Rais Kikwete: Nchi iko salama, atakaye jaribu atakiona cha mtema kuni

Mkuu Coalition yetu bado hujaiona tu? Hujasikia kemeo toka kwa Obama? Hiyo ni coalition tosha. Pia usidhani kwamba Museni yupo saaaana na Kagame. Majeshi ya nchi hizi mbili yalishapimana nguvu wakati wakigombea utajiri wa Congo. Kagame alionyesha kutomsikiliza mentor wake akamuonyesha kiburi hadi majeshi yao kupigana. M7 akipata nafasi tu ata revenge! Urafiki wao ni wa mashaka. Ndani ya Rwanda kuna kutoridhika kwingi. Wafuasi wa Ingabire na Nyamwasa nao wanatafuta opportunity, FDLR nao wapo! Mzee tusiende huko. Kagame atulie tu amalize uongozi wake kwa amani kisha apumzike asitake kuleta mbungi.
Anaweza kutumia terrorism halafu kukawa hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kumuhusisha,tutamvamia?
 
acha povu wewe.
Hivi unadhan adui akija tz na kukumbana na ndugu na jamaa wa familia za Mwangosi, waliouwawa soweto Arusha, waliouwawa kwenye maadamano ya Arusha tar 5, na wote wanaouwawa hovyo mitaani ,migodin,police stations etc na wote wanaoguswa na vifo vya watu hao hawatamsaidia kuwaficha, na kumpa habar mbalimbal juu ya tz na mwishowe unadhan kitatokea nn?
Jitahid kuwaza nje ya box japo najua shida ni kuwa unatumika.badilika bwana
vita ikiingia hataulizwa wewe ni dadake mwangosi, wala chadema kombora la kagame halitachagua...jitambue
 
Achana na ujambazi wa misitu ya Kimisi, Kasindaga na Burigi! Polisi si jeshi.

Vita si nzuri ndio maana JK akamshauri Kagame aongee na watu wake ili vita iishe na kuleta amani eneo hili la maziwa makuu. Badala ya Kagame kufanyia kazi huo ushauri yeye anaanza kuleta za kuleta. Utadream vipi dialogue huku mtu anakutukana na kukutishia. Ningekuwa mimi ndio amiri jeshi sasa hivi nimngetangaza jeshi kuwa katika high alert waziwazi.

Hawa wanafananisha vijana wa Mwamunyange na vijana wa Kova!!
 
Safi JK atakayejaribu atakoma.

Laiti ungejua gharama ya kuingia vitani ilivyo kubwa, usingeyasema haya.
Usinge shabikia vita. Ungeapa kukwepa vita kwa namna zote.

Ni aibu kubwa majirani zetu wameshaungana na wametuacha mchana kweupe pasipo kujificha.
Katika vikao viwili tu, wamesha kubaliana vitu maana vya kufanya ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa. Sisi tunapo hangaika kujibizana hapa, wao wanaweka mikakati ya kutafuta pesa za ujenzi wa hiyo reli.

Badala ya kuulalamikia uongozi wetu na kuutaka utoe maelezo ya kueleweka ya kwanini tuachwe na majirani zetu katika shughuli za kimaendeleo, ile hali tukijua kuwa tumegharamia kiasi kikubwa cha fedha ili kuufufua umoja wetu, tunazungumzia vita!

Eh Mungu tunusuru.
 
Jana nilikuwa naagalia Citizen TV ya kenya na taarifa zilisema kuwa Maraisi wa Kenya, Rwanda na Uganda wamekubaliana kujenga reli ya kisasa kutoka Mombasa, kupitia Nairobi kisha Uganda na halafu kutua Rwanda. Kagame anahangaika na maendeleo ya watu wake, JK wetu anatoa vitisho visivyo na maslahi kwa Taifa. Ajue tu kuwa vita kati yetu na Idd Amin ilitosha, hatutaki vita tena. Jenga reli toka Dar mpaka Kigali acha mbwe mbwe za majeshi.
Mkuu hizo ni mbinu za M7 na PK wanafikili wakisema wana mipango kabambe ya kujenga reli basi hilo tu litaifanya Tanzania ishituke na kujihingiza kichwa kichwa kwenye fast track za federation hisiyo na kichwa wala miguu, hawa jamaa wako obsessed na kutaka kutawala watu wengine - hidden agenda zao hizo walikuwa nazo muda mrefu tu. Watu wamesahau kwamba Mh.M7 aliwahi kutamuka anataka kuwa RAIS wa kwanza wa EAST AFRICA! Mh.Kenyatta halijui hilo, Kenyatta wanamtumia tu kwenye mbinu za kutaka kuonyesha kwamba Tanzania inatengwa ili tijisikie vibaya - mambo ya kitoto tu. Ukweli wa mambo si Uganda wala Kigali inaweza ku-afford kuipuuza Tanzania, bandari ya DSM hiko karibu kwa nchi zote mbili uwezi kulazimisha wafanya biashara kuingia gharama zisizo za lazima kutokana na tofauti za siasa, wafanya biashara makini hawa mix politics na business. Kitu kingine kinacho shangaza! Ni juzi juzi tu Rwanda imekaribishwa kwenye kundi la EA lakini imekwisha anza kuwa overly VOCAL na kijitia kimbele mbele kukosea hili na lile as if walio watangulia hawana akili; kuendelea kushirikiana na jamaa hawa ambao bado wako chini ya Administration Kigali ya sasa hivi ni ngumu - muda wote kijisifia kwamba wana PANADOL ya matatizo yote Duniani na kuwasema sema viongozi wenzao vibaya, Oh yes Rwanda iliwahi kutamka bila aibu kwamba kiongozi wao akipewa bandari ya DSM anaweza kuiendesha kwa ufanisi!!
 
Mkuu hizo ni mbinu za M7 na PK wanafikili Tanzania wakisema wana mipango hiyo basi Tanzania itashituka na kujihingiza kichwa kichwa kwenye fasta track za federation hisiyo na kichwa wala miguu, hawa jamaa wako obsessed na kutaka kutawala watu wengine na hilo walikuwa nalo muda mrefu tu watu wamesahau kwamba Mh.M7 aliwahi kutamuka anataka kuwa RAIS wa kwanza wa EAST AFRICA! Mh.Kenyatta analijuI hilo pale wanamtumia tu kama mbinu za kutaka kuonyesha kwamba Tanzania inatengwa - mambo ya kitoto tu. Ukweli wa mambo si Uganda wala Kigali inaweza ku-afford kuipuuza Tanzania, bandari ya DSM hiko karibu kwa nchi zote mbili uwezi kulazimisha wafanya biashara kuingia gharama zisizo za lazima kutokana na mambo ya siasa, wafanya biashara makini hawa mix politics na business. Kitu kingine kinacho shangaza ni juzi juzi tu Rwanda imekaribishwa kwenye kundi la EA lakini imekwisha anza kuwa overly VOCAL na kijitia kimbele mbele kukosea hili na lile as if walio watangulia hawana akili, kushirikiana na jamaa hawa ambao wako chini ya Administration ya sasa hivi "know all" watatuvuruga sana.
Ukiamua kufanya biashara na mtusi lazima na wewe uwe kwanza kama mtusi. Hawa jamaa ni untrustworthy and unreliable.

HaihitajiI hata kuchimba zaidi kupata uhakika wa maneno yangu. Mimi nilifahamu kuwa baada ya tarehe 1July 2007, EAC ilikuwa tayari imeishapoteza malengo na matarajio yake kwa wananchi wapenda amani, maendeleo na ukweli. Six years now, niliyokuwa napatwa wasiwasi nayo yameisha anza kujitokeza. I'm sorry lakini huu ndiyo ukweli.
 
