Rais Kikwete ajibu hoja ya JF kuhusu Meli Mpya Ziwa Victoria

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

JK: Mchakato wa kununua meli mpya umeanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mchakato wa kununua meli mpya kwa ajili ya kusafirisha abiria katika Ziwa Victoria umeanza kwa ajili ya ununuzi wa meli hiyo.

Rais Kikwete amesema kuwa kwa sasa wataalamu washauri wa kupatikana kwa meli hiyo, yaani Kampuni ya OSK-Ship Tech ya Denmark, tayari wamekamilisha upembuzi yakinifu juu ya aina ya meli inayofaa kwa matumizi katika Ziwa Victoria.

Rais Kikwete amesema kuwa fedha za ununuzi wa meli hiyo zitatengwa katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/2013 baada ya kuwa maandalizi yote ya ununuzi wa meli hiyo kuwa yamekamilika.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa kazi ya tathmini ya kuzikarabati meli za Mv Victoria, Mv Umoja na Mv Sengerema ambazo zote zinatoa huduma ya usafiri wa abiria na mizigo katika Ziwa Victoria umefanywa na sasa fedha zinatafutwa kwa ajili ya kuanza kazi yenyewe ya ukarabati.

Rais Kikwete ametangaza hayo leo, Jumatatu, Mei 30, 2011, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa eneo la Usagara, Bukumbi, Wilaya ya Misungwi, Mkoa wa Mwanza, kabla ya kuzindua rasmi barabara ya lami ya kilomita 90 kutoka Usagara hadi Geita.

Amewaambia wananchi hao, "Kwa upande wa usafiri katika Ziwa Victoria, ninafurahi kuwafahamisha kwamba mchakato wa kununua meli mpya umeanza. Hivi sasa wataalam washauri, yaani Kampuni ya OSK-Ship Tech ya Denmark, wamekwishakamilisha upembuzi yakinifu juu ya aina ya meli itakayofaa katika Ziwa Victoria."

Ununuzi wa meli hiyo utakuwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mheshimiwa Rais Kikwete wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana wakati alipowaahidi wananchi wa mikoa ya Ziwa kuwa Serikali yake ingenunua meli ya kusafirisha abiria ndani ya Ziwa hilo kuchukua nafasi ya Mv Bukoba iliyozama miaka 1996.

Tokea kuzama meli hiyo miaka 15 iliyopita ambako watu wanaokadiriwa kufikia 1,000 pia walipoteza maisha, Serikali haijapata kununua meli nyingine kwa ajili ya usafiri wa abiria katika Ziwa hilo na wasafiri wameendelea kutumia meli ndogo zaidi.

Mbali na Ziwa Victoria, Rais Kikwete pia aliahidi kununua meli ya abiria katika Ziwa Nyasa kuchukua nafasi ya Mv Mbeya iliyozama katika Ziwa hilo. Aidha, aliahidi kununua meli kwa ajili ya usafiri wa abiria katika Ziwa Tanganyika ambako meli inayosafirisha abiria ya Mv Liemba imekuwa inatumika kwa miaka 100 na imechoka na kuchakaa.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

30 Mei, 2011
Miaka 10 anazungumzia mchakato. Kila mahali mchakato hakuna kinachofanyika
 
Hakuna cha meli wala ngalawa hapo, time is not ccm's best friend for now, ahadi zilikuwa nyingi mno, haziwezi kutekelezeka teena!!
Meli, viwanja vya ndege, kigoma kuwa dubai, na mwanza wapi sijui... Haya bado kuuna wazee wetu wa iliyokuwa EAC, flyovers, mabasi yaendayo kasi, elimu kwa mtandao bila kusahau kujivua magamba.
Hii thread owners wa jf wataidelete
 
Jamani huyu ni rais wetu ahadi zake sio siasa bali ni ahadi ambazo zitatekelezwa,na kila ahadi lazima ziwe kwenye mipango naomba tuwe wavumilivu.

Nani mwenye haraka? Watu wamevumilia tangu walipozaliwa itakuwa sasa. Tunaendelea kuvumilia na kusubiri. Subira yavuta heri
 
ha ha ha huu uzi huu.. JK akiuona atacheka sana..

sema mswahili alivyo mtaalamu wa chenga atakwambia meli imeshafika sema wanamalizia taratibu za clearence bandarini...

then huyoooo kastaafu na kupotelea msoga kulima mananasi
 
umbembuzi yakinifu umeanza hizi ndizo kauli alizozizoea magufuli pia

nawaambieni magufuli tulimzoea kwa ahadi kama hizi. Mchakato ndio umeanza tender tumetangaza tutatafusta pesa kwa ajili ya swala hili.
 
Kama Mtakumbuka wiki iliyopita mwanajamvi mmoja aliwaambia wanamwanza wamuulize JK kuhusu ahadi yake ya kunua meli mpya ziwa victoria. Majibu ameyatoa, haya hapa:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

JK: Mchakato wa kununua meli mpya umeanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mchakato wa kununua meli mpya kwa ajili ya kusafirisha abiria katika Ziwa Victoria umeanza kwa ajili ya ununuzi wa meli hiyo.

Rais Kikwete amesema kuwa kwa sasa wataalamu washauri wa kupatikana kwa meli hiyo, yaani Kampuni ya OSK-Ship Tech ya Denmark, tayari wamekamilisha upembuzi yakinifu juu ya aina ya meli inayofaa kwa matumizi katika Ziwa Victoria.

Rais Kikwete amesema kuwa fedha za ununuzi wa meli hiyo zitatengwa katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/2013 baada ya kuwa maandalizi yote ya ununuzi wa meli hiyo kuwa yamekamilika.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa kazi ya tathmini ya kuzikarabati meli za Mv Victoria, Mv Umoja na Mv Sengerema ambazo zote zinatoa huduma ya usafiri wa abiria na mizigo katika Ziwa Victoria umefanywa na sasa fedha zinatafutwa kwa ajili ya kuanza kazi yenyewe ya ukarabati.

Rais Kikwete ametangaza hayo leo, Jumatatu, Mei 30, 2011, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa eneo la Usagara, Bukumbi, Wilaya ya Misungwi, Mkoa wa Mwanza, kabla ya kuzindua rasmi barabara ya lami ya kilomita 90 kutoka Usagara hadi Geita.

Amewaambia wananchi hao, “Kwa upande wa usafiri katika Ziwa Victoria, ninafurahi kuwafahamisha kwamba mchakato wa kununua meli mpya umeanza. Hivi sasa wataalam washauri, yaani Kampuni ya OSK-Ship Tech ya Denmark, wamekwishakamilisha upembuzi yakinifu juu ya aina ya meli itakayofaa katika Ziwa Victoria.”

Ununuzi wa meli hiyo utakuwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mheshimiwa Rais Kikwete wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana wakati alipowaahidi wananchi wa mikoa ya Ziwa kuwa Serikali yake ingenunua meli ya kusafirisha abiria ndani ya Ziwa hilo kuchukua nafasi ya Mv Bukoba iliyozama miaka 1996.

Tokea kuzama meli hiyo miaka 15 iliyopita ambako watu wanaokadiriwa kufikia 1,000 pia walipoteza maisha, Serikali haijapata kununua meli nyingine kwa ajili ya usafiri wa abiria katika Ziwa hilo na wasafiri wameendelea kutumia meli ndogo zaidi.

Mbali na Ziwa Victoria, Rais Kikwete pia aliahidi kununua meli ya abiria katika Ziwa Nyasa kuchukua nafasi ya Mv Mbeya iliyozama katika Ziwa hilo. Aidha, aliahidi kununua meli kwa ajili ya usafiri wa abiria katika Ziwa Tanganyika ambako meli inayosafirisha abiria ya Mv Liemba imekuwa inatumika kwa miaka 100 na imechoka na kuchakaa.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

30 Mei, 2011

hahaaaaaaaa.................mtukuuufuuuuuuuuu
 
Mambo mengine humu tukijikumbusha yanatia kinyaa. Tangu 2011 mpaka hii 2015 mchakato huo haujesha au labda fedha iliishapigwa juu kwa juu? Hata ukarabati wa meli zote zilizotajwa haukufanywa na sasa hivi zimepaki Mwanza South hazifanyi kazi.
 
njia ya mwongo fupi itafika tu 2015. ahadi zake zísipotekelezwa matokeo yake ni kushindwa vibaya kwa ccm uchaguzi ujao, nahisi jk alifurahi ilipotabiliwa mwisho wa dunia maana anajua ndio salama yake, na mungu huenda amegaili kuimaliza dunia ili kumuadhiri jk.

We jamaa uliona mbali sana !
 
Watanzania ni watu wasahaulifu sana na bahati mbaya hawana utaratibu wa kuweka kumbukumbu za ahadi za wanasiasa!

Nchi yetu hapa ilipo inahitaji uongozi wa Chama kipya maana kinaweza kuja na sera mpya badala ya mazoea ya kudanganywa na wagombea wa ccm.

Yaani wanaahidi vitu vingine huku hata nafsi zao zikionesha dhahiri kuwa ni uwongo!

Watanzania tubadilike!!
 
Kama wanavyojitangaza wenyewe ''CCM NI ILE...ILE.....!!!!. Hivyo watanzania tusitegemee mabadiliko yoyote kama ccm itarudi madarakani.
 
Ukisikia mwanasiasa anataja neno 'upembuzi yakinifu', tambua kuwa hapo hakuna kitu....
 
Hii ni kauli ya kuwapumbaza wanao tarajia jambo fulani. Ukizingatia, upeo wa wapewa ahadi kuwa mdogo, dhahiri yake ndo haya tunayo yasikia kwenye kampeni hizi za sasa.
 
Back
Top Bottom