Radio Imaan, Shura ya Maimamu, Basuta na Bakwata Mnatudhoofisha Waislam kwa siasa za Tanzania

Umefanya Utangulizi Mzuri sana, lakini bado hauja unganisha kichwa cha habari na habari yenyewe. Nina Maana ni jinsi gani hao uliowataja wanahusika na malalamiko yako.

Radio imani siku hizi kila siku lazima waje na mada ambayo majadiriano yake ni ya kisiasa! na mbaya zaidi siasa za kukilinda chama kimoja na kukishambulia chama kingine (huo ni mtazamo wangu) Mie nilitegemea kama wangeamua kuingia katika siasa basi wangekuwa balanced wangemnusuru anayedhurumu na anayedhurumiwa hiyo ndiyo dini ya ALLAH inavyotaka.

Sasa wao Radio iman kuungana na Shura ya maimamu,Basuta na baadaye Bakwata (habari ya Mkuu wa wilaya ya igunga) Kutengeneza mada za kisiasa zitakazopelea uma huu wa kiislam kuwachukia wakristo wakati wengine ni ndugu zetu tunaishi nao nyumba kwa nyumba, maofisini, mashuleni n.k si busara kabisa!

Huwezi kuuondoa munkari kwa munkari mwingine! Ni kweli waislam tuliaachwa nyuma pengine kwa maksudi au kwa bahati mbaya la muhimu hapa si kutengeneza mazingira ya chuki na baadae inaweza kuzuka vita bali nikutafuta njia sahhi nasi tufikie au tuvuke walikofikia wakristo.

Haitatokea hata siku moja eti nchi hii ikawa ya waislam tu! Aliondoka Mtume (SWA) akawacha makafiri na kiama kitasimama bado wanaompinga ALLAH wapo ndiyo maana kuna pepo na moto.
 
Naomba kuuliza. Hivi kuna taasisi ngapi zinazotolea matamko masuala ya waislam Tanzania
1. BAKWATA
2. SHURA YA MAIMAM
3. WANAHARAKATI WA HAKI ZA KIISLAM
4. RADIO IMAN
5. BARAZA LA MAULAMAA
6. SHIA ITHNAASHERI JAMAAT
7. ISMAILIA JAMAAT
8. BOHORA JAMAAT
9. BARAZA LA SUNNA TANZANIA
10. SHEIKH KUNDECHA(Sikumbuki anawakilisha platform ipi)

Hivi katika hali kama hii proper organization itatoka wapi?

Mi nafkiri waislam tungeanza na kuweka our own house in order.
Tuweke priorities za waislamu ni zipi, both za kiibada na kidunia. Hakuna huu upuuzi wa kulalamika tu kusikoisha, while busy pointing the
finger to fault all others BUT ourselves.

Mathalan, sasa hivi kuna millions wa muslims lakini hakuna mfumo mzuri wa kukusanya zakaat, moja kati ya nguzo tano za uislam.
Na hizi zakaat kama zingekusanywa kwa viwango alivyopendekeza Allah, na kusimamiwa vizuri, zingetosha kabisa kuendesha Mahakama
ya Kadhi, na other charities za kijamii bila kuitegemea serikali kuu.

Badala yake kama alivyosema muanzisha mada, BAKWATA na BASUTA wamekua watumwa wa vyama vya siasa na kusahau kabisa wajibu
na nafasi yao juu ya umma wanaouongoza. Its a pitty, to live and witness these times.

Thanks, well said brother.Muslim leaders should work on what you've just proposed instead of keeping on dancing the ccm song! Or lamenting on nonsense as long as CDM is involved!
 
The issue here is not a solution... situation ilivyo we have to be wise to make choices: between ccm/cuf/cdm

Ukiangalia (kwa wale tunaoshiriki katika uongozi wa kiislam) when it comes to muslims interests...there is no difference.

CCM=CDM=Maaskofu...

Kwa ufupi msimamo wa chadema na ccm na maaskofu kuhusu madai yetu ni moja..so what is the choice?

We go for lesser evil...chama ambacho leo kinavua hijabu, kinamsimamisha padre what will happen wakichukua dola?