Nani kakwambia kazi ya jeshi ni kulinda Twiga? Kwani TANAPA wanakazi gani? Umechanganya mada mkuu.

ndege ya vita ya nchi nyingine kutua kwenye ardhi ya tz bila taarifa na kuondoka bila kukamatwa inamaanisha jeshi la tz halina uwezo wowote waz kulinda mipaka yetu.
 
jmushi1,Atakuwa amepata tetesi kwamba nchi inataka kuvamiwa?

Kwasababu hata huo mfano wa vita dhidi ya Idi Amini ilikuwa ni kutokana na uvamizi.
Mkuu hata Nyerere na Iddi Amini yalianza hivihivi mara kuwe na tuhuma za Amini kufanya vikao vya siri na Kenyatta mara Nyerere aseme hawezi kaa meza moja na muuaji mara EAC kuvunjika mara Uganda wamevamia Tanzania,tena kwenye those recent years Nyerere katoka kuwapiga mkwara kina Kamuzu Banda kuhusu mipaka ya Ziwa Nyasa kama ilivyo saa hizi,so HISTORIA INAJIRUDIA SEMA THIS TIME ITS RWANDA,...hata matusi ya KAGAME KWA KIKWETE NYERERE ALIYAPATA TOKA KWA AMINI NA WATU WAKADHANI NI BIFU ZAO BINAFSI KUMBE HADI NCHI ZINAHUSIKA,cha muhimu serikali iwe makini saaana na wananchi tumwombe MUNGU sana kwasababu any great civilization always start to fall from within ALL GREAT POWERS HUWA ZINA COLLAPSE AFTER BEING CORRUPT FOR A LONG TIME
 
Laiti ungejua gharama ya kuingia vitani ilivyo kubwa, usingeyasema haya.
Usinge shabikia vita. Ungeapa kukwepa vita kwa namna zote.

Eh Mungu tunusuru.

Duh! kuna hoja zingine humu ni tabu kujua kama mtu yuko serious au anafanya comedy show.

1. Ni kweli; gharama za vita kubwa, lakini ni kubwa "both ways" kwetu sisi na kwao wao akina kagame. Hatutwendi vitani kama kumchokoza mtu, tunakwenda vitani kulinda nchi yetu.

2. Kwa saizi ya uchumi wetu, na saidi ya uchumi wa Rwanda; wao wanyarwanda ndiyo wanaotakiwa kuogopa gharama za vita zaidi kuliko sisi. Ukizingatia wao hawana bandari, lazima bidhaa zao zipitie kenya na Uganda ili zifike kwao. Wakati wa vita mfumuko wa bei utakaotokea Rwanda utatosha kuwafanya Wanyarwanda wamgeuke kaagame.

3. Kwa wale wanaosema bora rais wetu angekuwa kama Kagame. Kuwa makini na unachokisema. Hakuna Mnyarwanda hata mmoja anayejua lini Kagame ataondoka madarakani. Sisi tunajua ni lini urais wa JK utafikia mwisho. Mfumo wetu wa demokrasia yetu changa unatuwezesha kubadilisha rais kila baada ya miaka mitano. Rwanda hawana mfumo huo kwa sababu kagame hawezi kuruhusu mfumo huo.

4. Hakuna nchi ambayo viongozi wake wote wanakuwa "great". Nchi haipigi hatua kwa kuwa na "viongozi imara", bali hupiga hatua kwa kuwa na "taasisi imara". viongozi wanakuja na kuondoka. Taasisi ziko pale pale. Hata mataifa makubwa kama marekani, chna na urusi; siyo kwamba kila siku wanakuwa na viongozi imara. Mfano rahisi ni Jimmy Carter wa marekani. Alikuwa rais dhaifu sana. Lakini kwa kuwa nchi ina taasisi imara, muda wake ukapita waka viongozi wengine.


5. Na kwa wale wabongo ambao wanamfagilia kagame. Waulize wanyarwanda wenye asili ya kihutu watakupa uhalisia mwingine kuhusu Rwanda. Jeshini, serikalini na idara nyingine nyeti za Rwanda, ni lazima uwe wa kabila la watusi. Na ndiyo maana kagame anakataa kuzungumza na rebels kwa sababu siyo watu wa kabila lake.

