Proper recording: Nini kilimbadili Mzee Mwanakijiji?

Nimezipitia hoja za MMM ni hoja nzuri zenye malengo ya kutuongoza hapa tulipo na kule tunapoelekea je watanzania wako tayari kuyakubali mabadiliko kifikra zaidi. wakati furani sizani kama CDM kimekubali mabadiliko na kuondokana na malumbano ya kila siku na yasiyo na majibu, Tujishahihishe
 
aje mwenyewe atujuze ila nina uhakika MMM alikuwa hapati kitu chochote toka ccm bali ccm wenyewe ndio waliomchosha hadi kumbadilisha.

Je inawezekana sasa huko aliko anapata alichokitaka baada ya kukikosa ccm?
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji,ebu kuwa fair kwa chadema tafadhali,ni ombi tu mkuu!Ebu ona unavyojichanganya na kutuchanganya at the same time...Hapo chini ni kigezo kuhusu mgombea ama kiongozi wa chadema.

Lakini tena kipimo chako wakati wa JK kilikuwa hicho hapo chini...

Mkuu hizo ni double standards zinazoonyesha uonevu wa wazi kabisa!

basi uwe unasoma kitu ambacho wewe mwenyewe unanukuu; usichukue neno moja; na usome toka mwanzo. Vinginevyo itabidi nianze kwenda pole pole na kunyambua neno baada ya neno. Nimesema sababu za "kisiasa" halafu nikaendelea... kama haikueleweka ningeweza kuingia ndani zaidi..
 
1.MKJJ yuko katika payroll ya Serikali katika kazi ya usalama wa Taifa. Majukumu yake hayafuati muundo wa kawaida(organogram) uliopo.

2. MKJJ ni mhitimu wa shahada ya kwanza (BA in Political Science)- Tanzania na pia Shahada ya uzamili (MA in Mass Communication & Media Arts)- USA. Baadaye alifaulu vizuri sana mafunzo ya upelelezi (Intensive course in Nationalism & Espionage) – Cuba chini ya Mwalimu wake gwiji aliyempenda sana kwa jina Mosses Powel . Hii inaeleza sababu ya MKJJ kupewa nafasi ya kuwa muhudumu (Usher) mmojawapo katika mazishi ya Powell 22.01.2005. Alipelekwa pia Trinidad & Tobago kwa ajili ya mafunzo ya ukakamavu na ulinzi wa kujikinga chini ya kitivo cha Powell ambaye ndiye mwanzilishi wa mashambulizi ya Sanuces Ryu Jujutsu lakini bahati mbaya MKJJ hakuwa mzuri sana katika somo hili.

MKJJ baada ya kushauriwa , alichagua kuendelea zaidi kubobea katika mbinu za kipepelezi za steganografia (steganography), Saitografia (Cytography) na Utafiti (Research) siraha zilizompa nafasi kupata mazoezi kwa njia ya vitendo katika Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Ministry of Defence).

3. Kwa sasa MNKJJ anafanya kazi ya kunusa na kuwachanganya Watanzania kwa kuandika na kuongea kwa style ya kukandia Serikali kwa sana kupitia majamvi na majukwaa mbalimbali kama vile JF na magazeti mbalimbali yaliyo katika mtandao.

4. Kwa kutumia utaalamu wake wa sanaa na fani ya uandishi na utangazaji, MKJJ anajificha ndani ya mbinu ya kijasusi ijulikanayo kama ‘The Italian Strategy of Tension with False Flag'. Ingawa ni mwanachama CCM lakini anapokuwa mtandaoni huvaa ngozi ya mbwa mwitu na kujiita Mkuu wa Taasisi ya Kitanzania ya Demokrasia, Maendeleo na Amani (TAKIDEMA). Kazi zake ni kama ifuatavyo:-

a. Kuanzisha mada chokozi (provocative topics) zenye kuleta hisia kali akisukuma makombora kwenye Serikali ikiwa ni namna ya kuwachokoza wananchi ili mnapoanza kusema au kuandika basi yeye anachukuwa notisi zake na kuwakabidhi waliomtuma kwa ajili ya kurekebisha panapotakiwa haraka iwezekanavyo mfano katika moja ya jibu lak leo humu katika thread hii amesema aliyependekeza IGP Mahita aondolewe na ndie alitoa pendekezo la kugawa Dar-es-Salaam kama mikoa ya polisi (kanda). Pendekezo hili lilichukuliwa mara moja.. Hadhira yake kusudiwa ni hasa Watanzania walioko nje na hususani wasomi ambao wanaweza kuleta upinzanina ndio hawa aliokwaruzana nao wakati anapinga swala la uraia wa nchi mbili. sababu iko wazi nayo ni "you are either with us or against us.....I'M out!!

