Rais Kikwete ajibu hoja ya JF kuhusu Meli Mpya Ziwa Victoria

Hahahaa, am sure mtaishia kuona ama kusikia mchakato tu, kitu chenyewe hakitatokea
 
njia ya mwongo fupi itafika tu 2015. ahadi zake zísipotekelezwa matokeo yake ni kushindwa vibaya kwa ccm uchaguzi ujao, nahisi jk alifurahi ilipotabiliwa mwisho wa dunia maana anajua ndio salama yake, na mungu huenda amegaili kuimaliza dunia ili kumuadhiri jk.
 
Hakuna coordination kati ya Ikulu na Wizara?

QUOTE]

Sio kwamba hakuna cordination,ni kwamba hiyo mipango haipo kabisa hiyo ni lugha ya kisiasa kuwapumbaza wananchi waone kuna kitu serikali inafanya..
 
wana shinyanga na sisi tumkumbushe rais ile ahadi yake ya kutujengea chuo kikuu kahama, na lami vijijini

Hiki hapa

university.jpg
 
Mwanza watapata meli kama rais alivyo ahidi, kwani CHADEMA hawatoi ahadi? Acheni upumbavu nyie. Semeni roho inawauma kuona Kikwete anawajibika si mlitegemea atatulia tu ikulu na kuruka majuu, sasa anawaonyeshea kuwa yeye ndio BABA yenu nyie vifaranga wa CHADEMA.
 
Jamani huyu ni rais wetu ahadi zake sio siasa bali ni ahadi ambazo zitatekelezwa,na kila ahadi lazima ziwe kwenye mipango naomba tuwe wavumilivu.
ukisema tuwe wavumilivu ina maana tuendelee kuvumilia shida no way, tutamtaka kila ahadi aliyoahidi anatekeleza akishindwa tutamhoji.
 
Mwanza watapata meli kama rais alivyo ahidi, kwani CHADEMA hawatoi ahadi? Acheni upumbavu nyie. Semeni roho inawauma kuona Kikwete anawajibika si mlitegemea atatulia tu ikulu na kuruka majuu, sasa anawaonyeshea kuwa yeye ndio BABA yenu nyie vifaranga wa CHADEMA.
sio chadema tu waliiotoa ahadi kila chama kilichokuwa na mgombea urais kilitoa ahadi na wengine hadi za kujenga kiwanda cha silaha, lakini chadema na hivyo vyama vingine havikushinda kwa hiyo hawawezi kutekeleza ahadi yoyote waliyoahid aliyeshinda ndo kazi kwake kuzitekeleza alizoahidi maana inawezekana wananchi ziliwavutia. huu ni wakati wakutekeeza ahadi si kutoa ahadi ya kutekeleza ahadi.
 
Benito:
That kind of thinking ifute kabisa kama unaitakia hii nchi maendeleo..!
Ujue kwamba hii sirikali sisi ndiyo tumeifanya iongoze kama inavyoongoza...!tumelala much,we weakened her.
sisi ndiyo tulaumiwe na siyo sirika na JK yaamkini they are natural weak...who we are waiting to them out for us..?
some how now CDM wananifurahisha sana na huwa wanatofautiana kwa lengo la kujijenga...go example we must be pleased for them!

chakufanya Wananchi tuipe sirikali deadline one month tunaingia barabarani kama umeme wa uhakika usipo kuwepo,sukari isipopungua bei.
 
waha JF hebu naomba msaada katika haya

1) kwa nini tunahitaji ushauri wa aina ya meli ya kutumika ziwa victoria wakati tayari kuna meli kibao tu zinafanya kazi pale/ zimeshafanya kazi pale

2) Na kama ni kweli tunahitaji ushauri, hivi bado mpaka leo hatuna watu wa kufanya kazi hiyo hapa kwetu mpaka tupate ushauri wa watu kutoka nje.

naomba msaaada kwa haya
 
Hakuna cha meli wala ngalawa hapo, time is not ccm's best friend for now, ahadi zilikuwa nyingi mno, haziwezi kutekelezeka teena!!
Meli, viwanja vya ndege, kigoma kuwa dubai, na mwanza wapi sijui... Haya bado kuuna wazee wetu wa iliyokuwa EAC, flyovers, mabasi yaendayo kasi, elimu kwa mtandao bila kusahau kujivua magamba.
 
