Rais Kikwete: Nchi iko salama, atakaye jaribu atakiona cha mtema kuni

Adui yetu namba 1 ni mfumo wa kiutawala, namba 2 ni mfumo wa kiutawala na namba 3 ni mfumo wa kiutawala. Tukiwaondoa hawa maandui wa3 tutasonga mbele.
 
Mkuu hayo mawazo yako ni mawazo ya kibavicha yaliyojaa uhuni kama jk angekuwa na roho mbaya leo slaa tusingekuwa naye alipokuwa anachochea vurugu na kusema nchi haitatawalika angesha tundikwa shaba kwisha lakini kwa uvumilivu wa jk leo bado yupo.
Acheni maneno ya uongo za uzishi..dr.slaa aliongelea mambo ya uonevu kwa raia, policcm kupiga na kuuwa raia..ndio akasema inabidi rais achikue hatua madhubiti kwa usalama wa raia wake...wakiacha wananchi waendelee kunyanyasika watachoka..then ncho haitatawalika.tatizo lenu vijana wa buku 7 mnapenda sana kubadilisha maneno.acheni hio ujinga aisee :target;:
 
Mkuu hayo mawazo yako ni mawazo ya kibavicha yaliyojaa uhuni kama jk angekuwa na roho mbaya leo slaa tusingekuwa naye alipokuwa anachochea vurugu na kusema nchi haitatawalika angesha tundikwa shaba kwisha lakini kwa uvumilivu wa jk leo bado yupo.
Acheni maneno ya uongo za uzishi..dr.slaa aliongelea mambo ya uonevu kwa raia, policcm kupiga na kuuwa raia..ndio akasema inabidi rais achikue hatua madhubiti kwa usalama wa raia wake...wakiacha wananchi waendelee kunyanyasika watachoka..then ncho haitatawalika.tatizo lenu vijana wa buku 7 mnapenda sana kubadilisha maneno.acheni hio ujinga aisee :target:
 
Jamani nimechoka, kama Kagame anasema akikutana na aliyesema haya maneno "Jk" ni atampiga, sijui ngumi au makofi, mateke? Ila huu ni msemo sawa na aliosema Iddi Amini miaka 30 iliyopita kuwa "anatamani apande ulingoni na JK Nyerere na wapigane Ngumi - anyway Idi Amini angemtoa mzee kwa KO, ila kwa hili la PK nadhani tunaweza shuhudia JK akipingwa makofi kwenye moja ya mikutano ya EAC, SADDAC, etc endapo watakutana,mara 10 tusikilize matamko kuliko haya kutokea........kwa vyovyote vile tuingie vitani au hapana huwa sipendi dharau kwa nchi yangu, namshukuru Mungu sikuwa mkuu wa majeshi au sijawahi kuwa mwanajeshi, nadhani ningekuwa na ujuzi huo ningeomba kuwa wa kwanza kwenda front, ki ukweli nilimuunga mkono Membe wakati Mama Banda alipokuwa anachonga (alitakiwa kupigwa) and kiukweli natamani vikosi vyetu vingekuwa vishaweka shield huko Karagwe, Ngara, na Kigoma, commanding PK to seat on a round table ..hivi taratibu za kujiunga na jeshi zipoje? naipenda nchi yangu, naipenda bendera yangu - wa kwanza Mungu, Mungu ibariki Tanzania, ninawalaaani viongozi waoga na wezi
 
tanzania ndio nch pekee inayopakana na chi zote za africa mashariki, plus drc, zambia, malawi na mozambique.
rwanda watapigwa pande zote ndani na nje ya nchi yao.
#tukoimara
 
tehe tehe nna wasiwasi na wanajeshi wetu wanajifanya wababe kwa raia zake kama kule mtwara na hata hapa kariakoo na kuwa dhaifu kwa maadui zake. sudan na rwanda. kunapenda tujue kama wewe utakuwa salama ukipita anga zake
 
Kwa ufupi tu ni Kwamba JK hana uwezo wa kupigana vita sababu uchumi ndiyo kiashira kikubwa cha uwezo wa nchi vitani. Vikosi vya majeshi ndiyo tunavyo, na ari ya upiganaji wanayo. Sasa je, tuta kwenda vitani kwa kutegemea misaada ya wahisani? Au tujiulize ni uchumi gani imara ambao JK ameujenga utakao muwezesha kupigana vita two fronts yaani Malawi na Rwanda? Au vita ana fikiri ni kupeleka tu majeshi?

