Rai: Waziri aliyetuma SMS kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo awajibishwe!

Kuna mdau kaanzisha thread na kaleta barua nyingi zikionyesha mawasiliano kati ya Maafisa wa Bandari na TRA , naona haionekani tena .Sijui Mods wameificha!
 
Na yule mama hakutaka kumung'unya maneno kamtaja live mbele ya kamera....ila nae PM kwann hakwenda nae wazir mhusika
 
Huyu waziri alikua anaujua uozo ulioko Bandarini. Ni kwanini amuandae huyo mtendaji mkuu wakala wa vipimo? Huyu waziri ni miongoni mwa mawaziri wanaomhujumu Rais Magufuli! Hii ni aibu kubwa kwa mtu mwenye dhamana kubwa kama waziri na hii ni kukosa uaminifu katika kazi za umma.

Hii tabia inatakiwa ikomeshwe mara moja na wengine wajifunze, Waziri mkuu anwajibishe huyu waziri aliyetuma hiyo sms! Maana idingetumwa hiyo sms pengine hali ingekutwa mbaya zaidi na Waziri mkuu kuijua hali halisi ya mazingiza haya.

Nadhani waziri mkuu mwenyewe amejionea na amesikika jinsi snavyohujumiwa na wenzake wazi wazi! sasa achukue hatua mara moja.Hizo flowmetres zingine inamaana isingetumwa sms zote zingekutwa zimegandiana kutu hapo.
Mimi naushangaa sana ujumbe mwingi ktk mtandao huu unaotaka Waziri aliyemwamuru Mkuu wa Vipimo vya mafuta kuhakikisha vinafanya kazi awajibishwe. Kwanza, hatuna hakika kuwa ni kwa sababu ya kujua kwake kwamba Waziri Mkuu aikuwa aende bandarini. Yawezekana alisikia linasemwa tu ktk korido zao kuwa bado mita za mafuta hazifanyi kazi akatoa amri ile. Pili, hata kama alijua kuwa Waziri Mkuu anakwenda, kuwajulisha wa chini yake 'kusafisha nyumba yao' kabla ya ugeni ndio utaratibu wa binadamu, na ni utaratibu wa kiofisi dunia nzima. Tatu, ziara za kushtukiza si za kawaida wala za kiutaratibu wa ofisi na si za kuendelea kushabikia. Ni utendaji kazi wa karne za nyuma, na siyo kazi ya Waziri Mkuu au Rais, isipokuwa katika mwendelezo wa kampeni na kushangiliwa. Mapungufu yaliyoonekana katika ziara za kushtukiza yanaweza kuonekana kiofisi bila shtukizo la Wakuu. Kama yalijificha huko nyuma ni swala la utashi wa viongozi, si kwa sababu haiwezekani kiutaratibu wa kiofisi. Shtukizo zinatakiwa kuwa za vyombo vinavyohusika na jinai na zinafanyika kwa siri na kufanikiwa zaidi kuliko shtukizo za Wakubwa zinazokwenda na vyombo vya habari, hasa picha. Nne, kama kuna makosa makubwa au ya muda mrefu utayajua bila kushtukiza, kama ambavyo humu humu mnajua kuwa mita za mafuta hazikufanya kazi kwa miaka 5 hata kama Waziri Mkuu angezikuta zinafanya kazi jana, kwa hiyo kuamriwa na Waziri kufungua mita za mafuta hakufuniki ukweli wowote. Tano, atakuwa kiongozi wa ajabu sana, awe Waziri au Mkuu wa Vipimo au yeyote, atakayeacha kurekebisha hata chembe ya upungufu mara tu atakapojua kuwa Mkuu anakuja kukagua penye upungufu. Katika mtandao huu tujisahihishe tusije kuwa tunatoa ushauri kuwa: ukisikia Mkuu anakuja, acha uchafu hivyo hivyo aukute huyo Mkuu ili ziara yake ya kushtukiza ifanikiwe.
 
Unapompa mwanao jina ni vizuri kuwa makini eti Muhongo atakuwa hivyo hivyo muongo muongo.
 
Muhongo alishakosa sifa za Uwaziri tangu awamu ya 4. Nashangaa kwanini alirejeshwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kwa nini msione kama muhongo alik
Mimi naushangaa sana ujumbe mwingi ktk mtandao huu unaotaka Waziri aliyemwamuru Mkuu wa Vipimo vya mafuta kuhakikisha vinafanya kazi awajibishwe. Kwanza, hatuna hakika kuwa ni kwa sababu ya kujua kwake kwamba Waziri Mkuu aikuwa aende bandarini. Yawezekana alisikia linasemwa tu ktk korido zao kuwa bado mita za mafuta hazifanyi kazi akatoa amri ile. Pili, hata kama alijua kuwa Waziri Mkuu anakwenda, kuwajulisha wa chini yake 'kusafisha nyumba yao' kabla ya ugeni ndio utaratibu wa binadamu, na ni utaratibu wa kiofisi dunia nzima. Tatu, ziara za kushtukiza si za kawaida wala za kiutaratibu wa ofisi na si za kuendelea kushabikia. Ni utendaji kazi wa karne za nyuma, na siyo kazi ya Waziri Mkuu au Rais, isipokuwa katika mwendelezo wa kampeni na kushangiliwa. Mapungufu yaliyoonekana katika ziara za kushtukiza yanaweza kuonekana kiofisi bila shtukizo la Wakuu. Kama yalijificha huko nyuma ni swala la utashi wa viongozi, si kwa sababu haiwezekani kiutaratibu wa kiofisi. Shtukizo zinatakiwa kuwa za vyombo vinavyohusika na jinai na zinafanyika kwa siri na kufanikiwa zaidi kuliko shtukizo za Wakubwa zinazokwenda na vyombo vya habari, hasa picha. Nne, kama kuna makosa makubwa au ya muda mrefu utayajua bila kushtukiza, kama ambavyo humu humu mnajua kuwa mita za mafuta hazikufanya kazi kwa miaka 5 hata kama Waziri Mkuu angezikuta zinafanya kazi jana, kwa hiyo kuamriwa na Waziri kufungua mita za mafuta hakufuniki ukweli wowote. Tano, atakuwa kiongozi wa ajabu sana, awe Waziri au Mkuu wa Vipimo au yeyote, atakayeacha kurekebisha hata chembe ya upungufu mara tu atakapojua kuwa Mkuu anakuja kukagua penye upungufu. Katika mtandao huu tujisahihishe tusije kuwa tunatoa ushauri kuwa: ukisikia Mkuu anakuja, acha uchafu hivyo hivyo aukute huyo Mkuu ili ziara yake ya kushtukiza ifanikiwe.
Hata mimi nawashangaa hawa sijui GT...kwani Muhongo ni mratibu wa ziara za waziri mkuu za kushtukiza ...kwa nini wasione kuwa alikuwa ana act kunusuru taifa kuendelea pata hasara...yani wana kimbilia ku conclude kuwa aim ilikuwa kuwa rescue hawa watendaji...huyu mzee sijui amewakosea nini????kwani hana mamlaka ya kutoa order????!!!!
 
Kama
Yule Mkurugenzi kataja kabisa kwamba aliyemtumia sms ni Sospeter Muhongo.
Ingawa Waziri alituma sms ambayo pia ni moja ya mawasiliano yasiyo rasmi, lakini bado huyo Mkurugenzi kaonesha udhaifu mkubwa. Hakupaswa kuongea kwamba nilitumiwa sms. Sijui alibebwa huyo mama!!! Nae ni jipu bila shaka. Asipolitumbua Waziri Mkuu, Muhongo lazima atalikamua, maana limeota pabaya.[
Huyu Professor mjivuni ni shida,sasa naamini hata mchongo wa EPA alishiriki,kama siri ya safari ya waziri mkuu anaisema kwa mtu mdogo kama mkurugenzi wa vipimo,kiapo aliocho apa kuwa atalinda siri za serikali kiko wapi,na alitaka umma udanganywe kwa manufaa ya nani,si ajabu watu wanahangaika wapate uwaziri ili waendelee kutafuna nchi,lakini pia raisi anastahili lawama kwa uteuzi huu mbovu,mtu akituhumiwa hafai kushika madaraka,au amesahau usemi wa mke wa kaisari hatakiwi kutuhumiwa,pia watu walishangazwa na uteuzi wa huyu professor ,lakini Mungu ni mkubwa kamuonyesha Mheshmiwa raisi mapema kuhusu huyu mtu,na huyu nae ndie eti alitaka awe raisi,pia ndio maana hata watu walishangaa Maswi alipoteuliwa kuwa Naibu Kamishna mkuu wa TRA,wengine tulishangaa kuwa sasa raisi wetu kafikwa na nini na hizi teuzi za hovyo hovyo,na mwisho asisahau kuwa muonja asali,haonji mara moja.
 
SIJUI WENZANGU NIMESOMA STORY ZA MAFUTA NA MABARUA YALE NIMEGUNDUA N ,MCHEZO MREFU SANA SANAA NA WASIKU NYINGI...SI HAPO OMBI LANGU KWA MH WAZIRI MKUU TUMEMSIMAMISHA HUYU JIPU ALIIEFUNGA HIZI MITA MBONA AMJALITUMBUA JIPU ALIEMWAMBIA ATAFUTE MAFUNDI HARAKA

HIVI AMWONI DHAMBI...HUYU ALIETUMA MSG WAZIRI ALIKUWA ANATAKA KUFICHA NINI

MH RAIS EMBU KAENI MSIPEPESE MACHO VUENI JIPU HILO LITAWATUMBUKIA KABLA AMJAAZAA NALO MUULIZENI MSTAAFU

USIKUMWEMA
 
Mkuu, unajua psychology ya kutambika?

Labda utuambie waziri kosa lake ni lipi ambalo linafanya astaili kufukuzwa? Je, hilo la meseji tu au kuna lingine? Kama ni meseji....Basi sio kosa la kumfukuzisha mtu kazi.
 
Back
Top Bottom