Tutaendelea kupambana hadi Muumba wetu atakapotuchukua au haki itakapopatikana
Unalalamika kuwa cdm kinavua hijabu ukijua wazi kuwa waliofanya hivyo hawakuagizwa na cdm. Mchemba mwigulu kafumaniwa na mke wa kada wa ccm, je ni busara kusema ccm ni wazinzi?

Unasema cdm wamemsimamisha padre, nani kakwambia padre, sheikh, au mchungaji anakatazwa kugombea uongozi wa siasa? Nadhani pia unasumbuliwa na udini au wivu na chuki dhidi ya kanisa katoliki. Unajaribu kuhamishia maji ya bahari ya hindi ktk ziwa Rukwa.

Unasema mtaendelea kupambana hadi muumba atakapowachukua. Kupambana na nani? Kwa nini upigane vita ambayo una uhakika utashindwa? Hayo ni mafundisho ya dini au madhehebu gani? Unataka kutuaminisha kuwa Uislam unafundisha vurugu, mapambano na mafarakano? Rafiki zangu ambao ni waislam wanapingana na dhana hii.

Nakushauri uzingatie mafuzo ya dini yako.

U say ccm=cdm=maaskofu, and that u go for the lesser evil. Evil is evil. Is this islamic teaching or ur teachings or cheatings? U may wish to join islamic theological college.
 
Naomba kuuliza. Hivi kuna taasisi ngapi zinazotolea matamko masuala ya waislam Tanzania
1. BAKWATA
2. SHURA YA MAIMAM
3. WANAHARAKATI WA HAKI ZA KIISLAM
4. RADIO IMAN
5. BARAZA LA MAULAMAA
6. SHIA ITHNAASHERI JAMAAT
7. ISMAILIA JAMAAT
8. BOHORA JAMAAT
9. BARAZA LA SUNNA TANZANIA
10. SHEIKH KUNDECHA(Sikumbuki anawakilisha platform ipi)

Hivi katika hali kama hii proper organization itatoka wapi?

Mi nafkiri waislam tungeanza na kuweka our own house in order.
Tuweke priorities za waislamu ni zipi, both za kiibada na kidunia. Hakuna huu upuuzi wa kulalamika tu kusikoisha, while busy pointing the
finger to fault all others BUT ourselves.

Mathalan, sasa hivi kuna millions wa muslims lakini hakuna mfumo mzuri wa kukusanya zakaat, moja kati ya nguzo tano za uislam.
Na hizi zakaat kama zingekusanywa kwa viwango alivyopendekeza Allah, na kusimamiwa vizuri, zingetosha kabisa kuendesha Mahakama
ya Kadhi, na other charities za kijamii bila kuitegemea serikali kuu.

Badala yake kama alivyosema muanzisha mada, BAKWATA na BASUTA wamekua watumwa wa vyama vya siasa na kusahau kabisa wajibu
na nafasi yao juu ya umma wanaouongoza. Its a pitty, to live and witness these times.

Mashallah! ndugu yangu katika imani hayo uliyasema ni muhimu kabisa
 
Islam ni dini iliyokamilia!

Haiitajiki abadani nasema!! mfumo mwingine toka nje ya uislam ili utendeke au ufanye kazi sawia! Uislam ni mfumo pekee ambao hukuacha chochote! yani hata jinsi ya kunya (kujisaidia mtaniwia radhi) dini hii imefundisha.

Ole wenu nyie shura ya maimamu, ole wenu ninye basuta, ole wenu ninyi bakwata ole wenu nyie radio imani kwa kuichukua dini yetu hii tukufu na kuifanya mseto na siasa chafu za Tanzania!!! na kutudhoofisha waislam wote ulimwenguni haki hamtakuwa na majibu ya kumpa ALLAH siku saa itakaposimama.

Leo Kagame wa Rwanda anaupromoti uislamu Rwanda kwa kuwa katika maafa ya Rwanda ni waislam pekee ambao walisimama katika dini hawakujichanganya na mavyama au makabila ! hawakujiusisha kabisa na vita ile mbaya kwa sababu Uislam uliwakataza kutambuana kwa makabila.