Vita vya Kagera 1979 vili yumbisha uchumi wa nchi hii hadi leo makovu bado yapo. Sasa huyu Jamaa anapo jisifia kuwa na uwezo wa kuilinda nchi tuna mshangaa.
 
Ulitaka aseme kuwa hana uwezo wa kuilinda nchi ili ufurahi we mamruki!? Ktk uchumi huu huu unaouona ww kuwa goigoi tutawachakaza wote hao, we subiri uone!
 
tutawakopa wauza madawa ambao ni watoto wake, marafiki zake na makada wa chama chake ambao mpaka leo amemywea kuwatangaza licha ya kujitapa kuwa list anayo
 
Ulitaka aseme kuwa hana uwezo wa kuilinda nchi ili ufurahi we mamruki!? Ktk uchumi huu huu unaouona ww kuwa goigoi tutawachakaza wote hao, we subiri uone!

Tanzania haina uwezo wa kupigana hata na comoro!!nchi imeoza kabisa inayegemea mpaka wafadhili kununua condom sasa hii ni nchi au utumbo
 
uemenena vema . huyu aliyeanzisha thread ni lazima atakuwa mTutsi kwa hakika wasije wakasingizia hali mbaya ya uchumi. vijana wetu wamepumzika miaka mingi wanahitaji kufanya mazoezi ili wapande vyeo kwahiyo yeyote chezea TANZANIA CHAKAZA YEYE KABISA
 
Kwa ufupi tu ni Kwamba JK hana uwezo wa kupigana vita sababu uchumi ndiyo kiashira kikubwa cha uwezo wa nchi vitani. Vikosi vya majeshi ndiyo tunavyo, na ari ya upiganaji wanayo. Sasa je, tuta kwenda vitani kwa kutegemea misaada ya wahisani? Au tujiulize ni uchumi gani imara ambao JK ameujenga utakao muwezesha kupigana vita two fronts yaani Malawi na Rwanda? Au vita ana fikiri ni kupeleka tu majeshi?

Vita vya Kagera 1979 vili yumbisha uchumi wa nchi hii hadi leo makovu bado yapo. Sasa huyu Jamaa anapo jisifia kuwa na uwezo wa kuilinda nchi tuna mshangaa.

Vipi tena ? Unaleta habari za uchumi !!!! Nguvu tunayo, sababu tunazo, nia tunayo, hela zipo .
Kabla ya kuporomosha habari za uchumi , soma , tazama, tafuta historia za nchi tofauti, hivi unajua kama USA uchumi wake ulikua baada ya kumaliza World war 2.

Need more ?
 
Ulitaka aseme kuwa hana uwezo wa kuilinda nchi ili ufurahi we mamruki!? Ktk uchumi huu huu unaouona ww kuwa goigoi tutawachakaza wote hao, we subiri uone!

nchi ingekuwa salama hao wasomali na waethiopia wanaofia ktk malori wanapita wapi, je ndege ya jeshi ya qatar iliyoingia na kubeba twiga bila kufahamika ingepita wapi? tafakari..acha kuwa mamluki wa chama...nchi yetu kwanza.
 
Tanzania haina uwezo wa kupigana hata na comoro!!nchi imeoza kabisa inayegemea mpaka wafadhili kununua condom sasa hii ni nchi au utumbo

Kwa nini unaendelea kuwa mwananchi wa nchi iliyooza?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kikwete, kweli nchi iko salama?

Lula wa Ndali Mwananzela
RAIA MWEMA

Toleo la 309
31 Jul 2013

WAKATI wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, Rais Jakaya Kikwete alizungumza na kuwahakikishia Watanzania kuwa nchi iko salama na kuwa mtu yeyote ambaye atachezea mipaka yetu basi atapigwa kama tulivyompiga Idi Amin katika Vita ya Kagera.

Rais Kikwete alizungumza na kushangaliwa na habari za kauli yake hiyo kali ambayo ilionekana kuwalenga Joyce Banda wa Malawi na Paul Kagame wa Rwanda, ilipewa kipaumbele kwenye vichwa vya magazeti na habari siku zilizofuata. Wapo ambao waliamini kauli hiyo ya Kikwete na kuipokea wakifikiria kuwa kwa vile Rais kasema basi ndivyo ilivyo. Naomba kupendekeza kuwa ni wajibu wetu kama raia kuhoji kauli kama hiyo hasa katika mwanga wa matukio mbalimbali ambayo yamehusisha vyombo vya usalama.

Vyombo vya Usalama na Ufisadi
Ni vigumu sana kwa nchi kuwa salama hasa kama vyombo vya usalama na maofisa wa usalama wanahusishwa katika uhalifu na ufisadi. Hili ni muhimu kulifikiria, kulijadili na kuliweka wazi. Wananchi wanapoambiwa kuwa nchi iko salama wanatarajia kuona usalama kweli upo; lakini kama matukio mbalimbali yanaonesha kulegalega kwa usalama huo kuambiana kuwa nchini “salama” ni sawa sawa na kuvalishana mashada ya mawaridi kwenye jua kali na kupakana poda kwenye maji! Na wapo ambao wanaweza kuimba kwa sauti “tumependekeza”!

Yapo matukio mbalimbali ambayo yanatufanya tuhoji ukweli na umakini wa kauli hii; matukio ambayo yanaashiria siyo tu kulegalega kwa hali ya usalama nchini na hasa kuingiliwa kwa vyombo vya usalama na wahalifu wa kimatiafa. Our security organs have been deeply and strategically compromised. Naomba mpendwa msomaji nigusie kwa juu juu tu matukio machache ambayo yanaashiria kuwa japo tuna watu wanavaa sare za jeshi, wanapigiana saluti, na kuzungumza kama wenye mamlaka ukweli wa mambo ni kuwa tuna hali mbaya sana katika vyombo vya usalama ambavyo vimekaa kisiasa zaidi.

Kashfa ya Meremeta
Hii ni mojawapo ya kashfa ambazo zinadokeza tu jinsi ambavyo vyombo vya usalama vimeingiliwa. Kwa wanaokumbuka serikali imekataa katakata kuchunguza kashfa hii kwa jina la “usalama wa taifa”. Machache yanayojulikana ni kuwa kikundi cha mamluki wa Afrika Kusini wakishirikiana na mamluki wa kimataifa wa uhalifu waliingia nchini na inaaminika walishirikiana na vigogo wa JWTZ/Serikali kuingia kwenye machimbo ya Meremeta, wakachota dhahabu na kufanya shughuli nyingine ambazo ziliwaingizia pesa haraka haraka.

Ni Meremeta hii ndiyo iliyozaa Tangold na Deep Green Finance kwa wanaokumbuka. Majina ya wahusika wake ni vigogo wa CCM na serikali. Pamoja na jitihada za Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono na wabunge wengine na wanaharakati kutaka serikali ichunguze jambo hili serikali imekataa katakata. Maajabu yake ni kuwa watu wale wale waliopewa Meremeta miaka michache baadaye wamerudi tena nchini na kupewa mikataba mingine –safari hii katika kutafuta mafuta – kwenye Ziwa Tanganyika na huko Mkuranga. Ni hao hao ambao walichunguza na kupata mafuta huko Uganda na baada ya muda wakauza hisa zao na kutokomea kwingine. Sasa hivi mgodi wa Meremeta umefungwa, waliochuma wamechuma na waliolindwa wamelindwa; halafu tunaambiwa nchi iko salama!

Ujangili wa nyara na dawa za kulevya
Hivi karibuni tumesikia jinsi baadhi ya maofisa wa serikali hasa majeshi yetu wakikamatana wenyewe kwa wenyewe wengine wakijihusisha na biashara ya dawa za kulevya na wengine wakifanya ujangili. Tayari kuna taarifa nyingi tu za maofisa ambao wamekamatwa wakiwa na shehena za meno ya tembo zenye thamani ya mamilioni kama siyo mabilioni ya shilingi. Na hili halijabagua; wapo maofisa wa JWTZ, wapo wa Polisi, na wapo wa Magereza.

