Rais Kikwete awaombe radhi Wanyarwanda

Status
Not open for further replies.
Wewe unaonekana huna hata chembe ya diplomatic heart, wenzio wanadiplomasia kuomba radhi ni chorus of a day, Kikwete ni mmojawapo!

funga bakuli lako wewe pandiki la kitutsi safari ya kurudi kwenu imewadia
 
Hivi huyu EasyFit ndiye George Maziku wa tiGo 0659985064 au tunamshambulia wakati kanukuu toka kwenye gazeti hiyo barua ya G. Maziku?
Du mm nakuanzia hapahapa kwa lolote huna akili, yaani Wanyarwanda na hasa Watutsi wanavyowatesa wenzao leo JK akawaombe radhi kwa lipi? hasa
  • Kwanza kawafukuza Wageni wote hasa ninyi Wanyarwanda
  • Pili hakuhudhuria vimukutano vya hao Marais Watutsi huko Nairobi, hapo nampongeza asicheke na nyani watatubakizia mabua.
  • Tau hatuna ugomvi na Wanyarwanda sisi tunawasaidia DRC hata km kuna Wanyamulenge
  • Tano na mwisho JK anajua historia yote ya Kagame kuitungua ndege ya habyarimana kwani enzi hizo alikuwa ni Waziri wa mambo ya nje
Hivyo kinachobaki ni kuwatwanga tu ngoja niisikilize kwanza hotuba yake ya mwezi maana kawagusia huko koa wa Kagera
 
Last edited by a moderator:
KUNA msuguano wa waziwazi unaoendelea kati ya Tanzania na Rwanda kufuatia ushauri wa Rais Jakaya Kikwete kwa mwenzake Paul Kagame, kumtaka akae na kuzungumza na waasi wa FDLR.

Msuguano huo ulianza muda mfupi tu baada ya kumalizika kwa kikao cha viongozi wa nchi za Maziwa Makuu kilichofanyika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) na kuhudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, chini ya uenyekiti wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Rais Kikwete alimtaarifu Rais Museveni kile walichojadili baada ya yeye kuchelewa kufika. Alisema ni vema serikali za Rwanda na Uganda zikakaa na kuzungumza na makundi ya waasi wa nchi zao, na kulitolea mfano kundi la waasi wa Rwanda la FDLR.

Inasemekana ushauri huo uliungwa mkono na Rais Museveni, lakini ulipingwa vikali na Serikali ya Kigali, na tangu wakati huo hadi sasa yamesikika matamshi ya ubabe kutoka kila upande.

Alhamisi wiki hii, Tanzania kupitia kwa Ofisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa Ally, imetoa onyo kwa Kigali kuwa wasithubutu kuanzisha vita dhidi ya Tanzania kwa kuwa kitendo hicho kitajibiwa vikali.

Onyo hilo la Dar es Salaam limekuja kutokana na kauli ya vitisho inayodaiwa kutolewa na Rais Kagame hivi karibuni mjini Kigali kwamba: “Sitapoteza muda wangu kumjibu Kikwete, inajulikana maana kuna mahali hataweza kuvuka…haiwezekani.”

Kwanza lazima nikiri kuwa ushauri huo wa Rais Kikwete ni mzuri kutokana na dhamira njema iliyobeba ushauri huo. Dhamira inayolenga kuyapatia ufumbuzi wa kudumu matatizo ya kiusalama yanayozikabili nchi za Rwanda, Uganda na DRC kwa miongo kadhaa sasa.

Hata hivyo, ushauri huu haukuwa sahihi na haukutolewa mahali sahihi. Haukuwa sahihi kwa sababu haukuzingatia ukweli na mtazamo wa Kigali juu ya kundi la waasi la FDLR.

Kundi la FDLR linaundwa na wanamgambo wa Interahamwe na wanajeshi wa zamani wa jeshi la nchi hiyo chini ya aliyekuwa Rais wa Rwanda hayati Juvenal Habyarimana anayedaiwa kuuawa na vikosi vya Rwandese Patriotic Front vya Rais Kagame mwaka 1994 wakati akitokea Tanzania kwenye mazungumzo ya amani kati ya serikali yake na Kagame.

Interahamwe na lililokuwa jeshi la Habyarimana ndio waliotekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani wa Rwanda mwaka 1994. Waliposhindwa vita mwaka 1994 dhidi ya vikosi vya Rais Kagame, walikimbilia katika misitu ya DRC iliyo mashariki mwa nchi hiyo na kuunda kundi hilo la FDLR.

Rais Kagame na mamilioni ya wananchi wa Rwanda wa kabila la Watutsi na Wahutu wachache wenye msimamo wa wastani, ni waathirika wakubwa wa ukatili na unyama uliofanywa na FDLR, na bila shaka hawajasahau wala kusamehe.

Rais Kikwete alipaswa kuzingatia ukweli huu kabla ya kuamua kutoa ushauri wake. Kama angezingatia ukweli huu kabla, bila shaka asingethubutu kumshauri Rais Kagame kukaa meza moja na kundi ambalo halijawahi kuomba msamaha kwa Wanyarwanda wala kuonyesha kujutia uovu wao.

Halafu Rais Kikwete alikosea kutoa ushauri huo mbele ya mkutano ule. Hapakuwa mahali sahihi kwa jambo zito kama hilo. Angetafuta nafasi nyingine, na kwa maoni yangu angezungumza na marais wenzake kwa faragha, ama wote kwa pamoja au mmoja mmoja.

Angepata nafasi nzuri zaidi ya kufafanua dhamira ya ushauri wake, na pia angeweza kuona mwitikio wa Rais Kagame juu ya ushauri huo. Ninaamini msuguano wa sasa usingekuwepo kwa sababu wangejadiliana kwa kina na kuyamaliza mambo yote katika chumba kilichofungwa milango.

Sasa ushauri unataka kuzaa vita ya majirani wawili wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Bila shaka madhara yake ni makubwa. Mbali na kusababisha kuharibika kwa mahusiano kati ya nchi hizi, pia zitapoteza maisha ya watu wake na rasilimali, na hivyo kuteteresha uchumi wa kila moja.

Ni imani yangu Watanzania wengi hawataki na hawawezi kuunga mkono uamuzi wa kuingia vitani na Rwanda. Watanzania hawapo tayari kwa vita vingine, baada ya vile vya Uganda vya mwaka 1978. Tunataka kujenga nchi yetu kiuchumi, kisiasa na kijamii kukimbizana na wakati kwa sababu tupo nyuma sana.

Namshauri Rais Kikwete awaombe radhi Wanyarwanda, amuombe radhi Rais Kagame. Ampigie simu amwambie yaishe kwa kuwa hakukusudia kumuudhi wala kumkumbusha machungu ya unyama wa Interahamwe, amwalike Dar es Salaam wanywe chai na mnyinyo.

Na George Maziku
0659985064
Matapishi matupu peleka u p u pu wako mbele
 
Umetumwa na nani weye! Peleka unafiki kwenu sio hapa.
Kwani PK alivyokuwa anashabikia kuwa DRC wakae meza moja na M23 hakuliona hilo! Leo hii anashauriwa autumie ushabiki wake huo kwa mambo yake na waasi wake unakuwa mchungu! Hata haya hamna nyie!
hakuna kitu cha kuomba msamaha. In fact, PK na Rwanda ndio wanapaswa kuomba radhi!
 
Mkuu naona ushauri wa George Maziku unaanza kufuatwa hata ni kwa mlango wa nyuma.
Hakika umefuatwa..hicho ndio kilipaswa kufanyika. unajua shida kubwa iko na nchi hii? azma ya mwalimu kupambana na ujinga bahati mbaya haikukamilika..alistaafu vita hii ikiwa katikati na mbaya zaidi wale aliwaamini waiendeleze hawakuwa na maono kama yake, usishangae leo hata profesa wa chuo kikuu japo ni mahiri wa kutoa mihadhara na kufundisha lakini bado ni mjinga!!elimu haijambadilisha amekariri tu maana ya elimu lakini fikra bado zina minyororo ya UJINGA..! si maprofesa tu, kingine kibaya watu wa aina hii wapo wamejipenyeza hadi kwenye vyombo vyetu muhimu vinavyoendesha serikali!! ndio maana usishangae kuona michango ya kumtukana kagame na kukataa ukweli, ukisoma between the lines unaona IGNORANCE ya hali ya juu kabisa, tumekwama, dawa ni kuwaondoa hawa..hawajui kazi yao, hakuna serkali inalipa mtu kuwa shabiki wake kusifia au kutetea upuuzi.
sasa kikwete ametafakari akakumbuka alipojikwaa na hilo ndio suluhisho, huangalii ulipoangukia!matamshi hayakua mujarabu pia jukwaa halikuwa muafaka yeye kutoa ushauri huo kwa kagame!
 
Mimi nadhani Rais Kagame anatakiwa amwombe radhi Rais Kikwete kwa kumtolea Maneno ya kashfa na vitisho vya kumshambulia kwa ushauri ambao alikuwa na uhuru wa kuukubali au kuukataa.
 
Kikwete ana tabia ya uswahili na maneno ya kwenye kanga. Na ndiyo hata wenake wa eac wanamtenga. Kwa akili yake anafikiria tu kujikoma kwa nchi za mzgharibi ili apewe misaada.
 
We kweli Mweh.u mwenye uswahili nani sasa kati ya JK na PK? Alikuwa na uhuru wa kukataa ushauri wa JK na wala asingemlazimisha, ye akaona ngoja akamjibu kwenye mkutano wa mke wake.

Hata huyo PK na wenzake wote ni vibaraka na pia atakujaje kwenye mkutano wa Watutsi wote?
 
huyu atakuwa mnyarwanda aliyekimbia kigoma wakati wenzie tulipowafukuza warudi kwao sasa hivi kashika keyboard anaandika shit zake
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom