VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Kwako Zitto,
Najua kuwa sasa wewe ni mwanachama wa chama kipya kitakachozinduliwa tarehe 29 mwezi huu kiitwacho ACT-Tanzania. Najua pia kuwa umekuwa ukihusishwa na chama hiki tangu kilipopata usajili wa muda na baadaye wa kudumu chini ya Mwenyekiti Kadawi Limbu,ambaye pia alianzisha chama cha ADC. Najua tena kuwa wewe Zitto umekuwa ukikanusha na kukana kuhusika na ACT-Tanzania wakati ukiwa CHADEMA. Ukajiunga mara tu ya kufukuzwa uanachama CHADEMA.
Zitto,
Chokochoko za tuhuma dhidi yako za usaliti zilihusishwa na mkakati na jitihada zako za kuwania Uenyekiti wa CHADEMA. Imeaminishwa hivyo ingawa yawezekana isiwe kweli. Mchoro wako unaochorwa ni mtu mzalendo,mpenda mapambano ya kidemokrasia na unayechukia rushwa na ufisadi. Mchoro wako hauoneshi usakatonge wako. Wewe na wapambe wako mmekuwa mkiufurahia mchoro huu. Yaweza ukawa si mchoro sahihi. Onesha ukweli wa mchoro huo sasa.
Zitto,
Tafadhali usigombee nafasi yoyote ya uongozi ndani ya ACT-Tanzania hapo tarehe 29 Machi, 2015. Jioneshe kuwa wewe si msaka madaraka;hukuwa unahusika na ACT-Tanzania tangu mwanzo na kwamba wewe si mpenda vyeo na msakatonge. Ukigombea chochote au kudai umeombwa kugombea chochote, Tanzania itathibitisha pasi na shaka kuwa wewe ndiye mchoraji bora wa michoro ya kisiasa ikuhusuyo ingawa huchori kitu sahihi.
Ni ushauri na rai tu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam