Propaganda za kusaulisha watu Mambo muhimu kwa ajili ya kuuwa Demokrasia zipo CCM na CDM Kulikoni?

Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,581
758
Wapo wana siasa ambao mimi naamini ndio wana siasa uchwara na mapandikizi ya kuuwa demokrasia hapa Tanzania ambao kila usiku na mchana wanadhani Watazania bado ni wajinga wa kudanganywa kwa maneno wakidhani kuwa wao ni maarufu na kuwa kwatumia umaharufu wao wanaweza kufanya lolote kupotosha umma. Ni kweli karne nyingi sasa Watanzania tumeishi kwa kudanganywa na kupewa ahadi hewa na wanasiasa kila uchaguzi ukifika, lakini ni mtu mpumbavu pekee ambaye bado anaweza kuamini kuwa bado tupo katika nyakati za kudanganywa kama watoto na kupotoshwa kama mataahira.


Ifike wakati wana siasa wajue sasa sio wakati wa propaganda za kuahada na kutoa ahadi za uongo tena. Eti wapo watu wanaotaka kutwambia kuwa wapo wezi hapa Tanzania wakujadiliwa na kuchukuliwa hatua kuliko EL! Hawa watu wanataka tusahau sio tu sura na tabia ya huyu mtu EL, lakini pia wanataka tusahau hata kutoa maoni yetu katika kufuma katiba mpya, hawa ni watu hatari, lazima tuwaogope kama ukoma bila kujali fedha na ukubwa wa mtandao walio nao. Watu hao wameibua adithi tamu iitwayo Watanzania walioficha fedha nje ya nchni, hivi punde wametoa single mpya kuwa Dr. Slaa ana kadi ya CCM. Hizi adithi zote ni upuuzi mtupu na upotoshaji mkubwa wa Umma ili waache kuelekeza mawazo na nguvu zao katika mambo ya msingi na muhimu kwa Taifa letu.

Shida sio kuweka fedha nje ya nchni, shida ni kuiba mali ya Taifa bila kujali mwizi anazitunza wapi, kabla ya kupewa ushahidi na majina ya watu wenye akaunti nje nchni tuambiwe waliiba wapi na katika tukio lipi la wizi (EPA, Meremeta, Deep Green nk). Kama ilivyo vile vile shida sio kadi gani aliyonayo Dr. Slaa, sisi tunamuhitaji mchapa kazi aliyejitolea kwa faida yetu na maslahi yetu bila kuweka ubinafsi na umimi na kutafuta umaharufu na fedha haramu hata kama angekuwa CCM yamkini watanzania wangempenda kwa dhati kwa tabia hiyo. Huu si muda wa mchezo tena tupo kikazi zaidi wanasiasa wajue hivyo.

Hawa maadui wa Demokrasia wapo CCM na pia hapo CDM; ni vyema ikaeleweka nchni kwanza na Taifa daima bila CCM na pia bila CDM. wale wanaopoteza muda kulinda CCM kwa mapanga, marungu na bunduki wajue gharika halizuiliki kwa stahili hiyo, wasome alama za nyakati na wakae tayari. Kama kuna mtu anaipenda CCM aache kupoteza muda kwa maneno afanye vitendo, alete sera na apambane na matatizo ya wananchni usiku na mchana matunda yataonekana. CCM haiwezi kutimiza ahadi zake kwa umma iwapo Dr. Slaa atarudisha kadi ya CCM, wala hiyo haikuwa katika ilani ya CCM na ahadi za Kikwete kwa Watanzania.

Muda unaopotezwa na wanasiasa wetu kwa mambo ya kipuuzi kama haya, hauna tija na hauwezi kumsadia mwananchni wa chini aliyekwama kutokana na sera mbovu za maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kama hatuna wanasiasa wenyewe muono basi wapo wapi wataalam wetu waingie zaidi katika siasa kuokoa jahazi maana inaoneka wengi wa hawa tulio nao ni hovyo zaidi hawana uwezo wowote wa kutuendeleza wao ni kujadili watu na kupotosha umma tu!

Wale wana CCM walio CDM sasa ni wakati wakurudi kwenu maana punde kidogo mtaumbuka zaidi. Mshauri mzuri wa CCM kwa leo sio anayepoteza muda kuangaika na CDM bali ni mtunzi mzuri wa sera mbadala kwa ajili ya kujibu matatizo lukuki katika jamii yetu, bila hivyo hakuna kupona hata Dr. Slaa akijiuzulu na hata CDM ikifa, CCM itakwenda na maji tu.

Wale wasiotaka demokrasia ya vyama vingi na kupoteza muda kutafuta namna ya kuviuwa vyama mbadala wajue njia ya kutafuta haki kwa kutumia vyama vya siasa ni bora kuliko njia zingine zote zilizopo hapa Dunia, wasitafute balaha kwa sifa za kupita na ubinafsi wao.

Nawatakia wana jf wote heri ya mwaka 2013, tupambane mpaka kieleweke tusibabaishwe na wanasiasa uchwara.
 
Back
Top Bottom