Na kuna watu kabisa wamekaa huko wakasoma na kuamini! Dr. Who (basi mfanye googling basi)! kadizoooo
 
yani mtoa mada unataka mtu awe na mawazo aliyokuwa nayo mwaka 2006,?masikhara haya!
 
Anyway wether umesema au lah si issue, kwani lengo langu ni kujadili na si kubishana.Sijui umekiri au ni lugha tuu kuwa na options chache kuwa CDM wanauwezo wa kujipanga kuchukua madaraka.Sijui kama wana uwezo na nia nini tena mnataka washauri?

Umekiri kuwa wana mtaji mkubwa wa mapenzi ya watu wengi.Ila ujue pia utakuwa na kipindi kigumu sana kukataa kuwa huo mtaji umejengwa kwa mipangilio na uongozi bora na si vinginevyo.Sasa hivi CDM ni envy kwa vyama vingine.Hizi blah blha kuwa CCM imechokwa ua inashindwa haiwezi explain kwa nini Si CUF ,NCCR au mwingine aliyekuwa juu ya CDm anaweza grab chochote.Kwa sasa CDM wanaonewa wivu mpaka na watu wasiojua wachukue njia ipi kujiingia katk siasa.Watu waliochelea ingia CDM na sasa wanajiuliza mswali ingia CCM sasa wanishia kupata hasir ana wivu.Kwa vile wanaona wamechelewa jiweka mahali pa kupata ubunge wa bwerere kama wa CCM.

Kama CDM wameweza beat all odds na kuweza vuta mapenzi ya watu wote hata wale wanaofundishwa ktk makundi yao kuwa CDM si ya kwao, bado wanaruka ukuta wakawe na mpenzi wao mpya CDM, wamekuwa na mipango inayowavunja hadi wapinzani kwanini unsema hawastahili?Kwangu naona kama vile wale watoto wa Dar, wanaoona kijana wa mkoani akipendwa na warembo kiasi cha kuwa na uhuru wa kuchagua wakati mabishoo wa wa mjini wakijituma sana kujaribu tumia fahari zao.Mwisho huishia sema kuwa huyu jamaa hastahili mchukua huyu demu.Huyu ni mrugaruga tuu...Hapo ndio unajiuliza nani wa kusema mwanamume anastahili au lah?Kama raia watapiga kura na CDM kushinda kwani utumie neno hash hivi kuwa "si wanastahili?"

Tupe maelezo.

Nitakuambia kitu kimoja (au viwili) na vinahusiana. Watu wengi wana mapenzi sana na CDM si kwa sababu wanajua CDM itafanya nini; wana mapenzi kwa sababu wanajua CCM imefanya nini. NI mapenzi yanayotokana na chuki. Mapenzi haya hayakuanzia CDM; baada ya vyama vingi kurudi wale waliokuwa wamechoshwa na CCM mara moja wakajitambua kuwa ni wapinzani na wakaenda nyuma ya wale waliokuwa wanaipinga CCM. Nakumbuka vizuri sana 1995 nilimpigia kura Mrema; tulikuwepo watu wengi ambao tulichagua NCCR kwa sababu ya kuchoshwa na CCM na kutaka kitu kipya.

Lakini na pili na hili ni kubwa sana natumaini utalizingatia; wengi ambao tumekuja kuiunga mkono CDM na kuisaidia tunafanya hivyo kwa sababu ya kuamini kuna potential ya kuweza kuja kushika madaraka. Ni potential hii ambayo inawapa watu wengi matumaini kuwa CDM ikitulia, ikajipanga na kujitengeneza kweli inaweza kuwa chama cha kuweza kushika madaraka. Sasa usifikirie kupendwa kunakotokana na hili kunatosha. La hasha! Na itakuwa ni makosa makubwa zaidi kufurahia vigelegele, chereko na shangwe na kuamini kuwa hawa watu watakuwa pale siku zote kwa vile CDM inapendwa.

Watu wanaipenda kwa sababu wanaichukia CCM na hawaoni mwingine wa kumpenda na wanaipenda kwa sababu inawapa matumaini kuwa inaweza kuwa. Binafsi, sasa hivi nitafanya yote ninayoweza kuweza kusaidia CDM ishinde na kufanya vizuri zaidi 2015. Lakini siko tayari kusaidia ili ipate wabunge wengi na ijipange tena kwa 2020! utakuwa ni wazimu. Kama haitajipanga kushika madaraka ya nchi 2015 wakaendeleea na status quo itakuwa ni jukumu la dhamiri kuanza kuipinga kwa sababu itakuwa inasimama kama kikwazo; watu wanatumaini lakini tumaini halilipi!