Kama Mtakumbuka wiki iliyopita mwanajamvi mmoja aliwaambia wanamwanza wamuulize JK kuhusu ahadi yake ya kunua meli mpya ziwa victoria. Majibu ameyatoa, haya hapa:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

JK: Mchakato wa kununua meli mpya umeanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mchakato wa kununua meli mpya kwa ajili ya kusafirisha abiria katika Ziwa Victoria umeanza kwa ajili ya ununuzi wa meli hiyo.

Rais Kikwete amesema kuwa kwa sasa wataalamu washauri wa kupatikana kwa meli hiyo, yaani Kampuni ya OSK-Ship Tech ya Denmark, tayari wamekamilisha upembuzi yakinifu juu ya aina ya meli inayofaa kwa matumizi katika Ziwa Victoria.

Rais Kikwete amesema kuwa fedha za ununuzi wa meli hiyo zitatengwa katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/2013 baada ya kuwa maandalizi yote ya ununuzi wa meli hiyo kuwa yamekamilika.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa kazi ya tathmini ya kuzikarabati meli za Mv Victoria, Mv Umoja na Mv Sengerema ambazo zote zinatoa huduma ya usafiri wa abiria na mizigo katika Ziwa Victoria umefanywa na sasa fedha zinatafutwa kwa ajili ya kuanza kazi yenyewe ya ukarabati.

Rais Kikwete ametangaza hayo leo, Jumatatu, Mei 30, 2011, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa eneo la Usagara, Bukumbi, Wilaya ya Misungwi, Mkoa wa Mwanza, kabla ya kuzindua rasmi barabara ya lami ya kilomita 90 kutoka Usagara hadi Geita.

Amewaambia wananchi hao, "Kwa upande wa usafiri katika Ziwa Victoria, ninafurahi kuwafahamisha kwamba mchakato wa kununua meli mpya umeanza. Hivi sasa wataalam washauri, yaani Kampuni ya OSK-Ship Tech ya Denmark, wamekwishakamilisha upembuzi yakinifu juu ya aina ya meli itakayofaa katika Ziwa Victoria."

Ununuzi wa meli hiyo utakuwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mheshimiwa Rais Kikwete wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana wakati alipowaahidi wananchi wa mikoa ya Ziwa kuwa Serikali yake ingenunua meli ya kusafirisha abiria ndani ya Ziwa hilo kuchukua nafasi ya Mv Bukoba iliyozama miaka 1996.

Tokea kuzama meli hiyo miaka 15 iliyopita ambako watu wanaokadiriwa kufikia 1,000 pia walipoteza maisha, Serikali haijapata kununua meli nyingine kwa ajili ya usafiri wa abiria katika Ziwa hilo na wasafiri wameendelea kutumia meli ndogo zaidi.

Mbali na Ziwa Victoria, Rais Kikwete pia aliahidi kununua meli ya abiria katika Ziwa Nyasa kuchukua nafasi ya Mv Mbeya iliyozama katika Ziwa hilo. Aidha, aliahidi kununua meli kwa ajili ya usafiri wa abiria katika Ziwa Tanganyika ambako meli inayosafirisha abiria ya Mv Liemba imekuwa inatumika kwa miaka 100 na imechoka na kuchakaa.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

30 Mei, 2011

Ahadi atatimiza Magufuli.... Mchagueni... aendeleze libeneke...

Nimefurahishwa hapo kwenye taarifa kuwa Bajeti ilishatengwa balaa Meli hakuna... si Mchezo...
 
Mwanza watapata meli kama rais alivyo ahidi, kwani CHADEMA hawatoi ahadi? Acheni upumbavu nyie. Semeni roho inawauma kuona Kikwete anawajibika si mlitegemea atatulia tu ikulu na kuruka majuu, sasa anawaonyeshea kuwa yeye ndio BABA yenu nyie vifaranga wa CHADEMA.

Kuwajibika lini mkuu bado Hatujaiona hiyo meli na Bejeti ilishatengwa na Pesa sijui zimeshaliwa....! sio Wivu Mkuu
 
Kama Mtakumbuka wiki iliyopita mwanajamvi mmoja aliwaambia wanamwanza wamuulize JK kuhusu ahadi yake ya kunua meli mpya ziwa victoria. Majibu ameyatoa, haya hapa:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

JK: Mchakato wa kununua meli mpya umeanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mchakato wa kununua meli mpya kwa ajili ya kusafirisha abiria katika Ziwa Victoria umeanza kwa ajili ya ununuzi wa meli hiyo.

Rais Kikwete amesema kuwa kwa sasa wataalamu washauri wa kupatikana kwa meli hiyo, yaani Kampuni ya OSK-Ship Tech ya Denmark, tayari wamekamilisha upembuzi yakinifu juu ya aina ya meli inayofaa kwa matumizi katika Ziwa Victoria.

Rais Kikwete amesema kuwa fedha za ununuzi wa meli hiyo zitatengwa katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/2013 baada ya kuwa maandalizi yote ya ununuzi wa meli hiyo kuwa yamekamilika.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa kazi ya tathmini ya kuzikarabati meli za Mv Victoria, Mv Umoja na Mv Sengerema ambazo zote zinatoa huduma ya usafiri wa abiria na mizigo katika Ziwa Victoria umefanywa na sasa fedha zinatafutwa kwa ajili ya kuanza kazi yenyewe ya ukarabati.

Rais Kikwete ametangaza hayo leo, Jumatatu, Mei 30, 2011, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa eneo la Usagara, Bukumbi, Wilaya ya Misungwi, Mkoa wa Mwanza, kabla ya kuzindua rasmi barabara ya lami ya kilomita 90 kutoka Usagara hadi Geita.

Amewaambia wananchi hao, “Kwa upande wa usafiri katika Ziwa Victoria, ninafurahi kuwafahamisha kwamba mchakato wa kununua meli mpya umeanza. Hivi sasa wataalam washauri, yaani Kampuni ya OSK-Ship Tech ya Denmark, wamekwishakamilisha upembuzi yakinifu juu ya aina ya meli itakayofaa katika Ziwa Victoria.”

Ununuzi wa meli hiyo utakuwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mheshimiwa Rais Kikwete wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana wakati alipowaahidi wananchi wa mikoa ya Ziwa kuwa Serikali yake ingenunua meli ya kusafirisha abiria ndani ya Ziwa hilo kuchukua nafasi ya Mv Bukoba iliyozama miaka 1996.

Tokea kuzama meli hiyo miaka 15 iliyopita ambako watu wanaokadiriwa kufikia 1,000 pia walipoteza maisha, Serikali haijapata kununua meli nyingine kwa ajili ya usafiri wa abiria katika Ziwa hilo na wasafiri wameendelea kutumia meli ndogo zaidi.

Mbali na Ziwa Victoria, Rais Kikwete pia aliahidi kununua meli ya abiria katika Ziwa Nyasa kuchukua nafasi ya Mv Mbeya iliyozama katika Ziwa hilo. Aidha, aliahidi kununua meli kwa ajili ya usafiri wa abiria katika Ziwa Tanganyika ambako meli inayosafirisha abiria ya Mv Liemba imekuwa inatumika kwa miaka 100 na imechoka na kuchakaa.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

30 Mei, 2011

acha uongo mbona hyo report n ya zaman
 
Akili za wana wa mtaa wa lumumba utazijua tuu akili ndogo kaa panzi alimbizavyo upepo mwishowe hupoteza mwelekeo.
 
Bora angenyamaza kuliko kutoa majibu ya kitoto

watanzania hawataki kusikia neno mchakato umeshaanza huo upuuzi kabisa

miaka kumi mchakato hujafika mwisho? Mtatafutia kura hadi makaburini

aende bukoba na kigoma akapige magoti kuwataka radhi
 
Back
Top Bottom