Rais Kikwete na safari za nje

Haya ndiyo matunda ya kuwa kondoo.Nakumbuka hata Yona naye alisema hivyo hivyo kuwa tutaona maisha mazuri kwa watanzania katika kipindi chake.Naye akala akapita,Membe naye anakula atapita ..story goes on and on.
Ndugu zangu bila ya kujipanga vizuri na kuimarisha upinzani hakutakuwa na mafanikio yoyote yale.Watanunua manisani patrol,mercedes,mijumba nk...kwa hela na jasho letu.

-Wembe
 
Sishauri serious investor aende kuinvest Tanzania

Urasimu uliopo Dar es salaam port hauna mfano mtu bora aende zake Msumbuiji au Uganda lakini siyo Tanzania
 
Kuna habari kuhusu safari za nje za aliyekuwa rais wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, ambazo ziliandikwa kwenye gazeti la RAI la
Novemba 27 - Disemba 3, 2003 (wakati bado linamilikiwa na Jenerali Ulimwengu na waandishi wenzake, na kabla hawajauza hisa
kwa Rostam Aziz na wafanyabiashara wenzake - au sijui ni kwa Rostam Aziz peke yake?).

"Rais huyo hulipwa dola za Marekani 30,000 (sawa na sh.32,000,000) kwa siku wakati wa ziara hizo..."

"Mpaka wakati ripoti iliyozaa makala hii inaandikwa mwaja jana [mwaka 2002]...Rais Obasanjo alikuwa amefanya ziara 93 za nje za jumla ya siku 279, na wakati huo akiwa bado katika kipindi chake cha kwanza cha miaka minne ya urais wake."

Kwa mujibu wa habari hizo, Rais Obasanjo katika miaka mitatu ya mwanzo ya urais wake alikuwa amelipwa dola za Kimarekani milioni 8.37 kwa uhalali kabisa kwa mujibu wa viwango anavyostahili kama rais wa Nigeria.

Hapo bado mshahara wake.

Na memsap wake (Mola aweke roho yake mahala pema peponi) alikuwa anapata dola 12,000 kwa mwezi, ikiwa ni posho ya mavazi, kwa mujibu wa habari hizo za RAI.

Kwa mujibu wa hoja niliyoisikia hivi karibuni JK ni mtu makini na anaona njia halali ambayo anayo kwa ajili ya kula 'matunda ya uhuru wa Tanganyika na mapinduzi ya Zanzibar' ni kwa kupanga safari za nje ambako taratibu halali zitamuwezesha naye kupata posho nzuri tu ya safari.

Ukichukulia kuwa amekaa muda mrefu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na pengine alionja hizo posho katika safari zake za uwaziri, inaweza kuleta mantiki kuwa hiyo ndiyo anaona kwake kuwa njia halali ya kujipatia riziki.

Inawezekana wakati wakereketwa wanachakarika kumpigia debe awe rais wa Tanzania, Mheshimiwa alikuwa anawaza: "siku nikiukwaa urais, safari za nje zitanikoma!"

Hoja yangu ndogo ni kuwa JK amesahau kuwa yeye siyo tena Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Somo la leo: Usiige kwenda haja kwa tembo...

Foti Mwarobaini
 
Foti Mwarobaini,'
Umemwaga point. Mbali na safari za nje, Mwungana kishakula katika kashfa za IPTL, uwekezaji wa madini( Sinclair ni rafiki yake wa miaka 18). Kwa hiyo hii ya safari za nje ni kujiongezea tu ulaji bila kuonekana kuwa ni mlafi.
 
Foti Mwarobaini,'
Umemwaga point. Mbali na safari za nje, Mwungana kishakula katika kashfa za IPTL, uwekezaji wa madini( Sinclair ni rafiki yake wa miaka 18). Kwa hiyo hii ya safari za nje ni kujiongezea tu ulaji bila kuonekana kuwa ni mlafi.

Kikwete kama vile asivyoridhika kwenye mambo binafsi ni vigumu sana kuridhika na pesa ambazo ameshakwiba hadi leo. Afrika mashariki (na kati) imekwisha kabisaaa:

Hebu jikumbushe tena maraisi wa Afrika mashariki:

1. Kaguta
2. Kibaki
3. Kagame
4. Kikwete
5. Kabila

Jamani hizi k zimezidi hadi inakumbusha KKK ya America!
 
Waziri kachemka.

MWekezaji yeyote ajaye Dar inabidi aingie mkataba na serikali kisha kwa wakati wake aingie mkataba na mleta mvua ili umeme usikatike.

Serikali atawapa Rushwa mpaka mkataba utinge na mleta mvua je atampa Rushwa naye?

Hizo safari hazina maana yeyote Rasi akishugulikia umeme na maji tu wenyewe wataanza kuja.
 
akili yake ndogo sana huyu,yaani anaenda kutafuta gharama za safari za maraisi wote wa Africa atupe tulinganishe? then what? tumsifu JK gharama zake ndogo au....membe grow up!
 
Serikali atawapa Rushwa mpaka mkataba utinge na mleta mvua je atampa Rushwa naye ?

.. Hii ndiyo yenyewe, maanake mbavu sina ... just to imagine unampelekea mleta mvua rushwa!!

