu nilichokwishasema. Hakuna anayekataa watumishi wenye tuhuma kusimamishwa kazi wakati wa uchunguzi wa tuhuma zao. Watumishi kama wana tuhuma wangeweza kusimamishwa na mawaziri lakini kwa sababu Rais Magufuli tangu aingie madarakani hajatoa tangazo 'instrument' ya kukasimisha mamlaka yake kwa Mawaziri, Mawaziri hao kisheria wanakuwa hawana mamlaka hayo. Hili ni kosa la Mwanasheria Mkuu kushindwa kumwongoza Rais katika masuala ya kisheria.

Kama ni mkristo mkatoliki, hii ni sawa sawa kuwa na shemasi. Shemasi anaweza kufanya karibia mambo yote, na anajua mambo yote anayotakiwa kuyajua padre lakini kuna baadhi ya mambo hawezi kufanya kwa sababu tu hajawekwa wakfu, anapowekwa wakfu inatafsiriwa kuwa amekasimiwa mamlaka yale aliyopewa Petro na Kristo .
 
Sidhani kama mtoa mada amemuelewa Lissu,kwenye hoja zake amejikita kwenye sheria kwamba mwisho wa siku akitokea aliyetumbuliwa akaenda mahkamani basi ataishinda serikali na hapo kuamriwa kumlipa mtu aliyekwapua mali za serikali.

Ndiyo sababu anajikita kwenye kutumia sheria za nchi ili kuondokana na uwezo wa serikali kushtakiwa.Tusiwe kama majuha kwamba kila Rais au Watawala wakifanyacho ni sahihi!Kuna issue za Katiba na sheria za nchi,hata rais hayupo juu ya sheria.Nyie CCMizi mzipoteze maana ya ujumbe.

Kajikiteni kwenye issu ya kiti cha Enzi cha Chama cha Majipu
Bahati nzuri hotoba yote ya Lissu ipo humu Jf.
Lissu katika hotuba yake alikuwa anapigania utawala wa kisheria. Sasa unapokuja na kunyofoa mistari michache toka katika hotuba ya Lissu ili kutetea unachokitaka unajidhwlilisha.
Ushabiki wa bure kwenu Lumumba, "Lissu ni kama msaafu au Biblia kwenu, na pasipo kumsoma/kumnukuu kwa mapana yake hamtoweza kumwelewa na zaidi mtachanganyikiwa
Mpaka sasa upinzani umepwaya sana maana hivi karibuni walisema JPM anafanya waliyokuwa wanataka Leo wamegeuka tena duuuuu! Kwaheri lisu
Akili ndogo yeyote haiwezi kuelewa philosophical presentation! Lissu kaongea na wenye akili kubwa, punguani yeyote hawezi kuelewa maudhui!
 
Bahati nzuri hotoba yote ya Lissu ipo humu Jf.
Lissu katika hotuba yake alikuwa anapigania utawala wa kisheria. Sasa unapokuja na kunyofoa mistari michache toka katika hotuba ya Lissu ili kutetea unachokitaka unajidhwlilisha.
Ushabiki wa bure kwenu Lumumba, "Lissu ni kama msaafu au Biblia kwenu, na pasipo kumsoma/kumnukuu kwa mapana yake hamtoweza kumwelewa na zaidi mtachanganyikiwa
wewe wacha kufananisha vitabu vitakatifu na mambo yakijinga
 
Taratibu, tutaona rangi halisi za wanafiki waliokuwa wanaimba mabadiliko.
Hivi mtu anayesimamia kitengo 'kilichopeteza' makontena 11,000 unamfanyaje? Unamuacha ofisi wakati uchunguzi unaendelea?

Wewe waache ili waje wapoteze kura nyingi zaidi 2020...wapinzani wako mtegoni, kwa hakika ule usemi 'wataisoma namba' unatimia. wapinzani wataupoteza umma....
 
Back
Top Bottom