Utanielewa baadaye nikimaliza kazi ya tatu ya CDM kuelekea 2015. Usinielewe vibaya kabisa CDM ndani ya miaka hii mitatu imefanya vizuri lakini vile vile tunashuhudia its weakest points na hizo zinatisha zaidi kwani hazikuwepo 2010! think about it.
 
1.MKJJ yuko katika payroll ya Serikali katika kazi ya usalama wa Taifa. Majukumu yake hayafuati muundo wa kawaida(organogram) uliopo.

2. MKJJ ni mhitimu wa shahada ya kwanza (BA in Political Science)- Tanzania na pia Shahada ya uzamili (MA in Mass Communication & Media Arts)- USA. Baadaye alifaulu vizuri sana mafunzo ya upelelezi (Intensive course in Nationalism & Espionage) – Cuba chini ya Mwalimu wake gwiji aliyempenda sana kwa jina Mosses Powel . Hii inaeleza sababu ya MKJJ kupewa nafasi ya kuwa muhudumu (Usher) mmojawapo katika mazishi ya Powell 22.01.2005. Alipelekwa pia Trinidad & Tobago kwa ajili ya mafunzo ya ukakamavu na ulinzi wa kujikinga chini ya kitivo cha Powell ambaye ndiye mwanzilishi wa mashambulizi ya Sanuces Ryu Jujutsu lakini bahati mbaya MKJJ hakuwa mzuri sana katika somo hili.

MKJJ baada ya kushauriwa , alichagua kuendelea zaidi kubobea katika mbinu za kipepelezi za steganografia (steganography), Saitografia (Cytography) na Utafiti (Research) siraha zilizompa nafasi kupata mazoezi kwa njia ya vitendo katika Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Ministry of Defence).

3. Kwa sasa MNKJJ anafanya kazi ya kunusa na kuwachanganya Watanzania kwa kuandika na kuongea kwa style ya kukandia Serikali kwa sana kupitia majamvi na majukwaa mbalimbali kama vile JF na magazeti mbalimbali yaliyo katika mtandao.

4. Kwa kutumia utaalamu wake wa sanaa na fani ya uandishi na utangazaji, MKJJ anajificha ndani ya mbinu ya kijasusi ijulikanayo kama ‘The Italian Strategy of Tension with False Flag’. Ingawa ni mwanachama CCM lakini anapokuwa mtandaoni huvaa ngozi ya mbwa mwitu na kujiita Mkuu wa Taasisi ya Kitanzania ya Demokrasia, Maendeleo na Amani (TAKIDEMA). Kazi zake ni kama ifuatavyo:-

a. Kuanzisha mada chokozi (provocative topics) zenye kuleta hisia kali akisukuma makombora kwenye Serikali ikiwa ni namna ya kuwachokoza wananchi ili mnapoanza kusema au kuandika basi yeye anachukuwa notisi zake na kuwakabidhi waliomtuma kwa ajili ya kurekebisha panapotakiwa haraka iwezekanavyo mfano katika moja ya jibu lak leo humu katika thread hii amesema aliyependekeza IGP Mahita aondolewe na ndie alitoa pendekezo la kugawa Dar-es-Salaam kama mikoa ya polisi (kanda). Pendekezo hili lilichukuliwa mara moja.. Hadhira yake kusudiwa ni hasa Watanzania walioko nje na hususani wasomi ambao wanaweza kuleta upinzanina ndio hawa aliokwaruzana nao wakati anapinga swala la uraia wa nchi mbili. sababu iko wazi nayo ni “you are either with us or against us.....I'M out!!

this shit is old but funny as hell
 
Umenikumbusha mbali sana, ndio mchakato wenyewe wa mabadiliko huo. Hakuna kisichobadilika isipokuwa mabadiliko

Mzee Kitilanimekusoma sana, hapo umepasua jipu. Labda kwa kuongezea mkumbushe muanzisha mada kuwa ndiyo maana ya kuwepo usiku na mchana.
 
basi uwe unasoma kitu ambacho wewe mwenyewe unanukuu; usichukue neno moja; na usome toka mwanzo. Vinginevyo itabidi nianze kwenda pole pole na kunyambua neno baada ya neno. Nimesema sababu za "kisiasa" halafu nikaendelea... kama haikueleweka ningeweza kuingia ndani zaidi..
Madhara ya unachokisema hayaangalii kama uliyasema kwasababu ya kisiasa wala kidini wala chochote.Nimekusoma vyema kabisa na nimenukuu pale ambapo panaonyesha hoja yako ya msingi kabisa.

