Proper recording: Nini kilimbadili Mzee Mwanakijiji?

CHADEMA hawatashusha wafuasi na wanachama wake kutoka sayari nyengine ni hawa hawa waliokuwa CCM, CUF, NCCR nk hivyo usimshangae MMM kubadilika kimawazo kwani hata maandiko yanaonyesha Paul jinsi alivyokuwa mkatili kwa watu waliokuwa wakihubiri habari za ufufuko wa Kristo kabla yeye Paulo hajaokoka!
 
Actually muda huo nilikuwa mdogo kiumri (I mean kuweza kupiga kura) lakini nilikuwa nikiifuatilia Jambo Forums by then. Ni kama naona Mzee Mwanakijiji si yule niliyekuwa namsoma enzi hizo hasa ikizingatiwa kwenye thread hiyo alitoa madai mazito ya viongozi wa CDM kutaka kumuahidi vyeo ili ajiunga na chama. Sijui nini kilitokea MMM akabadilika.

Ukweli ni kuwa MM bado haeleweki, ni kama uwa anabadilika badilika kila mara. Kuna wakati uwa anakuwa mpinzania mzuri wa CCM na serikali yake, ila kuna siku uwa anakuwa mkali dhidi ya upinzani na hasa CDM. Na nadhani bado anashaka dhidi ya uongozi wa CDM, maana kuna kipindi wakati wa uchaguzi wa CDM kule Arumeru Mashariki alisema kuwa kama CDM wakishindwa basi uongozi wa CDM uachie ngazi. Ukweli ni kuwa tulishinda na kwa kweli aliambulia matusi na kejeli toka kwa vijana machachari wa CDM humu JF.
 
Mie sidhani kama kabadilika sana. nakumbuka katikakati mwaka 2010 wakati suala la CCJ linapamba moto humu JF alionekana kuiponda sana CDM na kuiunga mkono CCJ na kuna thread moja kama atakumbuka, niliweka post kwa kusema something like "There is more in MMK and CCJ than what meets the eye' -- yaani "Kuna zaidi ndani ya MMK na CCJ kuliko inavyoonekana kwa macho."

Mnajua alivyonijibu? Aliandika something like "You appear to be smart person in this issue." Yaani "Unaonekana kuwa mjanja sana katika ishu hii."

Nina hakika nilimgusa mahala fulani -- hasa kuhusika kwake katika mradi wa CCJ, ambao wengi tunaamini ulikuwa ni mradi wa CCM kuidhoofisha CDM, hasa pale awali.

Lakini nachompendea MMK ni kwamba huwa hafichi sana undani wape hasa unapom-corner kwa hoja madhubuti.

Nawasilisha.
 
Ninaelewa kuwa sisi the then generation, kila mtu alikuwa gamba just for the sake of school na mambo mengine!
 
MMK acha usharobaro!! Mara nakunywa chai, mara mwenye maswali zaidi aulize, ooh usiulize nimekunywa chai na nini!! Si bora ukae kimya tu!! Aaah!! Yaani hili moja umeshindwa litolea ufafanuzi unahitaji mengine!!? Au kuwekewa thread basi umeiona pepo!!? Jibu hoja bwana MMK vp!!?

Watu wengine bwana......!!!!
 
Mie sidhani kama kabadilika sana. nakumbuka katikakati mwaka 2010 wakati suala la CCJ linapamba moto humu JF alionekana kuiponda sana CDM na kuiunga mkono CCJ na kuna thread moja kama atakumbuka, niliweka post kwa kusema something like "There is more in MMK and CCJ than what meets the eye' -- yaani "Kuna zaidi ndani ya MMK na CCJ kuliko inavyoonekana kwa macho."

Mnajua alivyonijibu? Aliandika something like "You appear to be smart person in this issue." Yaani "Unaonekana kuwa mjanja sana katika ishu hii."

