Proper recording: Nini kilimbadili Mzee Mwanakijiji?

Ni wakati wa mabadiliko kama kitila alivyosema. Nakumbuka sana hata Kitila alikuwa anamtetea sana zzk pale ud-kiswahili. Niliwahi kumuuliza kwa nini zzk huwa anazumzia kugombea urais kila cdm inapokuwa na issue muhimu? mfn pale arumeru m. ni kutaka ku shift attention? Leo nimeona kitila kabadilika alipokuwa anatoa ufafanuzi wa makala yake aliposema "zzk kutangaza kugombea urais ni kosa la kimantiki na kitamaduni". Broadly speaking, kosa la timing. mfn, kama kuna uchaguzi kesho, zzk atazungumzia kugombea urais leo badala ya keshokutwa.
 
Mto mkubwa wowote ule, mfano NILE hutokea mbali sana ukiwa kakijito kadogo sana, kadri unavyokaribia destination e.g baharini huwa kuna vijito vingi sana vinajiunga, hata vile vinavyokauka kabla ya kiangazi. Inawezekana MMM umemwonea katika hili, wapo watu ambao wamebadilika gafla kuliko hata yeye, hiyo ndio hali halisi kwa sababu mto umekaribia destination
 
Can s.o summarize what mmk has written
It's too long a story for ma liking.
Please, Summary in three words
 
Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2005 niliamini kuwa Tanzania inahitaji mabadliko makubwa ya kiuongozi. Niliamini kabisa kuwa kiongozi atakayekuja atatakiwa kuwa mtu mwenye kukubaliwa na wananchi na ambaye atatumia kukubaliwa huko kuanzisha program ya haraka ya mabadiliko ili kuchochea maendeleo Tanzania. Sikumuona kiongozi huyo katika upinzani. Nilikuwa sahihi.
Kikwete alipopitishwa na kuwa mgombea wa Urais mimi nilikuwa miongoni mwa watu ambao tulimuunga mkono kwa sababu mbalimbali. Ya kwangu ilikuwa ni sababu ya kisiasa zaidi. Kwamba, alionekana kupendwa na kukubaliwa na wananchi wengi sana. Wakati ule niliandika makala kadhaa kwenye mitandao ambazo zilielezea jukumu hili. Katika makala moja nilielezea kuwa Kikwete anaingia katika uongozi wa taifa letu wakati wananchi wanahitaji kiongozi atakayewaamsha kujiletea maendeleo. Nilisema ni mzigo tuliomtwisha Kikwete. Na nikatoa angalizo wakati ule endapo Kikwete atashindwa kukidhi matamanio ya Watanzania hakuna tena mwanasiasa mwingine yeyote ndani ya CCM atakayeweza kufanya hivyo kwa siku za karibuni.
Ushindi wake wa asilimia 80 ya wapiga kura ulikuwa ni ushindi wenye kurindima. Uliacha mwangwi wa kila nchi. Tuliomuunga mkono tuliamini kuwa atasimama na kuliongoza taifa letu vizuri zaidi akitumia mandate aliyokuwa ameipata. Furaha za Kikwete kuingia madarakani hazikudumu. Kikwete hakuitikia wito wa historia na badala yake alianza kuonesha udhaifu ambao wale waliokuwa wanamjua kabla walikuwa wanautambua; hakuwa kiongozi mwenye kuhamasisha (inspire) wananchi wake. Akaanza kufanya mambo ambayo mara moja mimi binafsi nilitambua ni alama za kiongozi dhaifu.
Hiki ndicho kilichotokea; ni kutambua kuwa CCM haiwezi kuleta mabadiliko tunayoyataka ; ni kutambua kuwa mabadiliko tunayoyataka yanatakiwa yaongozwe na fikra maridhawa ambazo zinaweza kugusa wananchi na wakazielewa. Siyo uzuri wa watu, na utamu wa majina yao bali uzuri na ukweli wa hoja zao.
Ni muumini wa fikra na si mfuasi wa watu
Sasa mtu anaweza kufikiria kuwa mimi nilikuwa mfuasi wa Kikwete; hapana. Mimi ni mfuasi wa fikra na kwa wanaonijua wanafahamu kuwa ni muumini wa fikra sahihi za Mwalimu Nyerere. Fikra hizi ambazo nimejifunza kwa kina na ninaendelea kujifunza siku kwa siku ninaamini ni sehemu ya alama za taifa letu. Baada ya Kikwete kushindwa kuonesha uongozi wa taifa letu na kutuhamasisha kujenga jamii ya kisasa niliamua wakati ule kuanzisha harakati za mapambano ya kifikra; yaani wananchi wetu ili waweze kubadilisha kura ni lazima kwanza wabadilishe fikra!
Ninaamini kimsingi mambo yafuatayo ambayo nimetokeo ya kujifunza Fikra za Mwalimu Nyerere:
a. Usawa wa watu wote unaotokana na usawa wa utu: Nimewahi kuliandika hili baadaye kuwa Nyerere aliona usawa siyo ule wa kisheria kutokana na wote kuwa “sawa mbele ya sheria” kama ilivyo Marekani bali ni usawa ambao unatokana na wote kuwa ‘sawa sababu ya utu wao’. Kwamba hakuna binadamu mwenye utu zaidi ya mwingine
b. Uongozi ni utumishi siyo ulazimishi: Ninaamini kuwa mtu anayetaka kuwa kiongozi anapaswa kuwa mtu anayetaka kutumika siyo kutumiwa au kutumikisha wengine.
c. Maendeleo ni ya watu siyo vitu: Mojawapo ya mambo makubwa kabisa niliyojifunza kutokana na fikra za Mwalimu ni dhana kuwa maendeleo ya vitu bila maendeleo ya watu ni udikteta wa vitu. Watu ndio msingi, kiini, sababu, lengo na njia ya maendeleo. Utawala wa CCM (hasa kuanzia Mkapa) umeweka mkazo mkubwa sana kwenye kuendeleza vitu; wanajivunia vitu, wanatuonesha vitu. Siyo watu walioendelea!
d. Siasa ni chombo tu cha kuchochea mabadiliko. Binafsi nachukulia siasa kama chombo cha kusaidia kuleta mabadiliko. Ninaamini siasa ikitumiwa vizuri kama kisu inaweza kutumika kumchuna ng’ombe vizuri, kukata majani, na hata kuchimba ardhini ili kuleta tunachotaka. Ikitumiwa vibaya inakuwa kama jambia mikononi mwa kichaa! Ina madhara. Hivyo ni muumini wa “siasa bora” na siyo “bora siasa”.
e. Wenye kushika madaraka wanashika kama dhamana si haki.
Ngoja nipate castle lager moja kwanz
 