6. Jeshi la rwanda liko vizuri. Lakini halina uwezo wa kutusumbua sisi. Isitoshe Rwanda ni nchi ambayo imegawanyika kikabila. Kwa hiyo ni rahisi kupata taarifa za kiintelijensia kutoka ndani ya rwanda. [sitegemei kama kagame atapewa taarifa za kiintelijensia na chadema, "but you never knwo"].
Kwa sabau ya mgawanyiko wa kikabila wa rwanda, ni rahisi hata kuanzisha "civil war" ndani ya rwanda.

7. Majirani zetu hawajaungana. Kihistoria, hakujawahi kutokea urafiki wa Rwanda na Kenya. Ule mkutano wao ulikuwa ni "gimmick" tuu. Kenya haiwezi kuihujumu Tanzania kwa sababu ya rwanda. Isitoshe, East African community haiwezi kuendelea kuwepo bila ya Tanzania. Tanzania ndiyo inaziunganisha nchi zote za East-Africa. Kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni. EAC ilikuwepo bila ya Rwanda. EAC Haikuwahi kuwepo bila ya Tanzania.

8. Tanzania tuko milioni 40. Kiuchumi, tukii-suspend EAC; Kenya wataumia kiuchumi. Bidhaa zao hazitauzwa kirahisi hapa kwetu kama ilivyo sasa. Kupoteza soko la watu milioni 40; muulize mchumi yoyote atakwambia madhara yake.

9. Nadhani kwa leo haya machache yanatosha.
 
brother you have spoken well kabisa na nimejifunza kitu kutoka kwako lakini kitu kimoja nataka kukuuliza kwenye hizo analysis kuhusu diversion in RWANDA ina maana KAGAME hajui hayo?
 
Mheshimiwa, Mtukufu Rais wangu mwenye weledi wote wa urahis! Nimeipenda sana kauli yako juu ya usalama wa nchi yako siku ile ya kukumbuka mashujaa wetu pale Kaboya, Kagera. Pamoja na hayo, sisi wananchi wako si salama hata wakati huu ambapo hakuna vita na adui yeyote wa nje.

Wakati huduma za tiba na uzazi ni duni au hazipo kwa wengi. wakati hata maji yetu ya kunywa mtoni yanatiwa sumu za migodini na viwandani. Wakati watoto wetu wanafaulu mitihani kwa kupewa alama za ufaulu za mezani kutokana na elimu duni itolewayo. Wakati wakulima na wafugaji wanapigana kutokana na sera mbovu za ardhi na mipango ya maendeleo. Wakati wafanyakazi halisi na si wale wa kuweka saini au kusinzia wakilalamikia ujira duni wapewao baada ya kutimiza wajibu wao. Wakati wamachinga wakifanywa wakimbizi ndani ya nchi yao huku serikali yako ikishindwa kutengeneza ajira.

Wakati wananchi kila leo wanakumbwa na bomoa bomoa na kuhamishwa isivyostahili ili kupisha wenye vyao na wanyonyaji waishi wapendavyo. Wakati wananchi wakishuhudia hata raslimali zao zikipolwa bila hata ya kujulishwa kilichomo kwenye mikataba au kuwa na nguvu ya kuhoji chochote bila ya kupata vipigo. Wakati mafisadi na wanyonyaji mliowabatiza jina la uwekezaji wakiahidiwa pepo kwa gharama yoyote kinyume na walalahoi. Wakati bunge linapokuwa kamati ya chama tawala na hivyo kuacha kutetea haki za wananchi na badala yake kuwa muhuri wa uovu na kituo cha matusi.

Wakati polisi wakiwa mstari wa mbele kubambikiza kesi, kutesa raia hata kwa kuwalenga mabomu. Wakati msajili wa vyama na Tume ya uchaguzi vinapokuwa na double standards. Wakati mchakato wa katiba mpya ukichakatwa ili ulinde maslahi ya watu wachache; Wakati hamasa za kutugawa wananchi kwa misingi ya ukabila, ukanda, uchama na uduni vikitiwa kasi ya kuzimu. Wakati uhai wa Tanzania kama Jamhuri ya Muungano ukiwa mashakani pasipo kufikiri hatima ya wale ambao wametumia uhuru wa mwenyezi Mungu kuishi popote walipopenda ndani ya nchi yao.