Nina hakika nilimgusa mahala fulani -- hasa kuhusika kwake katika mradi wa CCJ, ambao wengi tunaamini ulikuwa ni mradi wa CCM kuidhoofisha CDM, hasa pale awali.

Lakini nachompendea MMK ni kwamba huwa hafichi sana undani wape hasa unapom-corner kwa hoja madhubuti.

Nawasilisha.

wengine huwa tunapend kuangalia kwa jicho la ndege hasa mwewe.....mkuu ze kalang mwanakijiji ni zaidi ya hapo na hapa atakuja kubrash tu hataeleza sana....signature yangu inafanan na tabia yake
 
Binafsi naweza kumsemea kitu kimoja.
Kwamba ameamua kua kama "mimi",...mpinzani daima.
Wapeleke wapinzani madarakani,wakifika usiwapigie makofi,waambie fanyeni
kazi lakini mimi bado ni mpinzani,na this time,nawapinga nyie kwa mabaya yote
mtakayo fanya.
 
Hili hapa nitalijibu vizuri sana; ngoja ninywe chai kwanza maana kwa kweli sijabadilika kifikra.... stay tuned...msitoke..

kwani we mzee hiyo chai unaenda kuinywea Paris kama Mobutu Seseseko? Acha mbwembwe bana, we mjibu dogo. Mbona hata mimi mwaka 2000 na 2005 nilimpigia kura Lipumba?!
Nakumbuka ticha wangu wa thandethkuli alinifundisha. 'Speak the truth, ashame the devil' Comeon MMK, Dont be a coward!!
 
Mkuu MMM, binafsi huwa napenda sana kusoma makala zako pia. Nadhani pia wengi wa watanzania wasiokuwa na access na mitandao au magazeti na wale wasiopenda kusoma pia wangefunguka kifrika kama wangezisikia mada zako kwa njia ya hotuba. Swali ambalo ningependa kujiuliza ni Is that it? Unajificha chini ya hilo jina na unatoa mada nzuri sana, but do you have a plan to come out in future?
 
MMK acha usharobaro!! Mara nakunywa chai, mara mwenye maswali zaidi aulize, ooh usiulize nimekunywa chai na nini!! Si bora ukae kimya tu!! Aaah!! Yaani hili moja umeshindwa litolea ufafanuzi unahitaji mengine!!? Au kuwekewa thread basi umeiona pepo!!? Jibu hoja bwana MMK vp!!?

Watu wengine bwana......!!!!

Vipi ndugu umekosa riziki yako ya kila siku nini?
Au kakutamanisha kwamba anakula?
pole pole banaaa
 
Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2005 niliamini kuwa Tanzania inahitaji mabadliko makubwa ya kiuongozi. Niliamini kabisa kuwa kiongozi atakayekuja atatakiwa kuwa mtu mwenye kukubaliwa na wananchi na ambaye atatumia kukubaliwa huko kuanzisha program ya haraka ya mabadiliko ili kuchochea maendeleo Tanzania. Sikumuona kiongozi huyo katika upinzani. Nilikuwa sahihi.

Kikwete alipopitishwa na kuwa mgombea wa Urais mimi nilikuwa miongoni mwa watu ambao tulimuunga mkono kwa sababu mbalimbali. Ya kwangu ilikuwa ni sababu ya kisiasa zaidi. Kwamba, alionekana kupendwa na kukubaliwa na wananchi wengi sana. Wakati ule niliandika makala kadhaa kwenye mitandao ambazo zilielezea jukumu hili. Katika makala moja nilielezea kuwa Kikwete anaingia katika uongozi wa taifa letu wakati wananchi wanahitaji kiongozi atakayewaamsha kujiletea maendeleo. Nilisema ni mzigo tuliomtwisha Kikwete. Na nikatoa angalizo wakati ule endapo Kikwete atashindwa kukidhi matamanio ya Watanzania hakuna tena mwanasiasa mwingine yeyote ndani ya CCM atakayeweza kufanya hivyo kwa siku za karibuni.

Ushindi wake wa asilimia 80 ya wapiga kura ulikuwa ni ushindi wenye kurindima. Uliacha mwangwi wa kila nchi. Tuliomuunga mkono tuliamini kuwa atasimama na kuliongoza taifa letu vizuri zaidi akitumia mandate aliyokuwa ameipata. Furaha za Kikwete kuingia madarakani hazikudumu. Kikwete hakuitikia wito wa historia na badala yake alianza kuonesha udhaifu ambao wale waliokuwa wanamjua kabla walikuwa wanautambua; hakuwa kiongozi mwenye kuhamasisha (inspire) wananchi wake. Akaanza kufanya mambo ambayo mara moja mimi binafsi nilitambua ni alama za kiongozi dhaifu.

Hiki ndicho kilichotokea; ni kutambua kuwa CCM haiwezi kuleta mabadiliko tunayoyataka ; ni kutambua kuwa mabadiliko tunayoyataka yanatakiwa yaongozwe na fikra maridhawa ambazo zinaweza kugusa wananchi na wakazielewa. Siyo uzuri wa watu, na utamu wa majina yao bali uzuri na ukweli wa hoja zao.

Ni muumini wa fikra na si mfuasi wa watu
Sasa mtu anaweza kufikiria kuwa mimi nilikuwa mfuasi wa Kikwete; hapana. Mimi ni mfuasi wa fikra na kwa wanaonijua wanafahamu kuwa ni muumini wa fikra sahihi za Mwalimu Nyerere. Fikra hizi ambazo nimejifunza kwa kina na ninaendelea kujifunza siku kwa siku ninaamini ni sehemu ya alama za taifa letu. Baada ya Kikwete kushindwa kuonesha uongozi wa taifa letu na kutuhamasisha kujenga jamii ya kisasa niliamua wakati ule kuanzisha harakati za mapambano ya kifikra; yaani wananchi wetu ili waweze kubadilisha kura ni lazima kwanza wabadilishe fikra!

Ninaamini kimsingi mambo yafuatayo ambayo nimetokeo ya kujifunza Fikra za Mwalimu Nyerere:

a. Usawa wa watu wote unaotokana na usawa wa utu: Nimewahi kuliandika hili baadaye kuwa Nyerere aliona usawa siyo ule wa kisheria kutokana na wote kuwa "sawa mbele ya sheria" kama ilivyo Marekani bali ni usawa ambao unatokana na wote kuwa ‘sawa sababu ya utu wao'. Kwamba hakuna binadamu mwenye utu zaidi ya mwingine;

b. Uongozi ni utumishi siyo ulazimishi: Ninaamini kuwa mtu anayetaka kuwa kiongozi anapaswa kuwa mtu anayetaka kutumika siyo kutumiwa au kutumikisha wengine;

c. Maendeleo ni ya watu siyo vitu: Mojawapo ya mambo makubwa kabisa niliyojifunza kutokana na fikra za Mwalimu ni dhana kuwa maendeleo ya vitu bila maendeleo ya watu ni udikteta wa vitu. Watu ndio msingi, kiini, sababu, lengo na njia ya maendeleo. Utawala wa CCM (hasa kuanzia Mkapa) umeweka mkazo mkubwa sana kwenye kuendeleza vitu; wanajivunia vitu, wanatuonesha vitu. Siyo watu walioendelea! Na vile vile maendeleo siyo kuongeza idadi ni kuongeza ubora! Hivyo, kuongeza mashule mengi ya sekondari na walimu wengi bila kuongeza ubora wa elimu inayotolewa huwezi kuyaita maendeleo. Nyerere alisema kujenga barabara, majengo na vitu vingine ni maendeleo tu kama vitu hivyo vyote vinamfanya mwanadamu ayamudu mazingira yake vizuri zaidi na kumfanya aishi maisha bora. Ukijenga barabara nyingi za kisasa ambazo zinatumiwa na watu wenye maisha ya juu wakati maskini bado wanatembea pembezoni mwa barabara hizo huwezi kuyaita hayo maendeleo. Angalau si kwa yule anayetembea barabarani na kukoswakoswa na gari!


d. Siasa ni chombo tu cha kuchochea mabadiliko. Binafsi nachukulia siasa kama chombo cha kusaidia kuleta mabadiliko. Ninaamini siasa ikitumiwa vizuri kama kisu inaweza kutumika kumchuna ng'ombe vizuri, kukata majani, na hata kuchimba ardhini ili kuleta tunachotaka. Ikitumiwa vibaya inakuwa kama jambia mikononi mwa kichaa! Ina madhara. Hivyo ni muumini wa "siasa bora" na siyo "bora siasa";

e. Wenye kushika madaraka wanashika kama dhamana si kama haki yao. Mojawapo ya mambo muhimu yanayoniongoza ni kuwa sina heshima ya kutukuza mtu mwenye madaraka kwa sababu anapigiwa saluti au anaitwa mheshimiwa. Wote kwangu hawa ni watu waliopewa dhamana na dhamana yenyewe ni ile inayotokana na wananchi. Sijali sana nani anashika cheo gani; ninachojali ni nini anafanya mwenye cheo hicho kutumikia wananchi.

f. Raslimali za Tanzania ni kwa ajili ya kunufaisha Watanzania. Msingi huu kwangu ni msingi mkubwa wa mawazo yangu juu ya uchumi. Siamini kabisa kuwa raslimali zetu ni kwa ajili ya kunufaisha mataifa ya kigeni. Katika hili naamini katika usawa siyo wa vitu bali wa nafasi (equality of opportunity).

g. Viongozi ni lazima wawajibike kwa wananchi na wasipowajibika wawajibishwe na wasipowajibishwa wabishiwe! Sipendi kabisa watu wanaokubali kauli za viongozi au watu wenye madaraka kwa sababu wanawaheshimu.

Sasa kutokana na hizo hapo juu (nyingine nimeziweka pembeni) nilijikuta nabadili mwelekeo wa jinsi gani naweza kufikisha mawazo yangu. Nirudi kwenye hoja iliyotolewa kuhusu ile insha ya Mbowe na kwanini sikuamini kuwa ameonesha uongozi (na bado naamini niko sahihi na wengine wote wanaomini kinyume wamekosea!)

Ikumbukwe kuwa makala ya Mbowe iliandikwa mwishoni mwa mwaka 2009 (Disemba 2). Lakini kabla ya kuandika makala yake hiyo ni vizuri kujiuliza nini kilikuwa kinatokea nchini na kwa kiasi gani kilishabadilisha mwelekeo wangu wa kumuona Kikwete kama sehemu ya suluhisho la matatizo yetu na kuwa yeye na chama chake ni sehemu yatatizo.
Nilianzisha mada yenye kujadili bajeti ya kwanza ya Kikwete (ile ya 2006/2007).

Hii ndiyo ilikuwa bajeti ya kwanza ya utawala wa Kikwete. Nilisema hivi wakati ule kuhusiana na hilo "Ni kutokana na utekelezaji wa bajeti hii ndo tunaweza kwa haki kuanza kumhukumu Kikwete na watendaji wake." Nilihitimisha kuwa ilikuwa ni "bajeti ya kiinimacho".

Lakini kitu kingine ambacho kilitokea na ambacho kiliniaminisha kuwa Kikwete na CCM ni tatizo ni mwitikio wa serikali ya Kikwete na Bunge la CCM juu ya filamu ya "Darwin's Nightmare". Nilishangazwa na mwitikio huo na hasa kitendo cha Kikwete kukanusha kuwa watu wetu hawali mapanki (makayabo) na vile vile kukataa kuwa silaha zilikuwa hazisafirishwi katika ardhi yetu kama ile filamu ilivyodokeza. Hili lilinishangaza. Na nilishangaa zaidi pale Bunge lililokuwa kwenye kikao cha bajeti lilipotoa kauli ya kumuunga mkono Kikwete.
Kwa wanaokumbuka ndio ripoti ile ya "Tanzania's Role in Arms trafficking" nilipoandika ikikusanya taarifa mbalimbali. Mpaka mkubwa ulizidi kati yangu na watawala na kwa kiasi fulani na watu ambao mwanzoni tuliwahi kuwa marafiki (japo si wakaribu).
Niliewa tatizo ni zaidi ya mtu mmoja ni chama chenyewe!

Novemba ya mwaka ule (mwezi mmoja kabla ya makala ya Mbowe) niliandika ile makala ya "The arrogance of power). Nilielezea mle ni kwanini tunasumbuka sana na hiki kiburi cha wenye madaraka.

Sasa tukio jingine ambalo siwezi kulisahau ni tukio la Mauaji ya wale wafanyabiashara wa vito vya thamani katika ile kesi maarufu ya Zomba. Wakati ule nilielewa kwa undani zaidi pia jeshi la polisi ni tatizo kubwa zaidi na nilikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kutaka IGP Mahita aondolewe na ndio nilitoa pendekezo la kugawa Dar-es-Salaam kama mikoa ya polisi (kanda). Pendekezo hili lilichukuliwa mara moja.

Sasa hadi wakati ule nilikuwa nalenga katika kuamsha watu ndani ya watawala kuanza mabadiliko ya kuongoza vizuri. Mwaka 2006 ulipoisha kitu kimoja kilikuwa dhahiri; viiongozi wabovu hawageuki kuwa wazuri wakishika madaraka bali wanathibitisha ubovu wao zaidi. Na hili ni kwa sababu wakati ule sakata la Richmond lilikuwa limeiva na tukaona mwitikio wa serikali. Mwaka 2007 ulipokuja nilikuwa nimeshaweka mawazo yangu sawa zaidi kuwa kanuni ninazozipigania haziwezekani tena chini ya CCM! Kumbuka sikubadilika msimamo wangu au fikra zangu; nilibadilika ni wapi naweza kuona fikra hizo zinatekelezeka zaidi!

Mapema mwaka 2007 ilipatikana picha ambayo wengi labda mnaikumbuka. Ilikuwa ni katika sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar ambapo viongozi waliokuwa jukwaani walionekana wamechoka na kusinzia akibakia Seif Sharrif tu akiwa macho. Niliandika mada wakati ule na kuiita "Taifa la viongozi waliolala".

Lakini ni ile makala ya "Kuanguka kwa CCM Unabii utatimia" ndiyo ambayo labda iligusa fikra za watu wengi zaidi. Ni makala ambayo ilikuja mapema 2007 (Januari 20). Kwa yeyote anayeweza kusoma anajua kabisa kuwa ni wazi kuwa makala yangu ilikuwa inautenganisha moyo wangu toka CCM kuufanya ukubaliane na fikra zangu. Nilikulia ndani ya CCM, nimekuwa Chipukizi na kushiriki hata mbio za mwenge. Kwa hiyo hisia zangu zimechukua muda kukubaliana na kile ambacho nilikuwa nakiona kiakili. Labda niseme akili yangu ilishaikataa CCM mapema zaidi kabla ya hisia zangu kufanya hivyo.

Mojawapo ya makala zangu ambazo labda wengi hawakuisoma ni ile ya Pongezi ya Miaka 30 ya CCM. Hii ilikuwa ni Februari 2007. Makala ile ilichora kwa upande wangu mpaka wa kifikra (ikumbukwe ni baada ya kauli yangu kuwa moyo bado ulikuwa CCM). Katika makala ile nilisema hivi "Hata hivyo kama nilivyosema, ni bora uungane nami kutoa pongezi hizo sasa na leo kwani kuanzia wiki ijayo, miaka mingine thelathini inaanza, miaka ambayo itakuwa ni tofauti. Anayedhania kuwa miaka thelathini ijayo itakuwa ni ya hadaa na utawala wa CCM mtu huyo hajui kusoma ishara za nyakati."

Nilihitimisha kwa maneno haya "miaka thelathini iliyopita tunasema hongera CCM, kwani si kidogo, lakini inatosha"! Mstari ulikuwa umekamilika.

Sikurukia behewa la chama kingine
Kinyume na watu wengine ambao wanatoka huku na kuingia kule mimi niliendelea na nimeendelea kubakia kuwa huru kifikra. Kanuni zangu zikibaki pale pale lakini nikitamani sana kuona chombo kipya chenye kuweza kubeba matumaini ya Watanzania kinatokea. Sikuwa muumini wa CDM ilivyokuwa wakati ule na sikuamini kwa muda mrefu kama inaweza kutuongoza kuelekea matumaini. Hata sasa hofu yangu hii bado ipo na inanisumbua sana.

Baada ya kuibuka kwa ile ripoti ya Mafia wa Tanzania niliweza kuona matumaini; niliandika makala ile ya "Twawapa Notisi watawala wetu". Ikumbukwe kuwa ni mimi ndiye niliyebadilisha kauli ya "viongozi wetu" na kuwa "watawala wetu". Leo hii wananchi wetu wengi (wanasiasa na wasio wanasiasa) wanajua tofauti ya haya mawili.

Mwezi wa tano mwaka 2007 niliandika makala ya "Je wapinzani watatuongoza". Makala hii iliangalia wakati ule kama kuna tumaini katika upinzani. Na shauri watu wasome makala hiyo kuweza kuangalia nilichokuwa ninakisema wakati ule wakati tunaangalia ujio wa uchaguzi wa 2010.

Kuelekea uchaguzi wa 2010
Kuelekea uchaguzi wa 2010 nilikuwa nimeshaamua kuwa upinzani unahitaji kupewa nafasi; lakini siyo kupewa nafasi kama hisani bali kustahili nafasi. Niliandika ile makala ya "CHADEMA kutoka hapa mpaka kule" na wiki chache kabla ya uchaguzi niliandika ile makala ya "Pembetatu ya Ushindi". Makala hizi mbili zilikuwa na lengo la kukichochea CDM kuweza kuonesha kweli kinataka kushika hatamu za uongozi wa taifa hili.

Bahati mbaya sana uongozi wa CDM haukuwa na lengo hasa la kushika hatamu za uongozi wa taifa wakati ule. Hawakujipanga kushika utawala na hili kwa kweli lilisikitisha sana kwa sababu kama ilivyo leo hii bado wanafikiria kwa msingi wa "mimi nipate"! Matokeo yake leo CDM kiko katika hali iliyokuwepo 2007! Kikipendwa zaidi, kikikubalika zaidi lakini kikifanya sifuri kujipanga kushika madaraka!

Mojawapo ya swali kubwa zaidi ambalo yapaswa kujibiwa ni ilikuwaje nilikuwa naiunga mkono CCJ? Kwanza ni kwa sababu za ukweli kwamba nilishakata tamaa na CDM na niliamini kuwa ili CDM iamke inahitaji chama kingine cha upinzani ambacho kingeiwashia moto nyuma. CCJ kilikuwa ni chama ambacho endapo kingepata usajili wa kudumu kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 basi mazingira ya kisiasa yangebadilika sana. Lakini kitu kingine ambacho wengi walikuwa hawakijui ni kuwa katika vita kuna mbinu; kwangu CCJ ilikuwa ni diversion tactic ya kunipa uhuru kufanya kitu kikubwa zaidi ya kuisadia CDM ishinde. Na nilifanikiwa sana kwani wakati watu wanahangaika na mimi na CCJ, CDM ilikuwa inapangwa kufanya vizuri zaidi!

Nimebadilika?
Ningeweza kuandika kwa kirefu sana juu ya hili lakini sijioni kama nimebadilika. Vile ninavyovisimamia bado ni vile vile na imani yangu kuhusu uwezekano wa kujenga taifa la kisasa bado ipo pale pale. Kilichobadilika zaidi ni kuwa ninaelewa zaidi kuwa wanasiasa wanataka mabadaraka zaidi kwa ajili ya madaraka. Ni kama Kikwete alivyoutaka Urais kwa ajili ya Urais. Mbowe bado hajaonesha uongozi na kipimo cha kushindwa kwake kilionekana 2010; viongozi wengine ndani ya CDM nao wanapata shida ya kuonesha uongozi na badala yake kuelekea 2015 CDM inaweza kwenda ikiwa imegawanyika kuliko CCM!

Wanaofikiri kuwa ati itakuja kujipanga baadaye wanajidanganya. CDM ilitakiwa iwe imeshajipanga sasa hivi kuelekea uchaguzi wa 2014 na ule wa 2015. Badala yake mwaka huu tumeshuhudia malumbano ya ajabu sana na visa vya ajabu vikitokea. Utagundua kuwa sijawahi kwa mwaka huu kutoa maoni yangu kuhusu hili kabisa na labda nitalitolea maoni lakini naendelea kukata tamaa na inakatisha tamaa! Nilisema wakati wa uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki ningekuwa na uwezo ningewatia bakora viongozi wa CDM na nilimaanisha! Na nilisema wangepoteza Arumeru Mashariki Mbowe na uongozi wote wa juu wangetakiwa kujiuzulu; na hata sasa labda kesi inaweza kujengwa ya kwanini wajiuzulu mapema zaidi (bado sijamaliza kuijenga hii hoja, inshallah).

Bado siamini kuwa CDM ilivyo sasa iko tayari kushika hatamu za uongozi wa taifa letu. Ndio maana utaona kuwa mimi pia siyo muumini wa "tuiondoe kwanza CCM halafu tutajua mbele ya safari". Siamini katika kuiondoa CCM ili tuingize chama kingine alimradi turidhike kuwa tumeiondoa CCM. Ninaamini yatupasa tuiondoe CCM kwa sababu kuna chama kingine kina sera na dira nzuri kwa taifa; kina viongozi wenye busara, na kinasimamia kanuni za msingi zilizojenga taifa letu. Chuki haitoshi kuwa sababu ya mabadiliko makubwa; inaweza kuwa kichochea lakini sababu inapaswa kuwa sera bora, dira bora, uongozi bora na mtazamo bora kuliko unaotolewa sasa. Bahati mbaya CDM imejikita sana katika kuonesha kile ambacho baadhi yetu tulishakijua - CCM haistahili kuendelea kuongoza kwani sera zake zimeshindwa, itikadi yake imekufa na mwelekeo wake ni wa upotofu. Hitimisho hili hata hivyo, halitufikishi kwenye kukubali CDM kama chama tawala alimradi.

Inawezekana nimebadilika; lakini mwenyewe sijioni hivyo; zaidi naona nimethibitika kabisa katika yale ninayoyaamini. Sivutwi na hotuba hewa, au na mivuto ya umaarufu wa watu. Sipimi watu kwa kuangalia nani anaungwa mkono zaidi au nani haungwi mkono. Ninapima watu kwa fikra zao na mambo wanayoyasimamia lakini kwa jinsi gani wanaongozwa na kanuni (principle oriented) kuliko wanaoongozwa na matukio (events-oriented). Watu wanaoongozwa na matukio huitikia matukio yanapotokea; wanaoongozwa na fikra huitikia hata wakati kuko kimya!


Na. M. M. Mwanakijiji
 
Back
Top Bottom