FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 716
Siku hizi ninakuwa mtazamaji tu.... ila sijakata tamaa ...
Mkuu hata mimi huwa kuna wakati nashikwa na hasira natamani ningekuwa karibu na viongozi(wezi) hawa ningwazaba vibao.Huyu Membe anafikiri anaongea na mtoto wake wa chekechekea.Siku hizi ninakuwa mtazamaji tu.... ila sijakata tamaa ...
Hivi Membe ana akili kweli? Uganda na S.A wanaenda kutafuta wawekezaji kwa maana wameshaweka miundombinu sawasawa. Sasa mmungwana mambo ya muhimu kama barabara, maji na umeme yahajakaa vizuri anakimbia kutafuta wawekezaji wa nini? Nani alimwambia kuwa tunahitaji kwenda kuomba wamachinga waje Tanzania? Nenda Kariakoo ndio utajua hakuna wawekezaji kuna wamachinga wa kichina wengi tuu. Muungwana anatakiwa akae kwanza nchini aweke mambo sawa kabla hajaenda kutafuta hao wawekezaji. Hivi hata kwenye madini kuna haja ya kwenda kuwapigia watu magoti?
Kuweka hiyo miundombinu kunahitaji pesa, na hizo pesa zitapatikana kutokana na uwekezaji. Au unazungumzia miundombinu ya aina gani? Kama tungekuwa na uwezo wa kuweka hiyo miundombinu kwa hela yetu wenyewe, wawekezaji tungetafuta wa nini? Tungewekeza wenyewe tu!
Nadhani pia watu wanaokosoa safari za Rais hawajatupa hoja za maana, hawajatoa uthibitisho au ushahidi kuwa safari hizi za rais ni nje au kinyume na majukumu yake. .
African Union Chairman, will this weekend lead Africa in the much publicised EU-AU Summit in Lisbon, Portugal.
The Summit, which is scheduled for December 8 and 9, will discuss contemporary global issues that affect the two continents and establish the basis for a long-term strategic partnership between Europe and Africa.
Kauli imetulia kabisa....You attract investment by building a conducive environment. That is done on the ground and not in the air.
Siku hizi ninakuwa mtazamaji tu.... ila sijakata tamaa ...
Ana kila sababu ya kutetea utalii wa JK kwa sababu wote huwa pamoja (JK na Membe) kwenye safari hizo.Halafu huyu Chinga asitufanye sie hatuna access na foreign media that anaweza kutughilibu kwamba Museveni na Mbeki wamesafiri mara nyingi zaidi kuliko JK.Naamini safari za Mbeki au Museveni tangu waingie madarakani miaka kadhaa iliyopita hazifui dafu kwa huyu Vasco da Gama wetu.
People will invest where there are ample and reasonably priced supplies of water and electricity, good communications, transport, skilled workforce, security and good policies.
Wana JF,
Ukisikia kuna mawaziri vilaza kama some other JF members said a few weeks ago Membe is one of them. Kweli a foreign minister of a poor country like Tanzania anawezaje kulinganisha uwezo wa kusafiri wa raisi wa Tanzania na raisi wa Nigeria, Egypt, Sudan, South Africa au hata Kenya!
Kusoma kwake John Hopkins I wish mngedadisi wale walioko DC wakati anasoma ndo mngeweza ku-conclude kuwa si ajabu Membe ku articulate namna hiyo. Hayo niliyo ya nukuu hapo juu toka kwa Ndugu Augustine Membe wetu hawezi kuya articulate wala kuelewa kuwa ndizo basic factors za kujenga uchumi, na eleze wazi ni mwekezaji gani aliyeletwa na raisi kushughulikia hayo ; au Richmond na Buzwagi?
Mwisho namalizia kwa kusema kuwa safari za nje ndiyo mojawapo ya sources ya forex kwa watu kama Membe; proof juzi tu last December kashusha 2007 Nissan Patrol toka DT Dobie worth US$65,000.00 "kwa hela za mshahara na mkopo wa benki" utaambiwa hivyo. Ukweli unauma!