Pwani: Magari yagongana uso kwa uso, wanne wafariki

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
azamtvtz_1691056381981.jpeg
azamtvtz_1691056381981 (1).jpeg


Watu wanne wamefariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Prado walilokuwa wamepanda kugongana uso kwa uso na gari ya mzigo aina ya Scania majira ya saa nane usiku katika eneo la Mapatano, Kata ya Mbwewe, Halmashauri ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Waliofariki katika ajali hiyo ni dereva wa Toyota Prado, pamoja na abiria watatu waliokuwa kwenye gari hilo.

Kamanda ya Polisi Mkoa wa Pwani, Piusi Lutumo, amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Prado ambaye alihama upande wake na kugongana uso kwa uso na gari hilo la mizigo.

Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika Zahanati ya Lugoba mkoani Pwani kwa ajili ya uchunguzi na kutambuliwa na ndugu wa marehemu.

CHANZO: AZAM TV

===

Ajali ya gari, iliyotokea jana Jumatano usiku katika kijiji cha Mapatano, Kata ya Mbwewe, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani, imepoteza maisha ya Mkurugenzi wa Benki ya ABSA na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Tawi la Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo kupitia taarifa yake iliyotolewa leo Alhamisi Agosti 3, 2023 na kusainiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutuma.

Katika taarifa hiyo, imesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana Agosti 2, saa 2:30 usiku, ikihusisha gari aina ya Toyota Prado na Scania. Taarifa hiyo imebainisha kuwa gari ya Toyota Prado ilikuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, na kwamba ilikuwa ikiendeshwa na Nechi Msuya, huku Scania ilikuwa ikitokea Arusha na kwamba iliendeshwa na Philipo Mtisi.

Taarifa hiyo iliwataja waliofariki kwenye jali hiyo kuwa ni Nechi Msuya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 45 hadi 50, Dayana Mageta, mfanyabishara na makazi wa Dar es Slaam anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hadi 45, Nora Msuya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hadi 45 ambaye ni mwalimu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Tawi la Dar es Salaam, na abiria wa kike ambaye jina lake halikufahamika na anakadiriwa kuwa na miaka 30 hadi 35. Polisi imeeleza chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Prado kuhama kutoka upande wa kushoto wa barabara kwenda upande wa kulia kisha kogongana uso kwa suo na lori hilo. (Imeandikwa na Nasra Abdallah)

 
Kila siku tunapiga kelele suala la upanuzi wa barabara ya Morogoro road, line mbili za kupishana zitaendelea kusababisha ajali kila siku

Kuna haja ya upanuzi wa hivi barabara serikali iangalie hili ni muhimu sana maana hizi barabara inatumiwa sana na magari mengi na ndio inayofungua nchi.
 
Umejenga majumba makubwa Tabata, kisirisiri ili mumewe asijue, sasa sijui itakuaje? Kamq nakiona vile kibenten chake kikiwa tajiri.

Mumewe alikua haongei chochote kwake cz pesa hana

Natoka muda wowote saa yeyeto, naenda nchi za njee nakaa miezi hadi mwaka, sitaki mume unipangie pesa ni zangu elimu ni yangu
 
Back
Top Bottom