Usalama wetu u mashakani zaidi, na amani yetu ni ya kufikirika zaidi na utulivu wetu ni wa kitambo tu. nahisi kuwa ipo siku tutalipuka na kusambalatishwa na kusambaa kuliko wasambaa wa torabora kama SOTE, tusipovunja ukimya na kuadresi ishuz kama zilivyo badala ya kuzipaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

Ugonjwa hauponi kwa kudai kuwa huna ugonjwa bali kwa kuukiri na kuchukua hatua stahiki, hata kama zinauma. Wewe ndiwe amiri jeshi mkuu mwenye dhamana hivyo usisubiri kila mtu aunde kikundi chake cha ukakamavu ili ajilinde kama CCM, CUF na CHADEMA mlivyoanzisha vikundi vyenu. Fanya maamuzi sasa, chukua hatua mpendwa,vinginevyo usalama wetu u mashakani.

Asalaam aleykum.
 
Mkuu mambo haya ashaambiwa sana, lakini ataishia kusema Ni Upepo Tu, Utapita.
Mkiendelea kusema sana atasema kuwa "Nawakata Mapembe, hata ukiwa nani sikuogopi"!

Kilichopo sasa ni kila mtu pale alipo achukue hatua binafsi.
 
Ni kweli Tanzania ni nchi yetu na popote nitakapoenda nitaitwa mgeni maana nchi yangu ni Tanzania. Nchi yetu kwa sasa ina maadui wengi na maadui hawa wananguvu sana. Tunao maadui Rushwa, Ufisadi, Kushuka kwa kiwango cha elimu, udini, hali ngumu ya maisha n.k. Masikitiko yangu makubwa nikwamba serikali iliyopo madarakani baada ya kupoteza nia ya kumundolea mwananchi hawa maadui, imeamua tengeneza maadui wa nje ya Tanzania. Eti Paul Kagame naye ni adui na serikali inatoa vitisho kwake. Haya yanafanyika for whose benefit? Je tutatokaje kwenye tope hili zito na deep ambalo tumezamishwa na viongozi wetu? Vijana wengi hawana tena mapenzi na nchi yao. Wanaridhika na ujira mdogo na haramu wanaopewa ili washinde mitandaoni wakipost mambo ya upuuzi kutetea upuuzi. Adui yetu ni nani?
 
Kila taifa linauharifu wa aina tofauti tofauti na duniani kote kunauharifu ikiwa ni pamoja na watu kupigwa risasi mambo haya hutokea hata marekani ambako wanakila kitu kikubwa ni vyombo vyetu kuongeza mipango na mikakati ya ulinzi.
 
Mkuu mambo haya ashaambiwa sana, lakini ataishia kusema Ni Upepo Tu, Utapita.
Mkiendelea kusema sana atasema kuwa "Nawakata Mapembe, hata ukiwa nani sikuogopi"!

Kilichopo sasa ni kila mtu pale alipo achukue hatua binafsi.
Mkuu hayo mawazo yako ni mawazo ya kibavicha yaliyojaa uhuni kama jk angekuwa na roho mbaya leo slaa tusingekuwa naye alipokuwa anachochea vurugu na kusema nchi haitatawalika angesha tundikwa shaba kwisha lakini kwa uvumilivu wa jk leo bado yupo.
 
Mkuu kitu cha muhimu kila mwananchi ajilinde mwenyewe...haya mapoliccm yanatumika kukilinda ccm na sio wananchi.
 
Udini ni hoja ya watawala kutugawa,mbona mtaani hatuulizani dini zetu?Adui ni ccm,uvivu na woga wa watanzania kuwafurumisha mkoloni mweusi
 
Back
Top Bottom