Hivi wabunge kazi yao ni kupitisha miswada tu? Mbona migogoro na kero za wananchi katika majimbo yao zipo lakini hawajishughulishi?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,278
2,041
Viongozi wa TANZANIA wengi wao ni watu wa Maofisini tu. Tumesikia Mkurugenzi wa Mabasi ya Mwendokasi hajawahi kutembelea Kituo cha Mabus cha Gerezani toka ameteuliwa yeye ni OFISINI tu kuidhinisha MAFAILI ya MALIPO.

Safari zake ni Nyumbani Ofisini na akisafiri ni MASAKI ULAYA OFISINI Lakini kutembelea VITUO vya mabus yake kusikiliza Kero za Watumishi na ABIRIA hajawahi kufanya toka ateuliwe.

Vivyo hivyo na WABUNGE wetu Wao kazi yao kubwa ni Kuhudhuria BUNGE na KUPITISHA MISWADA na kusubiri kulipwa POSHO na MSHAHARA wa MIL.16 kwa Mwezi.

Mbunge arudipo JIMBONI kwake ni Kuhudhuria Vikao vya MADIWANI na kulipwa POSHO na kurudi nyumbani kupumzika. JIMBONI kwa kila MBUNGE kuna MIGOGORO ya ARDHI na shida mbalimbali za wananchi km Maji Afya Umeme Madawati na kadhalika, lakini huwezi kusikia MBUNGE kaanza ZIARA ya kutembelea JIMBO Lake KUTATUA MIGOGORO HIYO Mbunge anamsubiri RAIS, MAKAMU wa RAIS, WAZIRI MKUU au WAZIRI wa Wizara husika AFIKE ndio AUTATUE huo MGOGORO.

Hii ni AIBU kwa VIONGOZI wetu MNALIPWA Mishahara MINONO na MIKUBWA lakini Mnakaa tu Maofisini na BUNGENI hamtaki kusikiliza na kujionea Shida na Matatizo ya Watumishi na WANANCHI.Hao ndio VIONGOZI wa TANZANIA.
 
Naomba nikurekebishe kidogo.
Kazi yao kusaini posho za vikao na kurudisha gharama walizotumia kwenye uchaguzi. Isipokuwa wachache ndani na nje ya ccm.

Miswada yenyewe wanayopitisha unadhani ni kwa maslah mapana ya nchi au kujipendekeza kichama?
 
Back
Top Bottom