Kama ulitumia sababu ya kisiasa kukubaliana na JK kwasababu ya watu wengi kumsapoti,je ni sababu gani uliyoitumia kutokukubaliana na watu wengi wanaomsapoti mgombea wa chadema?
 
Nitakuambia kitu kimoja (au viwili) na vinahusiana. Watu wengi wana mapenzi sana na CDM si kwa sababu wanajua CDM itafanya nini; wana mapenzi kwa sababu wanajua CCM imefanya nini. NI mapenzi yanayotokana na chuki.
Ukisoma katiba ya chadema huwezi kujuwa watakachokifanya?Ndiyo maana nikasema contextually,wewe hukubaliani na uongozi wa chadema.

Watakachofanya chadema,kila siku viongozi wake wanahubiri majukwaani,ni kinyume kabisa na walichofanya ccm kwa miaka 50 toka uhuru!
 
Madhara ya unachokisema hayaangalii kama uliyasema kwasababu ya kisiasa wala kidini wala chochote.Nimekusoma vyema kabisa na nimenukuu pale ambapo panaonyesha hoja yako ya msingi kabisa.

Kama ulitumia sababu ya kisiasa kukubaliana na JK kwasababu ya watu wengi kumsapoti,je ni sababu gani uliyoitumia kutokukubaliana na watu wengi wanaomsapoti mgombea wa chadema?

mgombea gani? kama unasema 2005 ni sababu ile ile ya kisiasa. Lakini ukumbuke 2010 nilimuunga mkono mgombea wa CDM kwa sababu za kisiasa vile vile pamoja na kuwa aliungwa mkono na watu wengi.
 
Ukisoma katiba ya chadema huwezi kujuwa watakachokifanya?Ndiyo maana nikasema contextually,wewe hukubaliani na uongozi wa chadema.

Watakachofanya chadema,kila siku viongozi wake wanahubiri majukwaani,ni kinyume kabisa na walichofanya ccm kwa miaka 50 toka uhuru!

thats exactly my point...

Unajua watafanya nini kuhusu usalama wa taifa? watafanya nini kuhusu polisi? watafanya nini kuhusu elimu yajuu? hivi umesoma lini kweney hiyo mikutano ya majukwaani ambacho CDM watakifanya. Nitafutie mkutano mmoja wa karibuni ambapo CDM wamesema wao wakiingia madarakani watafanya nini kunipa mfano.
 
Nilishawahi kusikia kwamba elimu itakuwa bure licha ya kwamba sikumbuki vyema the details.Pia nilisikia issue kama mfuko wa sementi kuwa elfu tano.Kwa ujumla,walisema watalishghulikia pia tatizo la mfumuko wa bei.

Hayo ya polisi na mengineyo,nakubali kuwa wanaweza kuyazungumzia.Lakini kumbuka hata mwalimu alipochukuwa nchi,hakujuwa alifanyie nini jeshi hadi pale aliponusurika kupinduliwa.

Kiukweli mkuu,ninaamini kwamba hayo maeneo yote yanahitaji overhaull,na ninaamini kwamba kuiondoa ccm madarakani ni kama uhuru wetu wa pili.Only this time ni kutoka kwa mkoloni mweusi.

Ninachoweza kusema,ni kweli nakubaliana na wewe kwamba wanatakiwa waseme ni kwa kivipi wataoperate,licha ya kwamba wanajitofautisha na ccm,lakini ni vyema wakatanabaisha kuwa mabadiliko hayo yatakuwa ya namna gani.

Lakini ebu tuchukulie tu mfano mmoja wa serikali za majimbo,je hujui namna zinavyo operate ama mfumo huo unavyofanya kazi?

Je hujui namna serikali isiyokuwa na ufisadi namna inavyo operate?

Hujui ni namna gani mikataba ikiingiwa kwa manufaa ya taifa ni kwa namna gani wananchi watanufaika na mikataba hiyo?

Hayo tu yenyewe yanaweza kukupa mwangaza kwa mbali.Lakini hilo la kuwepo na details,nadhani ni suala ambalo wanahitaji kulifanyia kazi.

Pia unaposema hujui watafanya nini kuhusu usalama wa Taifa una maanisha kitu gani?Kwamba wataivunja hiyo taasisi?Ama una maana gani haswa kuhusu national security?

Ina maana una wasiwasi na chama hicho kuhusiana na kumaintain national security?

Ama unamanisha ni kivipi wataifanyia taasisi hiyo mabadiliko?
 