Mwanakijiji,sijaelewa unaposema mwaka 2010 viongozi wa CDM Walishindwa kuonyesha uongozi.kwa maoni yako walitakiwa wafanye nini
 
Mwanakijiji nadhani umejieleza sana vizuri tena sana. Lakini niliwahi kukutaka upime zaidi mawazo yako kwa manufaa ya Taifa. Kama ukiweza kuondoa kabisa ubinafsi wako katika fikra na maono yako kisiasa kuhusu Tanzania, utaona kuwa mpaka sasa hakuna sababu yoyote kubakia CCM maana si chama kitakacho leta mabadiliko yoyote kwa raia wa Tanzania, bali kitalenga tu kuleta mabadiliko ya vitu na siasa. Sasa nilitaka upime je kuendelea kukikataa chama pekee kilichojitutumua hadi leo kumvalisha paka kengele unalisaidia Taifa kiasi gani?
Je ungetumia umahiri na uzoefu wa kisiasa kukishauri hiki chama au chama kingine chochote ili kiimarike zaidi na kuepesha huo utabiri wako wa mgawanyiko isingekuwa manufaa zaidi kwa Taifa lako? Kwanini unataka kuona vimeshaundwa na vimeshaimarika ndiyo uingie kwa mbwembwe na sifa? Au usifu? Wakati wapiganaji wanapambana wewe unakaa pembeni na kuwabeza? NAdhani inafaa ukae ujiulize zaidi. Hawa CDM kazi wanayoifanya siyo ya kubeza hata kidogo. Kama unabisha jaribu kufuatana nao uombe kuwa mgeni rasmi, ukaone wanavyokumbana navyo. Nadharia ni nyingi mno kupitiliza kwenye hii makala yako. Tafadhali acha kunywa chai ndiyo uandike makala, anza kuandika ndiyo unywe chai!
Nawasilisha!
 
Mkuu mwanakijiji salam,nimesoma kwa kina hatua kwa hatua na kwakweli naona ni busara kwangu kukipa nafasi kichwa changu kutafakari,umekuwa role model wangu kwa miaka minne sasa so kwa fikra jengefu umekuwa ukinijenga sana kiasi huwa najitahidi kusoma na kuwaza kwa mapana labda kuna siku nitakuwa kama wewe,nafaham u will proud kuwa na mfuasi wa fikra chanya.be blessed mkuu!
 
Naona jukwaa linakaribia kukamilika sasa,
karibu sana mkuu wangu Speaker!
Furaha kuwa nawe jukwaani baada ya kupotea kitambo kidogo.

Tuko pamoja mkuu.
Majukumu sometime yana tukimbiza humu hasa tunapokua porini.
 
lori alilopanda au analoliendesha mwanakijiji likipata ajali ujue na mimi nipo ndani na ajali inanihusu,na likipata mafanikio ya kufika salama uje na mimi ninajivunia mafanikio.
BRAVO MM.
 
Mkuu MMM, Nimekusoma na nimekuelewa, pengine dhamira zetu zinashabihiana kwa kiasi fulani...hivi Mkuu wangu unafikiri ni rahisi kuing'oa chama kilichojengwa ktk misingi ya ujamaa? chama ambacho sote tulikuwa tunaabudu na kukitumikia pasipo shuruti? wewe mwenye umekiri bado hisia zako zinasikilizia nyimbo zile za kishujaa sembuse WENYE DHAMANA NA VYOMBO VYETU VYA ULINZI? Bado huoni haja ya kumuomba MBOWE radhi na kumpongeza kwa hatua kubwa aliyoifanya ya kuijenga CDM yenye kupigwa vita na VYOMBO VYA DOLA kupitia ORGANS zao mbali mbali kama Msajili wa vyama, Tume ya Uchaguzi, Wakuu wa mikoa na wilaya, NCCR, CUF, TLP nk? Mimi naamini ktk yale unayoyaamini na kupigania Mkuu, Ila Transformation ya VYOMBO vyetu vya ULINZI ni muhimu sana kwa mustakbali wa nchi hii, bahati mbaya sana mchakato huu unaenda taratibu sana kwani kuna KIZINGITI kingine cha MATAIFA makubwa wanalinda MASLAHI yao thru CCM...Funguka Mkuu...Tupe Mkakati Mbadala badala ya kulalamika na kukata tamaa...
 
MMk naona umetoa mawazo mazuri , ila je nini kifanyike kwa chama kama CDM ili kiweze kushinda,?
Manake wameanzisha ile operation sangara, sasa M4C mpaka vijijini ili kuamsha fikra za watu huko na kubalisha mawazo ya wapiga kura, sasa je nini wanakosa hapa ili waweze kufanikisha malengo yao? Japokuwa tunaona M4C haiungwi mkono na baadhi ya wana CDM ambao wao wanajua wana malengo yao binafsi,(msafara wa mamba kenge hawakpsekani).
 
Mwanakijiji ni kweli CDM haijajipanga vema kuchukua uongozi wa nchi hii,lakini kwa maoni yangu inatokana na tabia za Watanzania,hasa wasomi kuwa wabinafsi zaidi badala ya kuangalia maslahi ya taifa. Wasomi wanakimbilia CCM kwa maslahi yao badala ya maslahi mapana ya jamii. Tu-wanafiki zaidi na wengi wetu hatulipendi taifa letu... Haishangazi sasa tumekwama karibu kwa kila kitu.
 
Wakuu naomba nisamehewe maana najua si sahihi hata kidogo kujadili watu lakini kwa hili nafsi imezidiwa nguvu, nimeona nifanye hivyo.

Kwanza nianze kukiri mapema kabisa Mzee Mwanakijiji japo simfahamu na hatujawahi kuonana ni mentor wangu na kwa kiasi kikubwa amenijenga katika ujenzi wa hoja na upanuzi wa uelewa wa masuala mbalimbali.

Nimekuwa nikifuatilia kila anachoandika humu JF na kwenye machapisho mbalimbali kuanzia magazeti ya Tanzania Daima, Mwanahalisi (Mungu asaidie lirudi maana nimeugua kwa kulikosa),Majarida ya Cheche, Kitabu cha Majeruhi wa Mapenzi na mara kadhaa nimeelezwa majina kama Lula Ndali Mwananzela yanayotumiwa kwenye magazeti ya Raia Mwema na Mwananchi ni yeye.


Hakikanimekuwa sikosi maandiko yake.Nimekuwa nikihangaika sana kuhakikisha sipitwi na anachoandika. Kila Jumatano nimekuwa nikinunua magazeti ya Tanz. Daima, Raia Mwema na Mwanahalisi na Jumapili nimekuwa siachi kununua gazeti la Mwananchi kwa sababu yake. Ninapokosa makala zake nimekuwa naumia sana.

Lakini katika upekuzi wangu humu Jamii Forums (Enzi hizo Jambo Forums) nimekumbana naThread iliyonishtua ya Mh. Freeman Aikael Mbowe (Mwenyekiti wa CDM) aliyoipost JF mwaka 2006 yenye kichwa cha ‘The OnlyThing We Have To Fear……’ mara baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa mkuumwaka 2005.

Uzi huo wa Mh. Mbowe unaweza kusoma https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/947-the-only-thing-we-have-to-fear.html

Kilichonishtuasi Mbowe kupost thread JF, la hasha, ni msimamo aliokua nao Mzee Mwanakijiji dhidi ya upinzani na mageuzi kwa ujumla nchini. Katika kuchangia thread hii pamoja na akina Kitila Mkumbo, Mkandara, Nyani Ngabu, John Mnyika kujitahidi kumuelewesha MMM bado alikuwa na msimamo hasi dhidi ya upinzani na ama kwa hakika alikuwa ‘Real pro-CCM’ na naweza kudiriki kusema aliouona upinzani kama uliopoteza dira na usio na uwezo wa kuleta mabadiliko na kuaminiwa na wananchi.Niko tayari kukosolewa.

Moja ya nukuu ya MM kwenye mjadala huo ni hii
“
Lazima tuwaone viongozi hawa wakiongoza ndipo tutavutiwa navyama vyao!! Nilikuwa nakiheshimu Chadema sana, lakini baada ya kampeni zamwaka jana na hadi leo wamenikatisha tamaa!! Sasa naanza kukiangalia kwa karibuCUF huku moyo wangu bado uko CCM!!
“

Kwenye thread hiyo, MM aliitetea CCM dhidi ya maovu yote iliyokuwa ikitupiwa dhidi na wapinzani. MM alisimama kidete kupinga madai ya CCM kununua shahada za kupigia kura, kuwanunua viongozi wa upinzani, matumizi makubwa ya nguvu za dola dhidi ya upinzani nk. nk.

Hakika ukitazama michango ya MM kwenye thread hiyo ya F. Mbowe hasa jinsi alivyokuwa supporter mzuri wa CCM na kuuponda upinzani na harakati za mageuzi huwezi kuamini nini hasa kilitokea Mzee Mwanakijiji akabadilika na kuwa huyu ninayemsomaleo.I mean kuwa against na CCM na doings zake zote.

Wazomoja lililonijia ni labda pengine MM alikuwa anapata maslahi fulani manono kutoka CCM na ndiyo yaliyokuwa yanamuweka kwenye huo msimamo hasi dhidi yamabadiliko na sasa maslahi hayo hayapati tena, yamezibwa na ndiyo sababau ya yeye kubadilika. Vinginevyo nini hasa kilimbadili Mzee Mwanakijiji?

Kwahiyo kulingana na maneno yako hayo kwenye rangi nyekundu unataka kuwaaminisha watu kwamba kama MMM alikuwa akipata maslahi kwa kuitetea CCM na baadaye kuyakosa hivyo anayapata huko anakotetea kwa sasa? Hivyo mzee mwanakijiji ni mtu wa kufuata maslahi na mambo ya msingi si ndivyo? Lakini mimi nadhani kama si maslahi kama ulivyotanabaisha, kubadili msimamo kwa kuelekea kwenye mambo ya msingi sio kosa wala dhambi.
 
MMK ni Gifted writer,ila sijajua kwanini anawa accuse vingozi wa CDM kwa umimi?Ingawa atakuwa na wakati mgumu kutetea kuwa huo umimi kuwa upo na upo kwa akina nani ktk chama.Ila pia atakuwa na wakati mgumu kutuambia (akina tomaso sisi)kama vyama vyote vina umimi kwanini aone umimi wa CDM kuliko mwingine?

Kwa hili tunarudi palepale kwa warioba na Wengine.Tatizo la hii nchi ni pale wataalamu fulani wanapotumia taaluma zao kucheza na mipaka iliyo blurred zaidi ili kufanya mengi nje ya mipaka.Sasa hapa vipimo mara nyingi kuwa ni vitu tofauti sana,conventional wisdom, na inner values nyingine ambazo watu wengi huamua ziacha kwa vile hakuna anyeweza uliza au thibitisha,sanasana wataishia kuona mambo yanayo click vichwani tuu.hadi pale mtu mmoja atakaposema kuna kitu kinanishangaza ndipo wataokea wengi sana wakisema "...hata mimi....".Then kila mtu taunganisha dot anavypenda haraka sana.
 
Ukweli ni kuwa MM bado haeleweki, ni kama uwa anabadilika badilika kila mara. Kuna wakati uwa anakuwa mpinzania mzuri wa CCM na serikali yake, ila kuna siku uwa anakuwa mkali dhidi ya upinzani na hasa CDM. Na nadhani bado anashaka dhidi ya uongozi wa CDM, maana kuna kipindi wakati wa uchaguzi wa CDM kule Arumeru Mashariki alisema kuwa kama CDM wakishindwa basi uongozi wa CDM uachie ngazi. Ukweli ni kuwa tulishinda na kwa kweli aliambulia matusi na kejeli toka kwa vijana machachari wa CDM humu JF.
teh teh.Mimi huyaona haya kwa mchambuzi na mkandara.
 
Back
Top Bottom