BTW huyo Membe baada ya kupewa unaibu waziri wa mambo ya ndani alihamia haraka haraka nyumba za serikali pale Kijitonyama na kuipangisha nyumba yake. Basi baada ya kuukwa uwaziri foreni, nyumba ya serikali ikawa haina hadhi ikabidi ahamie nyumbani aliyokuwa anakaa Asha Migiro laini baada ya ukarabati wa mamilioni ya shilingi kuiweka kwenye standard inayokubalika. Sasa sijui nayo itabidi atupe run-down ya gharama za matengenezo za nyumba wa mawaziri wa nje Africa nzima ili tufanye comparison! Jamaa anajiandaa 2015 kumrithi muungwana!
 
...alivyopewa unaibu waziri walifura sana akaenda kulalamika kwa kina kawawa na mwinyi kuwa kamsaidia sana jamaa kusuka mipango lakini anataka kumtosa...cheo alichokitegemea tangu mwanzo ni hiki alicho nacho sasa....sasa hivi he is really happy..na anaendelea na mikakati yake ya 2015
 
Jamani humu sie wenye elimu na mwamko tunaona wazo la Membe ni la kijinga..nasikitika kuwakumbusha kuwa siasa hizi anazofanya Membe zinawapa zinaleta ufanis sana kwenye ccm. Walalahoi walio wengi wanarithika nazo. Je, mwandishi alimuuliza Membe iwapo serikali itakuwa tayari hiyo list ya gharama atakazoleta kwa wananchi zihakikiwe na chombo huru?

Siku za nyuma nakumbuka Wahusika wa Jumba la malkia wa uingereza nao walitoa kauli kama hii kuwa Ufalme wa UK una gharama ndogo sana kulinganisha na falme za nchi nyingine..sikuona kauli ya aina ilete mtafaruku sana; labda ni sababu ufalme hauigiwi kura kukaa madarakani.
 
Waziri huyu aliyepewa kibarua cha kupigia pafyumu safari za raisi nje ya nchi!!Waziri huyu ambaye kibarua chake ni kutetea hata kile ambacho hakiamini!!!Waziri huyu ambaye amefikia hatua ya kutukana profesion yake!!!Waziri huyu ambaye anautamani sana uraisi/ukuu wa jamhuri yetu bikira akiwa na ndoto yakuwa wizara ya mambo ya nje ni stepping stone kwenda IKULU!!!Waziri huyu mtu wa ajabu kweli!!!

Leo ninamvaa kwa kumfikishia ujumbe kwamba;Amepewa dhamana ya kuwaongoza wasomi wenye weledi kupita yeye na tunamuona kuwa kituko anapotaka kutulaghai kwa taarifa za kitoto akijitahidi sana kutumia cost benefit analysis.

Ni uwendawazimu na busara yenye makengeza ya ajabu kutoa Tsh 1Billion kufuatia ama kuhemea Tsh 1 Million.

Mwanahakati_msemahovyo
Kizazi cha DOT COM
Kutoka Kaya Maskini Sana Tanzania
 
I wish huyu bwana Membe siku alipokuwa akimwaga hizo pumba zake angetokea raia mwema wa kumchampa maswali. Kwanza, since when Tanzanian governence should be compared with other countries? Kama anataka kucompare kwa nini asicompare kila kitu anacompare trip za nje? Aanze kwanza na uchumi, afya, infrastracture and education za hizo nchi anazotaka kutufananisha nazo.

Unajua hawa viongozi wanajisahau kwamba sisi ndio waajiri wao, na pale wanakula pesa ya walipa kodi pasipo kuifanyia kazi. I will be so surprise kama 2010 JK atapata steep slop reelection. Maana kuna kila sababu ya kufanya Tanzania the second kenya
 
Sishauri serious investor aende kuinvest Tanzania

Urasimu uliopo Dar es salaam port hauna mfano mtu bora aende zake Msumbuiji au Uganda lakini siyo Tanzania


Mkuu, na hizi bandari unazoongelea ndio zimeshikwa na akina Karamagi na wanajisi wengine wa uchumi, sasa unategemea nini mpaka hapa? Kawaida mzigo unaokuwa bandarini huwa unalipiwa kila siku, sasa unapomcheleweshea mtu mzigo wake kutokana na urasimu na gharama za mzigo huwa zinaongezeka.
Tunahitaji watu makini katika nyanja kama hizi.
 
bado umemsahau

6.Kurunziza


Sheikh Yahya Alikwashesema,Watu wanaokuwa na Herufi M pamoja na Kitu they mostky likely kuwa Viongozi.

Mwandosya
Makamba
Madabida
Membe
Mathayo David
Malechela
Mwinyi
Mkapa
Mugabe
Moi
Mbeki
Mwanawasa
Mongella(MRS)
Mwanakijiji


sasa Odinga wapi na wapi?
 
Hizi ndio gharama za kuusaka uRais kwa tiketi ya SiSiem, sharti utetee uzandiki, ubadhilifu, uchafu na mengine ya jinsi hiyo; Membe is just paying price, Spika Sitta nae anaendelea kulipa kwa kwenda mbele kila kukicha!

Lakini sisi tunaoweza kutafakari shurti tuwafikishie ujumbe wenzetu wa Mashinani maana wao huamini kila kitu mradi tu kisemwe na kiongozi. Bila hivyo viongozi kama Membe/Sitta tutakuwa nao 2015; viongozi wanaopofuka kwa sababu ya kuutaka uRais au cheo chamani. Tutegee nini tukiwa Rais wa staili hii?!
 
cheo alichokitegemea tangu mwanzo ni hiki alicho nacho sasa....sasa hivi he is really happy..na anaendelea na mikakati yake ya 2015

Nimekupata fika Phill. Hebu tusubiri maanake yeye ndiye alikuwa campaign manager wa JK 1995!
 
Back
Top Bottom