Rais Kikwete ajibu hoja ya JF kuhusu Meli Mpya Ziwa Victoria

bibikuku

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
832
495
Kama Mtakumbuka wiki iliyopita mwanajamvi mmoja aliwaambia wanamwanza wamuulize JK kuhusu ahadi yake ya kunua meli mpya ziwa victoria. Majibu ameyatoa, haya hapa:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

JK: Mchakato wa kununua meli mpya umeanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mchakato wa kununua meli mpya kwa ajili ya kusafirisha abiria katika Ziwa Victoria umeanza kwa ajili ya ununuzi wa meli hiyo.

Rais Kikwete amesema kuwa kwa sasa wataalamu washauri wa kupatikana kwa meli hiyo, yaani Kampuni ya OSK-Ship Tech ya Denmark, tayari wamekamilisha upembuzi yakinifu juu ya aina ya meli inayofaa kwa matumizi katika Ziwa Victoria.

Rais Kikwete amesema kuwa fedha za ununuzi wa meli hiyo zitatengwa katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/2013 baada ya kuwa maandalizi yote ya ununuzi wa meli hiyo kuwa yamekamilika.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa kazi ya tathmini ya kuzikarabati meli za Mv Victoria, Mv Umoja na Mv Sengerema ambazo zote zinatoa huduma ya usafiri wa abiria na mizigo katika Ziwa Victoria umefanywa na sasa fedha zinatafutwa kwa ajili ya kuanza kazi yenyewe ya ukarabati.

Rais Kikwete ametangaza hayo leo, Jumatatu, Mei 30, 2011, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa eneo la Usagara, Bukumbi, Wilaya ya Misungwi, Mkoa wa Mwanza, kabla ya kuzindua rasmi barabara ya lami ya kilomita 90 kutoka Usagara hadi Geita.

Amewaambia wananchi hao, “Kwa upande wa usafiri katika Ziwa Victoria, ninafurahi kuwafahamisha kwamba mchakato wa kununua meli mpya umeanza. Hivi sasa wataalam washauri, yaani Kampuni ya OSK-Ship Tech ya Denmark, wamekwishakamilisha upembuzi yakinifu juu ya aina ya meli itakayofaa katika Ziwa Victoria.”

Ununuzi wa meli hiyo utakuwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mheshimiwa Rais Kikwete wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana wakati alipowaahidi wananchi wa mikoa ya Ziwa kuwa Serikali yake ingenunua meli ya kusafirisha abiria ndani ya Ziwa hilo kuchukua nafasi ya Mv Bukoba iliyozama miaka 1996.

Tokea kuzama meli hiyo miaka 15 iliyopita ambako watu wanaokadiriwa kufikia 1,000 pia walipoteza maisha, Serikali haijapata kununua meli nyingine kwa ajili ya usafiri wa abiria katika Ziwa hilo na wasafiri wameendelea kutumia meli ndogo zaidi.

Mbali na Ziwa Victoria, Rais Kikwete pia aliahidi kununua meli ya abiria katika Ziwa Nyasa kuchukua nafasi ya Mv Mbeya iliyozama katika Ziwa hilo. Aidha, aliahidi kununua meli kwa ajili ya usafiri wa abiria katika Ziwa Tanganyika ambako meli inayosafirisha abiria ya Mv Liemba imekuwa inatumika kwa miaka 100 na imechoka na kuchakaa.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

30 Mei, 2011
 
Tatizo ni kwamba hatuna watu wa kumkumbusha rais. Akikumbushwa anatekeleza ahadi. Jk usitoe ahadi juu ya ahadi.
 
Ukweli ni kwamba fedha hakuna na ndio maana hata huo ukarabati wa hizo za zamani haujaanza!! Anasema fedha zinatafutwa; pengine anategemea zile za Rada zikirudishwa na ndio maana wamezishupalia!!
 
tanzania bwana,michakato kwenda mbele! Sasa hapo meli ishapatikana au bado? Suppose ushauri wake unakataliwa, anatafutwa mshauri mwingine na meli inanunuliwa 2016.
 
Ndo kamaliza ivo. keshanunua meli jukwaani.
Bado aende kigoma, mpanda, songea akajenge viwanja vya ndege.
Kama maeneno yangekuwa yanaumba JK angekuwa amefikisha TZ peponi
 
Niliwahi kusema huko nyuma the difference between a good leader and a greater leader ni kwamba a good leader anajuwa strenghts and weaknesses zake, lakini a great leader ni yule ambaye si tu anazijua strengths na weakeness zake bali anayezifanyia kazi weakeness zake.

Kikwete needs to sorround himself with great minds otherwise atajikuta anaongelea mchakato come 2015. Kwa nini sekali isi-encourage private sector itoe usafari huko Ziwa victria? hivi usafiri kati ya Dar na Zanzibar unatolewa na Serikali? Tangu lini Serikali ya kikwete ikwa competent kwenye mambo ya bishara na hasa usafirishaji? Reli, ATC isiyokuwa na ndege hata moja? au hata usalama wa barabarani ambapo kila kukicha ni ajali za mabasi?

Kufanya kosa sio kosa lakini kurudia kosa ndio kosa. Maadam alishafanya kosa wakati wa kampeni basi walau kipindi hiki he should get it right. Serikali isimamie sera na mikakati huku wakitafuta private sector ili kuwepo na ushindani. Mchakato!
 
Nchni maskini ni maskini tu! Maskini hata akili, kuna kuwa na umaskini hata wa viongozi siwezi kuamini kuwa hayo ndio yaliyompereka kuongea Mwanza! hayo maneno yalipaswa kusemwa na katibu mkuu wa wizara husika inayonunuwa meli siyo mwanasiasa tena Rais wa nchni!

Rais alipaswa kuwa Bizi na jinsi ya kufumuwa mikata ya madini ili watanzania wapate haki yako, katiba huru, matatizo ya muungano, kuunda upya idara ya Usalama wa taifa kabla haijafa kabisa, kuunda upya Jeshi la Polisi linalo wajibika kwa wananchni na kuheshimu haki za raia, kutengeneza mfumo wa utawala bora unaozingatia sheria na haki za raia wake, kufumuwa na kusuka upya idara za serikali zilizo paralize bila kusahau Elimu, Afya na kilimo.n.k

Sijui kama tutafika kwa mtindo huu.
 
bajet 2011-12!je gharama zitakuwa zimeshuka au kupanda?jk anaanzisha bend inaitwa longolongo jazz
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nchni maskini ni maskini tu! Maskini hata akili, kuna kuwa na umaskini hata wa viongozi siwezi kuamini kuwa hayo ndio yaliyompereka kuongea Mwanza! hayo maneno yalipaswa kusemwa na katibu mkuu wa wizara husika inayonunuwa meli siyo mwanasiasa tena Rais wa nchni!

Rais alipaswa kuwa Bizi na jinsi ya kufumuwa mikata ya madini ili watanzania wapate haki yako, katiba huru, matatizo ya muungano, kuunda upya idara ya Usalama wa taifa kabla haijafa kabisa, kuunda upya Jeshi la Polisi linalo wajibika kwa wananchni na kuheshimu haki za raia, kutengeneza mfumo wa utawala bora unaozingatia sheria na haki za raia wake, kufumuwa na kusuka upya idara za serikali zilizo paralize bila kusahau Elimu, Afya na kilimo.n.k

Sijui kama tutafika kwa mtindo huu.

Cha kushangaza ndugu Arafat ni hawa watu wa Ikulu wana-issue presss release kwamba mchakato wa kununua meli umeanza? Ni hivi majuzi tumesoma taarifa kwamba 33% ya watanzania hawana 'vyoo'! Hivi Ikulu wanasema nini kuhusu hili? Yaani nchi inaendeshwa kwa zima-moto!
 
Naona politicia tu hapo ,ikifika 2012 itakuwa 13 then 14 and finaly 2015 ,hakuna meli hapo
 
Ndo kamaliza ivo. keshanunua meli jukwaani.
Bado aende kigoma, mpanda, songea akajenge viwanja vya ndege.
Kama maeneno yangekuwa yanaumba JK angekuwa amefikisha TZ peponi

Nimecheka sana! Mkuu nimekugongea thanks!
 
Ndivyo jk alivyo na kama tunavyofahamu anatumia elimu yake ya chuo. Uchumi ndio, sijui kama tunajua jk ndio mwamuzi wa maisha ya watanzania au wananchi ndio wanajadili mahitaji yao. Wananchi tunavyoona ni kwamba jk anatoa maamuzi na anamwambia mkullo andika check na anamweleza ndulu toa pesa popote pale tutajaza mbele. Hivi ndivyo jk akiamka asubuhi na kuamua kwenda london, anamwambia mkewe unajisikiaje kwenda london leo.

"Tuharakishe kuwaondoa hawa mafisadi, incompetent leadership ni kitu kibaya sana duniani"
 
Kama Mtakumbuka wiki iliyopita mwanajamvi mmoja aliwaambia wanamwanza wamuulize JK kuhusu ahadi yake ya kunua meli mpya ziwa victoria. Majibu ameyatoa, haya hapa:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

JK: Mchakato wa kununua meli mpya umeanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mchakato wa kununua meli mpya kwa ajili ya kusafirisha abiria katika Ziwa Victoria umeanza kwa ajili ya ununuzi wa meli hiyo.

Rais Kikwete amesema kuwa kwa sasa wataalamu washauri wa kupatikana kwa meli hiyo, yaani Kampuni ya OSK-Ship Tech ya Denmark, tayari wamekamilisha upembuzi yakinifu juu ya aina ya meli inayofaa kwa matumizi katika Ziwa Victoria.

Rais Kikwete amesema kuwa fedha za ununuzi wa meli hiyo zitatengwa katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/2013 baada ya kuwa maandalizi yote ya ununuzi wa meli hiyo kuwa yamekamilika.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa kazi ya tathmini ya kuzikarabati meli za Mv Victoria, Mv Umoja na Mv Sengerema ambazo zote zinatoa huduma ya usafiri wa abiria na mizigo katika Ziwa Victoria umefanywa na sasa fedha zinatafutwa kwa ajili ya kuanza kazi yenyewe ya ukarabati.

Rais Kikwete ametangaza hayo leo, Jumatatu, Mei 30, 2011, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa eneo la Usagara, Bukumbi, Wilaya ya Misungwi, Mkoa wa Mwanza, kabla ya kuzindua rasmi barabara ya lami ya kilomita 90 kutoka Usagara hadi Geita.

Amewaambia wananchi hao, "Kwa upande wa usafiri katika Ziwa Victoria, ninafurahi kuwafahamisha kwamba mchakato wa kununua meli mpya umeanza. Hivi sasa wataalam washauri, yaani Kampuni ya OSK-Ship Tech ya Denmark, wamekwishakamilisha upembuzi yakinifu juu ya aina ya meli itakayofaa katika Ziwa Victoria."

Ununuzi wa meli hiyo utakuwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mheshimiwa Rais Kikwete wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana wakati alipowaahidi wananchi wa mikoa ya Ziwa kuwa Serikali yake ingenunua meli ya kusafirisha abiria ndani ya Ziwa hilo kuchukua nafasi ya Mv Bukoba iliyozama miaka 1996.

Tokea kuzama meli hiyo miaka 15 iliyopita ambako watu wanaokadiriwa kufikia 1,000 pia walipoteza maisha, Serikali haijapata kununua meli nyingine kwa ajili ya usafiri wa abiria katika Ziwa hilo na wasafiri wameendelea kutumia meli ndogo zaidi.

Mbali na Ziwa Victoria, Rais Kikwete pia aliahidi kununua meli ya abiria katika Ziwa Nyasa kuchukua nafasi ya Mv Mbeya iliyozama katika Ziwa hilo. Aidha, aliahidi kununua meli kwa ajili ya usafiri wa abiria katika Ziwa Tanganyika ambako meli inayosafirisha abiria ya Mv Liemba imekuwa inatumika kwa miaka 100 na imechoka na kuchakaa.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

30 Mei, 2011
Mambo yaleyale ahadi juu ya ahadi hizo zilipo hakuna pesa ya kuzilipea angalau kwa awamu moja baada ya nyingine sasa hizo za kununua mpya zitatoka wapi?Hata ahadi zenyewe zinatia mashaka ahidi angalau moja unapotoa zote kwa mpigo unatutia mashaka sitashangaa hata fidia za hao waliopoteza maisha yao katika MV bukoba hawajalipwa fidia.
 
Tuwe wavumilivu na kumwomba Mola atujalie afya njema ili tushuhudie uttekelezaji wake. Hakuna njia ndefu isiyokuwa na mwisho.
 
Huko huko Misungwi Mwanza Jk aliahidi:
1. Kufufua Atc,
2. Kujenga reli ya kimataifa hadi Burundi,
3. Kujenga reli ya kutoka Dar hadi Isaka, Mwanza, Kigoma na Mpanda

Wakati huo huo kamati ya Bunge ya miundo mbinu ilimtimua kwenye kikao waziri wa uchukuzi Omar Nundu kwa kushindwa kutenga fedha za kulifufua ATC, Reli na wakala wa meli katika bajeti ya 2011/2012.

YOTE HAYA YAMETOKEA JAMA

Sasa hapa Raisi anatoa ahadi ambayo wala Wizara husika haina taarifa yake, bado tuseme wasaidizi wa JK wanamwangusha au anajiangusha mwenyewe? Hakuna coordination kati ya Ikulu na Wizara?

Hapa kuna tatizo kubwa kuliko tunavyodhani!!
 
Jamani huyu ni rais wetu ahadi zake sio siasa bali ni ahadi ambazo zitatekelezwa,na kila ahadi lazima ziwe kwenye mipango naomba tuwe wavumilivu.
 
Back
Top Bottom