Nilishawahi kusikia kwamba elimu itakuwa bure licha ya kwamba sikumbuki vyema the details.Pia nilisikia issue kama mfuko wa sementi kuwa elfu tano.Kwa ujumla,walisema watalishghulikia pia tatizo la mfumuko wa bei.

Kweli miaka yote hii na utetezi wote huu unachokumbuka ni sementi 5000 na somehow kudeal na inflation? Huna chochote ambacho unajua wamesema watakuja kufanya kwa sababu unaamini watafanya hata kama hujui ni nini? Sasa unawaunga mkono kwanini? Well, kwa sababu wana nia nzuri ya kuiondoa CCM? au kwa sababu wana watu wanaozungumza vizuri sana kuhusu matatizo yetu? ama unawaunga mkono kwa nini? au hujali kutaka kujua nini wanataka kufanya?
 
MMK!! Aisee wewe ni hatari sana katika kuelekea ukombozi wa kweli wa M-tz!!

Nimefuatilia hoja zako na wana-JF kwa umakini, ila MMK wewe ni mmoja wa watakaorudisha nyuma ukombozi!! Yaani MMK unatuaminisha kwamba CDM hawakuwahi kuelezea nini kitafanyika kwa Polisi, UWT na Elimu ya juu!!? MMK, kweli!!?

Binafsi ningependa kuona watu kama wewe mnasaidiana na CDM kututoa tongotongo sisi kabwela, matokeo yake mnajivisha U-kondoo kutulaghai na kutuaminisha upuuzi ili mpate mnachokihitaji!!

MMK, wewe ni msomi, mtu mzima na muelewa wa mambo, kwanini mnajivua utu wenu na kujichomeka kwa watu wenye dhamira ya kweli ya kumkomboa Mtz na kuanzisha siasa za makundi(hapa narejea hapo juu unapokubaliana na Jmushi1, kwamba haukubaliani na uongozi wa juu wa CDM). MMK, najua unayasema haya kwa sababu chaguo lako ndani ya CDM yuko against!!

MMK, mtasema nini mbele ya Mwenyezi Mungu kwa kushiriki kutudidimiza sisi walala hoi kwa maslahi yenu binafsi!!?

Jamani, watz tumechoka lakini tunachoka zaidi pale nyinyi mloishika vizuri kasia mnapotuzamisha hata tunapojaribu kuinua vichwa vyetu kujiokoa!!

Eti nimebadilika!!! Muogopeni Mungu jamani!!
 
Kilichombadilisha MMM ni mabadiliko. Asiyesoma alama za nyakati, atapitwa na wakati. Nampongeza MMM kwa kufanya mabadiliko chanya, yaani kutoka mtazamo duni kuja mtazamo bora.
 
MMK!! Aisee wewe ni hatari sana katika kuelekea ukombozi wa kweli wa M-tz!!

Nimefuatilia hoja zako na wana-JF kwa umakini, ila MMK wewe ni mmoja wa watakaorudisha nyuma ukombozi!! Yaani MMK unatuaminisha kwamba CDM hawakuwahi kuelezea nini kitafanyika kwa Polisi, UWT na Elimu ya juu!!? MMK, kweli!!?

Binafsi ningependa kuona watu kama wewe mnasaidiana na CDM kututoa tongotongo sisi kabwela, matokeo yake mnajivisha U-kondoo kutulaghai na kutuaminisha upuuzi ili mpate mnachokihitaji!!

MMK, wewe ni msomi, mtu mzima na muelewa wa mambo, kwanini mnajivua utu wenu na kujichomeka kwa watu wenye dhamira ya kweli ya kumkomboa Mtz na kuanzisha siasa za makundi(hapa narejea hapo juu unapokubaliana na Jmushi1, kwamba haukubaliani na uongozi wa juu wa CDM). MMK, najua unayasema haya kwa sababu chaguo lako ndani ya CDM yuko against!!

MMK, mtasema nini mbele ya Mwenyezi Mungu kwa kushiriki kutudidimiza sisi walala hoi kwa maslahi yenu binafsi!!?

Jamani, watz tumechoka lakini tunachoka zaidi pale nyinyi mloishika vizuri kasia mnapotuzamisha hata tunapojaribu kuinua vichwa vyetu kujiokoa!!

Eti nimebadilika!!! Muogopeni Mungu jamani!!

pole pole taratibu.... tuko pamoja usishtuke sana. Kunywa maji kidogo na uvute pumzi. Harakati za mabadiliko siyo mbio za mita 100; ni Marathon!!!
 
Back
Top Bottom