Leo nyie mnatugawa kwa sababu ya mavyama wakati dini haitaki haki mnafanya dhulma kubwa. Allah akuongozeni na mrejee katika mstari.
chadema ni wadini naungana na bakwata na wanazuoni kuilaani
 
Yap mkuu,
Unajua dini yetu ilivyo yani ilipo haki ikubali hata kama inatoka kwa shetani ili mradi tu iwe ni haki ichukue na umwache shetani na ushetani wake! lakini pia dini yetu imeharamisha kukata undugu. Hivi leo kama ndugu yangu atakuwa ni mwanachama wa cdm eti naambiwa nimtenge khaa! matamko gani haya ya ajabu ajabu!
Sisi wenyewe waislam wa inchi hii hatuko sawa kutwa kucha tunapingana leo hawa idd kesho wengine halafu tunajifanya na matamko ya pamoja kwa mambo ya kipuuzi ambayo Allah ameyaharamisha!!
Hivi kweli sisi waislamu wa nchi hii hatuwezi kushikamana kwa mambo ya muhimu tukashikamane kwa siasa hizi za kizandiki! hatuna mashule, hatuna mahospital hatuna mavyuo tumebaki kutumika tu! jamani hivi mpaka lini??
haraam ikiwa kwa cdm vp kwa vyengine,mche Allah kama kweli ni muislam,kuna mitandao ya dini njoo tujifunze dini
 
chadema ni wadini naungana na bakwata na wanazuoni kuilaani

Janga lingine la kitaifa hili? Hivi nyie watu, lini mtakubali kuacha kutumika kama c.nd.m? Mnaacha kupambana na yule aliyewarudisha nyuma mnakazana na cdm ambao wanawatetea wote.

Na tazama busara za cdm, pamoja na kuwaandama mnakoagizwa na ccm kamwe hawajawahi kuwa attack waislam kama taasisi, wanadeal na mafisadi bila kujali muislam au mkatoliki.

Hebu nambie, katika list of shame ya mwembe yanga, Islam as institution imetajwa popote?

Amkeni ndugu zangu, acheni kupambana na wasiohusika.
Kwani mmeshawahi sikia lolote la cdm kuhusu kadhi?
 
Islam ni dini iliyokamilia!

Haiitajiki abadani nasema!! mfumo mwingine toka nje ya uislam ili utendeke au ufanye kazi sawia! Uislam ni mfumo pekee ambao hukuacha chochote! yani hata jinsi ya kunya (kujisaidia mtaniwia radhi) dini hii imefundisha.

Ole wenu nyie shura ya maimamu, ole wenu ninye basuta, ole wenu ninyi bakwata ole wenu nyie radio imani kwa kuichukua dini yetu hii tukufu na kuifanya mseto na siasa chafu za Tanzania!!! na kutudhoofisha waislam wote ulimwenguni haki hamtakuwa na majibu ya kumpa ALLAH siku saa itakaposimama.

Leo Kagame wa Rwanda anaupromoti uislamu Rwanda kwa kuwa katika maafa ya Rwanda ni waislam pekee ambao walisimama katika dini hawakujichanganya na mavyama au makabila ! hawakujiusisha kabisa na vita ile mbaya kwa sababu Uislam uliwakataza kutambuana kwa makabila.

Leo nyie mnatugawa kwa sababu ya mavyama wakati dini haitaki haki mnafanya dhulma kubwa. Allah akuongozeni na mrejee katika mstari.

Hapo kwenye red ninachoweza kusema ni kwamba: "If the theory doesn't fit the practice, ignore the theory!"
 
kama waislam wanasema cdm ina maslahi na wakristo,(mfumo Krist) ndo maana wao wam eamua kuwakumbatia sisiem? ili hali hawajaliwi?
 
Radio imaan wachokozi sana nilishawahi kuwasikia wakisema serikali ya ccm inawabagua waislamu kielimu hasa katika chuo cha udaktari kibaha eti waliohitimu mwaka huu waislamu walikuwa 25 tu. Kutokana na upendeleo wa serikali.
 
Heee!! tusipoangaluia Udini huu tumekwisha.
 
Back
Top Bottom