Proper recording: Nini kilimbadili Mzee Mwanakijiji?

Sikkujua kama unampima mtu (anaetarajiwa kuwa raisi) simply kwa kuwa naye anapendwa na watu wengi hata kama hao watu inajulikana fika "hawamjui" ipasavyo au kuna genge liko nyuma yake...being an 'insider' with connections you should have known better MMM. Otherwise, salute iko pale pale.
 
Mkuu hata "mabadiliko yanabadirika" ndiyo maana yanaitwa mabadiliko. Ni kwa sababu maisha ni dynamic siyo static kwa hiyo mabadiliko ni lazima pamoja na "mabadiliko kubadilika".

Kwa Mzee Mwanakijiji hakugeuka nyuma akawa jiwe bali ameitika wito wa mabadiliko na anasonga mbele.

Nampongeza kwa uhuru wa fikra unaozaa mabadiliko.

Lakini ukimsoma vizuri anaonekana kama hajabadirika, au la hajiamini.
 
Lakini ukimsoma vizuri anaonekana kama hajabadirika, au la hajiamini.


hiki kipande hiki umekiona mkuu?...hebu pitia katikati ya mistari hii


''Wakati ule nilielewa kwa undani zaidi pia jeshi la polisi ni tatizo kubwa zaidi na nilikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kutaka IGP Mahita aondolewe na ndio nilitoa pendekezo la kugawa Dar-es-Salaam kama mikoa ya polisi (kanda). Pendekezo hili lilichukuliwa mara moja.''
 
hata sisi 2005 tulivote ccm but not anymore ever since so its normal trust need to be earned!
 
Kaka MM Mwanakijiji nilipoona mada hii imeletwa hapa,nami mdogo wako nikatega masikio nipate majibu yako. Mimi nililisikia hili nje ya jamii forums kwa ndugu na jamaa,nimelazimika kusoma majibu yako kwa makini..kwa kiasi fulani nimekuelewa ila nina mashaka kidogo! Je kwa kutambua uliyoyayafanya baada ya kuonekana umewapa mgongo CCM,hao CCM hawakuchukua measures kukushawishi uwageuke CHADEMA in the future? unapoonyesha hauna imani kwa sana na CHADEMA hii sio ishara kwamba umeanza kuipa mgongo CHADEMA as well?(which means unaweza hata kurudi ulipotokea). Kuna baadhi ya watu ambao inasemekana wanaonekana kuwa tofauti na CCM kwa sasa ila wanakusanya nguvu na attention ya watu wengi na baadaye coming 2015 wanapiga u-turn na kuidondosha CHADEMA.Pia niliambiwa CCM walifanya mengi ulipoanza kuwa kinyume nao hasa wakilenga kukupoteza,yaani kukurudisha "back to zero" ni kweli? kama ndivyo ulifanya nini ku-survive?...Sio siri nina mengi nitakutafuta pia off jamii forums,hope utafunguka zaidi
 
Vision ya chama haiwezi kua kuondoa chama tawala madarakani. That is merely a consequence of the take over. What is the vision of CDM concerning key areas ya utawala? I believe that is what Mzee Mwanakijiji meant: Sio CDM ishinde ili [tu] CCM itoke madarakani.

Wewe na MMK sasa mnataka kutuchezea akili. Yaani CDM ikishinda bila visheni, basi itakuwa bahati mbaya na CCM haitatakiwa kuondoka madarakani.

Mimi naamini CDM ikishinda, basi wapigakura (majority of them) watakuwa wamekikubali chama hicho kutokana na udhaifu mkubwa unaoonyeshwa na CCM.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mimibaba kauli ya Dr Kitila Mkumbo inatokana na ile nukuu maarufu kuwa "the only thing that never changes is change itself"; ambayo ni logical reasoning tu kuwa there will ALWAYS be CHANGE, there was change yesterday, there is today and most certainly there will be one tommorrow. Kimsingi tunakubaliana katika kuamini kuwa life is so dynamic and so should a human be.
Lakini pia mimi huamini kuwa however dynamic life could there are BASIC principles of life which will never change. "...now there remain faith, hope, and Love, these three: but the greatest of them is Love...... "

Mkuu hata "mabadiliko yanabadirika" ndiyo maana yanaitwa mabadiliko. Ni kwa sababu maisha ni dynamic siyo static kwa hiyo mabadiliko ni lazima pamoja na "mabadiliko kubadilika".

Kwa Mzee Mwanakijiji hakugeuka nyuma akawa jiwe bali ameitika wito wa mabadiliko na anasonga mbele.

Nampongeza kwa uhuru wa fikra unaozaa mabadiliko.
 
Last edited by a moderator:
Ukweli husemwa:
Watu wengi humu JF hawamuelewi vizuri Mzee Mwanakijiji.


MMK ameanisha kuwa CDM au vyama vingine vya siasa siyo Baba wala Mama yake.


Kama wewe unategemea MMK ataandika makala ya CDM kama vile makala inayohusiana na Baba au Mama yake basi umepotea.


Tatizo la Watanzania wengi, Vyama vya siasa vimekuwa kama vile ni Baba na Mama yao. Na dhana hii ndiyo chanzo cha udikiteta na ukilitimba wa mawazo ambao umeanza kujionyesha humu JF. Mtu yeyote anayekikosoa chama ili kukijenga anaitwa msaliti au ametumwa na watu au chama furani kukiharibu. Dhana hii potofu ndiyo inajenga kundi la viongozi ambao kutokana na kupendwa mpaka kwa kiwango cha hata kuabudiwa, wanajijengea u-mungu mdogo katika chama na serikali na kile wanachokisema na kukitenda wanaamini ndivyo tu. Ndiyo maana MMK akasema,
Sivutwi na hotuba hewa, au na mivuto ya umaarufu wa watu. Sipimi watu kwa kuangalia nani anaungwa mkono zaidi au nani haungwi mkono. Ninapima watu kwa fikra zao na mambo wanayoyasimamia lakini kwa jinsi gani wanaongozwa na kanuni (principle oriented) kuliko wanaoongozwa na matukio (events-oriented). Watu wanaoongozwa na matukio huitikia matukio yanapotokea; wanaoongozwa na fikra huitikia hata wakati kuko kimya!

Na. M. M. Mwanakijiji

Yetu ni macho na masikio, Siasa za Tanzania zimejaa surprises. Kuelekea 2015 tutaona na kusikia mengi.
 
hiki kipande hiki umekiona mkuu?...hebu pitia katikati ya mistari hii


''wakati ule nilielewa kwa undani zaidi pia jeshi la polisi ni tatizo kubwa zaidi na nilikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kutaka igp mahita aondolewe na ndio nilitoa pendekezo la kugawa dar-es-salaam kama mikoa ya polisi (kanda). Pendekezo hili lilichukuliwa mara moja.''

oho. Kumbe ni kirusi.
 
hawezi kusema ukweli wote....hawezi

Hana ukweli wowote, kwenye main response yake kuna sehemu kasema

"Kikwete alipopitishwa na kuwa mgombea wa Urais mimi nilikuwa miongoni mwa watu ambao tulimuunga mkono kwa sababu mbalimbali. Ya kwangu ilikuwa ni sababu ya kisiasa zaidi. Kwamba, alionekana kupendwa na kukubaliwa na wananchi wengi sana."

akiwa anamaanisha kwamba, alimuunga mkono kikwete kwa kufuata mkumbo wa kupendwa na kukubaliwa na wananchi wengi. alafu kuna sehemu ingine tena kasema "Sivutwi na hotuba hewa, au na mivuto ya umaarufu wa watu. Sipimi watu kwa kuangalia nani anaungwa mkono zaidi au nani haungwi mkono. Ninapima watu kwa fikra zao na mambo wanayoyasimamia lakini kwa jinsi gani wanaongozwa na kanuni (principle oriented) kuliko wanaoongozwa na matukio (events-oriented). Watu wanaoongozwa na matukio huitikia matukio yanapotokea; wanaoongozwa na fikra huitikia hata wakati kuko kimya! "

Akiwa in principal anamaanisha kwamba hafuati mkumbo, sasa whichi is which? mjanja mjanja huyu mtu.


 
Ukitaka kuwajua vizuri hao watu wapo upande gani subiri coming two month before next presidential election. halafu huwafuatilie ndio utawajua, tafuta tu na za kampeni ya 2010 ndio utawajua vizuri. Huwa awamwangalii nyani usoni na hawatetemeki nina maana na member yeyote humu ndani asie fit kwenye sura zao. ziwe siasa za kyela CCM kwa CCM au za CDM kama za marehemu Regia Mtema (R.I.P) na ukienda huko kwenye urais losalale huko ndio uwaeleweshi kabisa.
 
Hana ukweli wowote, kwenye main response yake kuna sehemu kasema

"Kikwete alipopitishwa na kuwa mgombea wa Urais mimi nilikuwa miongoni mwa watu ambao tulimuunga mkono kwa sababu mbalimbali. Ya kwangu ilikuwa ni sababu ya kisiasa zaidi. Kwamba, alionekana kupendwa na kukubaliwa na wananchi wengi sana."

akiwa anamaanisha kwamba, alimuunga mkono kikwete kwa kufuata mkumbo wa kupendwa na kukubaliwa na wananchi wengi. alafu kuna sehemu ingine tena kasema "Sivutwi na hotuba hewa, au na mivuto ya umaarufu wa watu. Sipimi watu kwa kuangalia nani anaungwa mkono zaidi au nani haungwi mkono. Ninapima watu kwa fikra zao na mambo wanayoyasimamia lakini kwa jinsi gani wanaongozwa na kanuni (principle oriented) kuliko wanaoongozwa na matukio (events-oriented). Watu wanaoongozwa na matukio huitikia matukio yanapotokea; wanaoongozwa na fikra huitikia hata wakati kuko kimya! "

Akiwa in principal anamaanisha kwamba hafuati mkumbo, sasa whichi is which? mjanja mjanja huyu mtu.





wataalamu wote waliobobea kwenye mambo ya cytography na steganography huwa wako hivyo.....katu huwezi kumuelewa....
 
Umenikumbusha mbali sana, ndio mchakato wenyewe wa mabadiliko huo. Hakuna kisichobadilika isipokuwa mabadiliko

Mimi mwenyewe nimejua siasa za nchi yangu kwa kina nilipoingia JF mwaka mmoja uliopita. Mabadiliko ni kitu cha kawaida hasa ukiwa na open mind
 
Wakuu, binafsi nilikuwa shabiki wa huyu mkongwe wa JF. Nikagundua kwamba MMK amechanganya fani mbili tofauti na hivyo kujichanganya na kuchanganya wasomaji wa posts/makalazake. Nikaacha kufuatilia na kusoma anachokiandika.

MMK amechanganya SIASA na UANDISHI wa habari. Moja ya misingi ya uandishi wahabari ni impartiality wakati msingi wa siasa ni partiality. Mchanganyo huu unamfanya awe kinyonga asiye kinyonga kwani at one point anajuwa kwamba anatakiwa awe mwandishi na wakati huo huo mapenzi yake kwenye siasa yanakizanana misingi ya uandishi.

Hadi sasa sijui MMK anataka aonekane kwa sura ipi kati ya uandishi wa habari auuenezi wa siasa za Chadema anakokiri kuandika ilani ya chama. Nakumbuka nilishawahi kumuuliza MMK juu ya ili kwenye mijadala yetu hapa JF. Nikapatajibu kwamba yuko kisiasa zaidi na hiyo ikaondoa mvuto wa postings zake kwangu.


Nadhanikilichotokea ni kwamba MMK wakati alipokuwa mwanafunzi wa uandishi aligundua audience ya JF ilikuwa kisiasa zaidi na bila kusita akasoma alama zake. Akapatajukwaa na wasomaji wa kujifunzia. Kwa umakini akagundua kwamba upepo wa siasaza upinzani ndio zilizokuwa zinaongoza JF na kwamba audience yake ilikuwa inashangilia kila anapotembeza bakora chama tawala. Hapo ndipo alipoweka dalugaza uandishi chini na kuanza kazi mpya ya siasa. Kukazuka habari za yeye kununuliwa na Chadema na kwamba yuko kwenye payroll ya Chadema, habari hizi zikapunguza washabiki waliomwona kuwa ni mwandishi na sio mwanasiasa.

Kinachotokea sasa, nadhani kwa kuangalia response yake kwenye thread hii, niMMK kutoridhika na fukuto la urais ndani ya Chadema. Hajui, nadhani, nani ninani na kwanini. Mashaka haya, sitashangaa, yakamfanya akumbuke daluga zake zauandishi maana huko kunampa comfort zone. Sio kweli kwamba MMK yuko neutral kisiasa,sio kweli kwamba ni mwanasiasa asiyefungamana na upande wowote kama anavyojaribu kutuzuga. Hakuna mwanasiasa ndani ya vyama vingi asiyefungamana naupande wowote. Hayupo. Ameandika ilani ya CDM na leo tutamshangaa kama atakuwa anaishangilia CCM and it follows that MMK sio mwandishi neutral wa makala zasiasa. That is right, sio mwanasiasa neutral (kwasababu hakuna mwanasiasaneutral) na sio mwandishi neutral (kwasababu yuko affiliated na CDM).


Labda swali la msingi katika thread hii kwa MMK ni: Jeyupo CDM kwa moyo wake wote au alikwenda huko kwasababu alipata audience yafani yake ya awali? Swali la nyongeza ni lile nililokwisha muuliza miaka kadhaa iliyopita: Je yeye ni mwanasiasa au mwandishi?
 

Kikwete alipopitishwa na kuwa mgombea wa Urais mimi nilikuwa miongoni mwa watu ambao tulimuunga mkono kwa sababu mbalimbali. Ya kwangu ilikuwa ni sababu ya kisiasa zaidi. Kwamba, alionekana kupendwa na kukubaliwa na wananchi wengi sana. Wakati ule niliandika makala kadhaa kwenye mitandao ambazo zilielezea jukumu hili. Katika makala moja nilielezea kuwa Kikwete anaingia katika uongozi wa taifa letu wakati wananchi wanahitaji kiongozi atakayewaamsha kujiletea maendeleo. Nilisema ni mzigo tuliomtwisha Kikwete. Na nikatoa angalizo wakati ule endapo Kikwete atashindwa kukidhi matamanio ya Watanzania hakuna tena mwanasiasa mwingine yeyote ndani ya CCM atakayeweza kufanya hivyo kwa siku za karibuni.

Na. M. M. Mwanakijiji


Uchaguzi wa mwaka 2005 ulinifanya niugue sana moyoni kwa sababu nilijua JK atashinda kwa sababu uliyotaja hapo juu. Niliugua kwa sababu sikuona sifa za uongozi ndani yake na nilitegemea kuingia kwenye janga tulilomo leo. Nashangaa sana kusikia MMK naye alikuwa miongoni mwa watu walionifanya niugue vile.
Mtu yeyote makini alitakiwa kujua kuwa kupendwa na kukubalika kwa JK kulikuwa kwa kutengenezwa na mtandao alioujenga for more than 10 years (Tuliona jinsi magazeti, TV mpaka makanisa yalivotumika,we are seeing the same strategy kwa EL today). Nakumbuka nilivokuwa nikikereka kuwakuta wanawake wakimsifia JK, ukiwauliza kwa nini mnampenda JK hawakujibu na ukibahatika kupata jibu watakwambia ni handsome! ...upumbavu huu hata Nyerere aliuona 1995, ndio maana aliwaambia watu hatuchagui sura, na kama unampenda mualike ukanywe naye chai.
Kumuunga mtu mkono kwa sababu ya kupendwa na kukubalika na wengi bila kujiuliza kukubalika huko kumetokana na nini? ...ah!
 
Kubadirika ndio sifa ya binadamu, if you can't cope with the situation, just die. hivyo hata MMM kubadirisha mtazamo ni haki yake ya msingi
 
Ukweli husemwa:

wataalamu wote waliobobea kwenye mambo ya cytography na steganography huwa wako hivyo.....katu huwezi kumuelewa....

Mkuu, hayo maneno kwenye red yana maana gani au ulikuwa una maana ya cartography na stenography.
 
Back
Top Bottom