Na dalili zote zinaonesha kuwa wahusika hawa si wa vyeo vya chini tu kwani wapo ambao wenye vyeo vya juu ambao wamehusishwa na kashfa hizi. Na hapa ni lazima tukumbushie tu kuwa tunaowazungumzia ni wale waliokamatwa tu na nyara zile zilizokamatwa tu; je zile zilizofanikiwa kuuzwa na kupelekwa nje na wale ambao wamefanikiwa kujificha na hadi hivi sasa hawajulikani ni wangapi? Jibu lake kulifikiria tu inatisha! Ni wazi kuwa upo mtandao uliozama kwenye uhalifu na umezama hadi sehemu ambazo kuzitaja mtu unaona jasho linajaa viganjani. Halafu mtu anasema kuna usalama!

Kutoroshwa kwa wanyama kwenda Qatar
Hivi kweli mtu anaweza kusema kuwa nchi iko “salama” wakati ndege ya kijeshi ya Qatar ikiwa na watu wenye pasi za kidiplomasia imeweza kuingia nchi – inayolindwa na rada la bilioni 40!-na kuweza kuchukua lundo la wanyama na kuwapeleka kwao bila polisi hata mmoja kuwazuia, bila usalama wa taifa, bila wanajeshi na sifa zao zote kuweza kusema lolote? Na kuwa hata tulipolalamika waturudishie wanyama wetu wamekataa halafu genius mmoja serikalini anatuambia ati “wamekataa kutoa ushirikiano”. Hivi hakuna tena watu wenye uwezo wa kuthubutu?

Unaweza vipi kuendelea kuwa na uhusiano wa kibalozi na nchi ambayo imeiba wanyama wako? Au kwa vile wanatoa misaada ya hapa na pale? Kwamba JWTZ ambalo limepewa dhamana ya kulinda mipaka yetu hadi leo limeshindwa kutoa maelezo ilikuwaje jeshi la nchi nyingine limeingia nchini na kuondoka bila kusindikizwa hata na ndege ya mafunzo? Ati nchi iko salama?

Dawa ya kulevya na silaha haramu
Kama kuna mada ambayo tunaweza kuangalia kwa karibu ni hii; hivi hizi dawa za kulevya nchini zinaweza vipi kuingia, kusambazwa na kusafirishwa nchini huku viongozi wa serikali wakituambia ati wanazo ‘orodha’ za wauza dawa? Tena siyo viongozi wa serikali tu hata wa taasisi za kidini wanasema ati wanayo orodha yao lakini hakuna hata mmoja mwenye uthubutu wa kutaja wahusika? Waziri Mkuu anawabembeleza, Rais anabembeleza, Maaskofu wanabembeleza huku wao wanaendelea kupeta tu? Kweli nchi iko salama?

Tunaweza kuendelea kutoa mifano mingi ya kulegalega kwa mfumo wetu wa usalama. Sasa tunapozungumza ati tutampiga kama tulivyompiga Idi Amin hivi Kikwete anafikiria yeye ni Nyerere? Hivi anafikiria kuwa anaweza hata kusimama kwenye mabega ya Nyerere na kujilinganisha naye? Hivi uongozi ambao umeingiliwa hivi kweli unaweza kuhamasisha taifa kulinda mipaka kweli? Wananchi hawa hawa ambao vyombo vya dola vimeambiwa viwapige tu? Kweli nchi iko salama?
Iko salama kwa nani? Hivi ni nani hasa yuko salama nchini? Angalia nani hakamatwi halafu jiulize ni nani kweli yuko salama.

Kikwete, kweli nchi iko salama?

Lula wa Ndali Mwananzela
RAIA MWEMA

Toleo la 309
31 Jul 2013

WAKATI wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, Rais Jakaya Kikwete alizungumza na kuwahakikishia Watanzania kuwa nchi iko salama na kuwa mtu yeyote ambaye atachezea mipaka yetu basi atapigwa kama tulivyompiga Idi Amin katika Vita ya Kagera.

Rais Kikwete alizungumza na kushangaliwa na habari za kauli yake hiyo kali ambayo ilionekana kuwalenga Joyce Banda wa Malawi na Paul Kagame wa Rwanda, ilipewa kipaumbele kwenye vichwa vya magazeti na habari siku zilizofuata. Wapo ambao waliamini kauli hiyo ya Kikwete na kuipokea wakifikiria kuwa kwa vile Rais kasema basi ndivyo ilivyo. Naomba kupendekeza kuwa ni wajibu wetu kama raia kuhoji kauli kama hiyo hasa katika mwanga wa matukio mbalimbali ambayo yamehusisha vyombo vya usalama.

Vyombo vya Usalama na Ufisadi
Ni vigumu sana kwa nchi kuwa salama hasa kama vyombo vya usalama na maofisa wa usalama wanahusishwa katika uhalifu na ufisadi. Hili ni muhimu kulifikiria, kulijadili na kuliweka wazi. Wananchi wanapoambiwa kuwa nchi iko salama wanatarajia kuona usalama kweli upo; lakini kama matukio mbalimbali yanaonesha kulegalega kwa usalama huo kuambiana kuwa nchini "salama" ni sawa sawa na kuvalishana mashada ya mawaridi kwenye jua kali na kupakana poda kwenye maji! Na wapo ambao wanaweza kuimba kwa sauti "tumependekeza"!

Yapo matukio mbalimbali ambayo yanatufanya tuhoji ukweli na umakini wa kauli hii; matukio ambayo yanaashiria siyo tu kulegalega kwa hali ya usalama nchini na hasa kuingiliwa kwa vyombo vya usalama na wahalifu wa kimatiafa. Our security organs have been deeply and strategically compromised. Naomba mpendwa msomaji nigusie kwa juu juu tu matukio machache ambayo yanaashiria kuwa japo tuna watu wanavaa sare za jeshi, wanapigiana saluti, na kuzungumza kama wenye mamlaka ukweli wa mambo ni kuwa tuna hali mbaya sana katika vyombo vya usalama ambavyo vimekaa kisiasa zaidi.

Kashfa ya Meremeta
Hii ni mojawapo ya kashfa ambazo zinadokeza tu jinsi ambavyo vyombo vya usalama vimeingiliwa. Kwa wanaokumbuka serikali imekataa katakata kuchunguza kashfa hii kwa jina la "usalama wa taifa". Machache yanayojulikana ni kuwa kikundi cha mamluki wa Afrika Kusini wakishirikiana na mamluki wa kimataifa wa uhalifu waliingia nchini na inaaminika walishirikiana na vigogo wa JWTZ/Serikali kuingia kwenye machimbo ya Meremeta, wakachota dhahabu na kufanya shughuli nyingine ambazo ziliwaingizia pesa haraka haraka.

Ni Meremeta hii ndiyo iliyozaa Tangold na Deep Green Finance kwa wanaokumbuka. Majina ya wahusika wake ni vigogo wa CCM na serikali. Pamoja na jitihada za Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono na wabunge wengine na wanaharakati kutaka serikali ichunguze jambo hili serikali imekataa katakata. Maajabu yake ni kuwa watu wale wale waliopewa Meremeta miaka michache baadaye wamerudi tena nchini na kupewa mikataba mingine –safari hii katika kutafuta mafuta – kwenye Ziwa Tanganyika na huko Mkuranga. Ni hao hao ambao walichunguza na kupata mafuta huko Uganda na baada ya muda wakauza hisa zao na kutokomea kwingine. Sasa hivi mgodi wa Meremeta umefungwa, waliochuma wamechuma na waliolindwa wamelindwa; halafu tunaambiwa nchi iko salama!

Ujangili wa nyara na dawa za kulevya
Hivi karibuni tumesikia jinsi baadhi ya maofisa wa serikali hasa majeshi yetu wakikamatana wenyewe kwa wenyewe wengine wakijihusisha na biashara ya dawa za kulevya na wengine wakifanya ujangili. Tayari kuna taarifa nyingi tu za maofisa ambao wamekamatwa wakiwa na shehena za meno ya tembo zenye thamani ya mamilioni kama siyo mabilioni ya shilingi. Na hili halijabagua; wapo maofisa wa JWTZ, wapo wa Polisi, na wapo wa Magereza.

Na dalili zote zinaonesha kuwa wahusika hawa si wa vyeo vya chini tu kwani wapo ambao wenye vyeo vya juu ambao wamehusishwa na kashfa hizi. Na hapa ni lazima tukumbushie tu kuwa tunaowazungumzia ni wale waliokamatwa tu na nyara zile zilizokamatwa tu; je zile zilizofanikiwa kuuzwa na kupelekwa nje na wale ambao wamefanikiwa kujificha na hadi hivi sasa hawajulikani ni wangapi? Jibu lake kulifikiria tu inatisha! Ni wazi kuwa upo mtandao uliozama kwenye uhalifu na umezama hadi sehemu ambazo kuzitaja mtu unaona jasho linajaa viganjani. Halafu mtu anasema kuna usalama!

Kutoroshwa kwa wanyama kwenda Qatar
Hivi kweli mtu anaweza kusema kuwa nchi iko "salama" wakati ndege ya kijeshi ya Qatar ikiwa na watu wenye pasi za kidiplomasia imeweza kuingia nchi – inayolindwa na rada la bilioni 40!-na kuweza kuchukua lundo la wanyama na kuwapeleka kwao bila polisi hata mmoja kuwazuia, bila usalama wa taifa, bila wanajeshi na sifa zao zote kuweza kusema lolote? Na kuwa hata tulipolalamika waturudishie wanyama wetu wamekataa halafu genius mmoja serikalini anatuambia ati "wamekataa kutoa ushirikiano". Hivi hakuna tena watu wenye uwezo wa kuthubutu?

Unaweza vipi kuendelea kuwa na uhusiano wa kibalozi na nchi ambayo imeiba wanyama wako? Au kwa vile wanatoa misaada ya hapa na pale? Kwamba JWTZ ambalo limepewa dhamana ya kulinda mipaka yetu hadi leo limeshindwa kutoa maelezo ilikuwaje jeshi la nchi nyingine limeingia nchini na kuondoka bila kusindikizwa hata na ndege ya mafunzo? Ati nchi iko salama?

Dawa ya kulevya na silaha haramu
Kama kuna mada ambayo tunaweza kuangalia kwa karibu ni hii; hivi hizi dawa za kulevya nchini zinaweza vipi kuingia, kusambazwa na kusafirishwa nchini huku viongozi wa serikali wakituambia ati wanazo ‘orodha' za wauza dawa? Tena siyo viongozi wa serikali tu hata wa taasisi za kidini wanasema ati wanayo orodha yao lakini hakuna hata mmoja mwenye uthubutu wa kutaja wahusika? Waziri Mkuu anawabembeleza, Rais anabembeleza, Maaskofu wanabembeleza huku wao wanaendelea kupeta tu? Kweli nchi iko salama?

Tunaweza kuendelea kutoa mifano mingi ya kulegalega kwa mfumo wetu wa usalama. Sasa tunapozungumza ati tutampiga kama tulivyompiga Idi Amin hivi Kikwete anafikiria yeye ni Nyerere? Hivi anafikiria kuwa anaweza hata kusimama kwenye mabega ya Nyerere na kujilinganisha naye? Hivi uongozi ambao umeingiliwa hivi kweli unaweza kuhamasisha taifa kulinda mipaka kweli? Wananchi hawa hawa ambao vyombo vya dola vimeambiwa viwapige tu? Kweli nchi iko salama?
Iko salama kwa nani? Hivi ni nani hasa yuko salama nchini? Angalia nani hakamatwi halafu jiulize ni nani kweli yuko salama.

Jamaa nalo mbumbumbu hili anachanganya uhalifu na usalama kwa nini vijana wa bavicha wengi hwana akili.
 
055_2b82a.jpg

JK ana ugeni mwingi, yupo bize mno.
 
uliyoandika ni ukweli kwa asilimia zote hakika Tanzania tunaitaji wana habari wenye kuchunguza mambo muhimu katika Taifa letu na kutoa habari yenye ushaidi wa kutosha kama ulivyotoa.
 
Back
Top Bottom